Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

...mlisema kuwa Kikwete ni chaguo la Mungu mwaka 2005 wakati wa kampeni, kwa hiyo apewe kura, leo hii mnatamka vingine tena!
Hii hasa ndio sababu ya kukwepa kumwambia ukweli na badala yake anasema wasaidizi ndo wabovu... anaogopa maneno yao yasiwarudie!

Nyoosha msitari Baba Askofu; angalau waTanzania tutakuona wa maana zaidi kwa kupoza machungu ya uchafu wenu wa 2005.
======================
 
Huyu msaidizi wa askofu naye ana wazimu. Nani alisema kazi ya urais ni nyepesi? Kama hawezi kuwashughulikia ameshindwa kazi ajiuzulu.
 
Ndiyo upumbavu ule ule wa REDET "rais anapendwa ila baraza la mawaziri linamuangusha" ujing mtupu.
 
Utaelemewaje na mafisadi wakati wewe ni Ras wa nchi na katiba imekupa uwezo mkubwa katika kufanya maamuzi yako na pia vyombo vyote vya dola viko chini yako!? :confused:

Hajaelemewa na mafisadi, bali anawalinda kwa sababu na wao wanajua mabaya yake, lakini akitaka kuwashughulikia uwezo anao, nguvu anazo na sababu anazo pia Watanzania watamuunga mkono katika vita hivyo dhidi ya mafisadi.
 
Kiongozi wa dini unapokuwa mnafiki kiasi hiki ujue pia unafiki huohuo ndo unaomfanya JK aelemewe na hao watu wake.Kama kiongozi wa dini unashindwa kumwambia JK ukweli,ajue na JK ndivyo anavyoshindwa kuwaambia ukweli watu wake.
 
Nyangumi,

Hiyo inaitwa "vicious cycle of hypocrisy".Yaani ni kama tume ya kuchunguza rushwa imebainika kuwa plagued na rushwa.

Kama mpaka Askofu ana fail mtihani wa kusema ukweli, Quis custodiet ipsos custodes?
 
hao mafisadi ni wakisto au waislam?

Nadhani Mafisadi dini yao ni UFISADI, wangekuwa wanafuata maadili ya dini kama za Kikristo au Kiislamu wasingekuwa wanaendeleza dhuluma kwa Watanzania kwa kasi hii, hawa watu ni Majambazi.

Viongozi wa dini za Kiislamu na Kikristo wana nafasi kubwa kabisa ya kupigia makelele ujambazi huu unaoendelea pale Tanzania lakini kama unavyojua Bongo kumejaa Masheikh Ubwabwa na Maaskofu Divai ambao wanachojua ni kujaza matumbo yao na kujipendekeza kwa viongozi wa Serikali.
 
Nadhani Mafisadi dini yao ni UFISADI, wangekuwa wanafuata maadili ya dini kama za Kikristo au Kiislamu wasingekuwa wanaendeleza dhuluma kwa Watanzania kwa kasi hii, hawa watu ni Majambazi.

Viongozi wa dini za Kiislamu na Kikristo wana nafasi kubwa kabisa ya kupigia makelele ujambazi huu unaoendelea pale Tanzania lakini kama unavyojua Bongo kumejaa Masheikh Ubwabwa na Maaskofu Divai ambao wanachojua ni kujaza matumbo yao na kujipendekeza kwa viongozi wa Serikali.

Kweli kabisa mkuu, Ukristo na Uislamu wa kweli hauruhusu mtu kufanya dhuluma, wizi ama uonevu wa namna yoyote ile. Dini hizi zote mbili zinakataza uchafu wa namna hii, hawa mafisadi wanafanya haya kwa uchafu wao tu, na huenda wanatoa sadaka ama zaka kubwa tu makanisani na misikitini ambazo ndizo zinawapumbaza akina Kilaini na wenzake!
Very sad indeed!
 
Mwanzoni nilisoma haraka haraka nikapuuzia. Lakini baada ya kusoma kilichoandikwa hapo chini, inabidi nimpe shukrani Askofu kwa maneno yake ya Busara.

Ametoa maoni yake kwa ufasaha sana, na inabidi tujifunze kutoka kwake na kuona kama jee hii ndiyo nia nyingine ya kuleta mabadiliko badala ya ile ya kawaida tunayopendelea ya Upanga!


