Didia
JF-Expert Member
- Nov 9, 2010
- 719
- 258
Hujui unachokisema.
Huelewi nilichokiandika!
Hujui unachokisema.
kwenye thread hii unaweza kuona tofauti kubwa ya washabiki, wazalendo na wapenzi!! mpenzi huwa kipofu, shabiki anafuata mkumbo na mzalendo anaangalia ukweli
nani hakosei? Dogo alikosea yet ni mbunge na ana bright future!! anakosea Obama iwe nassari? anakosolewa obama iwe nassari??
Usifikiri kwa gazeti kuandika ndo kumsaidia Nassari ili aweze kuwa mbunge mwadilifu na competent. Alishaelewa aliteleza na akakiri then iweje mhariri kwa uroho tu wa kuuza gazeti anaanza kufufua habari ambayo mwenye kuitoa alisha clarify.
Mbaya zaidi kusema Nassari hana uzoefu ni sawa na kusema newly wed couple wapate uzoefu kwanza ndo waoane. Huku ni kuwakashifu watu wa Arumeru ambao tangu 2010 walitaka kumchagua.
1. He need to be advised on how to adress the mass independently...................he is just growing and unfortunately through turmoils...........so even if you/we admire and support young politicians as well we need to tell them to be kean on tress passing, to adress before the public effectively and efficiently you need either skills or charisma or the combination.....he need to check his score sheets for his benefit particularly and the general community
2. His chairman Hon Mbowe noticed it instantly but the history has it that .....the words uttered, time spoiled...........Josh's case stands to be the living example.......distinction between an error and a mistake has to be bolded thus
3. Despite salutation and hon. status vested in Him (Nassari), love and appreciation among us....... still he is not experienced as most of us would like the case to be ..... he has his homework still ahead of him...........to learn from the experienced and not necessarily to share the threshold with them
This is for us all....who wishes to be vocal and vibrant......cautious practice makes it perfect......politics always is a a game of opportunity...hunting for a weakness to capitalise on.....thus more opportunities you give the weaker you become
Tido Mhando alikuwa hana mahali baada ya kupigwa stop TBC. Kapata kibarua sasa anakipamba na kukilinda. Siku zote wanasema "Adui yako muombee njaa usiwe na haja ya kutafuta silaha ya kumpiga. Acha atimize matakwa kwa mabosi, M4C mwendo mdundo.
Vyama vya siasa viwafunde, viwalee wabunge vijana | Send to a friend |
Tuesday, 08 May 2012 21:25 |
0diggsdigg Naibu Kamishna wa jeshi hilo, Isaya Mngulu alidai kwamba mbunge huyo na wenzake ambao tayari wamekamatwa na polisi walitoa matamshi ya kashfa na uchochezi katika mkutano huo, zikiwamo za kumpiga marufuku Rais Jakaya Kikwete asikanyage katika Jimbo la Arumeru Mashariki na Kanda ya Ziwa kwa madai kwamba maeneo hayo ni ya Chadema. Habari zinasema mbunge huyo alijisalimisha polisi jana mchana mjini Arusha. Polisi wanasema matamshi ya vijana hao hayana maana yoyote kwa jamii na kusisitiza kwamba yana lengo la kuleta migongano kati ya Serikali na wananchi. Hata hivyo, maelezo kuhusu matamshi ya vijana hao yanatofautiana kutegemeana na misimamo kinzani ya kisiasa na kiitikadi ya watu wanayoyatoa. Lakini inadaiwa kuwa, mara tu baada ya matamshi hayo kutolewa jukwaani, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisimama na kuyakana kwa kusema huo siyo msimamo wa chama hicho na kwamba ni kauli binafsi za vijana hao aliosema wana damu iliyochemshwa kwenye moto wa gesi. Itakumbukwa kwamba tangu aingie bungeni