Vyombo Vya Rasmi vya Habari vya TZ, Havitimizi wajibu Wake, Njaa, Ukata, Ujinga!. Waandishi, Wamiliki Watakiwa Kujiongeza- Jicho Letu Star TV

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,506
113,621
Wanabodi,

Vyombo rasmi vya habari vya Tanzania, vimelaumiwa kuwa havitimizi wajibu wake wa kuwahabarisha Watanzania, kutokana na Waandishi wa habari kukabiliwa na njaa kali kufuatia kulipwa malipo kiduchu, vyombo vya habari vinakabiliwa na ukata mkubwa, wamiliki wanaendeleza ujinga kwa kuajiri watangazaji vihiyo.

Waandishi na Wamiliki wametakiwa kujiongeza kwa waandishi kujiongeza kwa kujielemisha zaidi, na wamiliki wametakiwa kujiongeza kwa kuwekeza zaidi kwenye taaluma na kulipa vizuri waandishi wazuri.

Mjadala kwa Mwanza unaongozwa Mtozi Leonard Mapuli akiwa na Mwalimu wa wanahabari kutoka Chuo cha SAUT, Denis Mpagaze. Kwa Arusha yuko Angelo Mwoleka na Mgeni ni mwandishi nguli Pati Magubira. Hivi vichwa vyote vinne ni vichwa vya ukweli, hivyo tegemea madini ya kuhabari kwenye bandiko hili.

