Vitu gani ambavyo ni mtego?

Maleven

JF-Expert Member
Sep 8, 2019
627
2,795
1. Ukiwa unaondoka ugenini wakakwambia mbona haraka, usiondoke kesho usubiri kesho kutwa n.k huo ni mtego. Ondoka, hapo wanajikosha tu.

2. Unaaga kwenda kazini, mpenzi wako anasema usiende mpunzike kidogo, huo ni mtego, ukibaki unajipunguzia credits.

3. Unaongea na mtu af anasema nikipata vocha ntampigia af nitakupa majibu, au nikipata hela ntafanya x. Huo ni mtego.

4. Unabembelezwa kutoa siri, unaambiwa ' ukiniambia mimi simwambii mtu' huo ni mtego

5. Amekuacha kwa akaenda kwa mwingine, kisha anarudi kusema we ndo anakupenda, huo ni mtego, ni uongo

Mtego mwingine?
 
Back
Top Bottom