Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Ushamba mzigo .nilipanda ndege nikaumwa na mkojo nafika chooni sioni shimo aisee nilipagawa .nilisoma Kila kitu ndani Hadi nikaona kitufe Cha kubinya ndio daaah choo kinafunguka.
duh kweli ushamba ni mzigo kwangu..kwahiyo mavi yanabaki kwenye ndege au yanadondoka chini halafu yana peperushwa na upepo? Yani sielewi hata vyoo vya treni na meli vipoje, aise ushamba ni mzigo kweli...
 
Ndege haizoeleki
Kuna siku rubani sijui ndege kama ilimzidi uwezo
Tulitua uwanja wa kisongo ule ni kama aliiachia au ilimponyoka hv kilisikika kishindo kikubwa puuuu
Nilipaniki roho mkononi
Pole boss
Uwanja wa Arusha ni changamoto kwa marubani wengi kwa namna topography ilivyo
 
duh kweli ushamba ni mzigo kwangu..kwahiyo mavi yanabaki kwenye ndege au yanadondoka chini halafu yana peperushwa na upepo? Yani sielewi hata vyoo vya treni na meli vipoje, aise ushamba ni mzigo kweli...
Kwenye ndege kuna tank la kuhifadhia uchafu(kinyesi) ndege ikitua huwa wanaenda kuumwaga.

Treni mara nyingi inapita porini unakunya kinadondoka chini. Na hairuhusiwi kutumia choo cha treni kama imesimama, kwenye meli sifahamu utaratibu ukoje
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom