Vituko vya ndoa Jamani

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,578
8,600
Wadau Mimi nimfanyakazi Mke wangu nimfanyakazi wote tunapata Mshahara sawa!!Lakini pesa zangu ndizo zinafanya kila kitu ndani!!Yeye ukimwuliza anasema wewe sindo baba mwenye nyumba!!Yeye zake nikununua mahitaji yake binafsi!!Sasa na Mpango wakumwachisha kazi je nitakuwa nimemkosea??kwani sioni sababu ya yeye kufanya kazi!!
 
Usimwachishe.. Ukitaka usipate pressure, acha kuuliza uliza mapato ya mwanamke. ZAKO ZENU, ZAKE ZAKE.. Mtaishi kwa amani.. Kwani mshahar a wako hautoshi kulisha nyumba?
 
Umwachishe Kazi ili iweje..? Hivi unadhani waliosema mwanamme ni kichwa cha familia walikosea??
Kwani huwa anakuomba hela ya saloon?lakini maisha ya sasa ni kusaidiana kama mtataka maendelea katika familia yenu .
Kaa na mkeo kwa upole na uongee nae ili mliweke hili swala sawa
 
Usimwachishe kazi, kama mshahara wake ananunulia mahitaji yake binafsi sioni tatizo kwani anakupunguzia matumizi kiasi fulani. Ukimwachisha kazi jitayarishe kuongeza matumizi ndani ya nyumba. Usichoke kumshauri umuhimu wa cost sharing.
 
Wadau Mimi nimfanyakazi Mke wangu nimfanyakazi wote tunapata Mshahara sawa!!Lakini pesa zangu ndizo zinafanya kila kitu ndani!!Yeye ukimwuliza anasema wewe sindo baba mwenye nyumba!!Yeye zake nikununua mahitaji yake binafsi!!Sasa na Mpango wakumwachisha kazi je nitakuwa nimemkosea??kwani sioni sababu ya yeye kufanya kazi!!

Hii ni ngumu sana hasa ukitilia maanani kwamba kipato chenu ni sawa. Wewe ungekuwa na kipato kikubwa zaidi labda mara mbili au hata zaidi kulinganisha na mwenzio labda ningemuelewa na huu utaratibu wake wa chako chenu, chake chake. Kaa naye muongee hili kwa kituo ikishindikana mtafute msaada kwa wenye busara walio karibu nanyi ili wawasaidie kuondoa hili purukushani katika ndoa yenu.
 
Nazaidi yeye ananidimandi kwalika kitu!!Mimi nakosa huduma za msingi kwakisingizio mimi nimfanyakazi siyo mama wandani!!As longer house gairl yupo!!Maana Housegairl ana mipaka yake yakuhudumia!!!Nitakompaili mawzo ya wadau nione!!
 
Ulitaka usaidiweje; tuulize tunaogharamia kila kitu tukueleze huko badget yake ni kubwa kiasi gani? Inawezekana umemwendea kwa kwa ubabe without reasoning! jaribu kujenga daraja mwache yeye akujie wewe na usiwe na haraka atachoka huyo !
 
kila siku nasema kuwa hii gender balance ni nadharia za majukwaani tu na kwa wanawake waliotosana na waume zao ndio wanaopromot ihii kitu. we hakikisha hakuombi hela kwa matumizi ya kipuuzi. msingi wa utegemezi pia uliujenga wewe so hayo ndio madhara yake
 
Mwanamke kuchangia pesa/mahitaji ndani ya nyumba inategemea sana na msingi wenu tangu mwanzo. Kama ndivyo ulivyomzoesha tangu mwanzo, itakuwia vigumu kumbadilisha kwa sasa. Na hilo ntalihesabu kati ya gharama ya makosa yako uliyoyafanya hapo awali.

Me nilianza tangu tuko girl friend na boy friend. Wanaume wangapi wakienda outing na wapenzi wao hujifanya hao ndo vidume, hata kama mwana dada nae pia ana mshiko? Ukiamua kuonyesha ukidume mwanzoni, basi uonyeshe mpaka mwisho wa safari.
 