Aristariko Konga
Desemba 12, 2007

SUALA la ufisadi, kula mali za umma na mikataba isiyoeleweka, ni gumzo hapa nchini hivi sasa. Hakuna ubishi tena, kwamba kuna mtu ambaye anaweza kusema mambo yako shwari. Amkani si shwari tena. Wiki iliyopita, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Method Kilaini, alitoa maoni yake binafsi, kuhusu mambo hayo. Hebu fuatilia.
26.jpg

Askofu Methodius Kilaini

“Ninakumbuka kuwa tulianza kulizungumzia suala la ufisadi tangu miaka ya 1990. Suala zima hili linahusu kula mali ya umma, kuwa na mikataba yenye mashaka na kila aina ya uovu katika kuendesha serikali yetu.

“Kwa hiyo, suala la ufisadi halikuanza hivi leo. Sisi tulianza kulijadili muda mrefu. Kelele zinazosikika hivi sasa zinaonyesha kuwa sasa tatizo limekuwa kubwa zaidi, kuliko wakati ule.

Tunao wajibu wa kuendelea kulipiga vita suala hili, ingawa vita yake ni ngumu sana.

“Kwa bahati mbaya sana tulipoachana na ujamaa, watu kadhaa, tena wachache wetu, wakajiingiza kwenye ufisadi. Mwanzo tulizungumzia rushwa ndogo ndogo, lakini hivi sasa imeshamiri rushwa kubwa, tena inayohusisha watu wachache… Watu wachache, rushwa kubwa.”

Askofu Kilaini anasema kwamba
wakati wa uongozi wa Awamu ya Tatu, chini ya Rais Benjamin Mkapa, kwa kufuata falsafa yake ya Ukweli na Uwazi, nchi iliingia katika ufisadi wa kimataifa, yaani rushwa kubwa.

Kwamba, wawekezaji kutoka nje, wanapoingia hapa nchini, wanakuwa na lengo la kutafuta masoko ya vitu vyao.

Kwa hiyo hata wanapoingia mikataba na nchi, basi wanakuwa na lengo la kujinufaisha kwa kutafuta masoko yao.

“Sasa, unaposema kwamba ufisadi wa kimataifa una maana kwamba serikali za nje zinaingia kutafuta masoko hapa kwetu. Wanaingia mikataba na sisi, na mikataba yenyewe ina mashaka mashaka kwa upande wetu.”

Askofu anasema kwamba vita dhidi ya
ufisadi wa kimataifa inakuwa ngumu sana kwa sababu utiaji wa mikataba yenyewe una usiri mkubwa, kiasi kwamba hata wale ambao wanatarajiwa kuwa wa kwanza kuupiga vita, wanashindwa kupata taarifa mapema kutokana na kificho hicho.

“Wale ambao wanapaswa kuwa wa kwanza kupiga vita suala hili, wanashindwa kupata taarifa na hata wanapokuja kuzipata, wanakuwa wamechelewa sana na mambo yamekwisha kufanyika na kuleta athari.”

Mara kadhaa wabunge wamekuwa wakilalamika ndani ya Bunge, kwamba mikataba hiyo ingekuwa inawekwa wazi mbele yao,
lakini upande wa serikali umekuwa ukipinga dhana hiyo kwa madai kuwa mambo mengi ni ya siri baina ya wale wanaoingia kwenye makubaliano ya mkataba.

“Lakini pia mambo ya ufisadi yana usiri mkubwa kwa kuangalia mikataba ya makubaliano, kiasi kwamba wanaopaswa kukemea ubovu wa mikataba hii hawapati habari wala nafasi kutokana na usiri huu.

“Kutokana na usiri huu, kazi ya kupigana vita na ufisadi inakuwa ngumu sana.
Hapa ndipo dhamira ya Rais (Jakaya) Kikwete inakuwa vigumu kutekelezeka,” anasema Askofu Kilaini.

Askofu Kilaini ni Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, la Kanisa Katoliki. Yeye ndiye namba mbili wa Mkuu wa Jimbo hilo, Polycarp Kardinali Pengo.

