TANZIA Mwakata, Shinyanga: Ajali ya magari matatu 'Lori, IST, Hiace' na Trekta yadaiwa Watu 20 wamefariki, 15 wajeruhiwa (Agosti 8, 2022)

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
AJALI (5).jpeg
Watu 20 wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha magari matatu na Trekta katika eneo la Mwakata barabara ya Isaka Kahama mkoani Shinyanga.

Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali hiyo imetokea majira ya saa nne usiku Jumatatu Agosti 8,2022 ikihusisha gari ndogo IST yenye namba za usajili T880 DUE, Hiace yenye namba za usajili T350 BDX, Lori na Trekta. Inaelezwa kuwa Hiace imegongana uso kwa uso na Lori/Scania yenye namba za usajili T658 DUW.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Hospitali ya Kahama watu 20 wamepoteza maisha na 15 kujeruhiwa katika ajali hiyo na majeruhi wanaendelea kupata matibabu.

"Watu 17 walipoteza maisha papo hapo eneo la tukio na watatu wamefariki baada ya kufikishwa hospitali, majeruhi wapo 15," taarifa inaeleza.

Mpaka sasa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga halijazungumzia kuhusu tukio hili, juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi zinaendelea.

=======================

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, Leonard Nyanduhu amesema ajali hiyo iliyotokea saa nne kasoro usiku Agosti 8, 2022 Kijiji cha Mwakata, Kata ya Mwakata Wilaya ya Kahama katika Barabara Kuu ya Isaka - Kahama imehusisha magari manne kugongana na kusababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa vyombo hivyo vya usafiri.

"Ajali ilihusisha gari lenye namba za usajili T880 DUE Toyota IST iliyokuwa inatokea Isaka kuelekea Kahama, iliigonga kwa nyuma trekta yenye namba T719 AUP ikiendeshwa na dereva ambaye hajafahamika na kusababisha vifo vya watu watatu waliokuwa kwenye gari ya IST.

"Wakati huo imeshatokea ajali nyingine eneo hilohilo kwenye barabara hiyo ambapo ajali ya pili ilihusisha gari la Hiace yenye namba T350 BDX ikiendeshwa na Salinja Lukelele (28) ikitokea Kahama kuelekea Isaka iliigonga kwa mbele gari yenye namba T658 DUW Scania ikiendeshwa na dereva ambaye bado hajapatikana na kusababisha vifo vya watu 13 waliokuwa kwenye hiyo Hiace," amesema Kamanda Mwaibambe.

"Hiyo Scania ilikuwa imepaki na huyo dereva wa Hiace akitokea huko alijua kabisa pale kuna ajali na kuna baadhi ya magari yalikuwa yamesimama lakini yeye akawa anafanya jitihada za kukwepa magari yaliyosimama ili awahi kule anakotaka kwenda matokeo yake akaenda kuivaa hiyo Scania.

“Kwenye hiyo IST waliofariki ni wanaume, uchunguzi wa awali unaonesha hiyo gari ilikuwa kwenye mwendo kasi imeharibika, iliingia chini ya Trekta, huenda dereva alikuwa amelewa kwani tumekuta pombe aina ya Kvant ndani ya gari,” ameongeza Kamanda Mwaibambe.

Amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama na majeruhi wanaendelea kupata matibabu.

“Ukiangalia muktadha wa hii ajali ni ajali ya uzembe mkubwa sana, hili trekta lilibeba kuni nyingi na halikuwa na Reflector, lakini pamoja na kwamba hii trekta haina reflector lakini IST ina taa aliingiaje chini ya trekta, mwenye IST na trekta wote wana makosa.

“Ajali ya pili nayo dereva wa Hiace anajua kabisa kuna ajali na magari yamesimama lakini anatoka mbio kuyapita magari hayo, huyu mwenye Scania aliona gari inayumba yumba kwa speed akapaki yeye akaivaa Scania," amesema.

Amewasisitiza watumiaji wa vyombo vya moto kuzinga
 
Kama nawaona wabrashi viatu wakishukuru maombi yao kujibiwa. Wangependa ajali kubwa kubwa kumthibitisha Kinana wrong.

Kazi kweli kweli.
 
Watu 19 wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha magari manne ikiwemo treka wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Ajali hiyo imetokea katika barabara ya Isaka kwenye kijiji cha Mwakata halmashauri ya Msalala.

Ajali hiyo imetokea jana Agosti 8 majira ya saa 4 usiku ikihusisha gari ndogo aina ya IST (T880 DUE), Hiace (T350 BDX), lori (T658 DUW) na trekta.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali, inadaiwa kuwa trekta hilo lilikuwa likiendeshwa bila kuwa na taa za tahadhari (hazard) na kusababisha kugongana na uso kwa uso na Hiace.

