Naibu Waziri Deogratius Ndejembi aagiza kufanyika tathmini ya ukarabati ya nyumba za waalimu Ruvuma na kuchukua hatua

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942

NAIBU WAZIRI NDEJEMBI ATOA MAAGIZO KWA KATIBU TAWALA WA MKOA NA WAKURUGENZI

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Mhe. Deogratius Ndejembi amemwagiza Katibu tawala wa Mkoa wa Ruvuma kuhakikisha anafanya Msawazo ndani ya Mkoa wake kwa maeneo ambayo yanaupungufu wa watumishi na kuwaelekeza wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa kufanya tathmini ya ukarabati ya Nyumba za waalimu na kuchukua hatua stahiki.

Mhe. Ndejembi ametoa maagizo hayo wakati akijibu mswali ya nyongeza ya Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini Mhe. Jonas Mbunda lililogusa katika sekta ya uhaba wa waalimu licha ya kwamba mgawanyo wa waalimu walioajiriwa hivi karibuni Jimbo hilo halijapata mwalimu alilouliza kuwa Je? Serikali inamkakati gani wa kuhakikisha inamaliza changamoto hii kwenye jimbo la Mbinga Mjini? - Mhe. Jonas William Mbunda

“Nichukue nafasi hii kumwagiza katibu tawala wa Mkoa wa Ruvuma kuhakikisha anafanya usawazo ndani ya Mkoa wake kwa maeneo ambayo yanaupungufu wa watumishi ikiwemo kupunguza kwenye yale maeneo ambayo yanawatumishi wengi na kuwapeleka katika maeneo yenye ufinyu ikiwemo jimbo la Mbinga Mjini” Naibu Waziri Ndejembi.

Kufuatia majibu hayo ya serikali likamuibua Mbunge huyo kuuliza swali la nyongeza lililogusa katika sekta ya uhaba wa waalimu licha ya kwamba mgawanyo wa waalimu walioajiriwa hivi karibuni jimbo hilo halijapata mwalimu alilouliza kuwa “Je? Serikali inamkakati gani wa kuhakikisha inamaliza changamoto hii kwenye jimbo la Mbinga Mjini?” - Mhe. Jonas William Mbunda

Awali katika Swali la Msingi la Mbunge huyo Naibu Waziri Ndejembi amesema Serikali imefanya tathmini ya hali ya Uchakavu wa miundombinu katika shule za msingi Nchini na kubaini uwepo wa miundombinu inayohitaji ukarabati mkubwa, mdogo, kubomoa na kujenga upya na isiyohitaji ukarabati ambapo kipaumbele kwa mwaka 2023/24 kitakuwa ni ujenzi wa vyumba vya madarasa na shule mpya.

Majibu hayo ikiwa ni kufuatia swali la Msingi aliloulizwa na Mbunge huyo kuwa kuwa “Je, lini Serikali itatenga fedha za ukarabati wa Madarasa, Nyumba za Walimu na Vyoo katika Shule za Msingi Jimbo la Mbinga Mjini?” - Mhe. Jonas William Mbunda

“Kuhusu hali ya uchakavu kwenye vyumba vya waalimu ni jukumu la Halmashauri kufanya tathmini ya Garama zinazohitajika kukarabati nyumba za waalimu zilizopo kwenye maeneo yao na kuzitengea bajeti ili zikarabatiwe nitumie fursa hii kuwaelekeza wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa kufanya tathmini ya ukarabati ya Nyumba za waalimu na kuchukua hatua stahiki” Mhe. Ndejembi

ftgyuhuhwer.jpg
 
Back
Top Bottom