Kilaini anasema kwamba,
ufisadi huu wa kimataifa (rushwa kubwa) unalindwa sana na viongozi walioko madarakani, kiasi kwamba mtu mdogo anapokuwa na ari ya kulinda maslahi ya taifa, hushurutishwa na wakubwa wake kwamba anapaswa kunyamaza na kuwasilikiza wao tu.

“Ufisadi wa kimataifa ambao ndio unaolisumbua taifa hivi sasa, unalindwa sana na walioko madarakani. Mtu akijaribu kuingilia kati anaambiwa ‘nyamaza’.

“Kwa hiyo serikali yetu ina kazi kubwa sana, na hasa Rais wetu Kikwete, ambaye ameonyesha moyo wa kutaka kupambana na tatizo hilo… Ana kazi kubwa kwa sababu kuna watu wanashirikiana na wawekezaji hawa wa nje ili kujinufaisha wao. Ni kazi ngumu sana kwake.”

Askofu Kilaini anasema kwamba pamoja na kwamba ufisadi wa kimataifa ulianza wakati wa Awamu ya Tatu, bado Mkapa alijitahidi kufungua milango ya uwekezaji kutoka nje.

Kwamba wawekezaji wa nje wanapokuja na vitu vyao pamoja na fedha, hutumia fedha hizo kuwanunua viongozi walioko madarakani, ambao ndio huingia katika duru za kusaini mikataba. Hapo ndipo hukubaliana na wageni hao, na kulisaliti taifa na watu wake.

“Wanakuja na vitu vyao na mapesa mengi sana.

Sasa wanapofika hapa wanayatumia mapesa haya kuwapa viongozi walioko madarakani. Viongozi wa aina hii, ambao ndio walipaswa kumsaidia Rais Kikwete, ndio hao hao wanakuwa wa kwanza kumkwamisha.

“Hao ndio wanaofanya dhamira nzuri ya Rais Kikwete, ya kupambana na rushwa hii kubwa, iwe ngumu kuitekeleza. Inabakia tu kusikia kelele za rushwa kwenye mahakama zetu hizi ndogo, ikiwahusu watu wadogo… Hii haitoshi.

“Tunashukuru
kwamba Awamu ya Nne, chini ya Rais Kikwete, imeunda Kamati ya Kuchunguza Mikataba ya Madini. Tunashukuru kwamba kamati hiyo ina watu kutoka upinzani. Unajua kunapokuwa na watu wa upinzani kwenye kamati kama hiyo inakuwa rahisi kwetu sisi kujua kinachofanyika. Wanatuambia kinachofanyika.

“Kwa hiyo, kama ndani ya kamati (ya kuchunguza mikataba ya madini) kuna watu wanaotaka kuchukua fedha kutoka kwa wawekezaji hawa wa nje, ili mambo yafichwe, basi kwa vyovyote vile watashindwa. Walau kuna uwezo sasa kuuliza na kuambiwa kinachoendelea ndani ya kamati.”

Askofu Kilaini anasema kwamba wabunge wana wajibu wa kutetea maslahi ya taifa, na hasa kupiga vita ufisadi huu wa kimataifa. Kwamba wakilindana, mwishowe wajue nchi ikizama na wao watakuwamo.


“Wabunge wajue kuwa tukizama, basi tunazama wote… Wao wakilindana tutatokomea wote… Tunawasifu wale wote wanaokuja juu pale maslahi yetu yanapokuwa hatarini. Wale ambao bado wana ‘usisi’ waache na wawaige wenzao.

“
Rais Kikwete ameonyesha moyo wa kukubali kuulizwa maswali magumu na kukubali kutafuta majibu ya maswali haya magumu. Kwa mfano, sisi wengine hatukutegemea kuona (Zitto Zuberi) Kabwe, ambaye alikuwa amepewa adhabu na Bunge, anakuwa kwenye Kamati ya Madini. Hatukutarajia kabisa.”

Zitto Kabwe, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, alisimamishwa ubunge Agosti mwaka huu, baada ya kuwasilisha hoja ya kutaka kupewa ukweli kuhusu mkataba wa uchimbaji madini eneo la Buzwagi, kanda ya Ziwa, ambao ulisainiwa London, Uingereza.

Baada ya hoja yake hiyo, iliibuka hoja nyingine inayopingana na hiyo, ikidai kuwa Zitto alikuwa akilidanganya Bunge, na hivyo kubebeshwa adhabu hiyo hadi Januari, mwakani. Hata hivyo, Askofu Kilaini anasema kwamba vyama vya upinzani vinao wajibu wa kusema ukweli pale panapostahili, badala ya kutafuta hoja za kupinga tu.
“Vyama vya upinzani visijione kuwa vinatafuta hoja za kupinga tu. Wapinzani wanao wajibu pia wa kutafuta suluhu wakati matatizo yanapojitokeza. Wawe na uzalendo. Waweke mbele uzalendo kila yanapokuja maslahi ya kitaifa.”
 
Ingepatikana statement ya Askofu ingesaidia sana, maana article ya kwanza inaonyesha Askofu yuko na rais wakati article ya pili jamaa amefanya uchambuzi wake zaidi kwa kutumia msingi wa maneno ya Askofu.

Sasa kuondoa spin ingepatikana statement aliyotoa Askofu.According to the first article he went short of condemning the whole government, in the process absolving the president REDET style (my beef).The second piece is more of analysis and maonyo/ kuamshana than reporting.
 
Mwanzoni nilisoma haraka haraka nikapuuzia. Lakini baada ya kusoma kilichoandikwa hapo chini, inabidi nimpe shukrani Askofu kwa maneno yake ya Busara.

Ametoa maoni yake kwa ufasaha sana, na inabidi tujifunze kutoka kwake na kuona kama jee hii ndiyo nia nyingine ya kuleta mabadiliko badala ya ile ya kawaida tunayopendelea ya Upanga!


Aristariko Konga​
Desemba 12, 2007

SUALA la ufisadi, kula mali za umma na mikataba isiyoeleweka, ni gumzo hapa nchini hivi sasa. Hakuna ubishi tena, kwamba kuna mtu ambaye anaweza kusema mambo yako shwari. Amkani si shwari tena. Wiki iliyopita, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Method Kilaini, alitoa maoni yake binafsi, kuhusu mambo hayo. Hebu fuatilia.
26.jpg

