Viongozi wetu walikotufikisha hapa, katiba ya Jamhuri ya Muungano hawakuijua?

Paul J

Senior Member
Oct 25, 2010
193
62
Ujenzi wa
Ujamaa na
Kujitegemea
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
Sheria Na.4
ya 1992 ib.6


9. Lengo la Katiba hii ni kuwezesha ujenzi wa Jamhuri ya
Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar au wa
chochote kati ya vyombo vyake na udugu na amani kutokana na
kufuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, amabyo inasisitiza
utekelezaji wa misingi ya kijamaa kwa kuzingatia mazingira
yaliyomo katika Jamhuri ya Muungano. Kwa hiyo, Mamlaka ya
Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na
shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha-

(a) kwamba utu na haki nyinginezo zote za binadamu
zinaheshimiwa na kuthaminiwa;

(b) kwamba sheria za nchi zinalindwa na kutekelezwa;

(c) kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia
ambazo zitahakikisha kwamba utajiri wa Taifa
unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa
manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia
mtu kumyonya mtu mwingine;

(d) kwamba maendeleo ya uchumi wa Taifa yanakuzwa
na kupangwa kwa ulinganifu na kwa pamoja;

(e) kwamba kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi
anafanya kazi, na kazi maana yake ni shughuli
yoyote ya halali inayompatia mtu riziki yake;

(f) kwamba heshima ya binadamu inahifadhiwa na
kudumishwa kwa kufuata Kanuni za Tangazo la
Dunia kuhusu Haki za Binadamu;

(g) kwamba Serikali na vyombo vyake vyote vya umma
vinatoa nafasi zilizo sawa kwa raia wote, wake kwa
waume, bila ya kujali rangi, kabila, dini au hali ya
mtu;

(h) kwamba aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi,
rushwa, uonevu au upendeleo zinaondolewa nchini;

(i) kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo
maendeleo ya wananchi na hasa zaidi
yanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondosha
umaskini, ujinga na maradhi;

(j) kwamba shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njia
zinazoweza kusababisha ulimbikizaji wa mali au njia
kuu za uchumi katika mamlaka ya watu wachache
binafsi;

(k) kwamba nchi inatawaliwa kwa kufuata misingi ya
demokrasia na ujamaa.
 
What is your opinion my dear? this written words have got no inspiration that may force someone to follow these rules. See what is written in religious books yet people can not possibly abide with those words!!!

Words has got nothing to do compared to actions!!! people swear in court, in marriages, etc yet they dont fulfill their vows!!!

Soma mstari wa mwisho kabisa............ HAKUNA DEMOKRASIA KWENYE UJAMAA!!! simply that sentence nullifies all other sentences.. that was just a passing time!!! nothing has been positively more than damages!

Unataka nikuambie kitu!!!

Mapinduzi ya kweli yanatakiwa yaanze na kukataa ideology zote za Nyerere na kujenga taifa jipya, kupiga kelele CCM na kumlinda muasisi wake ni kucheza na kinyesi cha nguruwe huku ukiamini cha mbwa hakinuki!!
 
Back
Top Bottom