Vyama vya Siasa na Matawi ya Ughaibuni

Je nitafute wakili sasa aweze kuweka pamoja karatasi hizi na kuangalia uhalali na nianze kwa kuulalamikia Ubalozi na Majaliwa Sharif ?Maana bila ya hivyo hawa hawatajifunza na Ubalozi hautakuwa unawatendea wasio wana CCM haki maana mume wa balozi ni CCM na Balozi ni Ubalozi wa Nchi chini ya CCM. Watanzania wengine tutahudumiwa wapi ?
 
Lunyungu mimi nadhani ungeendelea na uchunguzi wako the best way you see fit . Tafadhali keep us posted au kama utahitaji msaada then tushirikishe hapa bodini. Kuna dalili za kujifunza mambo mawili au matatu katika uchunguzi huu.

Kila la kheri.
 
Well I know little on CCM or opposition Politics but I guess hizi ni deal za maopportunist wanaotaka serikali itake note their presence and participation katika shughuli za kichama. Zaidi ya hapo sioni kwa nini chama kinachoshinda kwa 80% kitafute wanachama wengine nje ya nchi. This is just opportunistic move by some "smart fellaz". Ni opportunist kwa sababu wangekuwa na nia njema wangeanzisha foundation ya kuspearhead maendeleo ya nchi katika nyanja mbali mbali nyumbani. In anyway I wish them luck in this!


Nakubaliana na wewe kwa 100% ukizingatia kipindi kile walipata nafasi na walionana na JK na hvi karibuni Malecela. Wasiwasi wangu ni kama huo wa Lunyungu kwamba ofisi ya balozi isije kujikuta inatumbukia kwenye dimbwi na kuwa ofisi ya ccm. Hata wafadhili wataopatikana kufadhili chama either hapa au Tanzania contacts zao zitatoka pale pale ubalozini au kwenye kile kitengo cha uwekezaji pale London. Hivyo either direct au indirect ofisi ya balozi itatumika...and that is not good news.
 
Hao wasri lanka~Tamil Tiger~ndio wanakusanya michango mingi katika nchi mbali mbali za nje ili kwenda "kuikomboa" nchi yao. Wanatumia hata vitisho kwa wenzao ili wachange michango hiyo.

Sasa hivi baadhi ya wasrilanka wamewatolea nje na kwenda kuwashtaki katika serikali mbali mbali za magharibi. Hii imesababisha Tamil Tiger kuwekwa kundi la majasusi na hivyo kupigwa marufuku katika baadhi ya nchi. Naamini si muda mrefu watapigwa marufuku nchi zote za ulaya magharibi na North America.

Hawa Tamil Tiger naona walichangisha mpaka wameweza kununua ndege za kivita wanalisumbua jeshi la serikali kila siku.
 
Mikuki, I have a feel its a sense of insecurity and paranoia on the part of CCM. I think they just wanna find a way to keep tabs on...........

A confident party, that has all the resources in the country, has no need to branch out of the country. Surely, they dont need funds? I mean, misaada yote inakuja kwa jina la nchi, na anayeongoza ni CCM.

I would like to give a frank opinion on the members joining, but I will leave that as it is. But, surely the people who will join will be the ones who are already affiliated with CCM, or interest in god knows what. For someone to suddenly show interest in CCM (abroad), I have to question, what interests do they have for Tanzania? I mean, there are so many things that are not right in Tanzania, and the ruling party has been CCM. So if for all these years since independence, you can see that things aint right....why (as Mikuki says)......wangekuwa na nia njema wangeanzisha foundation ya kuspearhead maendeleo ya nchi katika nyanja mbali mbali nyumbani.

For that reason and many others, thats why I say, the opposition can win this game EASY!!! At the end of the day, they will divide people who care about Tanzania.
 
Mambo yameiva wandugu .Picha nimesha zipata za shughuli ila naomba mnipe anuani za ofisi za CCM LOndon tafadhali . Maana zinatakiwa ili watu waka visit wajionee . Tafadhali ofisi za London na Readig naombeni anuani zao .
 
Sheria za UK

It is often said that Britain has an unwritten Constitution. This is not quite true. Some of the British Constitution is written and some isn't. What is meant by 'unwritten' is that it is not written down in one volume as 'The British Constitution'. You could not go into a bookshop and order a copy of our Constitution in paperback!

Our Constitution is made up of four main parts called statute law, common law, conventions and works of authority. Of these, statute law is the most important and takes precedence over the others if there is a clash. Statute laws are the laws that have actually been passed by Parliament. The British Constitution can be considered to be 'living' as it is still developing.

