Vyeti vya uraia na yaliyonikuta - a true story

Mkuu usipende kukurupuka na theories zako na kusema huo ndio msimamo wa serikali. Mimi ni karani wa NIDA katika hilo zoezi linalozungumziwa hapa, na nakuhakikishia kuwa WAJUMBE WA NYUMBA KUMI WANATAMBULIWA NA SERIKALI KUU kama sehemu ya serikali ya mitaa.

Wajumbe wa nyumba kumi si lazima watoke CCM. Ni ule uzito tu wa mwitikio kutoka kwa watu wa vyama vingine kuchukua nafasi hizi ndio unasababisha ionekane kuwa hawa ni wajumbe wa CCM badala ya wajumbe wa nyumba kumi.

Yapo maeneo mengi tu ambapo wajumbe wa nyumba kumi wanatoka vyama vya upinzani, sasa mimi sioni shida ilipo ilhali hawa ni muhimu zaidi ktk suala la utambuzi. Nimejitahidi kueleza labda niongezee tu kwa mifano ili ndugu wengine mpate kuelewa.

Serikali kuu inatambua uwepo wa wajumbe wa nyumba kumi na inawatumia kufanikisha operesheni zake nyingi tu, mwenye akili na aelewe na mwenye kutaka kubisha na aendelee kubisha.

1. Askari akitaka kusachi nyumba yako analazimika kumtaarifu mjumbe wa nyumba kumi ili awepo na kushuhudia uhalali wa zoezi hilo na usalama wa mtuhumiwa.

2. Askari hawezi kukutia nguvuni mtaani kwako bila kumtaarifu mjumbe wako juu ya sababu ya kukuchukua isipokuwa kama itadhihirika kuwa unaleta hatari iliyo wazi.

3. Mahakama ikitoa SUMMONS ama wito mwingine wowote ule, wito huo utapitia kwa mjumbe wako wa nyumba kumi. Mwenyekiti wa serikali ya mtaa hawezi kujua wewe bwana Tiba umepanga chumba cha uwani nyumbani kwa nani kule Tandale, lkn balozi wako atajua.

4. Kwenye hili zoezi la Vitambulisho, NIDA inamlipa posho ya Tshs 10,000 mjumbe wa nyumba 10 kuwaongoza makarani kwenye nyumba zake na kuwasaidia kwa watu watakaogomea kutoa ushirikiano. Hii inadhihirisha serikali inawatambua wajumbe

5. Tarehe 26, tuna zoezi zito la Sensa, kumbukumbu yangu ya Sensa ya mwaka 2002, wajumbe wa nyumba kumi walituongoza kwenye nyumba zao. Hapa nitawapa ufafanuzi kidogo:
-Waweza kumuuliza mtu juu ya mume au mke wake ilhali amemzika juzi tu wewe karani hujui nadhaniutaishia kushangaa mama unayemhoji analia nini, lkn mjumbe ana nafasi ya kukutahadharisha
-Si rahisi mwenyekiti wa serikali ya mtaa kujua kama nyumba fulani ina wapangaji au ni kaya moja tu. Lkn mjumbe ana nafasi ya kuwa na taarifa zaidi.
-Wapo watu wanaficha taarifa za watu wenye ulemavu kwenye kaya zao, lkn mjumbe anaweza kujua taarifa hizi kwani anaishi nao hapo mtaani

Mimi siamini kama serikali haitambui wajumbe wa nyumba kumi. Ni sisi wananchi ndio tunadharau wajumbe kwa kutojua umuhimu wa ngazi yao katika utambuzi.

Kwenye daftari la WAKAZI lililoratibiwa na NIDA, kila individual alipaswa kudhaminiwa na watu wawili ili kuthibitisha ukaazi wake ktk mtaa. Wa kwanza ni MJUMBE na wa pili ni aidha MKUU wA KWAYA (kwa wenye makazi binafsi) au MWENYE NUMBA (kwa wanaoishi kwenye nyumba za kupanga), sasa ndugu zangu wajuaji hebu nielezeni, hivi Mwenyekiti wa serikali ya mtaa angewezaje kuwatambua watu wote wa mtaa wake?

Ndio wajuaji nyinyi nyinyi kesho mtasema kuna Msomali mtaani kwetu haeleweki anaishije lkn mwenyekiti yupo tu bila kujali kuna watu 18,303 katika Mtaa wa Mwongozo uliopo kata ya Makuburi. Yaani kwa akili zenu na mifano na manung'uniko, mnataraji mwenyekiti na wajumbe wake 9 wawajue watu woote hawa 18,000!

Tusipende kuwa wajuaji wajinga. NIDA imetangaza hivi kwenye vyombo vya habari: Ikiwa una mgonjwa, mlemavu au mzee katika kaya yako, RIPOTI KWA BALOZI WA NYUMBA KUMI, AMBAYE MARA BAADA YA KUTHIBITISHA KUTOJIWEZA KWA MHUSIKA ATAUTAARIFU UONGOZI WA SERIKALI YA MTAA JUU YA UWEPO WA MTU WA HITAJI HILO NA WAO WATAANDAA UTARATIBU WA KUFANIKISHA MTU HUYO KUJAZIWA FOMU NYUMBANI.

Hawakusema uripoti polisi wala mahakamani, wamesema kwa BALOZI WA NYUMBA KUMI. Mamlaka inatambua huyo ndio mtu wa karibu zaidi na wewe kuliko DIWANI na MKUU WA WILAYA. Na ndio maana wamelipwa posho na wamesaini kwenye rejesta ya wakaazi kuwadhamini watu wa nyumba zao.