Afisa muuguzi wa hospitali ya manispaa ya Kahama, Wilbert Mollel amesema kuwa jumla ya maiti 19 zimepokelewa sambamba na majeruhi 15.

Kaimu kamanda wa polisi mkoani Shinyanga ambaye ni kamanda wa Polisi Mkoani Geita ACP. Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa dereva wa trekta ambaye ni chanzo cha ajali amekimbia na juhudi za kumsaka zinaendlea.

Aidha Uongozi wa Mkoa wa Shinyanga ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Sophia Mjema umefika eneo la tukio na kulitaka jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kusimamia sheria ili kuepukana na vifo vinavyoepukika.

#AzamTVUpdates #AjaliShinyanga
Screenshot_20220809-104206.jpg
 
Hatari sana Mungu tuepushe na hii dhahma.

Nipo safarini kwenye bus nimepanda Dar Xpress tupo Segera driver kashapigwa torch zaidi ya tano na haelewi hivi hapa tumesimamishwa tena sijui hawa jamaa wanahongana hawa?ni mbio mbio utadhani sheria hamna.
 
Watu 20 wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha magari matatu na Trekta katika eneo la Mwakata barabara ya Isaka Kahama mkoani Shinyanga.

Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali hiyo imetokea majira ya saa nne usiku Jumatatu Agosti 8,2022 ikihusisha gari ndogo IST yenye namba za usajili T880 DUE, Hiace yenye namba za usajili T350 BDX, Lori na Trekta. Inaelezwa kuwa Hiace imegongana uso kwa uso na Lori/Scania yenye namba za usajili T658 DUW.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Hospitali ya Kahama watu 20 wamepoteza maisha na 15 kujeruhiwa katika ajali hiyo na majeruhi wanaendelea kupata matibabu.

"Watu 17 walipoteza maisha papo hapo eneo la tukio na watatu wamefariki baada ya kufikishwa hospitali,majeruhi wapo 15", taarifa inaeleza.

Mpaka sasa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga halijazungumzia kuhusu tukio hili,juhudi za kumtafuta Kamanda wa polisi zinaendelea.
Nimeppita hapo Mwakata eneo la ajari .peuoe Dana hakuna hata kona.
 
Yaah..ni hicho kijiji..mawe ya mvua yalikua yanashuka kama matofari..ilikua ni balaa..mvua iliyesha kijiji hicho hicho tu.

#MaendeleoHayanaChama
Kuna vizee vichawi Sana vya haya Mambo, Miaka ya nyuma Kuna kamoja walikaudhi wanakijiji wenzie kakatengeneza mvua ya mawe, mvua ilikuwa kubwa mno haikatiki mpaka wakakafuata nyumbani kwake walikuta kapo na vitendea kazi kanasema "zogo mvula" ,walipokaomba msamaha ikakatika
 
Hatari sana Mungu tuepushe na hii dhahma.

Nipo safarini kwenye bus nimepanda Dar Xpress tupo Segera driver kashapigwa torch zaidi ya tano na haelewi hivi hapa tumesimamishwa tena sijui hawa jamaa wanahongana hawa?ni mbio mbio utadhani sheria hamna.
Hao traffic bado wanafanya nini barabarani? Kinana alishasema wapungue wabaki wa Stendi tu. Basi likitoka Stendi Mbezi likutane na traffic Stendi Kibaha, Morogoro, Dodoma, Singida, Nzega, Shinyanga kisha Mwanza.
 
Hii nchi ni siasa tu mkuu,nguo nyeupe wamejaa barabarani tena wanang'aa zaidi ya walivyokuwa mwanzo.
 
Hao traffic bado wanafanya nini barabarani? Kinana alishasema wapungue wabaki wa Stendi tu. Basi likitoka Stendi Mbezi likutane na traffic Stendi Kibaha, Morogoro, Dodoma, Singida, Nzega, Shinyanga kisha Mwanza.
Kwani hao ndio wanaoendesha magari??yaani upuuzi ww dreva lawama ziende kwa trafiki??sio sawa, ajari nyingi zinasababishwa na uzembe wa madreva!!sasa kama ajari hii dreva wa ist ameligonga trekta kwa nyuma, na kuuwa watu wote waliokuwa kwenye gari hilo, likaja lori likasimama ili kutoa msaada kwa wahanga naye hakuchukua tahadhari, imekuja hiace, ikaligonga hilo lori, hapo trafiki analaumiwa vipi na ilikuwa usiku?!!
 
Back
Top Bottom