Gazeti la Mwananchi acheni uandishi wa bora liende

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,226
5,948

Wenje aunguruma Sengerema​

Sengerema. Mbunge wa zamani wa Nyamagana (Chadema), Ezekiel Wenje amesema Serikali imeshindwa kudhibiti mfumuko wa bei na kuwaacha wananchi wa Tanzania walikia na kutaabika.

Wenje ambaye pia ni mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Victoria, ametoa kauli hiyo leo Oktoba 20, 2022 kwenye mkutano maalumu wa chama hicho wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza.

Amesema Serikali imewatekeleza wananchi katika jambo la mfumo wa bei hasa upande wa mahitaji muhimu ya wananchi hususani chakula na kuwaweke wananchi njia panda.

“Wanakalia kuumiza wananchi kwa tozo zisizo na ulazima wanashindwa kuangalia jambo linalogusa maisha ya watanzania,” amesema Wenje.

Amesema wananchi sasa wanatakiwa kusimama na kuamua kufanya mabadiliko ya kweli ndani ya nchi ili wapate unafuu wa maisha na jambo hilo litaletwa na Katiba ambayo ni chaguo la wananchi.

Hivi sasa hapa nchini, wananchi wanalia kutokana na mfumuko wa bei, hii imesabibishwa na wafanyabiashara kupandisha bei ya vyakula, hali inayowafanya wananchi kulia na hali hiyo.

Sambamba na hilo, Wenje amesema zama zimebadilika, walikimbia nchi sasa wamerudi kuisuka Chadema, hivyo wanachadema wanapaswa kuungana kwa pamoja ili kuwasaidia wananchi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, John Pambalu amesema nchi hii wananchi wanatakiwa kufanya mabadiliko ili kuwaondolea msongo wa mawazo waliyonayo kutokana na mfuko wa bei.

Mabaliko haya nikudai katiba mpya ambayo nimkombozi wa Watanzania wote, hivyo wanatakiwa kuwa wamoja ili wasonge mbele.

Paul Lufungulu ni mjumbe wa mkutano mkuu wa wilaya ya Sengerema, amesema wako tayari na wamejiandaa kutembea kwa kila kijiji kutoa hamasa kwa wananchi juu kilio cha katiba mpya.

Maye katibu mwenezi wa Chadema Jimbo la Sengerema, Stanley Kakele amesema wamejipanga kuhakikisha jamii inapata elimu juu uwepo na wakatiba mpya.

Oktoba 20, 2022 mlituandikia kuwa Wenje alikuwa akiunguruma Sengerema
leo Januari 10, 2023 mnatuhabarisha kuwa Wenje alitoroka nchi na yuko Marekani anatarajiwa kurejea hivi karibuni na wenzake Lema na Lissu

Lissu, Lema na Wenje kurejea nchini mwezi huu​

Dar es Salaam. Wakati Chadema ikitarajia kuzindua mikutano ya hadhara Januari 21, mwaka huu, viongozi wake walioko nje ya nchi, Tundu Lissu, Godbless Lema na Ezekia Wenje wanatarajiwa kuwa miongoni mwa washiriki katika mikutano hiyo, Mwananchi limedokezwa.

Mikutano ya hadhara ya chama hicho inatarajiwa kuanza baada ya Rais Samia Suluhu Hassan, mbele ya viongozi wa vyama 19 vya siasa vyenye usajili wa kudumu, kutangaza Januari 3 mwaka huu kuondoa zuio lililokuwepo.

Zuio hilo liliwekwa mwaka 2016 na Rais wa wakati huo, John Magufuli akitaka mikutano hiyo ihusishe wabunge na madiwani pekee waliochaguliwa, huku wengine wakitakiwa kufanya mikutano ya ndani ambayo nayo wakati mwingine ilikuwa inazuiwa.

Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho-Bara, yupo Ubelgiji na Lema, mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, anaishi Canada huku Wenje akiwa nchini Marekani na wote kwa pamoja waliondoka nchini wakihofia usalama wao baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Katika uchaguzi huo, Lissu alikuwa mgombea urais akichuana na mgombea wa CCM, Magufuli àmbaye aliibuka mshindi huku Lema akishindwa kutetea ubunge wa Arusha Mjini dhidi ya Mrisho Gambo wa CCM.
Taarifa za Lissu na Lema kurejea nchini, zimedokezwa na chanzo chetu ndani ya Kamati Kuu ya Chadema iliyoketi hivi karibuni, kuwa Lissu na Lema watakuwa nchini kabla ya Januari 21, mwaka huu.

Chanzo hicho kilisema kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika kwa mtandao Januari 5, mwaka huu kupokea taarifa ya maridhiano baina ya CCM, Serikali na Chadena pamoja na mambo mengine, kiliazimia wanasiasa hao warejee nchini.

“Suala la usalama si tatizo, kwani tayari Serikali ilikwisha kutoa taarifa bungeni kupitia kwa Waziri (Yusuph) Masauni kuwa nchi iko salama na kuwataka walioko nje warejee nchini kuijenga nchi.”

Katika kusisitiza hilo, mjumbe huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema, “lakini unaweza kuwacheki sasa Lissu na Lema wenyewe watakwambia maandalizi yao yamefikia wapi lakini kwenye uzinduzi wa mikutano watakuwepo.”

Ingawa Chadema haijaweka wazi uzinduzi huo utafanyikia wapi, gazeti hili lina taarifa kwamba utafanyika katika Kanda ya Mashariki yenye mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

“Mikutano itaanza Dar es Salaam kisha kwenda kanda zingine. Na Chopa ‘helkopta’ itatumika kwa ujumbe wa mwenyekiti Mbowe ambaye atafanya uzinduzi kanda zingine tisa na baada ya hapo mikutano itakuwa kila mahali,” kilidokeza chanzo chetu.

Alipoulizwa kwa simu kama atakuwepo katika uzinduzi wa mikutano hiyo, Lissu alijibu kwa ufupi, “nitarejea nyumbani muda si mrefu kaka, tutatoa taarifa rasmi muda si mrefu.”

Wakati Lisu akisema hivyo, Wanje kwa upande wake alipoulizwa alikiri suala hilo kuzungumzwa katika kikao cha Kamati Kuu na kuwa wamekubaliana kurejea nchini.

Alisema Lissu ndiye atakayetangulia na wengine watafuatia.
“Lissu atatangulia kisha mimi nitaingia Februari 5 na tayari tiketi nimeshakata. Kweli tungeweza kuja siku ya uzinduzi wa mikutano, lakini unajua tena mambo ya ratiba binafsi,” alieleza Wenje anayeishi Marekani.

Wenje alisema kwa kuwa mikutano imesharuhusiwa, kurejea kwao kutaongeza nguvu katika maandalizi ya uchaguzi wa mwaka 2025, kupitia majukwaa ya siasa.

Jitihada za kumpata Lema hazikuzaa matunda baada ya simu yake kutopokewa na ujumbe uliotumwa kwake haukujibiwa.

Kauli ya Chadema
Hata hivyo, akizungumza na Mwananchi jana, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu alisema kina Lissu waliondoka wakiwa na sababu za msingi, hivyo hata kurejea nchini lazima wajiridhishe kama mazingira ni salama.

“Kama chama tungetamani wote tuwepo tuijenge Chadema ili tujiandae na 2025, haya ndiyo matamanio ya chama na ushauri ni kwamba kama wanaweza kurejea warejee.

“Hatuoni tatizo lolote kwa sasa, lakini haya mambo kwa kuwa mwisho wa siku yanamkuta mtu binafsi, lazima ajiridhishe kwa nafsi yake. Lakini Chadema hatuoni tatizo lolote bahati nzuri Lissu siku nyingi alitangaza kurudi baada ya Serikali kusema hali ni salama,” alisema Mwalimu aliyekuwa mgombea mwenza wa Lissu katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Huu uandishi lengo lake nini?
 
