Vituko vya ndoa Jamani

mie niko radhi aniwachishe kazi ............as long as ananilipa mshahara kama ule ninaopewa kazini mwisho wa mwezi! holla
 
hahha no name ...............unajua hapo unatiliana ile mikataba ya pesa kuwa transfered moja kwa moja kutoka account yake mwisho wa mwezi. yaano ukitua tu kutoka kazini unagawanywa juu kwa juu benki! hahahha

lazima ajiju :D
 
Mkuu wala usihangaike tuliza kichwa tu, na mimi mwanzo ilikuwa hivyo hivyo ila nikapata suluhisho na sasa naishi kwa amani kabisa yaani. Niliamua kumuachia hayo mambo madogo madogo yote afanye yeye kama kupanga namna ya kutumia mishahara, sijui mshahara wake afanyie nini au sijui mshahara wangu mwezi huu ni ngapi na tuutumieje ni yeye tu, kulipia watoto shule ujenzi mdogo mdogo kila kitu chini yake mimi nashughulika na mambo makubwa makubwa tu kama je uchaguzi ujao utakuwa huru na haki? Rais ajae ya marekani atatoka chama gani au kulikuwa na ulazima wa marekani kuvamia Irak, mafuta yakipatikana TZ tutakuwa saklama? basi kwa sasa tunaishi vizuriiiiiiiii raha mustarehe!
 
mie niko radhi aniwachishe kazi ............as long as ananilipa mshahara kama ule ninaopewa kazini mwisho wa mwezi! holla

atakulipa hadi lini kumbuka kuna kufulia na kifo, mojawapo likitokea utajuta sana kwa uamuzi wako wa kuacha kazi
 
Naona wabeijing hapa mmepatia sehemu ya kusemea yaani mmeacha tatizo la msingi la bwana KakaKiiza mmegotea kwenye kuachishwa kazi. Kimsingi kumuachisha mwenzio kitu chochote achilia mbali kazi bila ridhaa yake si jambo la busara lakini hebu basi tumshauri huyu bwana especially ninyi ambao mnashikia bango na wazo lake la kumuachisha mkewe kazi na si wengine bali ni Nyamayao, bht na carmel. I wonder WoS na MJ1 sijawasoma kabisa hapa leo maana najua wakiingia hapa........mtamalizia wenyewe.

NisaidieKaka kusema maan imekuwa kama South Africa na Vuvuzela lengo lake lakuwepo limepotea nakuona niusumbufu kelele nk!!!
 
Mkuu hapo utakuwa umekosea mwenyewe awali. Hawa viumbe imeandikwa "muishi nao kwa akili". Ukikosea step tu na akakutune kama mitabendi ya radio, utapiga muziki kila kukicha na asicheze...Kama uliamua kuanza na kujibebesha jukumu la kumwachia mshahara wako aupangie matumizi, ni waz kuwa wakwake utapumzika kwa mambo yake. Japo ndoa ni wawili lakini inapokuja kwenye masuala ya vipato, wanandoa wengi wanakosa kushirikishana, mwengi ya kina mama hela zao zinahishia zaidi kwanye matumizi binafsi hasa "kujikwatua" au kusaidia kwa upande wa alikotoka (weyewe wanaita kwetu). Wakati huo huo akina baba huwa hela zao ukiacha matumizi ya nyumbani kama chakula na matunzo ya familia, nyingi huwa zinaishia kwenye "kinywaji" (kwa wale wanaokunywa).

Ikiwa hamjakaa na kupoanga vizuri nini mfanye katika maisha, ni ngumu sana kuwezana inapofika kwenye suala la matumizi la matunda ya jasho la kila mmoja wenu. Kuna wakati inafikia kukosa pia kuaminiana na kufichana vipato ikiwa mwenzako unaona anatumia zaidi kwenye maene yasiyo na tija. Wengi wa wanandoa huwa hawaambiani hata marupurupu wanayopata kwenye kazi zao ukiacha mshahara.

Ukiwa katika mazingira kama hayo ambapo mama hataki kutumia kipato chake kwa ajili ya familia kwa kuwa baba upo na wewe ndio kichwa cha nyumba, hapo maisha ni sawa na kuishi na hawara/ kimada ndani ya nyumba ambae hamuaminiani wala kuonena huruma kwa kusaidiana. Katika maisha ya jinsi hiyo, ni nadra kukuta kuna maendeleo ya dhati. Mkeo akizoea kutumia kipato chake kwa manufaa yake binafsi, ni dhairi kuwa inamjengea ulemavu wa kujua majukumu. Ikitokea bahati mbaya ukifa, hata kama ana kazi itamwia vigumu sana kumudu majukumu ya familia kwa kuwa ana kuwa amezoea kuishi kwa kipato cha mume zaidi. Ndio haina ile ya wanawake ambao mume akifa inakuwa kama amepoteza muelekezo kabisa hata kama ana kazi nzuri, inachukua muda mfupi sana utamkuta kishapata Bwana mwingine.