Well good idea but what are the achivements expected: You will make all illegal people vanish from associating themselves with this Embassy and the Jumuiya ya WTZ, secondly you will put scrutiny on all Tanzanians in the UK. Kwa hiyo wale wenye vibali feki sasa wakae mkao wa kulialia maana hawa jamaa ni wachunguzi kweli kweli na ndio mwisho wa matapeli tapeli wasio na mbele wala nyuma.

Hili swala nakuhakikishia litakuwa gumu kwa sababu moja kubwa anayelalamika sio serikali ya Tanzania ambayo ndio ina mikataba na UK.
 
Niliwahi kugusia huko nyuma kuwa kuanzisha matawi ya chama nje ya si halali kwani katiba ya CCM yenyewe haisemi hivyo. Kubwa zaidi ni kuwa ktk katiba yao kuna tawi, kata, wilaya, mkoa na taifa. Je hao wa london katika mlolongo huo wao wajigawa vp huko.

Mambo ya maana na ya msingi kama uraia wa nchi 2 hawataki, kupiga kura nje hakuna, badala yake wapo busy na kufanya mambo ya ajabu.

The million dollar question kwa alieuliza ikiwa Baba Balozi ndio chairman wa CCM, mie wa CUF au Chadema nitakuwa na imani ipi na mama Balozi kuwa ata kuwa neutral.

Mambo mengine sometimes mtu unatamani ungezaliwa Papua New Guinea ukawa unatembea uchi na kula sokwe tu.
 
Niliwahi kugusia huko nyuma kuwa kuanzisha matawi ya chama nje ya si halali kwani katiba ya CCM yenyewe haisemi hivyo. Kubwa zaidi ni kuwa ktk katiba yao kuna tawi, kata, wilaya, mkoa na taifa. Je hao wa london katika mlolongo huo wao wajigawa vp huko.


Masatu

Kwa hilo ningekushauri angalia vizuri katiba ya ccm hasa marekebisho yaliyofanywa hivi karibu kati ya 2003 to 2006.
 
Jamani wana JF ambao mko active na "threads" zinazoanzishwa, ningependa kuwaeleza kuwa, kama sikusahau, kabla sijajiunga na JF kwa kuwa nimekuwa nasoma hii "Forum" na nyingine muda mrefu; nakumbuka sana kuwa kuna wakati swala hili la kufungua Tawi nje ya nchi, na kwamba mume wa Balozi kuwa Mwenyekiti na mambo mengi tu yalijadiliwa.

Kama dasturi ya JF huwa hakuna thread hata moja,labda ambazo zimeandikwa kabla sijaanza kusoma threads za JF ambazo zilianzishwa kwa majadiliano na kufikia tamati yaani "conclusion" ambayo aidha inaelimisha,inarekebisha, au inabadilisha mambo.

Imekuwa kama JF ni mahala pa mzaha na porojo na mizaha, na matusi, na kebehi, na kujianika ujinga wetu. Ninachoshauri, kabla mtu hajaanzisha "thread", angalau afanye homework kidogo kupata hata "some facts" kuhusu anachotaka kuanzisha.

Hili swala liliongelewa sana, lakini sikusoma kilichotunufaisha,badala yake thread ilikufa "natural death"! Mimi niko kwenye kambi ya Wakimbizi Ngara kama mshauri wa maswala ya Kisiasa.Pamoja kuwa Mshauri wa maswla ya Kisiasa kwa Wakimbizi, pia tuna Tawi la CCM, ni Katibu. Hivyo naijua sana Katiba ya Nchi na pia ya CCM.

Katiba ya nchi haina mahala inazungumzia vyama vya Siasa nje ya Nchi, kwa maana hiyo hakuna uvunjaji wa Katiba ya Nchi kwa chama cha siasa kufungua Tawi nje ya Nchi.Katiba ya CCM inaruhusu( Fungu la II, 31 (1)d, na 31(2),ukurasa 22.Kwa hiyo, Matawi yanaruhusiwa na Katiba ya CCM kufunguliwa nje ya Nchi.

Swala la huyo Balozi kutomshughulikia mtu wa upinzani eti kwa sababu mume wake ni Mwenyekiti, ah, labda sijui kwa kuwa huku ni mbali na mliko. Lakini kimtazamo sioni uwiano wa mabo hayo mawili, na ni muda sasa tangu huyo mama awe Balozi huko, je kuna mmoja wetu katika JF au Watanzania wanaoishi huko Uingereza aliyekwenda Ofisini kwa Balozi akakataliwa kusikilizwa, au akapewa uamuzi wa husda kwa kuwa yeye si mwanachama wa CCM?