Kama bado unaamini wajumbe hawatambuliki, niambie kwa nini Serikali inawatumia kwenye mazoezi yao?

Kuwa karani wa NIDA si kwamba ndio unajua Muundo wa serikali ya mtaa, serikali ya mtaa haina wajumbe wa nyumba kumi pia huu si mtihani na hatushindani nikiangalia point zako zina mantinki lakini si sheria kwani katika ushirikishwaji jamii kuna mbinu nyingi ambazo serikali au wadau wa maendeleo wanatumia ili kufanya zoezi liwe rahisi sijakataa kwamba wajumbe au mabalozi si watu muhimu ila wanasaidia kupeleka zoezi kuwa rahisi. Na ndio maana huwa tunatumia zile local institutions (ambazo zipo according to regulations) pia kufanya zoezi lifanikiwe vizuri huwa kuna watu ambao wanakubalika katika jamii huwa wanatumiwa kutokana na nature ya maeneo yetu na ndio maana huwa wanatumika wajumbe na mabalozi wakati mwingine mpaka wazee maarufu na mashuhuri huwa wanatumika kutokana na zoezi husika.
Hakuna haja ya kutukanana kuitana wajinga kama unavyo-comment kama kweli wewe ni msomi nadhani unatambua UHURU WA KUTOFAUTIANI HOJA mwisho wa siku tunafikia consensus, hizi sio theory zangu ni utaratibu tu tunafahamishana mdau Las Mas Bobos ndio maana watu hatufahamiani na ID zetu za kichina lakini mtu akiuliza kitu tunamjibu based na experience iliyopo. Ni Dar pekee na sehemu chache za mjini ndio huwa wanatumia wajumbe kwani sehemu kubwa ya nchi utaratibu huo hautumike. Hii ni changamoto inayopelekea watu kutumia mpaka wajumbe na mabalozi either inaweza kuwa inatokana na ugawaji mbaya wa mitaa au katika mitaa kuna haja kutunga sheria kuweka structure nyingine ya chini ambayo itakuwa legally accepted kwa ajili ya kumsaidia mtendaji wa mtaa au mwenyekiti.

Hoja yako ni nzuri sana katika kutumia mabalozi ila tatizo linakuja pale unaposema kwamba nakunukuu
"Mkuu usipende kukurupuka na theories zako na kusema huo ndio msimamo wa serikali. Mimi ni karani wa NIDA katika hilo zoezi linalozungumziwa hapa, na nakuhakikishia kuwa WAJUMBE WA NYUMBA KUMI WANATAMBULIWA NA SERIKALI KUU kama sehemu ya serikali ya mitaa" (Wanatambuliwa kwa sheria ipi?
MUUNDO WA SERIKALI YA MTAA NI HUU HAPA CHINI SI WANGU HUO UNAOSEMA HAPO JUU NI SEHEMU YA KURAHISISHA ZOEZI NA KUFANYA VERIFICATION TU YA INFORMATION KWA KUWA ISSUE YA URAIA KWA TANZANIA NI VERY COMPLEX KWA KUWA WATU WENGI HAWANA DOCUMENT ZA KUWAONYESHA WAO NI KINA NANI.
Serikali ya mtaa katika ngazi ya kijiji inaundwa na wenyeviti wa vitongoji ambao hujachaguliwa na wananchi pia kuna mwenyekiti wa kijiji na wajumbe wengine 25 ambao wanaunda halmashauri ya kijiji na katika hawa wajumbe 25 angalau wajumbe 7 wawe wanawake (wote hawa ni wakuchaguliwa) ila kwa mjini kunakuwa na wenyeviti wa mitaa alafu kunakuwa na mtendaji wa kijiji kwa kijijini / mtendaji wa mtaa kwa mijini ambae ni mwajiriwa wa halmashauri ambae anatunza kumbukumbu zote za ofisi ya kijiji (ikiwa na maana hawa wengine ni wa kuchaguliwa wanaweza wakapigwa chini next uchaguzi hivyo kumbukumbu zote anazitunza yeye) kwa kuwa hawa wengine ni wanasiasa na role yao kubwa ni kusimamia utekelezaji wa shughuli zote za maendeleo kama zilivyopangwa. Mara nyingi na wao hukutana mara 4 kwa mwaka ambapo katika vikao hivyo Mwenkiti wake ni mwenyekiti wa kijiji (ambae ni mwanasiasa anamwakilisha rais) na Katibu ni Mtendaji wa Kijiji / mtaa na wajumbe hao 25 na maamuzi yanayofanyika hapa ni maamuzi halali ya serikali.

Tunakuja ngazi ya kata kuna Mtendaji wa Kata ambapo pia kunakuwa na halmashauri ya maendeleo ya kata maarufu kama WDC ambayo inaundwa na wenyeviti wote wa vijiji kwa vijijini au wenyeviti wa mitaa kwa mijini na Mwenyekiti wa kamati hii ya maendeleo ya kata ni Diwani (ambae ni mwanasiasa) na Katibu ni Mtendaji wa Kata (ambae ni mtendaji wa serikali) na wajumbe hao niliowataja na hukutana mara moja kila baada yya miezi mitatu kujadili issue zote za maendeleo zinazotokea katika mitaa au vijiji husika na maamuzi yatakayofanyika hapo ndio yanachukuliwa kama maamuzi halali.