Mkae chini mpange kwa pamoja, acha kuficha zako kwenye makoti au kabatini nae mweleze hivyo hivyo kuwa majukumu ya ndoa ni yenu wote (kwa shida na raha, magonjwa na huzuni).
Kumwachisha kazi haina suluhu, kwani itakuongezea mzigo tena hata hivyo vipodozi vyake itahamia kwenye hako kamshahara kako na pengine hata zile chache alizokuwa akimudu kutuma kwa wazazi wa upande wake (kama wapo na wanawategemea) zinapaswa zipukuchuliwe katika hako" ka salari" kako. Tena pengine si busara iwapo Mkeo amesoma kwa gharama za wazazi wake harafu wewe ushindwe kumsaidia kupata kazi au kumzuia hasifanye kazi, inakuwa kama vile umewadharau wale waliomsomesha mpaka alipofikia nawe ukamwona.
 
Naona wabeijing hapa mmepatia sehemu ya kusemea yaani mmeacha tatizo la msingi la bwana KakaKiiza mmegotea kwenye kuachishwa kazi. Kimsingi kumuachisha mwenzio kitu chochote achilia mbali kazi bila ridhaa yake si jambo la busara lakini hebu basi tumshauri huyu bwana especially ninyi ambao mnashikia bango na wazo lake la kumuachisha mkewe kazi na si wengine bali ni Nyamayao, bht na carmel. I wonder WoS na MJ1 sijawasoma kabisa hapa leo maana najua wakiingia hapa........mtamalizia wenyewe.

Ndiyo tatizo lao Wabeijing. Wameacha kujadili tatizo lilikuwepo la mke kubania mshahara wake na wameshikia bango kitu ambacho kwa sasa hakipo cha kumuachisha kazi ambacho kinaweza kisitokee.
 
Wadau Mimi nimfanyakazi Mke wangu nimfanyakazi wote tunapata Mshahara sawa!!Lakini pesa zangu ndizo zinafanya kila kitu ndani!!Yeye ukimwuliza anasema wewe sindo baba mwenye nyumba!!Yeye zake nikununua mahitaji yake binafsi!!Sasa na Mpango wakumwachisha kazi je nitakuwa nimemkosea??kwani sioni sababu ya yeye kufanya kazi!!

...pole sana kka. Mbona tu wengi tu yanayotukumba hayo?!...vumilia tu, si unakumbuka kiapo ulichokula iwe ni mbele ya kasisi au sheikh?...kumbuka, ni wewe mwenyewe ulipeleka posa kwao, ukaambiwa na mahari ukapeleka, siku ya ndoa ukaapa kwa viapo vyote utamtunza, utampenda na utamhudumia kwa kila kitu.
 
atakulipa hadi lini kumbuka kuna kufulia na kifo, mojawapo likitokea utajuta sana kwa uamuzi wako wa kuacha kazi

akifulia au kufa nitatafuta kazi ..........si elimu yangu nnayo! sioni sababu ya mtu kujilazimisha kwenda kazini mwanamke wakati mume uwezo anao na anakupa pesa unayotaka.
kwa upande wangu nafikiri kwnda kazini ni kwa staarehe yangu tu sitakiwi kulazimika kufanya hivyo........siku nikiamua nimechoka kazi, jukumu la kuhudumiwa na mume linabaki pale pale
 
quote_icon.png
Originally Posted by Mganyizi
Uki mwachisha kazi uwe tayari kumtimizia mahitaji yake yote... pamoja na ya kupaleka kwa serengetiboy

Hayo ndo mawazo ya jinsia ..me nyingi. Huenda hata huyo dada hataki kuchangia chochote ktk familia
akihofia mumewe kwenda kuhonga nyumba ndogo.
Mwacheni dada wa watu afanye kazi na atumie pesa zake kadri awezavyo. Kichwa cha familia na awajibike ili kutetea hiyo title yake.
 
Ndiyo tatizo lao Wabeijing. Wameacha kujadili tatizo lilikuwepo la mke kubania mshahara wake na wameshikia bango kitu ambacho kwa sasa hakipo cha kumuachisha kazi ambacho kinaweza kisitokee.

Hivi jamani mnadhani kuoa fasheni?
Hapo lazima kuna sababu ambazo mhusika hajataka kuziweka wazi!
Akiamua ku share cost basi na ashare, ila siyo kumlazimisha na kufikia hayo maamuzi!
 
...pole sana kka. Mbona tu wengi tu yanayotukumba hayo?!...vumilia tu, si unakumbuka kiapo ulichokula iwe ni mbele ya kasisi au sheikh?...kumbuka, ni wewe mwenyewe ulipeleka posa kwao, ukaambiwa na mahari ukapeleka, siku ya ndoa ukaapa kwa viapo vyote utamtunza, utampenda na utamhudumia kwa kila kitu.

you said it all. inaonekana wanaume wengine huwa hawajui maana ya kiapo wanachoapa.
 
Back
Top Bottom