Hapa ndipo narudia kuwakumbusha wana JF wenzangu kuwa, tuache hizi tabia za kuandika "threads for the sake of writting something". Tuanzishe "threads" ambazo zitatupa mafunzo, faida na upanuo wa akili zetu. Sio kufungua vinywa na ku "yap yap"

Vyama vya upinzani, na nyie funguweni Matawi yenu, maana mko huko siku nyingi na mnaharakati zenu za Siasa hata kabla CCM hawajafikiria kuanzisha harakati za kufungua Tawi. Nimesoma tayari wana Shina Reading. Nyie wapinzani mko wapi? Acheni kulalamika!
 
Lwama Papa,

Unazungumza kama katiba wa CCM ktk tawi hilo la Ngara..kwa hiyo kutokuwapa wananchi hoja ya msingi ni dhulma ya elimu unayozungumziwa hapa. Sisi sote humu sio wanachama wa CCM wala vyama vya Upinzani lakini unapofungua chama cha siasa nje ya nchi ukipitia ofisi ya BALOZI ni swala ambalo Katiba haizungumzii ktk ibara zote ulizotaja.
Pili, Sheria ya ufunguzi wa tawi la chama tawala nje ni swala linalohusu zaidi sheria ya Uingereza. Tunauliza kama inaruhusiwa kufungua tawi ndani ya Uingereza!
Hata Marekani ambako hawana ushirikiano kabisa na Cuba kuna vyama vya Wa -Cuba ambao ni wapinzani wa Castro!..Mifano mingine ndio kama hiyo ya Tiger wa Sri Lanka!
Marekani hakuna tawi la chama tawala cha Cuba wala sidhani kama kuna tawi la chama chochote kinachotawala nchi zaidi ya ofisi ya Ubalozi kuwakilisha nchi.

Tunachotaka kuelewa ni sababu ya CCM kufikia ufunguzi wa tawi hili nje!... mbali na sheria kila kinachofanyika ndani ya vyama vyetu kinatuhusu wananchi kwa njia moja ama nyingine.
Nitashukuru sana kama ukiyaona malalamiko ya watu humu ndani kuwa yana sura yake na vizuri ukawapa jibu badala ya kuwaona wao majuha! Kweli wewe umepata fundisho gani kutokana na mada hii toka huko ilikotoka!
 
Wazee heshima mbele, Mzee Lunyungu,

Ningependa kuuliza, tatizo ni nini hasa? Wananchi wachache wa-Tanzania walioko London kuamua Kufungua tawi la ccm au mume wa balozi kuwa mwenyekiti wa tawi hilo?

Kabla ya kujaribu kuiangalaia hii mada kwa makini!
 
Mimi huku naongelea Katiba ya Nchi na ya CCM inavyosema katika swala la kuanzisha Tawi nje ya Nchi, na ni katika kuwajibu au kuwafungua macho wachangiaji ambao walikuwa wanauliza uhalali wake kama unafuatilia mada.

Hayo ya huko mimi siyajui, kama Ubalozi kweli ndio umefungua Tawi, basi itakuwa ajabu kwangu, maana sidhani kama Ubalozi unaweza kufanya hivyo. Wewe Mkandara, una ashahidi kama Ubalozi ndio umefungua hilo Tawi? Maswala ya sheria za huko Uingereza, ni nyie mlio huko mtueleze sheria ya Uingereza inasemaje? Hili pia liliongelewa miezi nafikiri ipatayo minne iliyopita wakati mada hii hii ilipokuwa imeanzishwa. Ni nani kati yenu aliyefanya utafiti mpaka leo akaja na "statement" kuwa, sheria ya Uingereza inasema hivi au vile, hakuna. Kwa hiyo ni porojo na majungu na malumbano yasiyoleta faida wala kutuelimisha wana "Forum".

TUJISAHIHISHE JAMANI. huku usiku jamani natoka sasa Ofisini, naenda home.

Niko pale pale kukumbusha, ni vyema kuandika hoja ukiwa na takwimu, ushahidi. Bila hivyo tunaonekana kama wahuni tu. Lingine ambalo hukutaka kuligusa, mbona mada hii iliongelewa siku nyingi za nyuma na kutofikia tamati? Je hivi kweli hakuna mada nyingine za maana za kuanzishwa tuweze kuchangia, zaidi ya kurudia maswala yale yale?

Kwa mwendo huu tutapoteza wasomaji wetu wengi, maana mtu anapofikiria kusoma JF, anajirudi kwa kusema, ah, jamaa hawa hawana hoja za misingi katika "threads" zao.
 
Lwampa
Pole sana ndugu katibu wa CCM . Inaonekana umesoma lakini hujaelewa hoja yangu. Na kwa kukusaidia kama mwanzoni tuliongelea ikaishia hewani mimi sasa naaka kujua hadi Uhalali wa Majaliwa Sharif kuwa mwenyekiti . Ile ni kazi je ana kibali cha kufanya kazi UK ? Je huonio to be at the heart of Ubalozi wetu anaweza ku influency mambo pale yakawa ki CCM wakati Balozi ni wa watanzania ? Je umesha uona mgogoro huu sasa kwa Watanzania wanao kaaa UK .

Hapa tunataka kuangalia sheria za UK zinasemaje na uhalali wa CCM kutimia pesa zetu kuleta bendera za UK na kulipia majengo . Kumbuka CCM inapata ruzuku kubwa toka serikalini kwa kigezo cha uwingi wa Wabunge .

Mwisho naomba anuani za ofisi za London na reading tafadhali .
 
Mwisho naomba anuani za ofisi za London na reading tafadhali .

Pole mzee, naona umeuliza sana, nilikuwa nasubiri Yebo Yebo awasilishe anwani, ila naona kauchuna!! Hahaaa (Yebo Yebo natania mzee)

Nadhani Anwani ni;

213 High Street North,
East Ham,
E6 1JG.

Sasa sijui hapo juu unaandika nini? Ofisi ya CCM Landani, au CCM Office London.
 
(1). Uhalali wa mume wa balozi kuwa mwenyekiti wa tawi la ccm ambalo limeanzishwa na wananchi wachache wa-Tanzania, waishio London, je huu uhalali unakuwa in question kwa sheria zipi za bongo au za UK?

I mean ninaamini mume wa balozi ni mwananchi wa Tanzania aliyeko huko UK kwa sheria za kidiplomasia, ambazo ni makubaliano kati ya Tanzania na UK, kwenye kila ofisi yetu ya ubalozi nje kuna ofisa wa sheria, na wa usalama, kabla mume wa balozi kuwa mwenyekiti wa ccm au chama chochote huko nje, ni lazima mke wake ambaye ni balozi wetu awasiliane na hawa watu wawili ubalozini na kumpa okay mumewe kushiika hiyo nafasi, ni suala la wazi na very clear kwa mwananchi wa nchi yoyote duniani anayehusika na diplomasia, na kuhusu kibali cha kazi inategemea juu ya makubaliano kati yetu na serikali ya UK, ila ninaamini kuwa tunayo makubaliano ya namna hiyo yanyowaruhusu spouses wa maofisa wa ubalozi wao kwetu na sisi kwao kufanya kazi, otherwise binafsi sioni what is an ishu hapa, unless I am missing something?

au hili swali huenda linatakiwa kuelekezwa kwa serikali ya UK, badala ya wa-Tanzania!

(2). Anaweza ku-influence mambo ubalozini yakawa ki-ccm, you might have a point on this, lakini still, balozi wetu huko ni wa kuteuliwa na rais wetu ambaye ni mwenyekiti wa ccm taifa, au chama tawala, sasa nani anaweza kuwa na influence zaidi over balozi wetu huko, mwenyekiti wa taifa wa ccm au mume wa balozi ambaye mwenyekiti wa tawi dogo huko London? Serikali inaendeshwa na sera za ccm, ambazo moja ya kazi za balozi wetu huko nje ni kuzisimamia kwa nguvu zake zote kama alivyoapa mbele ya rais, sasa huyu mume ataongeza nini kwani msimamo wa ccm upo tayari ndani ya huyo balozi?

Uless Tanzania tunahitaji kuwa na sheria inayomkataza mume au mke wa kiongozi yoyote wa siasa, kujihusisha na siasa, ndani au nje ya nchi yetu, manake Anna Abdallah akiwa mwenyekiti wa UWT, na mumewe akiwa Spika wa bunge letu, si nayo ingekuwa a conflict of interest au? Waziri wa elimu na mke wa Spika, hiyo nayo vipi? Hatuwezi kisheria kuwalazimisha mke na mume kuwa na msimamo mmoja wa kisiasa, au kuwa na msimamo tofauti, nafikiri inapofikia hilo siasa comes to an end, the only problem ni pale tu hiyo influence inapokuwa inavunja any of our sheria au za huko UK, unless tena kama nina-miss something?