miezi michache iliyopita , mbunge huyo kijana amekuwa akitoa baadhi ya kauli siyo tu zinazotatanisha, bali pia zinazothibitisha kwamba pengine alipata ubunge kabla hajajiandaa au kuandaliwa kisaikolojia kubeba majukumu mazito ya ubunge. Nassari ana umri wa miaka 26 tu na tungetegemea chama chake kingemfunda kuhusu kauli zinazofaa na zisizofaa kutolewa hadharani. Kauli zake nyingi zimekuwa zikihusu tatizo la ardhi katika jimbo lake ambazo zimeonekana kuwahamasisha wananchi kuvamia mashamba ya wawekezaji. Lakini hoja yetu hapa siyo kumuhukumu mbunge huyo kijana au wenzake ambao wanadaiwa kutoa maneno ya uchochezi katika mkutano wa Arusha. Hatuwezi kufanya hivyo kwa sababu ya kuhofia kuingilia upelelezi wa polisi, hasa pia tukitilia maanani ukweli kwamba watuhumiwa hawajapata nafasi ya kuelezea upande mwingine wa shilingi. Hayo ndiyo matakwa ya maadili yanayosimamia taaluma yetu ya uandishi wa habari. Hata hivyo, tunachotaka kueleza hapa ni kwamba matatizo yanayowakumba wabunge vijana katika vyama vya siasa nchini hivi sasa yanatokana na viongozi wa vyama hivyo kushindwa kujenga mifumo ndani ya vyama vyao kwa lengo la kuwatayarisha vijana chipukizi na kuwajengea uwezo wa kubeba majukumu ya uongozi katika vyama hivyo katika ngazi zote za uongozi, yakiwamo ya ubunge. Viongozi hao wameshindwa kutambua kwamba uwezo wa vijana kuongea bungeni au kuvuta hisia za wananchi katika majukwaa ya kisiasa pekee hautoshi kuwafanya vijana hao wakidhi vigezo vya ubunge na kukubalika ndani na nje ya Bunge. Duniani kote vyama vya siasa vilivyo makini huanzisha taasisi na vyuo vya kuwajengea vijana uwezo wa kuongoza na kada hao ndiyo hutwaa uongozi wa nchi zao katika siku za baadaye. Hapa Tanzania hilo liliwezekana wakati chama cha TANU kilipoanzisha Chuo cha Kivukoni ambacho kilikuwa tanuru ya kupika viongozi wa baadaye tunaowaona hivi sasa. Bahati mbaya chuo hicho kilikufa na kuzikwa sawia na Azimio la Arusha Hii ni changamoto kubwa na pengine ni vyema vyama vya siasa vikatambua kwamba, vijana wakipikwa vizuri na kupata ujuzi katika uongozi, wakajua umuhimu wa maadili ya uongozi na uadilifu na wakaelewa itikadi za vyama vyao na wapinzani wao watakuwa tayari kushika hatamu za uongozi. Vinginevyo tutabakia kuwalaumu kina Joshua Nassari kwa kauli za uchochezi, huku tukikwepa kuondoa kiini cha tatizo. |
Unajua kinchotokea ni nini wandugu, ni ulimbukeni wa mawazo na upungufu wa fikra endelevu
kwa sababu jana wakati mweshimiwa Dogo Janja mbunge wa majimbo mawili ya kaskazini alipo
fika kuhojiwa baadhi ya maafisa police wenye kuaminika kuwa na vyeo vyao walisikika wakidhubutu kusema
eti, ndio ivyo sasa wao wana msikiliza aliyeko madarkani kwa hiyo kwa kuwa chadema ni chama
kinacholenga kuchukua dola wakiwa na wao madarakani nao wata watesa hao c.c.m....! Hii inatosha kuonyesha
umma na jamii nzima yakuwa isije ika kubaliana na ulimbukeni ulio jaa uchuro ndani yake kwa kuamini mia ya mia
vyombo vya habari, kwani kama hata walio kula viapo sio watu waadilifu kwa ujumla wao.....!
. Huu ni unafiki mkubwa na chuki binafsi kwani the same gazeti kwa kipindi chote karibu mwenzi mzima wa Kampeni za ubunge huko Arumeru liliweza kusikiliza na kuripoti kampeni za Nassari vizuri kabisa na wakati mwingi kumsifia.
Tido anatekeleza kazi alotumwa na EL. Mtindo huu huu wa kutumia magezeti ambayo yanaaminika kuwa makini ndo walotumia kumchafua Salim wakati wa mbio za uraisi mwaka 2005 kutumia Rai.
Tido Mhando anaruhusu haya?