Vita kati ya Seif na Hamad Rashid yaibukia Manzese

Comments kibao... habari haionyeshi nini chanzo cha ugonvi wao, nini wanagombania, kuna kosa gani limetendeka... cha zaidi haina hata mwendelezo. kama mtoa habari amepika ili kupima hisia zetu, amefanikiwa kiasi kikubwa. tumelipuka na hasira na kumaliza yote yaliyo mioyoni mwetu...

Kimtokacho mtu kinywani ndicho kilichoujaza moyo wake!

Ugomvi wao, soma MwanaHALISI la Jumatano iliyopita. Lilianika kila kitu.
 
Ukiona hivyo ni nyakati zileeeeee,wajawazito wanawachukia waume zao,usikute aliyeanzisha zogo ni wale magamba hii CUF iangalie sana kaburi hilooooooooooooooooo.
 
MAMBO si shwari ndani ya Chama cha Wananchi (CUF), baada ya mabounsa wa chama hicho kuvamia mkutano wa Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed, kufanya vurugu na kumwondoa mbunge huyo kwa nguvu.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Hamad Rashid mwenyewe, zinaeleza kuwa tukio hilo lililotokea jana kwenye ofisi ya CUF Kata ya Manzese jijini Dar es Salaam.Vurugu hizo zimekuja kipindi ambacho mbio za kuwania nafasi ya Katibu Mkuu wa chama hicho zikiwa zimeshika kasi.

Hamad Rashid

Akizungumzia vurugu hizo ambazo zilitokea saa 4:00 asubuhi, Hamad Rashid alisema yeye alifika katika eneo hilo baada ya kupata mualiko kutoka Ofisi za CUF Wilaya ya Kinondoni."Mimi nilikuja kufuatwa nyumbani na viongozi wa wilaya ili niende kutoa msaada wa viti na meza kutokana na kuwepo upungufu wa vifaa hivyo katika ofisi za eneo hilo," alisema Rashid.

Alisema kabla ya kumaliza kuzungumza na wanachama wa Kata ya Manzese, walitokea vijana wasiojulikana na kuanza kufanya vurugu zilizomlazimu aondoke katika eneo hilo.

Mbunge huyo ambaye aliwahi kuwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni katika bunge la Tisa, alisema msaada huo ni moja ya nia yake ya kutaka kutangaza nia ya kugombea nafasi ya Katibu Mkuu wa CUF.

Akawataka wanachama kuwa makini katika kipindi hiki alichoeleza kuwa chama hicho cha upinzani kimeanza kudhoofika na kinaonekana kupoteza nia ya kushika dola.

"Chama (CUF) kwa sasa kimekuwa hakina meno kutokana na kufifia kwa vuguvugu. Siasa za sasa ni ujasiri, nataka kugombea uongozi ili nionyeshe ujasiri wangu katika kukiokoa chama chetu kitoke hapa kilipo," alisema Rashid.

Alisema chama hicho kwa sasa kimekosa mvuto wa kisiasa kutokana na mfumo wa uongozi uliopo baada ya Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad kuonekana anafanya zaidi shughuli za kiserikali badala ya chama.

"Tunahitaji kufanya mabadiliko ya katiba ndani ya chama. Haiwezekani katibu mkuu ambaye ni mtendaji mkuu wa chama awe na madaraka makubwa ambayo yanamfanya ashindwe kufanya kazi ipasavyo ndani ya chama," alisema Rashid.

Aliwataka wanachama kukataa chama kufanya kazi za kinafiki kwani uamuzi unaonekana kutolewa na watu wachache na sio wanachama wote.

Mtatiro

Alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Julius Mtatiro alisema ofisi yake haikuwa na taarifa na mwaliko wa Mbunge huyo anaenda kutoa msaada katika kata ya Manzese na kama amefanya hivyo, sio ratiba ya chama ni ratiba yake binafsi.

"Hiyo taarifa ya Hamad Rashid alikuwa Manzese ndiyo kwanza naipata kwako, japokuwa hatuna utaratibu kama huo kiongozi mkubwa kama yeye atembelee kata bila taarifa. Niseme tu alichokifanya ni kinyume na taratibu za chama chetu," alisema Mtatiro.

Alisema utaratibu wa chama hicho ni kiongozi kutoa taarifa kama anaenda kutembelea sehemu fulani ili aweze kuandaliwa ulinzi katika eneo husika.

Mtatiro alisema watu waliofanya vurugu eneo la Manzese hawajatoka makao mkuu, kwani hajaona ratiba yoyote inayoonyesha kamati ya ulinzi ya CUF kama ilikuwa Manzese jana.

Alisema chama hicho kina ulinzi mpaka ngazi ya matawi, hivyo inawezeka vijana hao wakatoka katika kata husika. Walifanya hivyo baada ya kutokuwa na taarifa ya ziara yake na kugundua ameenda kinyume na utaratibu wa chama.

Lakini alipotakiwa kuzungumzia kuhusu suala la kutoa taarifa makao makuu, Hamad alisema "sio lazima kila kitu makao makuu wajue, kwani jukumu la kupeleka taarifa ya ujio wake lilikuwa ni la ngazi ya wilaya iliyomwalika.

"Sio kila kitu ninachokifanya wapate taarifa makao makuu. Mpaka sasa hivi nimeshafanya shughuli nyingi za kichama bila taarifa tatizo lao wanapenda kuyafanya mambo madogo madogo kuwa makubwa uongozi wenyewe sasa hivi haujielewi," alisema Rashid.

Awali, Kaimu Katibu wa Kata ya Manzese wa CUF Hamdani Ngurangwa alisema anashangazwa na vurugu hizo, kwani taarifa ya ujio wa kiongozi huyo katika kata yake kwa ajili ya kukabidhi viti na meza, zilifika ofisini kwake wiki moja kabla na alizipeleka katika ofisi ya mkoa.

"Taarifa hizi za Mheshimiwa Hamad Rashid alizileta mapema na tulizipeleka katika ofisi za CUF wilaya, lakini jibu tulilolipata lilitushangaza kidogo," alisema Ngurangwa.

Alisema taarifa ya kiongozi wa wilaya ilidai kuwa kutokana na agizo la makao makuu, viongozi hao hawatakiwi kushirikiana Hamad kwa jambo lolote katika ujio wake.

"Nilishindwa kutii agizo hilo kutokana na kutokuwa na barua ya maandishi kutoka makao makuu. Ndio maana nilimwalika mbunge huyo kuendelea na shughuli zake,"alisema Ngurangwa.

Hivi karibuni kumekuwepo mvutano wa chini kwa chini wa viongozi ndani ya chama hicho, ukihusishwa na kuwania nafasi ya ukatibu mkuu na uenyekiti wa chama hicho.

Baadha ya wanachama wanadai kuwa Maalim Seif na Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa ibrahim Lipumba ambaye hivi sasa yupo nje ya nchi kikazi wamekifanya chama hicho kukosa mvuto hususna Tanzania bara.

Maalim Seif baada ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa aliteuliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Hata hivyo, mabadiliko ndani ya chama hicho yanazuia na viongozi hao wa juu wakidai kuwa wanaotaka mageuzi ya uongozi wanavunja katiba ya chama.

Vuguvugu la kutaka mabadiliko ya uongozi ndani ya CUF ulipamba moto baada ya kumalizika kwa uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Igunga ambako mgombea wa chama hicho, Leonald Mahona aliambulia nafasi ya tatu, wakati katika uchaguzi mkuu uliopita alishika nafasi ya pili.

Katika uchaguzi huo chama hicho akilitumia nguvu kubwa ya fedha aikiwamo kutumia Helkopta katika kampeni zake na magari natimu kubwa ya viongozi wa juu wa chama.

Chanzo: Mwananchi
 
CUF ya kweli italetwa na wenye moyo wa dhati wa kuwatumikia wanacuf, Seif ni sehemu ya uongozi sasa wa serikali ya ccm so huwezi mwita ni mpinzani, Hamad ni mtu wa system! mkwe wa Kikwete, hana nia ya dhati ya kuiendeleza CUF, zaidi anaitafuta hiyo nafasi ili kupata prestage, ku controll mapato na zaidi kuidumisha ndoa yao na CCM, kwa ufanisi,na hata kuwezesha ndoa hiyo kupanuka zaidi.
 
Kwa Hamad Rashid huyu huyu tunayemfahamu sote bado huwa ni mwanachama hai wa Chama Cha Wananchi CUF?

Hebu nendeni taratibu vitabu vyake Mzee Mukama mkaangalie kama kweli huyu ndugu atakua amesitisha hivi karibuni kulipa ada yake ya uanachama wa kila mwaka pale sawa sawa na Mh Shibuda anavyoelezewa kufanya angali yuko CHADEMA geresha.
 
Hamad ni CCM, Seif ni CCM! wote ni wachumia Tumbo! wanatumia uelewa mdogo kisiasa walio nao wapemba kujinufaisha! Kumbuka wapemba ni watu wa dini sasa hawa wawili wanatumia turufu hiyo kuwanyonya!
 
MAMBO si shwari ndani ya Chama cha Wananchi (CUF), baada ya mabounsa wa chama hicho kuvamia mkutano wa Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed, kufanya vurugu na kumwondoa mbunge huyo kwa nguvu.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Hamad Rashid mwenyewe, zinaeleza kuwa tukio hilo lililotokea jana kwenye ofisi ya CUF Kata ya Manzese jijini Dar es Salaam.Vurugu hizo zimekuja kipindi ambacho mbio za kuwania nafasi ya Katibu Mkuu wa chama hicho zikiwa zimeshika kasi.

Hamad Rashid
Akizungumzia vurugu hizo ambazo zilitokea saa 4:00 asubuhi, Hamad Rashid alisema yeye alifika katika eneo hilo baada ya kupata mualiko kutoka Ofisi za CUF Wilaya ya Kinondoni.“Mimi nilikuja kufuatwa nyumbani na viongozi wa wilaya ili niende kutoa msaada wa viti na meza kutokana na kuwepo upungufu wa vifaa hivyo katika ofisi za eneo hilo,” alisema Rashid.

Alisema kabla ya kumaliza kuzungumza na wanachama wa Kata ya Manzese, walitokea vijana wasiojulikana na kuanza kufanya vurugu zilizomlazimu aondoke katika eneo hilo.

Mbunge huyo ambaye aliwahi kuwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni katika bunge la Tisa, alisema msaada huo ni moja ya nia yake ya kutaka kutangaza nia ya kugombea nafasi ya Katibu Mkuu wa CUF.

Akawataka wanachama kuwa makini katika kipindi hiki alichoeleza kuwa chama hicho cha upinzani kimeanza kudhoofika na kinaonekana kupoteza nia ya kushika dola.

“Chama (CUF) kwa sasa kimekuwa hakina meno kutokana na kufifia kwa vuguvugu. Siasa za sasa ni ujasiri, nataka kugombea uongozi ili nionyeshe ujasiri wangu katika kukiokoa chama chetu kitoke hapa kilipo,” alisema Rashid.

Alisema chama hicho kwa sasa kimekosa mvuto wa kisiasa kutokana na mfumo wa uongozi uliopo baada ya Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad kuonekana anafanya zaidi shughuli za kiserikali badala ya chama.

“Tunahitaji kufanya mabadiliko ya katiba ndani ya chama. Haiwezekani katibu mkuu ambaye ni mtendaji mkuu wa chama awe na madaraka makubwa ambayo yanamfanya ashindwe kufanya kazi ipasavyo ndani ya chama,” alisema Rashid.

Aliwataka wanachama kukataa chama kufanya kazi za kinafiki kwani uamuzi unaonekana kutolewa na watu wachache na sio wanachama wote.

Mtatiro
Alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Julius Mtatiro alisema ofisi yake haikuwa na taarifa na mwaliko wa Mbunge huyo anaenda kutoa msaada katika kata ya Manzese na kama amefanya hivyo, sio ratiba ya chama ni ratiba yake binafsi.

“Hiyo taarifa ya Hamad Rashid alikuwa Manzese ndiyo kwanza naipata kwako, japokuwa hatuna utaratibu kama huo kiongozi mkubwa kama yeye atembelee kata bila taarifa. Niseme tu alichokifanya ni kinyume na taratibu za chama chetu,” alisema Mtatiro.

Alisema utaratibu wa chama hicho ni kiongozi kutoa taarifa kama anaenda kutembelea sehemu fulani ili aweze kuandaliwa ulinzi katika eneo husika.

Mtatiro alisema watu waliofanya vurugu eneo la Manzese hawajatoka makao mkuu, kwani hajaona ratiba yoyote inayoonyesha kamati ya ulinzi ya CUF kama ilikuwa Manzese jana.

Alisema chama hicho kina ulinzi mpaka ngazi ya matawi, hivyo inawezeka vijana hao wakatoka katika kata husika. Walifanya hivyo baada ya kutokuwa na taarifa ya ziara yake na kugundua ameenda kinyume na utaratibu wa chama.

Lakini alipotakiwa kuzungumzia kuhusu suala la kutoa taarifa makao makuu, Hamad alisema "sio lazima kila kitu makao makuu wajue, kwani jukumu la kupeleka taarifa ya ujio wake lilikuwa ni la ngazi ya wilaya iliyomwalika.