Tukitika ngazi ya kata tunakuja katika ngazi ya wilaya ambapo kunakuwa na baraza la madiwani ambalo linaundwa na madiwani wote toka kata zote na mwenyekiti wake ni Mwenyekiti wa Halmashauri (kwa wilani au miji), Meya (Manispaa au Jiji) na Katibu wa baraza hili ni Mkurugenzi wa halmashauri (wilayani) au Mkurugenzi wa jiji/Manispaa (ambaye ni mtendaji wa serikali na kunakuwa na wataalamu wa halmashauri husika kwa ajili ya ufafanuzi wa mambo ya kitaalamu.

Kwahiyo maamuzi yote yanafanyika kwa style hiyo kuanzia ngazi ya chini mpaka yanafika wilayani na huo ndio mfumo wa serikali ya mtaa unavyofanya kazi, tukitumia watu wengine ni kwa nia njema tu ili zoezi liweze kufanyika na mara nyingi kwa mjini huwa halina shida kwa kuwa watu wengi ni waelewa tofauti na maeneo ambayo yana tofauti kubwa ya kisiasa.
Bila kusahau hapa kuna mambo mengine yanahitaji maamuzi ya wananchi wote hivyo mara baada ya serikali ya mtaa / kijiji kukaa hurudisha feedback kwa wananchi kupitia mkutano mkuu wa wananchi wote wa eneo husika hufanya maamuzi. Kwa kuwa system haifanyi kazi kama inavyotakiwa na kwa kuwa mfumo huu umetumika tangu nchi ipo kwenye chama kimoja na watu wengi wa mjini ni watu wa kwenda kwenye mishemishe yao na mara nyingi kiongozi wa mtaa anafuatwa mpaka pale kunapokuwa na issue ya msingi kama uchaguzi au mambo haya ya NIDA na ndio maana kunakuwa na kuhalalisha hivi vitu.

Natambua kuwa nchi inaongozwa na siasa na kwa utaratibu huo juu ndio namna gani serikali inavyofanya kazi ili interest za wanasiasa ziweze kufikiwa kwa haki na utaratibu na hivyo ndio mfumo wa serikali unavyofanya kazi na ili uweze kuepuka conflict na uwe safe katika issue ambazo kama ununuzi wa mashamba na verification ya vitu mbalimbali kama kufungua akaunti na mambo mengine lazima upite kwa watu hawa mwenyekiti wa mtaa/mtandaji wa mtaa au mtendaji wa kata.

Kama bado unaamini wajumbe hawatambuliki, niambie kwa nini Serikali inawatumia kwenye mazoezi yao?
Kwa kumalizia katika swali lako ulilouliza hapo nilipo-bold), linapokuja issue ya kampeni flani ya masuala ya maendeleo au uhamasishaji huwa serikali inatumia au inawaomba viongozi wa siasa, dini, makundi maalumu ili zoezi hili lifanikiwe hivyo hata NIDA wametumia hao watu kama sehemu ya kujirizisha tu lakini mwisho wa siku barua ya mtendaji ndio reference muhimu ambayo ndio ina muhuri wa serikali. Kwa issue ya NIDA, hii ni issue SENSITIVE ya uraia na ndio maana inakwenda beyond baada ya kugundua kuna weakness chini kwa kuwa kiutaratibu unapohamia mtaa wowote au kijiji chochote lazima uandikishwe kwenye daftari la mtaa au kijiji lakini watu hawafanyi hivyo na wahusika wa ofisi pia, ili kujirizisha ndio maana katika issue zote za uraia huwa tunakwenda zaidi kuangalia mpaka vyeti vya ubatizo, vyeti vya shule ya msingi ili wakufahamu zaidi. Na NIDA kutumia mabalozi wa nyumba kumi ni approach mojawapo ya kujirizisha maana watanzania wengi huwa hawajulikani lakini si kwamba wanatambulika na serikali lakini mwisho wa siku barua wanaotumia ni ya mtendaji wa kata hawa wengine ni mashahidi tu mdau lakini pia kikubwa kinachotakiwa ni zile information unazojaza kwenye fomu ili waweze kuzifuatilia. Hao wanatumika kwa kampeni mbalimbali za uhamasishaji shughuli za maendeleo kama chanjo, sensa na hata hili la NIDA kama mashahidi.
Hili somo ni zuri sana kama utabahatika kufanya kazi katika ngazi za mijini na vijijini ndio utaona tunachokizungumza kwani kwa maeneo ya vijijini wana practice kile ambacho mwongozo wa serikali za mitaa unavyotaka na nina uhakika kabisa siku mkianza kazi vijijini mtatumia wenyeviti wa vitongoji na si mabalozi. Ila kwa debate hii iliyoletwa na ndugu yetu Tiba labda tungetoa mapendekezo kwamba kwa mjini kuna haja kutengeneza structure zingine ndogondogo za kusaidia serikali ya mtaa kwani watu ni wengi na inakuwa ngumu kwa mtendaji wa mtaa au mwenyekiti kutambua watu wake. Nina practical experience ya kile ninachozungumza pia hata mie katika mazoezi niliyoshiriki kuna mazingira tumewatumia hao watu kama sehemu ya kuhakikisha zoezi linafanikiwa. TUMESHAPIGA HIZI KAZI SEHEMU MBALIMBALI ZA NCHI INAPOFIKA DAR HUWA TUNAFANYA KAMA HIVYO LAKINI UKIENDA SEHEMU NYINGINE ISSUE ZINABADILIKA. HIVI VITU TUNAVYOZUNGUMZA VIPO DOCUMENTED SIO VYANGU MDAU HATA UKIULIZA OFISI YA HALMASHAURI UNAPATA.

