Vita ya Gazeti la Mwananchi na Joshua Nassari- Limekosa hoja

Hili gazeti linatumiwa na ZITTO na Usalama wa Taifa (AKA) ZOKA. Nani asiyejua uhusiano wa Mhariri wa gazeti hilo, Denis Msaki na Zitto? Nani asiyejua uhusiano wa MSAKI, ZOKA NA ZITO?

NANI asiyejua kuwa Zitto anataka kuonekana yeye ndiyo mwanasisa makini na bora ndani ya CDM kuliko wengine.

GAZETI LA MWANANCHI limetia aibu katika hili. Linakubali kutumiwa na watu wenye maslahi binafsi tena kwenye tahariri? Uandishi gani huu usiyofuata maadili? Vyombo vya dola vimetangaza kufanya uchunguzi juu ya matamshi ya NASARI, KABLA YA UCHUNGUZI HAUJATOKA, gazeti linaandika tahariri? Aibu!

Brother TIDO hapa unaharibu sifa yako. Je, ikiwa Nasari atafikishwa mahakamani mtaweza vipi kujitetea kuwa TAHARIRI yenu hamkushinikiza polisi kuchukua hatua hiyo? Je, akipelekwa mahakamani na akashinda kesi, mtakuwa tayari kulipa fidia kwa mliyosababisha? Mbona mnataka kutumiwa kama KONDOM kwa maslahi ya kundi fulani - ZOKA NA ZITO kupitia kwa MSAKI?

Nawasilisha.

Kwa hiyo malengo ya gazeti ni kuchochea mahakama imfunge Nassari.Pia gazeti linaonyesha CDM kama chama hawakuwa makini kwenye uteuzi wake.Gazeti limevuka mipaka ya uandishi.Hakika huu ni uhuni na upumbavu wa hali ya juu!..
 
Nassari aliteleza, ni vema aambiwe ukweli!!

Nadhani kwa siku hizi kadhaa amejifunza, na asiendelee kudhani yeye ni mdogo, ni mtu mzima na ana nguvu kubwa ya ushawishi, kauli yake moja inaweza kuleta taaruki katika jamii!!

Tusonge mbele, hakuna kulala hadi kieleweke!!
 
Siri za Zitto nje




Na Saed Kubenea - Imechapwa 09 December 2009




Mawasiliano yake yanaswa
Aponzwa na mwandishi wa habari


SIRI kubwa kuhusu mwenendo wa Zitto Kabwe (Mb) ndani ya chama chake zimeanikwa mitaani na zinaweza kumzamisha kisiasa, MwanaHALISI sasa linaweza kuripoti.


Siku nne baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Willibrod Slaa kusema wamenasa taarifa za mawasiliano ya Zitto, baadhi ya taarifa zimepatikana jijini Dar es Salaam.


Kwa mujibu wa taarifa hizo, Zitto ananukuliwa akiapa kusaidia wagombea uongozi katika vyama vingine; na katika moja ya taarifa ananukuliwa akisema atasaidia David Kafulila kupata ubunge "hata kabla ya akina John Mnyika…"


Mnyika ni Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CHADEMA na Kafulila alikuwa Afisa Habari ambaye baada ya kuondolewa wadhifa huo amekimbilia NCCR-Mageuzi. Mnyika anatarajia kugombea ubunge jimbo la Ubungo.


Naye Zitto amenukuliwa na gazeti la Mwananchi la Jumatatu akilalamika kuwa ameingiliwa katika mawasiliano yake ya baruapepe (e-mail); jambo ambalo Mkurugenzi wa Upelelezi, Robert Manumba, amedakia haraka na kusema Zitto akiwapelekea malalamiko watashughulikia.


Kwa mujibu wa mpangilio wa taarifa husika, lazima aliyezitoa amepata ufunguo wa baruapepe (password) wa ama Zitto au mwandishi wa habari wa Mwananchi, Denis Msacky.



Karibu mawasiliano yote ni kati ya Zitto na Msacky juu ya "ushujaa" wa Zitto na jinsi anavyopendwa nje ya chama huku "akichukiwa" na viongozi wake wakuu.



Katika moja ya mawasiliano, inaonyeshwa kuwa Msacky alimwandikia Zitto akieleza, "Leo hii Mrema (Augustine Lyatonga) anasema anakuheshimu wewe, lakini si Mbowe; hivyo hivyo, Lipumba (Profesa Ibrahim) na James Mbatia wanasema wewe una visheni."


