Vurugu kubwa zimezuka ruanda baada ya ajali kutokea

MONSI WENGA

Member
Aug 7, 2011
51
34
Leo majira ya saa 18:30 jioni kumetokea ajali ktk kijiji cha RUANDA wilaya ya MBOZI barabara ya Mbeya Tunduma imetokea ajali ambapo mtoto mdogo mwenye miaka 12 amegongwa na kufariki papohapo hali ambayo imeleta taflani kwa wanakijiji kuweka magogo na kulala barabarani kuzuia magari ya pande zote mbili kupita. Jitihada za kamati ya ulinzi na usalama (W) kuwashawishi inagonga mwamba.
 
Hii nchi haina serikali? mbona watu wanajichukulia sheria mkononi siku hizi? ajali za barabarani ni kitu kinachoweza kutokea sasa inakuwaje watu wanaona kama kitu kisichoweza kutokea? Ninavyojua serikali ni chombo cha kuogopewa na kuheshimiwa, kazi yake kubwa ya ndani ni kusimamia sheria kwa kutumia vyombo vyake vya dola ikiwemo polisi na mahakama, sasa hawa raia wanaoamua kuziba barabara inakuwaje? kwani mahabusu zimejaa Tanzania?
 
Hivi umekuwa wakwanza kuchangia thread halafu unaongea pumba?UNAFIKIRI HAO WANANCHI WOTE NI WAJINGA WW TU NDO UNA AKILI.Ni busara ndogo tu inahitajika serikali imeweka matuta makubwa mbuga ya mikumi lkn maeneo wanayopita watu na watoto wameweka matuta kama rasta.so wananchi wana haki ya kutoa hisia zao kwa njia mbalimbali.Au ulitaka marehemu anavyosaliwa mchungaji au shehe akemee ajali?
 
Nipo eneo la tukio, suluhu imepatika baada ya wananchi kuahidiwa kujegewa matuta. Kwa mujibu wa maelezo ya wakazi wa eneo hili ajali zimekuwa zikitokea mara kwa mara na waliomba kuwekewa matuta eneo hilo lakini matuta yakawekwa sehemu isiyostahili amabapo hakuna makazi ya watu.
 
Hivi matuta huwa yanajengwa kila mahala bila ushauri wa kitaalamu??
hii nchi raia wamejichokea na serikali imejichkea
 
Nipo eneo la tukio, suluhu imepatika baada ya wananchi kuahidiwa kujegewa matuta. Kwa mujibu wa maelezo ya wakazi wa eneo hili ajali zimekuwa zikitokea mara kwa mara na waliomba kuwekewa matuta eneo hilo lakini matuta yakawekwa sehemu isiyostahili amabapo hakuna makazi ya watu.

Bila kutoa elimu ikiwemo matumizi sahihi ya barabara katika jamii haya matuta yatazagaa kila mahali nchi nzima. Tembelea nchi zingine hukuti matuta kama TZ ambapo elimu ni Zeroooo. Pigania elimu katika shule zetu za awali na msingi ndio siri wa kila kitu ikiwemo kilimo kwanza.
 
Matuta siyo suluhisho, wajengewe tunnels za kuvuka barabara kwenye highway zote.
 
Hii nchi haina serikali? mbona watu wanajichukulia sheria mkononi siku hizi? ajali za barabarani ni kitu kinachoweza kutokea sasa inakuwaje watu wanaona kama kitu kisichoweza kutokea? Ninavyojua serikali ni chombo cha kuogopewa na kuheshimiwa, kazi yake kubwa ya ndani ni kusimamia sheria kwa kutumia vyombo vyake vya dola ikiwemo polisi na mahakama, sasa hawa raia wanaoamua kuziba barabara inakuwaje? kwani mahabusu zimejaa Tanzania?
Hebu vuta taswira kidogo mtoto wako ndo awe amepata hiyo ajali
 
Hivi umekuwa wakwanza kuchangia thread halafu unaongea pumba?UNAFIKIRI HAO WANANCHI WOTE NI WAJINGA WW TU NDO UNA AKILI.Ni busara ndogo tu inahitajika serikali imeweka matuta makubwa mbuga ya mikumi lkn maeneo wanayopita watu na watoto wameweka matuta kama rasta.so wananchi wana haki ya kutoa hisia zao kwa njia mbalimbali.Au ulitaka marehemu anavyosaliwa mchungaji au shehe akemee ajali?

Huyo jamaa nimemuuliza, vipi kama mtoto wake ndo awe amepata hiyo ajali?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom