Vyama vya Siasa na Matawi ya Ughaibuni

Hivi Balozi wetu mpya kule Malaysia Balozi Cisco Mtiro anapeleka siasa za TMK Malaysia!
 
hivi hii ccm ina pesa za halali kiasi gani?
kama malaysia mkutano utafanyika petronas towers, na kutakuwa na drinks and all that. hizi pesa za kutumia kufungua matawi nje ya nchi zinatoka wapi?

tungependa wananachi kuahamishwa chama cha ccm kinajiendesha kwa pesa zipi?

wawe wawazi kwenye hili kwanza ndipo tutakapojua kuwa nia ya kuondoa ufisadi ipo......vinginevyo itakuwa ni kutubabaisha tu
 
Ukiona watu walio na uwezo mdogo wa kufikiri basi ni hawa wanaofungua matawi ya vyama nje ya nchi. Inaonekana kuwa hata hawajui kilichowapeleka huko.

Sidhani kama kazi ya balozi ni kwenda nchi za nje kutangaza chama chake. kama kazi ndizo hizi basi hatuna budi kuomba serikali ifute balozi hizi.
 
Hivi vyama vya upinzani vinakatazwa kufungau matawi nje ya nchi?Mbona wapo washabiki wengi CHADEMA huko USA akina mwanakijiji,mwafrika wa kike nk nao wao wanaweza fungua tawi lao huko USA!!

fail-1.gif
 
UK TUMEZOEA KUONA MUME WA BALOZI MWANAIDI MJAAR AKIFUNGUA MATAWI KILA KONA...SASA SIJUI HUYU JAMAA HANA KAZI AU VIPI MAANA MWANZO TULIAMBIWA NI MFANYA BIASHARA LAKINI LOOKS LIKE KUFUNGUA MATAWI YA CCM NDIO BIASHARA YAKE SAA ZINGINE NAMUONEA HURUMA HUYU MAMA KUACHA HIGH FLYING LAW CAREER NA KUKUBALI NAFASI HII MAANA SIE WENGINE HATUMPUZISHI KWANI NDIO KESHAKUWA KWENYE SIASA ...

lakini huko Malaysia hali ni tofauti....

Baada ya IPTL ambayo ina mizizi Malaysia sasa ni CCM tawi .Ndiyo maana nikahoji uhalali wa makada wa Chama kuwa mabalozi.Kama Ubalozini kutakuwa na tawi la CCM najiuliza huduma kwa Watanzanai wasio na vyama na wale wa upinzani inakuwaje ? Kujua yanayo tokea kwenye matawi ya CCM you need not anything mbadala .Walio viongozi wa CCM si wote kwamba ni watiifu ila wanafuata maslahi na baadaye tutajua kila jambo . Jiulize kwa nini London wamekwama na kila leo tunaona habari zao hapa JF ? Waacheni wafungue na msiwafuatishe .Ila watu wa akili fupi ughaibini ndiyo wana hangaika na CCM watu real watakata issue na kujipanfa kwa njia zingine .Wapinzani kuweni na njia nyingine za ku identify watu wenu na acheniu kufuata mambo ya Ki CCM.
 
mie nina hasira na huyu balozi wa Tanzania pale Uk sijaona kazi anayofanya zaidi ya kuhudhulia vijisherehe vinavyoandaliwa na vijana wa kitanzania wanao beba mabox na kusafisha vyoo.... hivi sisi wengine kina TLP tukimuomba awe mgeni rasmi ktk ufunguzi wa matawi yetu atakubali????

Nadhani na mme wake sasa anajikomba ili wakuu wamuone labda anaweza akala shavu...
""Huu ni wakati wa mapambano kati yetu na nyie madalali (mabalozi) mnaotafuta wateja wa kuwauzia rasilimali zetu""
Mama Maajar ndugu yako LOWASA tumeshamwangusha so kaa ukijua siku zako zinahesabika..
 
Ujumbe huu naona ni mzito .Maswali ya msingi kabisa yameulizwa.Je akiitwa na TLP aende kufungua ofisi zao ataenda huyu Balozo Majaliwa ?
 
Mimi Niko Malaysia Sheria Za Huku Haziruhusu Mwanafunzi Kujihusisha Na Mambo Yeyote Ya Siasa Hata Kufanya Kazi!! Asilimia Kubwa Ya Watanzania Huku Ni Wanafunzi Watu Wazima Au Wafanyabiashara Ni Wachache Sana, 85% Ni Below 23 Years Old. So Kimsingi Hilo Tawi Sana Sana Litakuwa Na Wanachama Wachache Sana.