Katika mawasiliano hayo ya Jumanne, 1 Desemba 2009, saa 6.45 adhuhuri, Msacky anaonyeshwa kumwambia Zitto pia kuwa, "CCM nao…wanakusifu kwamba pamoja na kwamba unawaliza sana, lakini ni kiongozi shupavu."


"Leo hii siasa za CHADEMA zingekuwa zinatisha kama ungekuwa mwenyekiti wa CHADEMA, vijana nchi nzima wangejiunga na chama, uko nao karibu, unaongea nao, una elimu nzuri, unajua mambo, unasoma sana," imeeleza sehemu ya mawasiliano kutoka kwa Msacky kwenda kwa Zitto.


Kinacholeta wasiwasi ndani ya CHADEMA kinaweza kuwa lugha inayotumiwa katika mawasiliano hayo. Kwa mfano, katika waraka huohuo, Msacky ananukuliwa akiandika:


"Wanataka kukumaliza, nami sitakubali mtu ammalize rafiki yangu nikiangalia…wanasema Mbowe hata Mbatia akikaa vema anaweza kumpita kama siasa za kufukuza zitaendelea. Muhimu, usisikilize watu, tulia, urudi tupange tufanye nini? Lakini ukweli ni kwamba sasa wanakuogopa…Mwenyekiti Mtarajiwa…"


Mawasiliano yanaonyesha kuwa Zitto hakufurahishwa sana na taarifa za Mwananchi kuwa amemsaidia Kafulila magari matatu kwenda Kigoma kufanya kampeni chini ya NCCR-Mageuzi, lakini Msacky anaonyesha kumfariji.


"Kaka, mimi nimeiona story, haina matatizo zaidi ya kuwafanya akina Mbowe kusitisha mpango mbaya dhidi yako maana wanaanza kuogopa. Hata Mrema Lyatonga amesema kwamba Zitto huwa unamsaidia akiwa na shida. This shows that ur a leader katika opposition, wewe ni mtu wa maridhiano, unakuza upinzani Kigoma," anaeleza.


Anasema, "Leo nasikia akina Mnyika wanahaha sana, waambie familia yako wasiingie katika mtego wa kuanza kuhojiwa na akina Kubenea (Saed wa MwanaHALISI), watawachanganya. Wewe usiongee kitu chochote, wabaki wanahaha, lakini for sure you are safe, na hizo kampeni za Mnyika kukuchafua huku akitaja majina ya Kafulila, ataziacha."


Akionyesha juhudi za kushawishi, kuliwaza au kufarakanisha, Msacky anaandika, "Katika hili Zitto, mimi niko na wewe, huna kosa ambalo umefanya, na wala usihofu maana wewe utakuwa nguzo ya upinzani Tanzania…Wanakupa majina ya ajabu, wanakuita Mr Dowans, wanatumia akina Halima Mdee kukuchafua katika magazeti…"


Awali Zitto alikuwa amemwandikia Msacky akisema, "Stori niliyoiona kwenye mwananchi itaniletea matatizo sana." Hiyo ilikuwa Jumatatu 30 Novemba 2009, saa 5.21 asubuhi. Baruapepe hiyo ilikuwa na kichwa kisemacho: "Muhimu na haraka."


Aidha, katika mawasiliano mengine, Zitto anaendelea kuonyesha kutofurahishwa na taarifa juu ya magari matatu kwa safari ya Kafulila.


Naye anaandika kwa Msacky, "tatizo la stori ni wingi wa magari, itaonekana mimi nina magari mengi na ni fisadi unajua? Hilo ndio tatizo."


Saini ya Zitto inatofautiana katika baadhi ya baruapepe. Pengine anaandika "zitto" na kwingine anaandika "Zi."


Moja ya mawasiliano ambayo yanazua mashaka yanaonyesha Zitto akikiri kuwa na mawasiliano na waasi nchini Kongo akiandika, "take it from me (niamini), nina contacts nyingi sana Congo na hao rebels (waasi) huwa wananiomba sana ushauri na kutaka kuwaunganisha."


