Vita ya Gazeti la Mwananchi na Joshua Nassari- Limekosa hoja

Pamoja sana kamanda.Nadhani Mhariri wa Mwananchi anapitia jukwaa hili.Anapaswa sasa afahamu watanzania wa leo si wa jana na asidhani kwa kashfa zake atachelewesha mageuzi.La hasha......

pia mhariri aangalie Nasari alikuwa anazungumza akiwa katika mazingira yapi? and I believe that's why Mbowe aliweka mambo sawa.
 
Mimi nashauri ni vizuri Tanzania hususan Tanganyika ingebidi warejee katika ule utaratibu wa zamani kwa wateule wote wa rais wa ndani na nje ya nchi laima wapite chuo cha diplomasia (oposite JKT Mgulani) kwa wiki tatu ili waweze kujitambua ikiwa pamoja kujua nafasi zao kwa jamii.

Na nani vizuri hata wabunge wangepita pale kupigwa msasa na kujitambua.

Pole sana Nasari.
Kumbuka heri kuteleza mwili kuliko kuteleza ulimi
 
mwananchi angalieni sana hii tabia yenu ya kuamini kuwa mna uwezo wa kuchafua au hata kupamba litakuja kuwapotezea imani sisi hatufuati kwenu kurasa nzuri bali hoja na uchambuzi hebu jitathmini hata RAI,MTANZANIA pia walikuwaga na nguvu wakajivuruga
 
Mwananchi ni gazeti ambalo halilalii upande wowote, mie ndio gazeti langu nambari wani, mbona anaposemwa rais na magazeti mengine hupigi kelele? kama kitoto kimekosea acha kisemwe, binafsi naona kweli alikuwa hajapevuka kiasi cha kwenda kugombea ubunge, na amekosea na kujishushia heshma yake na chama kwa ujumla.
tupo pamoja mkuu. huo ndo ukweli wenyewe. Dogo aliharibu kuongea vile. huyu bado ni mbichi ktk ubunge lakini ni very potential na uwezo anao sana tu. kinachotakiwa ni awekwe sawa na viongozi wake KWA SABABU MAGAMBA WAMEPANIA KUFUTA MMOJA BAADA YA MWINGINE kupitia mahakama.

Kinachotakiwa hapa ni kujaribu kwa kila njia kuepuka kesi zisizo na msingi ambazo zinapoteza muelekeo wa chama.
tusipokuwa makini tutajikuta CDM tuna kesi nyingi na mahakamani kukageuka ndo ofisi zetu. kila tukiamka tupo kwa pilato.
gazeti la mwananchi liko makini. Tulipende likiandika vizuri kuhusu CDM na tulipende likitukosoa! Tuache unazi usio na tija
 
Sitaki kuona waandishi wa Mwananchi wanajiona wao ni mabingwa wa habari.
Mbona magazeti mengine hayajashupalia hiyo ishu.
Nimekasirika sana.Kwa sababu hiyo,nimeamua kutonunua gazeti la Mwananchi na The Citizen kwa mwezi miezi saba.
Habari zote muhimu nitajua nitakapozipata.
Huo ni msimamo wangu,na huenda ukawa wa ajabu kidogo ila ni namna bora ya kuonyesha hisia zangu.
Ee Mwenyezi Mungu nisaidie.

If you had read Che's views on criticism you would have a different opinion
 
Back
Top Bottom