Pili Balozi Wetu Wala Hajishughulishi Na Hao Watu Kwanza Sie Ndio Kwanza Tumesoma Kwenye Blog Ya Haki Ngowi Vinginevyo Hata Hatuwajui Hao Wanaojiita Wana Ccm.
 
Kweli mfa maji haishi kutapatapa. Hivi mbona mi sijawahi kusikia Democratic au Republican wanafungua tawi London au Hongkong?.
 
mie nina hasira na huyu balozi wa Tanzania pale Uk sijaona kazi anayofanya zaidi ya kuhudhulia vijisherehe vinavyoandaliwa na vijana wa kitanzania wanao beba mabox na kusafisha vyoo.... hivi sisi wengine kina TLP tukimuomba awe mgeni rasmi ktk ufunguzi wa matawi yetu atakubali????

Nadhani na mme wake sasa anajikomba ili wakuu wamuone labda anaweza akala shavu...
""Huu ni wakati wa mapambano kati yetu na nyie madalali (mabalozi) mnaotafuta wateja wa kuwauzia rasilimali zetu""
Mama Maajar ndugu yako LOWASA tumeshamwangusha so kaa ukijua siku zako zinahesabika..

thats premature, kumbe hata kumuomba hujamuomba then unasema what you think might not turn out to be, ! subiri nikwambie hii ni simple. Andika barua wewe mwenyewe, iweke muhuri wewe mwenyewe then mtumie barua huyo balozi then utuambie atasemaje ! Akikataa binafsi nitamuona HAFAI !
 
Kweli mfa maji haishi kutapatapa. Hivi mbona mi sijawahi kusikia Democratic au Republican wanafungua tawi London au Hongkong?.

what happens in ccm, might not happen to dems or reps !! And i think people/political parties make decisions as events/situations unfold and not because they want to ! Je situations gani hizo ? i simply dont know.

Lakini still reps. au dems. kufungua tawi sehemu hizo wanaweza pale watakapoamua !
 
Sijui kuwa mada hii tayari imeshawekwa hapa au la. Kama ishawekwa mnisamehe.

Napenda kuuliza kuwa, hivi maana ya kuwa na matawi ya vyama vya siasa ughaibuni ni nini? Ni harakati gani za kisiasa zinazoendelea katika nchi za watu ambazo zinahitaji kuwa na chama cha siasa humo? Wakati ule wakati nchi nyingi zilikuwa bado zinagombea uhuru, tulishuhudia kuwepo kwa vyama vya siasa nchini mwetu. Vyama hivyo vilikuwa, kwa mfano, FRELIMO, ANC, MPLA, ZANU,ZAPU, SWAPO, PAC, PLO na kadhalika. Vyama hivyo vilikuwepo Tanzania kwa sababu haikuwezekana kuwa na harakati za kisiasa nchini mwao. Walipewa kibali na serikali ya Tanzania kuwepo kwa vyama humo nchini.

Je haya matawi yanayofunguliwa ughaibuni yana malengo gani? Ni jinsi gani wanachama wake wanaweza kushiriki katika siasa nyumbani? Watanzania tuishio ughaibuni kwa kiasi kikubwa hatuwezi kushiriki katika mambo ya kisiasa yanayoendelea nyumbani, hii ni pamoja na kupiga kura. Hivyo binafsi, sioni maana ya kuwa na matawi haya. Kama kungekuwa na uwezekano wa waishio ughaibuni kupiga kura, maana ya matawi anagalau ingekuwepo.

Watanzania wengi, tukiwa nje ya mipaka yetu, kitu kinachotujumuisha wote ni Utanzania wetu. Kitendo hiki cha umoja na undugu wa Watanzania unawashangaza wengi, hasa Waafrika wa nchi zingine ambao hawana umoja kama sisi. Mara nyingi tunaulizwa, 'je yule ni ndugu yako, mlikuwa mnafahamiana zamani'? Wakijua ndio kwanza mmekutana huwa wanashangaa, na jibu wanalopata ni, 'Sisi ni Watanzania.' Hapo ndipo wakati ambapo najivunia kuwa Mtanzania.