Katika moja ya mawasiliano, Msacky anamwonya Zitto kutotumia baruapepe ya "CHADEMA kwa mawasiliano ya siri" na kutaka amwambie mama yake Shida Salum akatae kuongea na waandishi wa habari. "…nasikia Mbowe anataka mama awe akiongea na waandishi, usikubali," alieleza.


Zitto alipoulizwa kuhusu taarifa ya Mwananchi kuwa anatembea na barua mfukoni ya kujiuzulu uanachama CHADEMA, alisema "Sina la kusema."


Alipong'ang'anizwa kwamba imekuwaje hawezi kuzungumzia suala hilo ambalo ni muhimu kwa mustakabali wake wa kisiasa kwa chama chake, Zitto alisema, "Ni kwa sababu sitaki kuingia katika malumbano na katibu mkuu wangu (Dk. Willibrod Slaa) kwani malumbano hayo hayataijenga CHADEMA."


Alipotakiwa kueleza juu ya baruapepe ambazo zinadaiwa kuwa mawasiliano kati yake na Msacky, haraka alijibu, "Sina la kusema."


Alipoelezwa umuhimu wa yeye kueleza msimamo wake juu ya baruapepe hizo, Zitto alijibu, "Chochote nitakachosema sasa hivi, kitawachanganya Watanzania.


"Sitaki malumbano. Hakuna sababu ya kuwachanganya Watanzania. Hiyo haina maana yoyote," alisema Zitto kwa sauti ya ukali. Zitto alikuwa akiongea kutoka Ujerumani kwa simu Na. +4915222493231.


MwanaHALISI ilimtafuta Msacky. Baada ya kuita kwa muda mrefu bila kupokelewa, hatimaye aliandika ujumbe "Kaka, niko katika kikao. Tuma ujumbe."


Msacky aliulizwa, "Kaka, tumesikia kwamba umetajwa katika sakata la Zitto na chama chake na kwamba wewe ndiye mtibuaji. Je, ni kweli?" Hakujibu ujumbe na alipopigiwa simu ilikuwa inaita hadi kukatika.


Gazeti lilipowasiliana na Mnyika na kumueleza kwamba amekuwa akitajwa katika ujumbe wa Zitto na Msacky, alikiri kupokea ujumbe huo wa baruapepe uliotoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa ni "Mtanzania mwema."


Alisema alipoona ujumbe mmoja unahusu Zitto kushauri Msacky kutochapisha habari za mkutano wake na waandishi wa habari, ndipo aliamua kupeleka ujumbe huo kwa Zitto.


"Nilimuuliza kuna hiki kitu nimetumiwa. Je, haya ni maandishi yako au kuna mtu ameingilia emaili yako na kujiandikia haya? Hadi leo hii, bado sijapata jibu," alisema Mnyika kwa sauti ya masikitiko. Alisema yeye hana cha kusema na kuongeza, "labda umuulize Zitto."


Alipoulizwa anachukuliaje suala hilo, Mnyika alisema, "Ukiniuliza mimi kwa upande wangu, nilitegemea mambo hayo yangemalizwa katika vikao vya chama na si kwa vyombo vya habari. Lakini kwa hatua ya hivi sasa, nadhani Zitto bado anayo fursa ya kulieleza hili.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe alipoulizwa juu ya madai ya kuwapo njama za kuhujumu chama chake zinazofanywa na Msacky kwa kumtumia Zitto, haraka alijibu, "tuna utaratibu wetu wa kushungulikia mambo ndani ya CHADEMA."


Alisema, "Sina la kusema. CHADEMA ina utaratibu wake wa kushughulikia mambo yake."


Kwa kadri mawasiliano ya Zitto na Msacky yanavyoonyesha na iwapo yatathibitishwa kuwa kweli, jambo ambalo linaanza kuthibitishwa na Zitto kwa kulalamika kuingiliwa kwenye faragha, basi uhusiano wake katika chama utakuwa umepata nyufa.


Wachunguzi wa siasa za upinzani nchini wanasema kwa hali hii, uwezekano wa Zitto kubaki ndani ya chama chake ni mdogo. "Ama atajiondoa mwenyewe au hatimaye atafukuzwa," ameeleza mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


Hata hivyo, Zitto amenukuliwa na Mwananchi akisema, "Sitaki kugombana na mtu mimi. Wala msiniweke kwenye kifungo cha siasa. Ni bora niishi huru kuliko katika mateso ya siasa za kipumbavu kabisa. Nitafanya maamuzi ambayo hayajawahi kufikiriwa."