Siku ukitaka kununua kaeneo au issue yoyote inayohitaji maeneo shamba, kiwanja umenunua fuata utaratibu niliokuambia ndugu yangu Las Mas Bobos hawa wengine watumie tu kama mashahidi kwa kuwa hata muhuri wa serikali hawana na endapo kutakuwa na tatizo kisheria utakuwa safe ila ukiwa na shughuli yoyote ya maendeleo ikiwemo kampeni ya chanjo, NIDA na mengine mengi isipokuwa mambo ya kuandikisha kupiga kura ni ruksa kuwatumia kwa kuwa ni wahamasishaji wazuri sana na wanasiasa wengi ni wahamsishaji wazuri na wanakubalika na mara nyingi ukiwatumia katika mazoezi mengi huwa yanafanikiwa.
Hata hiyo ya polisi ni kinyume wanavyofanya ila kwa kuwa balozi ni raia mwema kama mwingine na anaeenda kukamatwa anamfahamu si mbaya lakini kiutaratibu issue yoyote ya kiserikali lazima uripoti ofisi ya mtaa / kijiji pale unasema shida yako kwa kuwa mwenyekiti wa mtaa / kijiji ni MWENYEKITI WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA hivyo lazima ajue uwepo wako katika eneo lako, kama atakupa mtu akusindikize ni ruksa lakini kikubwa lazima apite ofisini kwani endapoi kutakuwa na shida katika kumkamata hapo ndio watajua.

HIZO CHANGAMOTO TULISHAPAMBANA NAZO SANA MWISHO WA SIKU TUKAJA KUELEWA MFUMO UNAVYOFANYA KAZI. SIKU AMBAYO UTAFANYA ISSUE AMBAYO INAHITAJI MAAMUZI HALALI YA SERIKALI SASA TUMIA WAJUMBE WAKO AU MABALOZI UONE KAMA HOJA ZAKO ZITAKUBALIWA.
NB
Kwa serikali kuu ipo hivi ila wao ni wasimamizi wakuu

Tunaanzia ngazi ya chini kabisa
-KATIBU TARAFA
-MKUU WA WILAYA
-MKUU WA MKOA
-MPAKA MAWAZIRI
 
Last edited by a moderator:
Mkuu usipende kukurupuka na theories zako na kusema huo ndio msimamo wa serikali. Mimi ni karani wa NIDA Wewe karani wa nida pamoja na bosi wako mkasome waraka wa katibu mkuu kiongozi - Paul Rupia wa 1.7.1992- juu ya kufutwa kwa mabalozi kiserikali.
 
Karani wa NIDA na bosi wako tafuteni waraka wa katibu mkuu kiongozi wa 1.7.1992 -wakati huo Paul Rupia- uliowafuta wajumbe wa nyumba 10 kama viongozi wa kiserikali.
 
Mkuu Jodoki Kalimilo si kwamba kumwita mjinga Tiba nilikosea au nitajisikia vibaya kurudia kufanya hivyo. Soma comments zake naamini utagundua anastahili kuitwa hivyo if you can read between the lines. Nakubaliana na mengi uliyoyasema na ni vile tu ka-button ka kugongea like hakapo lkn ulistahili moja.

Mfumo wa Jumbes na Liwalis tuliurithi kwa mkoloni na kama ulikuwa abolished basi naamini utekelezaji wake bado haujafanikiwa kwani mitaa mingi yenye ukereketwa wa kisiasa kuna mseto wa wajumbe wa vyama mbali mbali.

Nilichojaribu kumweleza mjuaji Tiba kufikia kumweleza mimi ni karani wa NIDA ni katika kupinga hoja yake kuwa wajumbe ni wa CCM. Mimi katika majukumu yangu sikufanya kazi na wajumbe wa CCM bali wa nyumba kumi. Na hata eneo ninaloishi mjumbe wetu wa nyumba kumi ni mwanachama wa CUF. Hapa kwetu siasa ilikataliwa na kisa cha kumchagua huyu ni hasira za wananchi kwa yule wa awali kwani alipeperusha bendera ya CCM nyumbani kwake na iliwakera watu wengi.

Kuhusu kutambulika kwao bado nitaendelea kusisitiza kuwa wanatambulika. Hata leo polisi akifika nyumbani kwako na search warrant basi kuepusha shari ya kisheria na kulaumiana baadae, huikabidhi kwa MJUMBE aisome ili zoezi la kusachi lifanyike akiwepo.

Kuhusu watendaji wa mitaa na kata, hawa si sehemu ya serikali ya mtaa. Afisa Mtendaji wa Mtaa na Afisa Mtendaji wa Kata ni waajiriwa wa Serikali Kuu kama wawakilishi wa Serikali Kuu katika Serikali ya Mtaa. Wanalipwa Mishahara na serikali kuu tofauti na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Wajumbe wao ambao hupata posho za halmashauri.

Jambo lililohitaji mjadala kwa Tiba ni uhalali wa kutozwa fedha kupata huduma kwa wajumbe lkn si nani amtambue kati ya mjumbe na vyeti. Hapa ndio paliponikera kwani alichokieleza kinaonesha hajui ni kwa nini serikali inafanya inavyofanya na bado hakuwa tayari kufikiri zaidi ya kujibu kifedhuli.

Hata sasa swali langu halikupata jibu toka kwake kwamba nikimpa cheti changu cha form four anaweza kuniambia ninaishi mtaa gani na aidha mimi ni raia wa Tanzania au lah?
 
Last edited by a moderator:
Karani wa NIDA na bosi wako tafuteni waraka wa katibu mkuu kiongozi wa 1.7.1992 -wakati huo Paul Rupia- uliowafuta wajumbe wa nyumba 10 kama viongozi wa kiserikali.

Kama unao uweke hapa mkuu tufaidi wote.

