Viwanja vinauzwa Ilala (Kipawa Mpya) bei milion 6 - vimepimwa

Ninawasiwasi na uwepo wa viwanja vingi na kwa bei hiyo kwa wakati kama huu ambapo ardhi imezidi kuwa ghali hasa eneo hilo. Kimsingi eneo hilo ninalifahamu vizuri, liliwahi kuwa na vurugu kati ya wenyeji na wahamiaji hadi kutishiana kuuana.
Binafsi ninamiliki eneo maeneo ya Buyuni ambako ni mbele zaidi ya KIPAWA MPYA, alafu unaingia ndani kama kilomita mbili. Eneo hilo linajengwa nyumba nyingi sana na Mfuko wa Pension (PSPF) kwa ajili ya makazi za kuuzwa na nadhani kupangisha pia.
Katika maeneo hayo kiwanja cha mita za mraba 1000 (1000sqm) huwezi kupata kwa bei chini ya shilingi za kitanzania milioni kumi (10m). Iweje kipawa mpya ambayo ipo jirani zaidi na barabara kubwa ukitokea mjini DSM viwepo viwanja vingi kwa bei ya 6m?
Nawaza tuuuuuuu

be carefuly guys!!!!!!!!!!
 
Ilala na Kinondoni yote ina mizozo katika upimwaji wa viwanja na ufidiaji... ni vema kuwa makini...
Nashauri wanaotaka viwanja ni vema waelekeze nguvu zao Temeke...Manispaa inapima viwanja vingi Gezaulole-na katika maeneo ambayo yatakuwa lulu miaka michache ijayo.!!
 
Mkuu ongea Taratibu wasije kujaa TMK,kwani hatuna tatizo la Foleni kama mbezi na tegeta.maana sasa ferry foleni ishaanza kuwa ndefu :(
 
Back
Top Bottom