Vita kati ya Seif na Hamad Rashid yaibukia Manzese

Hofu yangu ni kwamba,siku moja Hamad Rashid yanaweza kumkuta kama yale yaliyomkuta Prof Safari.
 
Hebu dadavua;

Hhamad Rashid anafungua tawi la CUF au lake? Maana sioni mantiki ya katibu wao kupinga - wote wazanzibari, wapemba, wanaume, majina yao Hamadi; kulikoni watu hawa fujo ughaibuni?
Pia wote wameacha Mauchafu videvuni mwao. Dawa ni kuwatafutia wembe na kinyozi mahili wa kuwanyoa madevu yao ndio watapata akili.
 
Hawa wapemba vipi? Si ndio hawa hawa kila siku wanapiga makelele Zanzibar ijitenge? Wapi na wapi kufungua matawi Manzese? Si wakafungue huko Kibanda Maiti na Mchamba Wima? Maugomvi yao ya ndani wasituletee hapa! Kweli Tanganyika tamu nimeamini.

Mwl alishawaambia Uzanzibar uko tu wawapo ndani ya Tanzania wakishaodnoka huko kuna Unguja na Pemba na wakigawanyika tena utasikiwa mimi M-Wawi na Mimi M-Chake hakuna cha upemba wala uunguja dhambi ya u-selfish haijawahi zaa upendo na umoja hata siku moja the devil is a liar!
 
Kweli Tanaganyika kutamu, na huyu Hamad Rashid anaishi Mikocheni Dar es salaam.

Na ndio wako busy kutukuza uzanzibari na kutaka kuvunja muungano. Wanafikiri ukivunjika tutawaacha waendelee kuishi mikocheni!
 
Hofu yangu ni kwamba,siku moja Hamad Rashid yanaweza kumkuta kama yale yaliyomkuta Prof Safari.

Prof aliahidi kuandika kitabu kuhusu yaliyompata kule. Sijui huo mradi uliishia wapi kwani ungewafungua macho wengi kuhusu chama hiki.
 
Leo saa tatu Hamad Rashid anafungua tawi jipya la Cuf Manzese karibu na mtaa wa Kosovo.

Seif katoa order kwa Mtatiro kuzuia. (STF) watatumwa hapo

Tawi linafunguliwa saa 3 usiku? Naona ni karibu masaa 4 yamepita baada ya saa 3 asubuhi na hakuna kinachoendelea
 
hamad rashid ni mroho sana wa madaraka nakumbuka ishu KUB aliwashawishi waume zake(ccm A)wabake kanuni ziwepo kambi mbili za upinzani bungeni..tokea hapo simwamini kabisa.
kwa maalim he has picked a wrong fight with a wrong person.,lipumba ataside na maalim
hamad rashid anasahau kuwa seif ni makamu wa rais,atatumiwa wazee wa kazi mda wowote.,..maalimseif atakuwadefended na ccm A kwa nguvu zote because it is in their best interest.
 
Nyerere aliwatimua wote hao kutoka CCM kwa uroho wa madaraka na ubinafsi wa upemba.Sasa Hamad Rashid kakosa uongozi wa upinzani bungeni bila kutarajia na CCM wakashindwa kumsaidia dhidi ya Chadema sasa anaua chama chake.Dhambi ya ubaguzi hiyo!!
 
Comments kibao... habari haionyeshi nini chanzo cha ugonvi wao, nini wanagombania, kuna kosa gani limetendeka... cha zaidi haina hata mwendelezo. kama mtoa habari amepika ili kupima hisia zetu, amefanikiwa kiasi kikubwa. tumelipuka na hasira na kumaliza yote yaliyo mioyoni mwetu...

Kimtokacho mtu kinywani ndicho kilichoujaza moyo wake!
 
Nyerere aliwatimua wote hao kutoka CCM kwa uroho wa madaraka na ubinafsi wa upemba.Sasa Hamad Rashid kakosa uongozi wa upinzani bungeni bila kutarajia na CCM wakashindwa kumsaidia dhidi ya Chadema sasa anaua chama chake.Dhambi ya ubaguzi hiyo!!

Hamna atakae muweze seif na cuf "yake" na wapemba 'wake",waziri wangu wa mambo ya ndani hamad rashid naona anachemka hajui kwamba seif ni "mungu" wa wapemba...mtasikia wapamba hawamtaki tena,hamuoni mwenzake juma duni na uchakaramu wote lakini kwa seif anakua ***** tu....
 
Back
Top Bottom