Yawezekana unadhani haya nimeyatunga mimi, lkn wewe jua tu kuwa ndio utaratibu uliopo na yule dada hakukosea. Hatupaswi kuwachallenge watekelezaji wa maagizo, tuzichallenge mamlaka zinazotoa maagizo hayo na hayo yafanyike kwa kuzingatia maudhui ya mamlaka katika kufanya hivyo.
 
Pia wewe Las mas kasome kesi ya madai na 127 ya 1993 alivyodaiwa balozi sh. 8000000 kwa kubughudhi mtu usiku kwa cheo cha balozi. waziri wa mambo ya ndani - mrema- alitaka kumlipia kutoka hazina lakini waziri wa sheria wa wakati huo- samwel sita akapinga, akasema alipe mwenyewe.
 
Mkuu Jodoki Kalimilo si kwamba kumwita mjinga Tiba nilikosea au nitajisikia vibaya kurudia kufanya hivyo. Soma comments zake naamini utagundua anastahili kuitwa hivyo if you can read between the lines. Nakubaliana na mengi uliyoyasema na ni vile tu ka-button ka kugongea like hakapo lkn ulistahili moja.

Mfumo wa Jumbes na Liwalis tuliurithi kwa mkoloni na kama ulikuwa abolished basi naamini utekelezaji wake bado haujafanikiwa kwani mitaa mingi yenye ukereketwa wa kisiasa kuna mseto wa wajumbe wa vyama mbali mbali.

Nilichojaribu kumweleza mjuaji Tiba kufikia kumweleza mimi ni karani wa NIDA ni katika kupinga hoja yake kuwa wajumbe ni wa CCM. Mimi katika majukumu yangu sikufanya kazi na wajumbe wa CCM bali wa nyumba kumi. Na hata eneo ninaloishi mjumbe wetu wa nyumba kumi ni mwanachama wa CUF. Hapa kwetu siasa ilikataliwa na kisa cha kumchagua huyu ni hasira za wananchi kwa yule wa awali kwani alipeperusha bendera ya CCM nyumbani kwake na iliwakera watu wengi.

Kuhusu kutambulika kwao bado nitaendelea kusisitiza kuwa wanatambulika. Hata leo polisi akifika nyumbani kwako na search warrant basi kuepusha shari ya kisheria na kulaumiana baadae, huikabidhi kwa MJUMBE aisome ili zoezi la kusachi lifanyike akiwepo.

Kuhusu watendaji wa mitaa na kata, hawa si sehemu ya serikali ya mtaa. Afisa Mtendaji wa Mtaa na Afisa Mtendaji wa Kata ni waajiriwa wa Serikali Kuu kama wawakilishi wa Serikali Kuu katika Serikali ya Mtaa. Wanalipwa Mishahara na serikali kuu tofauti na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Wajumbe wao ambao hupata posho za halmashauri.

Jambo lililohitaji mjadala kwa Tiba ni uhalali wa kutozwa fedha kupata huduma kwa wajumbe lkn si nani amtambue kati ya mjumbe na vyeti. Hapa ndio paliponikera kwani alichokieleza kinaonesha hajui ni kwa nini serikali inafanya inavyofanya na bado hakuwa tayari kufikiri zaidi ya kujibu kifedhuli.

Hata sasa swali langu halikupata jibu toka kwake kwamba nikimpa cheti changu cha form four anaweza kuniambia ninaishi mtaa gani na aidha mimi ni raia wa Tanzania au lah?

Hapo mdau Las Mas Bobos nimekuelewa nadhani nadhani tulitofautiana kidogo tu kwa baadhi ya sehemu, hao wajumbe unaowazungumzia wewe ni wajumbe ambao ukiwachukua wa mitaa yote ndio wanaunda serikali ya mtaa na huchaguliwa na wananchi hivyo kwa mantinki hiyo kutumika kama ni sehemu ya serikali ni sawa kwa kuwa wao kwa pamoja ndio sehemu ya hao wajumbe 25 wanaounda serikali katika ngazi ya mtaa japokuwa sina uhakika sana kama na mjini ni 25 au zaidi ila wanatakiwa wafanye kazi closely na hao wakuu wao wa mtaa ili kuweka sawa dhana ya serikali ya mitaa, mie nilichokuwa napiga kelele zaidi ni wale mabalozi wa nyumba kumi ambao wa CCM kwa muda mrefu wamekuwa wakitumika otherwise point zako ni nzuri mdau na wajumbe niliokuwa nafikiria ni wale wajumbe wa mashina wa chama.

Ila hapo kwenye watendaji wa mtaa na kata tena tunatofautiana labda tupeane muda tufuatilie ila mie navyojua ni serikali za mitaa kwa kizungu labda ina sound good yaani Local Government ambao ni waajiriwa wa halmashauri ya wilaya au manispaa. Hapo ndio maana tunasema ni serikali ya mitaa. Kwa kifupi Serikali ya mitaa (Local Government) inaanzia katika ngazi ya manispaa mfano kama upo Manispaa ya Kinondoni, Temeke au Ilala ukifika pale ofisini utakuta kuna Mkurugenzi wa manispaa ambae anafanya kazi kwa karibu na wakuu wa idara ambao ni jopo la wataalamu yaani Idara ya maendeleo ya jamii, Mipango, Ushirika, Ustawi wa jamii, Idara ya ujenzi, Mhhandisi wa maji n.k nadhani zipo kama idara 12 hivi alafu ukitoka hapo unashuka chini katika ngazi ya Kata hapa utamkuta Mtendaji wa Kata ambae anafanya kazi kwa karibu na wataalamu mbalimbali kulingana na uwezo wa serikali / halmashauri husika kuna sehemu zingine kuna wataalamu kama idara zilivyojuu hapo ambapo kama kuna issue zinatoka juu kwa Mkurugenzi kupitia kwa wataalamu wake wanashuka kwa Mtendaji wa Kata ambae ni link kati ya wataalamu na wananchi maana mwisho wa siku hawa wataalamu wakija chini watajichanganya na wananchi incase kama kuna nguvu ya wananchi inahitajika au kama wamekuja kwa ajili ya kutoa huduma flani. Anafanyaje kazi either atawaandikia watendaji wake wa mitaa kuwapa mwongozo na kama ni issue inahitaji maamuzi ataitisha mkutano wa kamati ya maendeleo ya kata na kuweka maazimio ya nini wafanye ili shughuli husika ifanyike kikamilifu.