Askofu Methodius Kilaini


“Ninakumbuka kuwa tulianza kulizungumzia suala la ufisadi tangu miaka ya 1990. Suala zima hili linahusu kula mali ya umma, kuwa na mikataba yenye mashaka na kila aina ya uovu katika kuendesha serikali yetu.
“Kwa hiyo, suala la ufisadi halikuanza hivi leo. Sisi tulianza kulijadili muda mrefu. Kelele zinazosikika hivi sasa zinaonyesha kuwa sasa tatizo limekuwa kubwa zaidi, kuliko wakati ule.
Tunao wajibu wa kuendelea kulipiga vita suala hili, ingawa vita yake ni ngumu sana.
“Kwa bahati mbaya sana tulipoachana na ujamaa, watu kadhaa, tena wachache wetu, wakajiingiza kwenye ufisadi. Mwanzo tulizungumzia rushwa ndogo ndogo, lakini hivi sasa imeshamiri rushwa kubwa, tena inayohusisha watu wachache… Watu wachache, rushwa kubwa.”
Askofu Kilaini anasema kwamba wakati wa uongozi wa Awamu ya Tatu, chini ya Rais Benjamin Mkapa, kwa kufuata falsafa yake ya Ukweli na Uwazi, nchi iliingia katika ufisadi wa kimataifa, yaani rushwa kubwa.
Kwamba, wawekezaji kutoka nje, wanapoingia hapa nchini, wanakuwa na lengo la kutafuta masoko ya vitu vyao.
Kwa hiyo hata wanapoingia mikataba na nchi, basi wanakuwa na lengo la kujinufaisha kwa kutafuta masoko yao.
“Sasa, unaposema kwamba ufisadi wa kimataifa una maana kwamba serikali za nje zinaingia kutafuta masoko hapa kwetu. Wanaingia mikataba na sisi, na mikataba yenyewe ina mashaka mashaka kwa upande wetu.”
Askofu anasema kwamba vita dhidi ya ufisadi wa kimataifa inakuwa ngumu sana kwa sababu utiaji wa mikataba yenyewe una usiri mkubwa, kiasi kwamba hata wale ambao wanatarajiwa kuwa wa kwanza kuupiga vita, wanashindwa kupata taarifa mapema kutokana na kificho hicho.
“Wale ambao wanapaswa kuwa wa kwanza kupiga vita suala hili, wanashindwa kupata taarifa na hata wanapokuja kuzipata, wanakuwa wamechelewa sana na mambo yamekwisha kufanyika na kuleta athari.”
Mara kadhaa wabunge wamekuwa wakilalamika ndani ya Bunge, kwamba mikataba hiyo ingekuwa inawekwa wazi mbele yao, lakini upande wa serikali umekuwa ukipinga dhana hiyo kwa madai kuwa mambo mengi ni ya siri baina ya wale wanaoingia kwenye makubaliano ya mkataba.
“Lakini pia mambo ya ufisadi yana usiri mkubwa kwa kuangalia mikataba ya makubaliano, kiasi kwamba wanaopaswa kukemea ubovu wa mikataba hii hawapati habari wala nafasi kutokana na usiri huu.
“Kutokana na usiri huu, kazi ya kupigana vita na ufisadi inakuwa ngumu sana. Hapa ndipo dhamira ya Rais (Jakaya) Kikwete inakuwa vigumu kutekelezeka,” anasema Askofu Kilaini.
Askofu Kilaini ni Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, la Kanisa Katoliki. Yeye ndiye namba mbili wa Mkuu wa Jimbo hilo, Polycarp Kardinali Pengo.
Kilaini anasema kwamba, ufisadi huu wa kimataifa (rushwa kubwa) unalindwa sana na viongozi walioko madarakani, kiasi kwamba mtu mdogo anapokuwa na ari ya kulinda maslahi ya taifa, hushurutishwa na wakubwa wake kwamba anapaswa kunyamaza na kuwasilikiza wao tu.
“Ufisadi wa kimataifa ambao ndio unaolisumbua taifa hivi sasa, unalindwa sana na walioko madarakani. Mtu akijaribu kuingilia kati anaambiwa ‘nyamaza’.
“Kwa hiyo serikali yetu ina kazi kubwa sana, na hasa Rais wetu Kikwete, ambaye ameonyesha moyo wa kutaka kupambana na tatizo hilo… Ana kazi kubwa kwa sababu kuna watu wanashirikiana na wawekezaji hawa wa nje ili kujinufaisha wao. Ni kazi ngumu sana kwake.”
Askofu Kilaini anasema kwamba pamoja na kwamba ufisadi wa kimataifa ulianza wakati wa Awamu ya Tatu, bado Mkapa alijitahidi kufungua milango ya uwekezaji kutoka nje.
Kwamba wawekezaji wa nje wanapokuja na vitu vyao pamoja na fedha, hutumia fedha hizo kuwanunua viongozi walioko madarakani, ambao ndio huingia katika duru za kusaini mikataba. Hapo ndipo hukubaliana na wageni hao, na kulisaliti taifa na watu wake.
“Wanakuja na vitu vyao na mapesa mengi sana.
Sasa wanapofika hapa wanayatumia mapesa haya kuwapa viongozi walioko madarakani. Viongozi wa aina hii, ambao ndio walipaswa kumsaidia Rais Kikwete, ndio hao hao wanakuwa wa kwanza kumkwamisha.
“Hao ndio wanaofanya dhamira nzuri ya Rais Kikwete, ya kupambana na rushwa hii kubwa, iwe ngumu kuitekeleza. Inabakia tu kusikia kelele za rushwa kwenye mahakama zetu hizi ndogo, ikiwahusu watu wadogo… Hii haitoshi.
“Tunashukuru kwamba Awamu ya Nne, chini ya Rais Kikwete, imeunda Kamati ya Kuchunguza Mikataba ya Madini. Tunashukuru kwamba kamati hiyo ina watu kutoka upinzani. Unajua kunapokuwa na watu wa upinzani kwenye kamati kama hiyo inakuwa rahisi kwetu sisi kujua kinachofanyika. Wanatuambia kinachofanyika.
“Kwa hiyo, kama ndani ya kamati (ya kuchunguza mikataba ya madini) kuna watu wanaotaka kuchukua fedha kutoka kwa wawekezaji hawa wa nje, ili mambo yafichwe, basi kwa vyovyote vile watashindwa. Walau kuna uwezo sasa kuuliza na kuambiwa kinachoendelea ndani ya kamati.”
Askofu Kilaini anasema kwamba wabunge wana wajibu wa kutetea maslahi ya taifa, na hasa kupiga vita ufisadi huu wa kimataifa. Kwamba wakilindana, mwishowe wajue nchi ikizama na wao watakuwamo.
“Wabunge wajue kuwa tukizama, basi tunazama wote… Wao wakilindana tutatokomea wote… Tunawasifu wale wote wanaokuja juu pale maslahi yetu yanapokuwa hatarini. Wale ambao bado wana ‘usisi’ waache na wawaige wenzao.
“Rais Kikwete ameonyesha moyo wa kukubali kuulizwa maswali magumu na kukubali kutafuta majibu ya maswali haya magumu. Kwa mfano, sisi wengine hatukutegemea kuona (Zitto Zuberi) Kabwe, ambaye alikuwa amepewa adhabu na Bunge, anakuwa kwenye Kamati ya Madini. Hatukutarajia kabisa.”
Zitto Kabwe, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, alisimamishwa ubunge Agosti mwaka huu, baada ya kuwasilisha hoja ya kutaka kupewa ukweli kuhusu mkataba wa uchimbaji madini eneo la Buzwagi, kanda ya Ziwa, ambao ulisainiwa London, Uingereza.
Baada ya hoja yake hiyo, iliibuka hoja nyingine inayopingana na hiyo, ikidai kuwa Zitto alikuwa akilidanganya Bunge, na hivyo kubebeshwa adhabu hiyo hadi Januari, mwakani. Hata hivyo, Askofu Kilaini anasema kwamba vyama vya upinzani vinao wajibu wa kusema ukweli pale panapostahili, badala ya kutafuta hoja za kupinga tu. “Vyama vya upinzani visijione kuwa vinatafuta hoja za kupinga tu. Wapinzani wanao wajibu pia wa kutafuta suluhu wakati matatizo yanapojitokeza. Wawe na uzalendo. Waweke mbele uzalendo kila yanapokuja maslahi ya kitaifa.”
NDG, zangu WATANZANIA,WAZALENDO, nacho jiuliza nyie mliopo mjini mtusaidie kujua maana HALISI ya FISADI kwani kwa sasa ukichukulia tafsiri ya SLAA na wenzie ASKOFU amepotea njia si amini anapotafsiri mafisadi kwa mtazamo huo bado anatumia DHANA ya SLAA ambayo si sahihi kabisa.