Kwa vile kipindi ni 90 min na yamezungumzwa mengi, siwezi kuyaweka yote nitaweka baadhi tuu kwa mtindo wa issues in a number formats za matukio makubwa ya kihabari nikianzia na kubwa kuliko la Sumaye kujitoa Chadema, Heche kushindwa na Mwanamke, nikimalizia na Mkandarasi aliyezimia.
  1. Sumaye kujitoa Chadema. Vyombo vya habari vimelaumiwa kwa kutowatendea haki Watanzania. Kwa vile habari ya Sumaye kujitoa Chadema ilitangazwa live mubashara na TV tangu mchana, na mitandao ya kijamii ikatangaza siku nzima. Haikutegemewa tena taarifa za TV na Magezeti ziishie kutangaza kitu kile kile kila mtu tayari anakijua, yalipaswa kwenda deep zaidi, kwa kusema kile ambacho Sumaye hakukisema, kitu kilichosababisha Sumaye ajitoe Chadema.
  2. Mwalimu Mpangaze akasema, fani ya uandishi wa habari ni tasnia muhimu, inayohitaji watu wenye akili na uwezo wa uchambuzi wa kina. Baada ya Sumaye kujitoa, na kutangaza alikuwa hataki uongozi na kutangaza mabaya ya Chadema huku akitangazwa live, vyombo makini vya habari, na waandishi makini, hawakutakiwa kuishia hapo, wangepaswa kuzama deep, kwanini Sumaye alijitoa CCM?. Siku anajitoa alisema nini?. Kwani amejiunga Chadema, tangu amejiunga Chadema amefanya nini, kwanini sasa anajitoa Chadema?. Akasema Sumaye ni mlalamishi, kila akishindwa, analalamika. Kule Mbulu alishindwa na Mary Nagu akalalamika, akagombea urais CCM akashindwa akalalamika na kutoa mabaya ya CCM, akalalamika na kujitoa CCM, Chadema na kugombea uongozi wa Kanda ya Pwani, mtu asiyetaka uongozi, anagombea nini?. Akagombea tena Pwani na kugombea Uenyekiti, baada ya kukataliwa Pwani, akajua pia Uenyekiti angekataliwa ndio kaamua kujitoa na kutaja mabaya ya Chadema, kama angeshinda angeyasema?. Mtu asiyetaka uongozi angekuwa mwanachama tuu wa kawaida, mtu hutaki uongozi, unagombea unashindwa unalalamika, unajitoa, huyu ni mtu wa namna gani, hivi ndio vitu media ilipaswa kuviandika.
  3. Arusha Mwoleka na Pati Magubira wakachangia kuangushwa kwa Sumaye, na Heche, Mwambe na Selasini, ni hatua nzuri ya kukua kwa demokrasia ya uchaguzi, watu wenye majina makubwa, siku zote wamekuwa wanatembelea nyota za ukubwa wa majina yao, sasa wapiga kura hawaangalii ukubwa wa jina bali wanaangalia uwezo na mchango wako kwa chama, Sumaye ni jina kubwa laini hana mpact yoyote kapigwa chini. Kule Kanda ya Ziwa, kitendo cha kidume Heche kushindwa na Mwanamke Esta Matiko ni fedheha kubwa kwa mwanamume wa mkoa wa Mara. Hii inaweza kupelekea hata Mbowe, anaweza kubakia peke yake kwenye kugombea Uenyekiti, kama wapiga kura wanajitambua, anaweza pia apigwe chini!.
  4. Pati Magubira ametoa mchango wa muhimu sana, amesema ili media iweze kutimiza majukumu yake kikamilifu, inapaswa iwe independent, na independence hiyo ilindwe na katiba, akasema Tanzania tulikuwa nchi ya chama kimoja na katiba iliyopo ni katiba ya chama kimoja. Tulipoanza mfumo wa vyama vingi, tulibadili sheria tuu kwa kutunga sheria ya vyama vingi lakini katiba bado ni ya chama kimoja, kwa katiba hii, vyama vya upinzani vitaendelea kunyanyasika na CCM itaendelea kutawala milele. Akaisifu awamu ya JK kuanza mchakato wa katiba mpya, lakini kwa awamu hii katiba sio kipaumbele chake, suluhisho ya manyanyaso ya vyama vya siasa ni katiba mpya.
  5. Mwalimu Mpangaze amesema, wamiliki wa media ni wafanya biashara, hawathamini contents wala waandishi, wao wanachojali ni pesa tuu, akatolea mfano chombo fulani cha utangazaji watangazaji wake walilalamika waongezwe mshahara na mazingira bora ya kazi, boss akawaita akawaambia, mimi ndio nimewasaidia sana kuwalipa hicho ninachowalipa, asietaka anaweza kuondoka saa hizi, kufika jioni nafasi zenu zimejaa, kweli jamaa waligoma, wakaondoka, jamaa akaita wana kwanya, wakaingia studio matangazo yakaendelea. Amesema wamiliki lazima wawekeze kwenye rasilimali watu, vifaa na ubunifu, watoe news nzuri, watengeneze vipindi vizuri, ndipo wapate watazamaji wengi na kuvutia matangazo wapate pesa zaidi.
  6. Pia Mwalimu Mpangaze akawasisitiza waandishi wa habari, individually kujiongeza, kwa kuongeza ubunifu, kujiendeleza kielimu na kufanya specialization, akaipongeza sheria mpya ya habari ilitoa grace period ya miaka 5 kwa waandishi wasio na taaluma, hivyo kuanzia mwaka 2021, uandishi ni taaluma, huna vyeti, uandishi utausikia. Akasema waandishi wana njaa na ni masikini wa kutupa, akashangaa mtu unaweza kuwa mwandishi huku huna gari?, mwandishi anayetembelea daladala, atawezaji kufika kwenye tukio on time?, atawezaji kuwahisha story newsroon to beat the deadlines?. Amewataka wamiliki wawalipe vizuri waandishi wao ili wasitegemee bahasha!.
  7. Habari ya Mkandarasi aliyezimia baada ya kukaripiwa na Waziri Jafo pia wameiangazi, uchokozi wa habari hiyo, ulianzishwa na Angelo Mwoleka kule Arusha, akisema japo jamaa alizimia, lakini mkono alilinda pochi isichomolewe!. Pati Magubira akachangia kilichofanyika is not fair, yule ni mtu mzima ni baba kwenye familia, ana mke na watoto, huwezi kumgombeza hivyo mbele ya kadamnasi ya watu ni kumdhalilisha na kuutweza utu wake.Hata kama kazi haiendi vizuri, kuna namna za kistaarabu za ufuatiliaji lakini sio kivile.
  8. Waliporudi Mwanza, Mtozi Mapuli akauliza hivi jamaa alizimia kweli au alijiangusha?. Mwalimu Mpangaze akasisitiza, hapo ndio tunapoona ukosefu wa maadili, ile ni emergence, kunapotokea dharura ya mtu kuanguka, waandishi wenye maadili hawapaswi kuonyesha ile picha ni kinyume cha maadili, ikitokea dharura, kila kitu kinabadilika, mwandishi hana uwezo wa kujua huyo mtu amezimia, amezirai au amekufa!, watu wanakosa maadili hadi kupiga picha maiti!. Mtu pekee mwenye mamlaka ya kihabari ya kusema kilitokea nini ni dakitari na sio mwandishi hata kama umeona.
  9. Mtozi Mapuli akakumbushia tatizo kubwa la media za Tanzania kukosa habari muendelezo, tukio limetokea, limeripotiwa, lakini hakuna chombo chochote kilichofuatilia hali ya yule mtu, nini kilimtokea, tatizo ni nini?, na sasa anaendeleaje. Ticha aja joke, jamaa alipoona kibano kinazidi, akaamua ajilaze chini maswali yasiendelee.
  10. Issue nyingi zilizungumzwa kifasaha sana, siwezi kuzikumbuka zote, ila kwa vile na mimi ni mwana habari, kuna issues nyingi za kihabari nimewahi kuzizungumza baadhi yake ni hizi
Media kuikosoa Serikali: Je, Tanzania tuna Strong Media au Strong ...
Vyombo Vya Habari Vya Tanzania, Havina Uwezo wa Uchambuzi wa ...
Je, Tanzania tuna Media Freedom kubwa kuliko UK na US? Tushuhudie ...
Tanzania tuna uhuru wa habari, ila media oga! Tungekuwa mbali sana ...
Uhuru wa Habari Tanzania:Jee Vyombo Viko Huru?. Jee Waandishi wa ...
Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa - Pasco ...
Kuelekea Octoba 2015: Je, Sasa ni Wakati wa Media Zetu Kufanya ...
Serious Media inaweza kuwabaini "wasiojulikana" Deo Masakilija ...
Uchumi wa Magufuli: Sekta Binafsi ina-Suffer. Yalianza Maduka ...
Media, Tumedhalilishwa!, Tumejidhalilisha!. Ni Matokeo ya Sheria ...
Magufuli kutawala kurasa za mbele za magazeti, Je anastahili hata ...