Nadhani hapa fanya ka-research kadogo nadhani mnamaliziamalizia kazi na hao watendaji unaweza ukawauliza wao ni waajiriwa wa serikali kuu au manispaa, wakikuambia ni manispaa basi hao kwa maana nyingine ni waajiriwa wa serikali ya mitaa au kwa kizungu Local Government. Nikipata muda kesho nita-search information za ofisi ya waziri tawala za serikali za mitaa (PMO - RALG) kama kuna maelezo mazuri.

Nadhani hii mada nzuri tukiunganisha michango yetu na kutumia akili zetu za kuzaliwa kuna vitu tume-gain, hii ndio raha ya JF hivyo tuonane ukishafanya utafiti for conclusion.
 
We umeyataka mwenyw, bint kakuaambia mpka uwe n barua y baloz wa nyumba kumi, afu na we unaulza yup? Ina mana haumjui baloz wa nyumba 10. Umeyataka ayo
 
Nadhani procedures zinazotumiwa zinaboa lakini ni za muhimu. Hata mimi ckujua kama walipita mtaani kuandikisha. Nilienda na nakala ya vyeti vyote na nikaambiwa natakiwa barua ya mjumbe. Ilibidi niifuate hiyo barua ni nipange ratiba nyingine ya cku ya kwenda kujiandikisha (nimefanikiwa)
Bila kufuata taratibu za wajumbe wa nyumba kumi nadhani kufoji kutazidi.
Passport na cheti cha kuzaliwa sio reliable sana (ukifuatilia utaratibu wa kupata hivyo vitu utagundua kuwa mtu anaweza akafoji information na kuvipata)

Upuuzi tu,wajumbe wanataka TSZ 2000 swala la nyumba mtu anayokaa halina tija kwao,tuache kuunga mkono upuuzi usio na maana,kwani hizo ID zitaandikwa mtu nyumba anayokaa ? kama issue ni utambulisho hakuna sababu ya kuogopa upuuzi wa 'kufoji' mtu akija na utambulisho kama pasport na copy zake inatosha,nyumba anayokaa waitakia nini wakati tunatafuta national ID, kama ni muhimu kujua watu wanakaa nyumba gani na mjumbe wao wa CCM ni nani basi ingekuwa Id cum sensa.
Hakuna umuhimu wa barua wa wajumbe wa nyumba 10 labda kwa wale ambao hawana utambulisho rasmi wa uraia wao kama vile cheti cha kupigia kura NK.
 
Mkuu Jodoki Kalimilo si kwamba kumwita mjinga Tiba nilikosea au nitajisikia vibaya kurudia kufanya hivyo. Soma comments zake naamini utagundua anastahili kuitwa hivyo if you can read between the lines. Nakubaliana na mengi uliyoyasema na ni vile tu ka-button ka kugongea like hakapo lkn ulistahili moja.

Mfumo wa Jumbes na Liwalis tuliurithi kwa mkoloni na kama ulikuwa abolished basi naamini utekelezaji wake bado haujafanikiwa kwani mitaa mingi yenye ukereketwa wa kisiasa kuna mseto wa wajumbe wa vyama mbali mbali.

Nilichojaribu kumweleza mjuaji Tiba kufikia kumweleza mimi ni karani wa NIDA ni katika kupinga hoja yake kuwa wajumbe ni wa CCM. Mimi katika majukumu yangu sikufanya kazi na wajumbe wa CCM bali wa nyumba kumi. Na hata eneo ninaloishi mjumbe wetu wa nyumba kumi ni mwanachama wa CUF. Hapa kwetu siasa ilikataliwa na kisa cha kumchagua huyu ni hasira za wananchi kwa yule wa awali kwani alipeperusha bendera ya CCM nyumbani kwake na iliwakera watu wengi.

Kuhusu kutambulika kwao bado nitaendelea kusisitiza kuwa wanatambulika. Hata leo polisi akifika nyumbani kwako na search warrant basi kuepusha shari ya kisheria na kulaumiana baadae, huikabidhi kwa MJUMBE aisome ili zoezi la kusachi lifanyike akiwepo.

Kuhusu watendaji wa mitaa na kata, hawa si sehemu ya serikali ya mtaa. Afisa Mtendaji wa Mtaa na Afisa Mtendaji wa Kata ni waajiriwa wa Serikali Kuu kama wawakilishi wa Serikali Kuu katika Serikali ya Mtaa. Wanalipwa Mishahara na serikali kuu tofauti na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Wajumbe wao ambao hupata posho za halmashauri.

Jambo lililohitaji mjadala kwa Tiba ni uhalali wa kutozwa fedha kupata huduma kwa wajumbe lkn si nani amtambue kati ya mjumbe na vyeti. Hapa ndio paliponikera kwani alichokieleza kinaonesha hajui ni kwa nini serikali inafanya inavyofanya na bado hakuwa tayari kufikiri zaidi ya kujibu kifedhuli.