Wadau Mimi nimfanyakazi Mke wangu nimfanyakazi wote tunapata Mshahara sawa!!Lakini pesa zangu ndizo zinafanya kila kitu ndani!!Yeye ukimwuliza anasema wewe sindo baba mwenye nyumba!!Yeye zake nikununua mahitaji yake binafsi!!Sasa na Mpango wakumwachisha kazi je nitakuwa nimemkosea??kwani sioni sababu ya yeye kufanya kazi!!

Huyo mwanamke hatendi kwa busara. Kama unakereka ni vyema ukamripoti kwa wazee wake au watu wangine walomzidi umri ambao anaweza kuwasikiza. Inavyoonekana ana tamaa sana ya mavazi na kujipodoa kwa gharama. Hiyo itakuja kuwakosti pale kipato chako kitakapopungua, cost sharing ni muhimu kama kuna mapenzi ya kweli na matumizi yenu yaende na kipato chenu.
 
lakini si unapenda uwe ndio kichwa cha familia yani uwe mwamuzi wa yote! sasa inabidi uhudumie familia yako, ukimwachisha kazi ujue pia itakulazimu kulipia yale mahitaji yake binafsi.
 
1.hana mapenzi ya kweli km angekuwa nayo mngesaidiana katika yote na katika mipango yote so sharing z the core
2.uyo alikubali kuolewa nawe ili uwe pbm solver cz u seems to b kidume fweza thats y so she dream to have easy n smooth life wth u so nw kuanza kumwimbia mwmbo wa cost sharing mh mh...sidhan km ataucheza sana sana atasema skuizi umebadirika aunipendi ............
3.bibie katokea machame?kibosho?au mkuranga?

pole kakangu .....duu mwambie shostito siyo kiivo bwana anatudhalilisha anafanya kaz stl anagandia ukaseja mh sa wasio fanya kazi waweje mmh shame on her!!!!!!
poleeeeeeeeeeeeee
 
Utamwachshaje kazi? how? yani asomeshwe yeye na wazazi wake wewe uje umwachishe kazi lol? vunja ukimya kaka, ongea na mkeo.
 
Usimwachishe.. Ukitaka usipate pressure, acha kuuliza uliza mapato ya mwanamke. ZAKO ZENU, ZAKE ZAKE.. Mtaishi kwa amani.. Kwani mshahar a wako hautoshi kulisha nyumba?

Mkuu Dreamliner nami nilitaka kumwambia hivyo hivyo. KakaKiiza achana naye fanya kama vile hana kazi wewe hudumia familia kama kawaida kama kipato chake kinatosha. Sisi engine tunao wafanyabiashara lakini hata chupi za watoto tunaombwa kutoka mifukoni mwetu
 
Utamwachshaje kazi? how? yani asomeshwe yeye na wazazi wake wewe uje umwachishe kazi lol? vunja ukimya kaka, ongea na mkeo.

U r very right Carmel, inawezekana analalamika lakini hajakaa na mkewe wakapanga hata maisha yao ya baadae....

Kwanza hatujui wana muda gani kwenye ndoa, kwa sababu kama ni mwili mmoja then watakuwa na lengo moja kwa ajili ya familia yao....

Ongea na mkeo kwa upole mpendwa, mueleweshe. Natumai atakuelewa. Good Luck
 
Wadau Mimi nimfanyakazi Mke wangu nimfanyakazi wote tunapata Mshahara sawa!!Lakini pesa zangu ndizo zinafanya kila kitu ndani!!Yeye ukimwuliza anasema wewe sindo baba mwenye nyumba!!Yeye zake nikununua mahitaji yake binafsi!!Sasa na Mpango wakumwachisha kazi je nitakuwa nimemkosea??kwani sioni sababu ya yeye kufanya kazi!!
Uki mwachisha kazi uwe tayari kumtimizia mahitaji yake yote... pamoja na ya kupaleka kwa serengetiboy
 
bado kuna mwanamke dunia hii ya leo unaweza kumuachisha kazi kirahic rahic tu?.....
 
Back
Top Bottom