kILAINI kama kiongozi alicho ongea ni Fikra na Hisia Tupu Ninge muelewa kama angewataja hao mafisadi wanaomuelemea RAIS kikwete au nyie mnao unga mkono mawazo haya watajani wale alio wataja SLAA we still have a lot of qns to ask, siku hizi imekua ni utaratibu wa mtu just to come ktk public na kuanza kusema MAFISADI MAFISADI Guys lets be more objective KILAINI kama anawajua awataje so that tuwajadili kama kweli ni mafisadi au la isiwe tuna ongozwa na HISIA zaidi KULIKO FACTS.

Rev, KUSHOKA anadai tujifunze tujifunze kipi kuongozwa zaidi na hisia au DHANA? kilaini ameshindwa kuwataja so that tuone kama kweli ni mafisadi au ni mawazo ya watu.

Kwahiyo kama kilaini anawajua awataje au wazalendo humu ndani tutajieni hao mafisadi bcs now adays kilakiyu ni mafisadi au kuna ENEO DAR linaitwa mafisadi? huku sis hatujui vijijini?Hapa kwetu kijiji cha BUGANGUZI wilaya ya MULEBA kuna jamaa alikua na kibanda then akawa mkulima mzuri wa kahawa after 3 yrs akajenga nyumba nzuri na akanunua pickup juzi kilabuni nae anaitwa FISADI najiuliza ukivuka kutoka ktk umasikini wa mlo mmoja akaenda ktk umasikini wa milo mitatu basi wewe ni fisadi?
Thats why nasema tuwe objective naona wengine wanaitwa mafisadi bcs wamesaini mikataba mibovu, why wasiitwe WAJINGA?HAWANA ELIMU YA KUTOSHA?etc,sasa ili niwa elewe kua KILAINI na wengine hawaongozwi na DHANA,HISIA au mawazo slaa na tindu lisu basi watutajie mafisadi na mifano hai ya ufisadi wao so that tujadili bila kuhukumu kwa ushahidi wa hisisa.

