Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Voda mmeshaniibia sana...tafadhari naomba account statement yangu kuanzia january...maana kuna mtu nilikua namtumia pesa kumbe account yake mlishaifunga na nilishawaambia mkaniambia mnalishughulikia...then mwezi jana nilinunua umeme mara nne na sikupata units niliwapigia mkanielekeza na kuniambia mtanirudishia pesa yangu ndani ya siku 7 matokeo yake mkarudisha miamara miwili ya mwisho ile miwili ya mwanzo hamkunirudishia sasa hii ndio nini? Na mpaka nikaona kinyaa kuwapigia tena..tafadhari naomba muangalie kama hamuamini naomba taarifa ya account yangu kuanzia januar mpaka tarehe 30 april
 
Jamani Vodacom kuna tatizo gani kuanzia juzi mtandao wenu mtu ukiongea zaidi ya dakika 1 mtandao unaanza kuzingua hvi mnafanya makusudi ili mtu ashindwe kukamilisha shida yake apige tena na muendelee kula hela au? Jamani me tangu kitambo nipo nanyi but if this will proceed nitawahama soon.
 
Watu wengi huku kwetu Geita wanahamia Tigo Sijui huko kwingine. Mfano unajiunga kifurushi cha dakika 100 harafu voda wanakupa sharti la kuzitumia ndani ya saa 24, ikitokea sababu ya kukukeep busy usipige simu kwa siku hiyo ukataka kupiga kesho yake unaambiwa muda wa kifurushi chako umeisha. Swali ukinunu dakika kwa fedha yako, zile dakika si inatakiwa iwe halali yako kutumia kama upendavyo zikiisha unanunua zingine bila kuwekewa limit? Mbona si hivyo kwa tigo? Na kwa LUKU? Ni Wizi huo halafu eti MB 8! Nawahama hivi karibuni!!
 
Kuanzia juzi mnaniibia kifurushi changu cha internet. MB 200 zinaisha baada ya kuperuzi muda mfupi tu tena vitu vya kawaida. Najiaandaa kuhama pamoja na familia yangu!
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania
[/QUOTE AISEEE VODACOM NIMEWACHOKA DATA BUNDLE UNLIMITED SHILLING 1000,, MTU UNATUMIA IKIFIKA 700 MB WANAKULIMIT,,,, NINI MAANA YA UNLIMITED BROWSING??? VODACOM ACHENI KUTUIBIA NA HUO WIZI WENU.. UNLIMITED INATAKIWA MPAKA MUDA ULIOJIUNGA UISHE SASA NYIE MNAWEKA LIMITATION ZENU ZA NINI?? NIKIPELEKA MALALAMIKO YANGU TCRA NADHANI NITAKUWA SAWA.... :teeth:
 
Kwanini vifurushi vya internet visiwe kama vocha??ukitumia mb zikiisha ujiunge tena sio mpaka masaa 24??
 
Kuwen kama tgo hawana mambo ya masaa 24 mb zako zkiisha unaruhusiwa kujiunga tena ata menu ya tigo ya tigo pesa unaweza kununua vifurush ukiwa ktk menu weken hii huduma mtufurahishe wateja wenu.
 
tatizo lingine ni hawa jamaa kutuibia mda wa hewani kila tunapoongeza salio, yani mnatuboa ile mbaya, na kama vipi tutaungana tuwashtaki kwa kosa la wizi wa mtandaoni
 
thanks vodacom kwa kutuboreshea network maeneo ya mkuu rombo........mmeonyesha jinsi gani mnatujali wateja....viva vodacom
 
Vodacom kwanini mmeshindwa kuboresha mtandao wenu hususan mteja akitaka kununua Luku? Hakika mmenichosha mno. Kwanza hamjibu haraka kuna wakati nilihitaji umeme jioni nyie mnatuma asubuhi. Leo tar 2.6.2015 naagiza umeme mnarudisha ujumbe eti nimekosea namba ya mita wakati sio kweli. Isitoshe mnashindwa kurudisha pesa mliokata. Natamani kutotumia mtandao huu kabisa kwa masuala ya Luku. Mmekosa namna ya kuondoa udhia huu?
 
Hili ni tatizo kubwa sana na wamelishindwa kabisa. Tumia mtandao mwingine tu maana hapa wameshindwa kabisa boresha hii adha ya mpesa. Ukikosea na inakuwa wkend na huna hela imekula kwako Kama unatumia voda
 
Kwa lipi Kowalski

Kuanzia mtandao kukatakata uje INTERNET ni shida vifurushi ndiyo hoi kabisa huko kwenye luku ndiyo mahututi kabisa wamebakiza M-PESA tu nisisahau kwenye kukatwa hela pasipo taarifa na ukiwapigia sm hakuna msaada wowote. Vodacom kazi ni kwetu
 
Nimenunua laini ya voda leo mchana. Nikaambiwa itakuwa tayari kwa matumizi baada ya saa moja toka niliposajiliwa. Sasa ni masaa 9 na nimepiga huduma kw wateja wanasema hiyo namba haijasajiliwa kabisa.

Shida ni nini? Kuna mwenye uzoefu???
 
Back
Top Bottom