(3). Uhalali wa tawi la ccm London kutumia pesa zetu kuleta bendera na kulipia jengo, ninataka kuamini kuwa jengo hilo linalipiwa na either ccm tawi la huko huko London, au zinatoka makao makuu ya ccm, unless kuna ushahidi kwamba pesa zinazolipiwa ni za ubalozi ambazo zinatumwa na serikali yetu kwa ajili ya matumizi ya ubalozi, hapo kweli kutakuwa na ishu, lakini kama hatuna huo ushahidi basi haya yatakuwa ni majungu!

Otherwise, sioni tatizo lolote lile chama cha siasa chochote kile bongo kuwa na tawi lake huko majuu, mbona tunajua kuwa Dc kuna tawi la cuf, ingawa la siri lakini lipo, na hata Boston lipo tawi la cuf, tatizo ni nini?

Unajua huenda kuna something ninaki-miss na hii ishu, ama sivyo so far sioni tatizo ni nini? Kama kuna hela za serikali zimetumika kwenye shughuli za hili tawi la ccm, basi ushaidi uwekwe hapa au wazi lili wahusika waulizwe, ili kulinda hadhi ya hii forum!
 
Lwama Papa,

Nadhani Lunyungu kakupa jibu zuri na yaonyesha wazi umerukia mada hii bila kuisoma na kutoa hukumu kwa sababu inahusu CCM. Kumbuka pia swala hili limeongezeka uzito baada ya kuwasili kwa Malecela hivi majuzi. Labda ningekubaliana na wewe kama ungesema hapakuwa na haja ya kufungua Mada nyingine badala ya hii....Kisha kinachozungumziwa hapa ni kuwepo kwa tawi hilo UK na waathirika ni Watanzania waishio UK sio maswala ya Katiba na sheria ya Tanzania ambayo haivuki mipaka bila kuzingatia kwanza sheria za nchi husika.
Unazungumzia maswala ya TZ wakati hapa watu wanzungumzia maswala ya UK na kuwepo kwa tawi la CCM huko UK.
Na umetaka ushahidi kutoka kwangu kama Balozi yetu imehusika na ufungua wa tawi hilo nadhani bora rejea safari ya Malecela nchini hapo.
leo hii ndugu yangu Mkeo akifungua tawi la CCM ndani ya kambi hiyo ya wakimbizi hali wewe ni Mshauri wa maswala ya kisiasa ktk kambi hiyo, italeta sura mbaya! kubali usikubali kwamba mkeo katumia nafasi yako kama mshauri wa kisiasa na pia Ukatibu wako wa CCM hapo Ngaraa kuanzisha chama ndani ya kambi ya wakimbizi!...
Wananchi wakiuliza sidhani kama wao ni wazushi wa mambo bali uzushi umetokana na kufunguliwa kwa chama..
 
Ama kweli wewe ES ni CCM! You seem to follow the rules... Mimi si mwanachama, si mkereketwa, si mfurukutwa, na wala si kada bali ni mfirigiswa.

Lakini ulichoongea naona umehitimisha vema. Mzizi wa fitna ukatwe! Ukweli uanikwe hapa kama kuna ubadhirifu wa hela zetu walalahoi umefanyika.

Na naomba maswali yakiulizwa usaidie kujibu maana Lwama Papa alikuwa anaangalia salio naona hata Kulikoni naye amezimika... Labda 'wese' limeisha
 
Mzee Worm,

Heshima mbele, hilo sijawahi kuficha toka tukiwa BCS kuwa ni mimi ni ccm damu, na wala sina aibu nalo, chama changu ni safi lakini pia kina uozo, na siku zote sian noma kukubali unapodhihirika kuwa upo na ukaonyeshwa hadharani,

Lakini cha muhimu pia ni heshima yaa hii forum, kuna mada nyingi za hivi karibuni ambazo zinaanza kutupelekea kwenye level za Darhotwire, ndio maana lazima tusimamie heshima ya forum, na ishu kama hii ya matumizi ya pesa za umma kwa shughuli ambazo sio za wananchi, huwa zinahitaji ushahidi, ama sivyo yanakuwa majungu!
 
Back
Top Bottom