Kwa maoni yangu naona kwamba kuanza kuwepo kwa matawi ya vyama vya kisiasa ughaibuni kutaanza kuleta mgawanyiko kwa Watanzania waishio huku. Hata siku moja sijawahi kusikia au kuona kama kuna matawi ya Republicams, Democrats, Labour, Conservatives, CDU au Forza Italia katika nchi zingine! Au huu ni mtindo mpya wa siasa za kimataifa ambao unahamishia siasa za ndani ya nchi, kwenda nchi zingine? Ikumbukwe kuwa, nauliza tu.
 
na kikwete nasikia yupo india labda ndo channel ya kum meet asiwasahau..viongozi kila siku kutibiwa india au wapo uk kusign mikataba mibovu na kujikimbilizia mali...in my view this is a scam kujipendekeza kwa serikali ya mafisadi...OPEN TO DEBATE!!
 
Kitia
Manufaa ya matawi kwa sasa si faida kwa Nchi bali wajanja kutumia nafasi kujitangaza na biashara zao na kupata tender na si zaidi ya hapo .Wanajua ukitaka kula na CCM beba bendera lao muda wowote na popote then utawasikia wanavyo kupa sifa na kula pesa .Ukweli upo wazi kwa baadhi ya Nchi sasa wadau wa CCM wanapate tender nono na ndiyo njia pekee CCM wanadhani chama chao kina nguvu .
 
Hawa watu wa UK na Asia wanaofungua haya mashina ya CCM wanaboa kweli. I'll put em on blast this coming sunday. I just can't stand them grrrrrrrrrr.
 
mijitu mingine bwana kwa kujipendekeza.........kweli inaudhi/inaboa sana
 
In principle hakuna ubaya kwa watu kushiriki katika mchakato wa siasa wa nyumbani kutoka ughaibuni, ningependa kuona hata kura tunaenda kupiga ubalozini na kwenye consulate zetu mbali mbali.

Lakini kinachoendelea sasa hivi ni kama members walivyosema hapo juu.Matawi haya yanaonekana kuwa ni "dili la ulaji" tu. Ukifuatilia kinachoendelea jumuiya ya CCM London sasa hivi ni aibu tupu.

As stated, I am not entirely against the idea of having these branches, but I would like to see them run in a more politically savvy way and taking a bigger socio-economic role.I frankly see a bigger role to be played by non-partisan Tanzania development associations zitakazosaidia kutuma hela nyumbani, kufanya biashara na nyumbani, kusaidia wakati wa misiba na sherehe nk kuliko haya mambo ya kushabikia vyama, hususan kwa chama kilichokuwa established kama CCM.

The way things are going now mimi naona wana promote idling, embezzlement na division tu.
 
Sijui kuwa mada hii tayari imeshawekwa hapa au la. Kama ishawekwa mnisamehe.

Napenda kuuliza kuwa, hivi maana ya kuwa na matawi ya vyama vya siasa ughaibuni ni nini? Ni harakati gani za kisiasa zinazoendelea katika nchi za watu ambazo zinahitaji kuwa na chama cha siasa humo? Wakati ule wakati nchi nyingi zilikuwa bado zinagombea uhuru, tulishuhudia kuwepo kwa vyama vya siasa nchini mwetu. Vyama hivyo vilikuwa, kwa mfano, FRELIMO, ANC, MPLA, ZANU,ZAPU, SWAPO, PAC, PLO na kadhalika. Vyama hivyo vilikuwepo Tanzania kwa sababu haikuwezekana kuwa na harakati za kisiasa nchini mwao. Walipewa kibali na serikali ya Tanzania kuwepo kwa vyama humo nchini.

..ni ujinga na na uroho wa madaraka ndio unaofanya watu kujipendekeza na kuanzisha vyama ughaibuni,kwa kifupi ni kama vile watu huwa wana-regret kuishi ughaibuni na at the same time wanataka kuvuna nyumbani, so kwa kujigawa ndo idea ya kuanzisha tawi nje ya nchi linapokuja ili ata later mtu atakapokuja kuomba dhamana ya wananchi(ubunge!!) aseme eti alikuwa mwanachama wa chama fulani tokea nje ya nchi kwa miaka kadhaa!! ni ulafi mtupu!! Lets not get fooled na hii scam!!This government led by J.Kikwete ni corrupt and ignorant government, inabidi ipingwe kama inavyopingwa China ktk olympics over Tibet!! Yes we can, tuanze vijijini! huko ndipo kwenye mizizi achilia mbali matawi!!...lets make a move!!
 
Back
Top Bottom