“Sio kila kitu ninachokifanya wapate taarifa makao makuu. Mpaka sasa hivi nimeshafanya shughuli nyingi za kichama bila taarifa tatizo lao wanapenda kuyafanya mambo madogo madogo kuwa makubwa uongozi wenyewe sasa hivi haujielewi,” alisema Rashid.

Awali, Kaimu Katibu wa Kata ya Manzese wa CUF Hamdani Ngurangwa alisema anashangazwa na vurugu hizo, kwani taarifa ya ujio wa kiongozi huyo katika kata yake kwa ajili ya kukabidhi viti na meza, zilifika ofisini kwake wiki moja kabla na alizipeleka katika ofisi ya mkoa.

“Taarifa hizi za Mheshimiwa Hamad Rashid alizileta mapema na tulizipeleka katika ofisi za CUF wilaya, lakini jibu tulilolipata lilitushangaza kidogo,” alisema Ngurangwa.

Alisema taarifa ya kiongozi wa wilaya ilidai kuwa kutokana na agizo la makao makuu, viongozi hao hawatakiwi kushirikiana Hamad kwa jambo lolote katika ujio wake.

"Nilishindwa kutii agizo hilo kutokana na kutokuwa na barua ya maandishi kutoka makao makuu. Ndio maana nilimwalika mbunge huyo kuendelea na shughuli zake,"alisema Ngurangwa.

Hivi karibuni kumekuwepo mvutano wa chini kwa chini wa viongozi ndani ya chama hicho, ukihusishwa na kuwania nafasi ya ukatibu mkuu na uenyekiti wa chama hicho.

Baadha ya wanachama wanadai kuwa Maalim Seif na Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa ibrahim Lipumba ambaye hivi sasa yupo nje ya nchi kikazi wamekifanya chama hicho kukosa mvuto hususna Tanzania bara.

Maalim Seif baada ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa aliteuliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Hata hivyo, mabadiliko ndani ya chama hicho yanazuia na viongozi hao wa juu wakidai kuwa wanaotaka mageuzi ya uongozi wanavunja katiba ya chama.

Vuguvugu la kutaka mabadiliko ya uongozi ndani ya CUF ulipamba moto baada ya kumalizika kwa uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Igunga ambako mgombea wa chama hicho, Leonald Mahona aliambulia nafasi ya tatu, wakati katika uchaguzi mkuu uliopita alishika nafasi ya pili.

Katika uchaguzi huo chama hicho akilitumia nguvu kubwa ya fedha aikiwamo kutumia Helkopta katika kampeni zake na magari natimu kubwa ya viongozi wa juu wa chama

Source:
CUF kwazidi kuchafuka
 
Ina maana ngangari kinoma tunaweza tusiisikie tena au naweweseka!
 
kuwa kiongozi wa serikali sidhani kama ni sababu ya kushindwa kukiongoza chama Hamadi aseme jambo jingine labda kuwa wamekaa muda mrefu ktk nafasi hizo sasa yanahitajika maono mapya
 
Afadhali huu moto unawaka kwao ndani kwa ndani, isingelikuwa hivyo wangesema wamefanyiwa fujo na Chadema.
 
Mie nauliza tu -- hivi kwa nini hali ya kudhoofika kwa CUF huku Bara kushikiwe bango na Mpemba -- Hamad rashid, badala ya watu kama Mtatiro au Lipumba?

Angalau Mtatiro aliwahi kutamka hadharani (baada ya Igunga) kwamba CUF imeshuka sana umaarufu. Lakini sijamsikia Lipumba akitamka hivyo hata siku moja.
 
Seif hamad aliwasaliti wenzie sasa yaelekea anatafuta mabaunsa kubaki madarakani....................huhitaji ratiba kutembelea wanachama wako..........
 
Waliposema CUF si chama cha upinzani hata Hamad alihamaki. Sasa anaanza kuona mwenyewe kuwa kwa mwendo huu CUF ni CCM B!

Eti mwenyekiti Lipumba yuko nje (US) kwa ziara ya miezi 6 ya kikazi!!!! Jamani huyu akipata urais si atavunja hata rekodi ya mzee wa safari??????

Per Diem za miezi 6 si mchezo, ndiyo maana Hamad analalamika wilayani kutopelekewa mgao wa posho!
 
nina mashaka na Hamad Rashid na kundi lake la kina Mnyaa huenda wana mpango wa siri wa kuivuruga CUF.CUF wasipochukua maamuzi magumu basi hawa watu wenye uchu wa madaraka watakisambaratisha chama.Lipumba arudi haraka kuja kuokoa jahazi.
 
Back
Top Bottom