MONSI WENGA
Member
- Aug 7, 2011
- 51
- 34
Leo majira ya saa 18:30 jioni kumetokea ajali ktk kijiji cha RUANDA wilaya ya MBOZI barabara ya Mbeya Tunduma imetokea ajali ambapo mtoto mdogo mwenye miaka 12 amegongwa na kufariki papohapo hali ambayo imeleta taflani kwa wanakijiji kuweka magogo na kulala barabarani kuzuia magari ya pande zote mbili kupita. Jitihada za kamati ya ulinzi na usalama (W) kuwashawishi inagonga mwamba.