Asanteni kufuatilia.

Nawatakia Jumamosi Njema.

Paskali
 
Tatizo huanza wanapofuatilia viongozi ambao hawapendi kufuatiliwa.

Hujui wanavyofanyiwa au unataka tu usikie tunasemaje!?
Nchi hii ni maskini, kila mtu ana njaa. Utatimizaje wajibu wako una njaa? Mmeisaidia ccm kuua upinzani ambao ndiyo ungekuwa chachu ya taasisi mbalimbali kutimiza wajibu wake.
Hii divide & rule iliyotengenezwa haiwezi kutuacha salama.
 
Wamiliki wa vyombo vya habari wanatamani kuona vyombo vyao vikiwa huru kama vile vya magharibi, Watawala wanataka vyombo vya habari view kama vya China muda wote visifie mambo ya watawala wanayoyafanya. Imagine tungekuwa na mijadala kama navyoona kule Aljaezera, CNN, CNBC, Fox, BBC, Sky news nk lazima wamiliki wangeajiri wasomi wakuendesha vipindi, kwa sasa TV zetu zinasubiri matukio ya live wakimaliza wanaweka muzic au tamthilia, redio zinajadili udaku asubuhi hadi usiku. Pascal Mayalla,
 
Hivi tujiulize watanzania wenzangu azory gwanda leo hii hajulikan alipo. Mkewe last week alikuwa ana commemorate his absence kwa machozi kbs na akatuonyesha jinsi ilivyo shida kwake kusomesha watt
Watanzania wote ambao ni mahodari wa kukosoa wenzano wapo kwenye key boar kutoa pole but hakuna mtanzania ambaye ameenda mbele kudai haki ya azory.

Lkn. Bado eti mtu anamkosoa paskali eti kawa mnafiki. Hivi mnataka apotee kama azory? Nafikir ifike mahali watanzznia wote tuamini kuwa tanznia inatuhitaj sote kwa umoja wetu na sio kundi fulan la.watu
 
Pascal Mayalla, post: 33700793, member: 17813"]
Wanabodi,


Hata usome vipi sasa hivi hakuna uhuru wa vyombo vya habari labda usifie tu, na kusifu tu hata usiposoma ni rahisi. Nimeangalia kipindi ni kizuri, japo Arusha camera ilikuwa na giza mno.
 
Hivi tujiulize watanzania wenzangu azory gwanda leo hii hajulikan alipo. Mkewe last week alikuwa ana commemorate his absence kwa machozi kbs na akatuonyesha jinsi ilivyo shida kwake kusomesha watt
Watanzania wote ambao ni mahodari wa kukosoa wenzano wapo kwenye key boar kutoa pole but hakuna mtanzania ambaye ameenda mbele kudai haki ya azory.

Lkn. Bado eti mtu anamkosoa paskali eti kawa mnafiki. Hivi mnataka apotee kama azory? Nafikir ifike mahali watanzznia wote tuamini kuwa tanznia inatuhitaj sote kwa umoja wetu na sio kundi fulan la.watu
Ni kama tunavyodhani akina Mbowe, zito na wachache ndio wapambane Sie tuje tishangilie ushindi tu... Hilo halitowwzekana
 
Back
Top Bottom