Waalimu Waungana na Madaktari katika Mgomo

Scolari Ndenga

JF-Expert Member
Aug 4, 2008
271
43
KAtika kile kinachoonekana kuchoshwa na longolongo za Serikali, waalimu 246 Wilayani Handeni wamegoma kuingia madarasani kufundisha na wameaapa mgomo unaendelea mpaka watakapolipwa stahiki zao. Hawa ni walimu wa wilaya mzima na leo wamevamia ofisi ya Halmashauri kutoa mwelekeo wao.

Kazi ipo mwaka huu
 
Hapa pana utamu wake,himahima na waadhiri nao wagome kisha wazee wa Traawu wahitimishe
 
Hahaaaa, na bado, nimewaambia hakuna aliye salama kwa sebene la Madoctor wa kweli hapa..... bado tunasubiri na wengine..
 
chanzo cha yote haya nia posho za wabunge ndiyo zilizopelekea watu akafahamu kuwa kumbe serikali ina pesa za kutosha basi nao walipwe madai yao halali tu

sasa kazi ipo
 
Bado tifu linazidi kusambaa, Wabunge si wanakazi nyingi kuliko wataalamu?

ndugu sitaki apa...kuna watu malikimbia umande kama prof majimarefu et all,alaf leo dr ulimboka alipwe lak9 na hawa jamaa wajipe posho!hapana!
 
Kitu kimoja ambacho walimu wanapaswa kujifunza kutoka kwa madaktari ni kutoyumba wanaposema wanagoma. Walimu wanachezewaga na serikali kwa kua wanajulikana ni watu wa kutishia nyau na nidhamu yao ya uwoga.

Ilipaswa hapa ngoma inaunganishwa bila kujali maswala ya notisi ya siku 90 wala nini. Lakini wakina Mukoba bado hawajachelewa
 
naona kazi inaanza..
Tunawasubiri wao tu..hakika wao wakigoma hatutasikia yale ya kuleta walimu toka jeshini.
 
Haya mambo ni wagumu,jueni umuhimu wa kila taaluma ya mtu,msilete siasa kwenye roho za watu,selikari sikieni.
 
Wabunge wengi wa XicMM wameiba kura au kuchakachua

Hawana deni kwa wananchi, hawawajibika kwa wananchi.

Sasa wananchi hasa waalimu na wananchi wataingia.

Sasa hawa wabunge na mawaziri sasa waonyeshwe kuwa hawako juu ya sheria.

Mawasiliano yafanyike ili waalimu wote nchi waungane.

Tuanzishe page ya facebook tusambaze ujumbe
 
Haya mambo ni wagumu,jueni umuhimu wa kila taaluma ya mtu,msilete siasa kwenye roho za watu,selikari sikieni.

Na polisi wako njiani, kipenga hakijasikika. Kuna mmoja ameniambia amesikia fununufununu wanaongea chini chini. tusubiri.
 
Back
Top Bottom