Rais Mwinyi awakabidhi vyeti vya uraia wa Tanzania wahamiaji wasiohamishika 3,319

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema nchi imeandika historia mpya kwa kuwakabidhi vyeti vya uraia wa Tanzania wahamiaji wasiohamishika 3,319 ambao wameishi nchini kwa zaidi ya miaka 50 wakiwa na asili ya mataifa jirani ya Burundi, Comoro, Msumbiji na Rwanda.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo leo tarehe 05 Septemba 2023 katika hafla ya kukabidhi vyeti vya uraia wa Tanzania kundi la Wahamiaji wasiohamishika Ikulu, Zanzibar.

Aidha, Rais Dk.Mwinyi amefurahishwa kutekelezwa ahadi yake aliyoitoa baada ya kuingia madarakani mwaka 2020 kwa kumalizika zoezi hilo na kuwafanya watambulike kuwa Raia wa Tanzania badala ya Wahamiaji wasiohamishika.

Vilevile, Rais Dk.Mwinyi ametoa wito kwa Idara ya Uhamiaji nchini kuziimarisha sheria zilizopo hususani sheria ya uraia wa Tanzania kwa kuwa sheria hii haijafanyiwa mapitio kwa kipindi kirefu kwa madhumuni ya kuiwezesha kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowahusu wananchi na wageni wanaofika nchini.

Mwinyi.png
 
uzanzibari au uraia wa Tanzania, kwanini asiwe Samia ndio wa kutoa vyeti hivyo? yeye ana mamlaka gani kwa Tanzania?
Kwa Tanzania yeye ni makamu wa kwanza wa Rais, yuko juu ya makamu wa Rais kiitifaki. Pia ni miongoni mwa wajumbe wa baraza la mawaziri, na anafanya kazi yoyote alivyoagizwa na Rais wa Tanzania nzima.
Kimamlaka anaanza Rais, anakuja Rais wa Znz halafu ndio makamu wa Rais
 
Back
Top Bottom