Hata sasa swali langu halikupata jibu toka kwake kwamba nikimpa cheti changu cha form four anaweza kuniambia ninaishi mtaa gani na aidha mimi ni raia wa Tanzania au lah?

ungeonyesha upeo mzuri wa uelewa ungetumia sheria inayowatambua wajumbe wa nyumba kumi kama viongozi wa kiserikali badala ya kutumia matukio ooh Polisi huwatumia kuwaonyesha search warrant OOh wanatumiwa hivi na vile,wajumbe wa nyumba kumi kutumika kunitambulisha kwenye zoezi la kupata ID ni upuuzi labda kama NIDA mmekuja kugawa unga wa njano kwa wenye njaa then ni muhimu kutambulishwa na mjumbe ili isije kuwa mnatoa msaada kwa kaya isiyostahili,issue ni national Id kwa watz na wakazi wa tz then swala la nyumba ninayoishi linakujaje wakati kesho hata leo baada ya kujiandikisha mtu anaweza kuhama ?
 
Kuuliza siyo ujinga.Naomba kujulishwa:
1.Zoezi ni la vitambulisho vya taifa kufuatana na Mkuu Las Bobos hapo juu alivyosema ni kwa watu wote waishio Tanzania na siyo raia peke yake.Ina maana hata wageni watapewa hivyo vitambulisho? Kama jibu ni ndio, ikiwa mgeni amekuja kwa muda mfupi - miezi au miaka/mwaka, inaleta maana kwa serikali kuingia gharama hii? Kwani hakuna utaratibu mwingine wa kuwatambua wageni? Na je, kutakua na zoezi lingine tena la utambulisho wa uraia? Nchi nyingine wana vitambulisho mbalimbali kama Green Card, Social Security ID etc. ili kuweza kuwajua watu na kuwafanya wawajibike kwa mambo mbalimbali.Je hili zoezi la NIDA linaweza kulinganishwa na upatikanaji wa kitambulisho gani? Je hicho kitambulisho kitatofautiana vipi na kile cha mpiga kura? Kwa maneno mengine, isingekuwa cost effective ku upgrade ama kile kitambulisho cha mpiga kura au drivers licence?

2. Mchangiaji mmoja ( Kiranga kama sikosei) kazungumzia vema kuhusu ukosefu wa anuani za makazi na kuwa watu wengi wanatumia P.O.Box etc. Pia hata mitaa ni kama haipo maeneo mengi.Sasa huu utambulisho wa makazi unawezekana au utafanikisha nini ikiwa, watu wengi wanaishi nyumb/vyumba vya kupanga na huhamahama, au hata mitaa haijulikani. Kuna kipengere kinamtaka mtu asema anaishi nyumba namba ngapi na mtaa upi.Huyu mtu akihama baada ya hili zoezi, ndio ina maana taarifa zake za ukazi zitabaki bado sahihi?

Nina maswali mengi sana baada ya kushiriki kwenye hili zoezi ila nitayaleta baadae.

Pia ninataka kusema kuwa kwangu binafsi sijaona tatizo la zoezi zima hata kutolewa sh. 2000/= sikutolewa, wala kusumbuliwa na waandikishaji.Badala yake nimepata experience nzuri tu ya kusaidiwa zaidi ya kusumbuliwa. Waandikishaji wasichana kwa wavulana walikuwa na moyo wa kuelekeza na hata kusaidia nje ya njia zao.Walijitolea hata kunipelekea fomu zangu wa hao wajumbe/mabalozi bila malipo yoyote baada ya kubaini napata shida ya kuwajua.( NB hawa wajumbe kwa kweli ni ishu siyo kila mtu anawajua! Tusilazimishe kuwa wanajulikana kama sehemu ya decentralisation ya local government).
 
Upuuzi tu,wajumbe wanataka TSZ 2000 swala la nyumba mtu anayokaa halina tija kwao,tuache kuunga mkono upuuzi usio na maana,kwani hizo ID zitaandikwa mtu nyumba anayokaa ? kama issue ni utambulisho hakuna sababu ya kuogopa upuuzi wa 'kufoji' mtu akija na utambulisho kama pasport na copy zake inatosha,nyumba anayokaa waitakia nini wakati tunatafuta national ID, kama ni muhimu kujua watu wanakaa nyumba gani na mjumbe wao wa CCM ni nani basi ingekuwa Id cum sensa.
Hakuna umuhimu wa barua wa wajumbe wa nyumba 10 labda kwa wale ambao hawana utambulisho rasmi wa uraia wao kama vile cheti cha kupigia kura NK.

Issue haikuwa barua. Kama ulibahatika kuandika jina lako wakati wanapita na wajumbe basi haina haja ya barua. Ila kama haukuandikwa inabidi mjumbe wako athibitishe. Simle logic.
Usiwe na mentality ya kukosoa kila kitu kinachofanywa, usifikiri wapinzani wakiingia watabadilisha kila kitu kinachokukera hapa Tanzania. U will be dissappointed my friend.
NB: Siungi mkono ujinga unafanywa na walio madarakani, najaribu kuwa rational tu. Msije mkaanza siasa hapa!
 
Serikali za mitaa zina anza na mjumbe wa nyumba kumi then mtendaji wa mtaa au kijiji.Tuwaheshimu bila kuali itikadi zao kisiasa kwani hata sisi twa weza kuwa na ushabiki katika sera furani, lakini tusiwe wanyonge wanapotaka kutunyonga.
 
Kuuliza siyo ujinga.Naomba kujulishwa:
1.Zoezi ni la vitambulisho vya taifa kufuatana na Mkuu Las Bobos hapo juu alivyosema ni kwa watu wote waishio Tanzania na siyo raia peke yake.Ina maana hata wageni watapewa hivyo vitambulisho? Kama jibu ni ndio, ikiwa mgeni amekuja kwa muda mfupi - miezi au miaka/mwaka, inaleta maana kwa serikali kuingia gharama hii? Kwani hakuna utaratibu mwingine wa kuwatambua wageni? Na je, kutakua na zoezi lingine tena la utambulisho wa uraia? Nchi nyingine wana vitambulisho mbalimbali kama Green Card, Social Security ID etc. ili kuweza kuwajua watu na kuwafanya wawajibike kwa mambo mbalimbali.Je hili zoezi la NIDA linaweza kulinganishwa na upatikanaji wa kitambulisho gani? Je hicho kitambulisho kitatofautiana vipi na kile cha mpiga kura? Kwa maneno mengine, isingekuwa cost effective ku upgrade ama kile kitambulisho cha mpiga kura au drivers licence?

2. Mchangiaji mmoja ( Kiranga kama sikosei) kazungumzia vema kuhusu ukosefu wa anuani za makazi na kuwa watu wengi wanatumia P.O.Box etc. Pia hata mitaa ni kama haipo maeneo mengi.Sasa huu utambulisho wa makazi unawezekana au utafanikisha nini ikiwa, watu wengi wanaishi nyumb/vyumba vya kupanga na huhamahama, au hata mitaa haijulikani. Kuna kipengere kinamtaka mtu asema anaishi nyumba namba ngapi na mtaa upi.Huyu mtu akihama baada ya hili zoezi, ndio ina maana taarifa zake za ukazi zitabaki bado sahihi?

Nina maswali mengi sana baada ya kushiriki kwenye hili zoezi ila nitayaleta baadae.

Pia ninataka kusema kuwa kwangu binafsi sijaona tatizo la zoezi zima hata kutolewa sh. 2000/= sikutolewa, wala kusumbuliwa na waandikishaji.Badala yake nimepata experience nzuri tu ya kusaidiwa zaidi ya kusumbuliwa. Waandikishaji wasichana kwa wavulana walikuwa na moyo wa kuelekeza na hata kusaidia nje ya njia zao.Walijitolea hata kunipelekea fomu zangu wa hao wajumbe/mabalozi bila malipo yoyote baada ya kubaini napata shida ya kuwajua.( NB hawa wajumbe kwa kweli ni ishu siyo kila mtu anawajua! Tusilazimishe kuwa wanajulikana kama sehemu ya decentralisation ya local government).

Mkuu sante kwa mchango wako. Hizi ndizo issues ambazo tunapashwa kupata majibu kwani eneo ninaloishi wakati wa kuandikishwa should not be an issue. Sijui NIDA wamejipanga vipi, lakini ingekuwa vizuri sana kama vitambulisho vya uraia vingeunganishwa na driving licence, TIN number na vyeti vya kupiga kura. TRA walifanikiwa kuunganisha TIN number na driving licence nafikiri hata NIDA can do the same. Hongera kwamba ulipata usaidizi wakutosha wakati wa kujiandikisha.

Tiba
 
ungeonyesha upeo mzuri wa uelewa ungetumia sheria inayowatambua wajumbe wa nyumba kumi kama viongozi wa kiserikali badala ya kutumia matukio ooh Polisi huwatumia kuwaonyesha search warrant OOh wanatumiwa hivi na vile,wajumbe wa nyumba kumi kutumika kunitambulisha kwenye zoezi la kupata ID ni upuuzi labda kama NIDA mmekuja kugawa unga wa njano kwa wenye njaa then ni muhimu kutambulishwa na mjumbe ili isije kuwa mnatoa msaada kwa kaya isiyostahili,issue ni national Id kwa watz na wakazi wa tz then swala la nyumba ninayoishi linakujaje wakati kesho hata leo baada ya kujiandikisha mtu anaweza kuhama ?

Huyu jamaa nayejiita Las Mas Bobos (Karani wa NIDA) kwa maelezo yake mwenyewe anajaribu kutumia nguvu nyingi, matusi na kejeli kutetea kasoro za NIDA kuwahusisha mabalozi kwenye hili zoezi. Mtu ambaye alijaribu kutetea kwamba barua ya balozi ina nguvu zaidi ya passport. Sijui kama anajua passport uwa inapatikana vipi? Eti passport inamtambulisha Mtanzania nje ya nchi tu. Kwa hiyo nikiwa na passport ya Tanzania ninaweza kuitumia nje lakini ndani ya nchi hapana? Nadhani hata nikienda leo kufungua account bank, wanaheshimu sana passport, lakini kwa NIDA passport is nothing (sijui/sina uhakika kama huu ni msimamo wa NIDA au wa huyu karani).

We still have a long way to go na bottom line ni kwamba, sikuandikishwa anyway!!!

Tiba
 
Serikali za mitaa zina anza na mjumbe wa nyumba kumi then mtendaji wa mtaa au kijiji.Tuwaheshimu bila kuali itikadi zao kisiasa kwani hata sisi twa weza kuwa na ushabiki katika sera furani, lakini tusiwe wanyonge wanapotaka kutunyonga.

Mkuu wewe haya umeyapata wapi?

Tiba
 
Huyu Ndimbo ni mto2 wa Mnyoto Ndimbo, nilipiga naye school Hanga seminary, naona amepotoka nitamshauri arudi kundini
 
Back
Top Bottom