Wiki iliyopita Kafulila aliwaambia waandishi wa habari kwamba Zitto atafanya maamuzi makubwa ambayo hawakutegemea.


Gazeti toleo lenye makala hii
 
Mwananchi ni Gazeti makini sana Tanzania.

Laiti lingekuwa makini na kutenda haki lingeanza kumshambulia Christopher Ole Sendeka aliyechochea wananchi wa Arumeru kuwafukuza watu wa Musoma waliokuwa wanampigia kampeni Nassari.Ina maana hili gazeti Mwananchi hawakuona? Walichoona leo ni kutenga kurasa maalum za kutukana CDM na Nassari bila hata kutumia haki kwa suala lililoko kwenye vyombo vya sheria.
 
Nassari aliteleza, ni vema aambiwe ukweli!!

Nadhani kwa siku hizi kadhaa amejifunza, na asiendelee kudhani yeye ni mdogo, ni mtu mzima na ana nguvu kubwa ya ushawishi, kauli yake moja inaweza kuleta taaruki katika jamii!!

Tusonge mbele, hakuna kulala hadi kieleweke!!

Hakuna anayetetea alichosema Nassari.Tunachopinga ni gazeti Mwananchi kutenga kurasa maalum kutukana CDM na Nassari huku wakiwa hawafanyi hivyo kwa watu wengine wanaotoa maneno makubwa zaidi yake
 
Mbona JK kamteua Mbatia kutimiza yale waliyokubaliana na Cameroun kuhusu haki za "Makundi mengine" ndani ya jamii lakini hawasemi kwamba amekosea!

Duu! mshkaji umewaza mbali sana ila hatujui labda yaweza kuwa kweli maana miaka fulani ya nyuma Lyatonga yalimtoka maneno kuashiria kwamba Mbatia yuko 'mule mule'!
 
NI HOJA KWA GAZETI LA MWANANCHI ILA KITU AMBACH NA WEWE UMEKOSEA NI:

1.Nimesoma kolamu ya maoni ya Mhariri: Kilichonishtua ni kuona taharri ya aina hii kwenye gazet la mwananchi likiihusu CDM. Niseme wazi gazeti la mwananchi ni gazeti bora kwa TZ, no one can deny that fact, nilipotafakari niligundua tahariri ile ni ya kujenga CDM

2. Kwa namna yeyote ile kama Josh Nassari katoa kauli kama hizo zinazoelezwa mimi kwa maoni yangu nasema si sawa. Kiongozi lazima uwe na uwezo wa 'kuhesabu' maneno kufikisha ujumbe ulele.

3. Nakubaliana na wewe (penye redi). Haiwezekani kijana Josh nasssari alikuwa hajajiandaa, siaamini unahitaji kusomea ubunge. kwanza kigezo ni kujua kusoma na kuandika. so hapo hata mimi natofautiana na tahariri ya mwananchi kwa nionavyo mimi.

4. Siamini ni mashambulizi; naona kama ni jambo zuri kwa CDM kulichukua. Kwa nini? Zote hizi ni njama za CCM kusikiliz na kuhesabu kila neno linalosemwa na CDM na kujitahidi kuwafungulia kesi, so mpaka 2015 viongozi wengi 'makini' wa chadema watakuwa na kesi na wenginejela.So kwa Chama makini kama Chadema should take that very positive. Na nashauri kuwe na kitengo cha 'consultuncy' pale CDM kuhusu mambo ya siasa na risks ambazo they might be coming na'mitigation' mesures suggestion

5. Mwananchi limekuwa likiandika mambo mema kuhusu CDM, leo wwamejaribu kuungalia nupande wa pili wa shs, tuwe wavumilivu, ndi changamoto na changamoto hujenga. Kumbuka Mwananchi limewahi kushutumiwa na CCM kukipendelea CDM, so wanavyoturn kwetu siku moja tusome kwa makini na kujirekebesha.

6.Tunajiandaa kuchukua nchi, tuwe makini na 'maadui'. Tuhesabu maneno kufikish ujumbe uleule.


VIVA CDM. Aluta Contunua Josh Nassari

kamanda upo realy. nakuunga mkono, kamanda mwenzetu alipotoka! kamanda mbowe ameliona hilo, aombe ladhi.
 
Tido Mhando alikuwa hana mahali baada ya kupigwa stop TBC. Kapata kibarua sasa anakipamba na kukilinda. Siku zote wanasema "Adui yako muombee njaa usiwe na haja ya kutafuta silaha ya kumpiga. Acha atimize matakwa kwa mabosi, M4C mwendo mdundo.
 
Pengine msome na hapa;

CHADEMA iwaonye Nassari, Heche
ban.blank.jpg


Edson Kamukara​
amka2.gif
MGEMA akisifiwa tembo hulitia maji. Hivi ndivyo wahenga wanasema, wakimaanisha kuwa mtu anapopewa sifa nyingi kwa jambo zuri alilotenda, baadaye hubweteka na kuharibu.
Ni ukweli usiopingika kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), nyota yake kisiasa iko juu kiasi cha wapenda mageuzi kuamini kwamba huu ndio mbadala wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2015.
CHADEMA kimekuwa chama makini chenye viongozi makini wenye kutambua mahitaji ya wananchi na kuyapigania pasipo kujali madhara yatokanayo na kudai haki hizo.
Viongozi wakuu wa chama hicho na wafuasi wao wamedhalilishwa vya kutosha na Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya dola ili kujaribu kuwakatisha tamaa na kuwafunga midomo lakini moto wake ndiyo kwanza unazidi kulipuka.
Bila shaka hii ni safari njema kwa CHADEMA kujipanga vema ili ikitokea wamechukua dola mwaka 2015, utawala wao uoneshe utofauti na huu wa CCM ambao hauko makini kila idara.
Lakini kama wasemavyo wahenga wetu kuwa penye wengi hapakosi jambo, ama kwenye msafara wa mamba na kenge wamo, ndivyo tunaweza kusema kuwa baadhi ya makada wa CHADEMA ni kama wameanza kulewa sifa na hivyo kufanya kinyume na tunavyowatarajia.
Jeshi la Polisi mkoani Arusha linawashikilia viongozi na wanachama watatu wa CHADEMA huku likiendelea kumsaka Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari.
Kwa mujibu wa jeshi hilo, Nassari na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Taifa (Bavicha), John Heche, Katibu Mwenezi wa CHADEMA Arusha Mjini, Emanuel Kombe na Ally Bananga, wanatuhumiwa kutoa maneno ya kashifa.
Kwamba walimkashifu mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete kuwa anao marafiki wa kike anaowatambulisha kwa baba yake, ambaye huwateua kushika nyadhifa mbalimbali kutokana na ushawishi wake.
Naibu Kamishna wa Polisi, Isaya Mngulu, ambaye ni mkuu wa kitengo cha ufuatiliaji na tathmini kitengo cha upelelezi (CID) makao makuu ya jeshi hilo, alidai kuwa watuhumiwa hao walitoa kashifa hizo mwishoni mwa wiki kwenye mkutano wa hadhara.
Nafahamu fika kuwa polisi wetu wanababaika kuwakamata viongozi wa CHADEMA kwa kuwa aliyesemwa ni mtoto wa rais, ila wangekuwa ni wapinzani wamekashfiwa na mtoto huyo wala polisi mpaka sasa wangetuambia hawana taarifa yoyote.
Hata hivyo, pamoja na udhaifu wa jeshi letu katika kusimamia na kutenda haki, sipendi kuwahukumu watuhumiwa moja kwa moja kwa hilo, lakini kama kweli walisema maneno hayo, hakika wanahitaji karipio kali kutoka kwa viongozi wao wa juu kwenye chama.
Nasema hivyo, nikikumbushia kuwa ni muda mfupi tangu umalizike uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, ambao ulimpa ushindi mkubwa Nassari, kijana ambaye hakusikika akitukana kuanzia mwanzo wa kampeni hadi siku ya kuchaguliwa.
Badala yake kilichotokea huko ni kwa kada wa CCM ambaye pia ni mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde, kuporomosha matusi mazito mikutanoni dhidi ya viongozi wakuu wa CHADEMA na kisha akaachwa pasipo kuonywa na chama chake wala kukamatwa na polisi kama wanavyotafutwa wakina Nassari.
Maandiko matakatifu yanasema; mtu mwema na mwenye busara, hawezi kulipiza jema kwa baya, hivyo CHADEMA wanapaswa kujiepusha na mchezo huu wa kutaka kuwaiga CCM, ambao wanatukana bila haya, wanatumia nguvu za dola kutisha watu.
Ni katika hatua kama hiyo, nashawishika kuwataka viongozi wa CHADEMA wawakemee Nassari, Heche na wenzao mapema ili wanapokuwa mbele ya jamii wazungumze masuala ya sera na namna ya kumaliza kero za wananchi wala si matusi.
Yawezekana hicho walichokisema kwa Ridhiwani kikawa na ukweli ama hapana, lakini jambo la msingi hapa ni je, hilo linawasaidia nini wananchi katika kuondoa kero zao? Hiyo ndiyo CHADEMA inayokwenda kushika dola kesho?
Nassari amejizolea umaarufu mkubwa kwenye kampeni za uchaguzi mdogo jimboni kwake, alionesha anao upeo mpana wa kung'amua mambo na vile vile Heche ni kiongozi wa vijana taifa ambaye uwezo wake tunaufahamu vema, sasa kwanini wafanye vitendo vya kukidhalilisha chama?
Lazima vijana wanaoingia katika siasa hizi za kisasa, watambue kuwa umaarufu wao si kusimama majukwaani na kutukana ama kupiga kelele tu bali ni kujadili mustakabali wa Tanzania ya kesho.
CHADEMA imekwishajipambanua kwa umma kuwa ni chama makini, chenye watu makini wa kufanya mambo makini ya kulikomboa taifa na si kujadili watu na madhaifu yao binafsi, hivyo nashauri uongozi uwakee hawa wanaotaka kutupeleka kusiko.
Siasa za maji taka wananchi wamezichoka na ukitazama kwa undani sana wenye kuzitumia ni wale walio na upeo mdogo katika kuchanganua masuala mazito yanayoligusa taifa kwa ujumla, hivyo na kina Nassari na Heche wawe makini wasitumbukizwe huko wakati wanao upeo mpana.



