Vyama vya upinzani bila TV, redio zenu au media zenye kuugemea upande wenu hamtoboi

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,641
46,298
Jambo mojawapo kubwa na la muhimu katika siasa za kushika dola ni kuweza kuwasiliana na kufikisha ujumbe wako kwa kwa wakati kwa wananchi walio wengi. Hiyo ni bila kujali ujumbe wako ni sahihi au sio sahihi.

Tatizo mojawapo kubwa la upinzani Tanzania ni kukosa vyombo vya habari vya kuusapoti na kusema mambo yake kwa nguvu.Hili ni jambo ambalo lina uweka upinzani kwenye nafasi mbaya "disadvantageous" kuwafikia wananchi.

Ukiangalia vyombo karibia vyote vya habari nchi hii 99% vimeegemea upande wa chama tawala cha CCM .Pia juu ya ziada ya hilo chama tawala kina TV na redio zake na gazeti lake. Pia kinatumia faida ya kuwa katika dola kutumia shirika la utangazaji la umma TBC.Kuna wakati upinzani ulikuwa na mahezeti yake yakapotezwa, ITV ilikuwa inajaribu kuwapa nafasi kubwa nayo ikawekwa kwapani ikatulia tuli.

Tanzania ya watu milion 60 ni vigumu sana kufikiwa kwa Twitter, Instagram au Facebook. Hilo ni kwa kuzingatia pia kwamba raia wengi wa vijijini hawajawahi kusikia hata baadhi ya hii mitandao ya kijamii. Wachache wenye Smartphone wanaishia WhatsApp.

Pia ni vigumu kufanya mikutano ya hadhara kuwafikia watu wote kwa sababu ya ukubwa wa eneo la nchi na gharama. Redio, TV, magazeti(kama enzi za Tanzania Daima, Mwanahalisi na Mawio) bado zinabaki njia kuu za kuufikia umma mkubwa na kupenyeza agenda za kisiasa za kudumu na zinazoibuka kila siku.

Upinzani ufanye mpango wa kuwa na media zao na pia wafanye mikakati ya kuonekana zaidi katika vituo binafsi vya sasa japo hili ni jambo gumu kwa sababu wamiliki wengi wa vyombo hivi wasingetaka kusuguana mabega na serikali ya chama tawala ili waendelee kulamba asali. Upinzania una kazi kubwa ya kufanya kuwa katika media kubwa.
 
Wanao regulate ni hao hao CCM, utatokea wapi ndugu? milango imefungwa kila mahali na ndiyo maana watu wanajikita kwenye Katiba mpya, hao si wajinga.

Anayeruhusu broadcasting yupo chini ya mamlaka ya CCM, kumbuka jambo hili...nyundo ya TCRA

Mfano mdogo tu hivi kwa nini hii Join the Chain ya CDM hawajaipekekwa kwenye TV iwe live Tanzania nzima tena kwa wakati mfupi badala ya kutembea mitaani mguu kwa mguu ? wanapenda kutembea mitaani siyo kwa tafasiri nyepesi.
 
Hata kufikisha ujumbe wa Katiba mpya kwa wananchi wengi hasa wa vijijini ili kuamsha ari unahitaji TV, redio na magazeti.
Wanao regulate ni hao hao CCM, utatokea wapi ndugu? milango imefungwa kila mahali na ndiyo maana watu wanajikita kwenye Katiba mpya, hao si wajinga.

Anayeruhusu broadcasting yupo chini ya mamlaka ya CCM, kumbuka jambo hili...nyundo ya TCRA

Mfano mdogo tu hivi kwa nini hii Join the Chain ya CDM hawajaipekekwa kwenye TV iwe live Tanzania nzima tena kwa wakati mfupi badala ya kutembea mitaani mguu kwa mguu ? wanapenda kutembea mitaani siyo kwa tafasiri nyepesi.
 
Kama wananchi wamewakataa hata wafanye hivyo vyote havitawasaidia

Wananchi gani hao? Kama wanachi wamewakataa unapataje Kura asilimia 57%tena za wizi? Tuache uongo, Bila kuharibu uchaguzi wa 2020 leo tungekuwa tunaongea mengine.
 
Back
Top Bottom