Huu uandishi lengo lake nini?
Mkuu comte , katika magazeti ya Kiswahili ya daily, gazeti la Mwananchi ndilo gazeti the best of the best. Tujifunze kuwa na appreciation ya kazi nzuri za media yetu, hii story ya kurejea makamanda, mwandishi ameitendea haki, kwanza ile tuu kumpata trusted source wa inside CC ya Chadema is not a joke!. Kisha akawatafuta Marekani, Ubelgiji na Canada, akawatafuta viongozi wa Chadema!, just appreciate uhabarishaji huu.

Hakuna any prescribed period ya kukimbia nchi ni muda gani!, mimi leo nipo Bongo, juzi kati nilihamia Burundi, Tulioitika Wito Kuhamia Burundi, Tumefarijika Sana Kumuona Former First Lady, Mama Salma Kikwete. Kumbe Rais Akiwa Mwanamke, Nchi Haina First Lady!
Hivyo inawezekana kabisa Wenje anaweza kuwa alikuwepo Tanzania akiunguruma Sengerema October 20, 2022 na October 23 akatimkia uhamishoni Marekani. Kwenye habari, the current facts ndizo zinazo matter most, makamanda Lissu, Lema na Wenje wameikimbia nchi wanaishi uhamishoni, Mama Samia kaitisha kikao cha maridhiano na kaiponya nchi , Chadema wakasusa!, tukawashauri, Chadema, P'se, Msisusie Mkutano wa Vyama, Wasilisheni Hoja Zenu Mezani, Zitamfikia Samia, Ana Nia Njema na Nchi Hii, Mpeni Ushirikiano!. wakakaa mezani, Mama kaponya taifa, sasa makamanda waliokimbia nchi, wanarejea!, isn't this good news?.
Please lets be appreciative for the good job done the local media!.
P
 
Paskali pamoja na kujitahidi kuwa weledi jambo ninalokubaliana na wewe, kwa hili la Wenje gazeti la Mwananchi limekosea. Wamesema wazi mda ambao Wenje amekuwa nje ya nchi na kwa kuunganisha na Lema na Lissu wanajenga taswira kuwa ilitokea baada tu ya uchaguzi wa 2020. Walau ndiyo picha niliyoipata mimi binafsi. Wao kama wahabarishaji walipaswa kuleta habari iliyokamilika bila kuacha maswali mengi.
 
Limekuwa gazeti la kitapeli sn
 
Mkuu comte , katika magazeti ya Kiswahili ya daily, gazeti la Mwananchi ndilo gazeti the best of the best. Tujifunze kuwa na appreciation ya kazi nzuri za media yetu, hii story ya kurejea makamanda, mwandishi ameitendea haki, kwanza ile tuu kumpata trusted source wa inside CC ya Chadema is not a joke!. Kisha akawatafuta Marekani, Ubelgiji na Canada, akawatafuta viongozi wa Chadema!, just appreciate uhabarishaji huu.

Hakuna any prescribed period ya kukimbia nchi ni muda gani!, mimi leo nipo Bongo, juzi kati nilihamia Burundi, Tulioitika Wito Kuhamia Burundi, Tumefarijika Sana Kumuona Former First Lady, Mama Salma Kikwete. Kumbe Rais Akiwa Mwanamke, Nchi Haina First Lady!
Hivyo inawezekana kabisa Wenje anaweza kuwa alikuwepo Tanzania akiunguruma Sengerema October 20, 2022 na October 23 akatimkia uhamishoni Marekani. Kwenye habari, the current facts ndizo zinazo matter most, makamanda Lissu, Lema na Wenje wameikimbia nchi wanaishi uhamishoni, Mama Samia kaitisha kikao cha maridhiano na kaiponya nchi , Chadema wakasusa!, tukawashauri, Chadema, P'se, Msisusie Mkutano wa Vyama, Wasilisheni Hoja Zenu Mezani, Zitamfikia Samia, Ana Nia Njema na Nchi Hii, Mpeni Ushirikiano!. wakakaa mezani, Mama kaponya taifa, sasa makamanda waliokimbia nchi, wanarejea!, isn't this good news?.
Please lets be appreciative for the good job done the local media!.
P
JF ibarikiwe kwa kuwa na uvumilivu wa takataka kama hizi katika kurasa zake.
 
Back
Top Bottom