h.sep3.gif

edkamukara@yahoo.com/ 0714717115/0788452350
 
Gazeti la Mwananchi nalipendea kwenye ile page ya Masoud Kipanya pamoja na kwenye ukurasa wa Kingo! page nyingine ni umbea business wala sinaga nazo time.
 
DOGO HACHA PUMBA INA BIFU NA Mh ZITTO NINI MBONA UNA MUINGIZA KWENYE ISSUE ZISIZO MHUSU Mh KAMA UNA BIFU NA CHUKI NAOMBA UTAFUTE SEHEMU YA KUMLAUMU SIO KUKURUPUKA WE MJINGA.....KWENYE SUALA LA NASSARY UTAKIWI UMU HUSISHE ZITTO ZUBERI KABWE....HUYU NI ZAIDI YA BRO KWA CDM....UWEZI KUMGROUP NA PUMBA ANAZO ONGEA NASSARY pmj na GODBLESS Lema huyu yupo KITAIFA ZAIDI.
 
NI HOJA KWA GAZETI LA MWANANCHI ILA KITU AMBACH NA WEWE UMEKOSEA NI:

1.Nimesoma kolamu ya maoni ya Mhariri: Kilichonishtua ni kuona taharri ya aina hii kwenye gazet la mwananchi likiihusu CDM. Niseme wazi gazeti la mwananchi ni gazeti bora kwa TZ, no one can deny that fact, nilipotafakari niligundua tahariri ile ni ya kujenga CDM

2. Kwa namna yeyote ile kama Josh Nassari katoa kauli kama hizo zinazoelezwa mimi kwa maoni yangu nasema si sawa. Kiongozi lazima uwe na uwezo wa 'kuhesabu' maneno kufikisha ujumbe ulele.

3. Nakubaliana na wewe (penye redi). Haiwezekani kijana Josh nasssari alikuwa hajajiandaa, siaamini unahitaji kusomea ubunge. kwanza kigezo ni kujua kusoma na kuandika. so hapo hata mimi natofautiana na tahariri ya mwananchi kwa nionavyo mimi.

4. Siamini ni mashambulizi; naona kama ni jambo zuri kwa CDM kulichukua. Kwa nini? Zote hizi ni njama za CCM kusikiliz na kuhesabu kila neno linalosemwa na CDM na kujitahidi kuwafungulia kesi, so mpaka 2015 viongozi wengi 'makini' wa chadema watakuwa na kesi na wenginejela.So kwa Chama makini kama Chadema should take that very positive. Na nashauri kuwe na kitengo cha 'consultuncy' pale CDM kuhusu mambo ya siasa na risks ambazo they might be coming na'mitigation' mesures suggestion

5. Mwananchi limekuwa likiandika mambo mema kuhusu CDM, leo wwamejaribu kuungalia nupande wa pili wa shs, tuwe wavumilivu, ndi changamoto na changamoto hujenga. Kumbuka Mwananchi limewahi kushutumiwa na CCM kukipendelea CDM, so wanavyoturn kwetu siku moja tusome kwa makini na kujirekebesha.

6.Tunajiandaa kuchukua nchi, tuwe makini na 'maadui'. Tuhesabu maneno kufikish ujumbe uleule.


VIVA CDM. Aluta Contunua Josh Nassari

Naungana mkono na wewe ,Jambo hili linabidi litazamwe kwa kina sana kwani tumejisahau na kuona kama CDM kina malaika kama viongozi.Kwa ustawi wa CDM kukosolewa na kujikosoa ni suala la msingi sana.

Mwananchi lishapata shutuma nyingi sana kuwa ni gazeti la CDM,linapendelea CDM,ila ukweli ni kuwa gazeti la Mwananchi ni gazeti makini lenye kuzingatia ukweli.So kulishutumu pindi linapoandika na kurekebisha kwa upande wa pili yaani CDM si sahihi .Kukosolewa ni kwa ustawi wa chama kinachotayarishwa kukamata dola.
 
Siri za Zitto nje




Na Saed Kubenea - Imechapwa 09 December 2009




Mawasiliano yake yanaswa
Aponzwa na mwandishi wa habari


SIRI kubwa kuhusu mwenendo wa Zitto Kabwe (Mb) ndani ya chama chake zimeanikwa mitaani na zinaweza kumzamisha kisiasa, MwanaHALISI sasa linaweza kuripoti.


Siku nne baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Willibrod Slaa kusema wamenasa taarifa za mawasiliano ya Zitto, baadhi ya taarifa zimepatikana jijini Dar e
https://www.jamiiforums.com/newreply.php?do=newreply&p=3878025
 
1. He need to be advised on how to adress the mass independently...................he is just growing and unfortunately through turmoils...........so even if you/we admire and support young politicians as well we need to tell them to be kean on tress passing, to adress before the public effectively and efficiently you need either skills or charisma or the combination.....he need to check his score sheets for his benefit particularly and the general community

2. His chairman Hon Mbowe noticed it instantly but the history has it that .....the words uttered, time spoiled...........Josh's case stands to be the living example.......distinction between an error and a mistake has to be bolded thus

3. Despite salutation and hon. status vested in Him (Nassari), love and appreciation among us....... still he is not experienced as most of us would like the case to be ..... he has his homework still ahead of him...........to learn from the experienced and not necessarily to share the threshold with them

This is for us all....who wishes to be vocal and vibrant......cautious practice makes it perfect......politics always is a a game of opportunity...hunting for a weakness to capitalise on.....thus more opportunities you give the weaker you become
 
Naungana mkono na wewe ,Jambo hili linabidi litazamwe kwa kina sana kwani tumejisahau na kuona kama CDM kina malaika kama viongozi.Kwa ustawi wa CDM kukosolewa na kujikosoa ni suala la msingi sana.

Mwananchi lishapata shutuma nyingi sana kuwa ni gazeti la CDM,linapendelea CDM,ila ukweli ni kuwa gazeti la Mwananchi ni gazeti makini lenye kuzingatia ukweli.So kulishutumu pindi linapoandika na kurekebisha kwa upande wa pili yaani CDM si sahihi .Kukosolewa ni kwa ustawi wa chama kinachotayarishwa kukamata dola.

Hili ni gazeti majitaka haiwezekani mhariri kutenga kurasa maalum kushambulia chama na mtu mmoja tena kwenye suala linaloshughulikiwa kisheria.Ni gazeti lisilo hata na chembe ya kutenda haki.
 
Back
Top Bottom