Nchii hii inavitu vya ajabu ukiangalia MEDIA inafurahisha sana waandishi wanaandika hisia zao kutaka kutufanya nasi tuwaze kama wao.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
mafisadi wa kwanza ni hao viongozi wa dini.

Wanaogopa kukemea ukweli wakati wanaona hali halisi ya wanchi
wanaona uovu wote unaotendeka. Wanaogopa kukemea.

ahh hata hamu ya kuwasikiliza imeisha kabisa...wamejaa usanii usanii. hawaoni mwenzao desmund Tutu anavyokemea panapostahili. Na yule askofu wa Zimbabwe anavyokemea, he is so daring. Hawa wa kwetu bado sana.
 
mafisadi wa pili ni sisi wenyewe tunaoshindwa kukemea ukweli na kukubali kila kitu tunachokisikia. ni mara ngapi sisi tumewakandamiza wale wanaojitokeza na kusema ukweli kwa kuwaona wanaojipendekeza na wapenda vyeo na waropokaji. unajua inakatisha tamaa. angalia katika swala hili la kilaini, angalau yeye ameongea katika style ya kifasihi, kifalsafa na kithiologia ambako alijifunza kwa muda wote mpaka kupata udaktari, ili sisi wengine tutafakari na kusonga mbele katika fikra, sisi tuliopembeni tunataka aongee kisayansi na kisheria sababu eti tumebobea huko. sisi wote sio wana sheria.

unajua tujifunze kupewa maneno matatu ili na sisi tuzalishe maneno yetu. sasa ulitaka ayataje wakati tayari yalishatajwa, si tautology hiyo, na akiyataja, yeye ni mahakama, mbona wewe hujayataja. yeye ni mtu kama wewe, anachokisema ni hearsays, kwani hayuko kwenye kamati ya draftsmen wa mikataba.

ninadhani tuangalie issue at hand badala ya kulaumu watu walio katika msafara mmoja katika kupinga rushwa. he who is in our side is not our enemy.
we need only one thing from our people citzens in this battle, only saying 'yes you are right' in our movement.

hata wakati wa kupigania uhuru, active and passive resistors are all known as participants in struggling for independence.

I MIGHT BE WRONG BUT I AM ALWAYS CLEAR, Said Lord Denning, the father of law in England.
 
Askofu Kilaini: Vita dhidi ya ufisadi iwe ya kitaifa
*Aitaka serikali ifanyie kazi ripoti wa Redet
*Awataka Watanzania kufanya kazi kwa bidii
* Azungumzia mahusiano ya kanisa na wanamaombi


Na Kizitto Noya
Mwananchi
Posted Date::12/15/2007

ASKOFU Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Methodius Kilaini amesema kuwa mjadala kuhusu ufisadi na rushwa unatakiwa kuwa wa kitaifa ili kusaidia kulinusuru taifa na matatizo yanayolikabili.

Kilaini alitoa kauli hiyo juzi katika mahojiano maalum na gazeti hili kwa lengo la kupata mtazamo wa Kanisa kuhusu mambo mbalimbali yaliyotokea nchini katika kipindi cha mwaka 2007 unaomalizika siku chache zijazo.

Askofu huyo alifafanua kuwa siri ya mafanikio ya Tanzania ipo katika kupiga vita ufisadi, rushwa na kutunza uzalendo, amani na umoja bila kusahau tunu ya uwajibikaji na mori ya kufanya kazi.

Akizungumzia hali ya kisiasa nchini alisema kuwa imeboreshwa kwa kiasi kikubwa hasa baada ya serikali kutoa uhuru mkubwa wa watu kutoa maoni.

Alisema Utafiti wa Taasisi ya Utafiti na Elimu ya demokrasia (Redet) na mijadala mbalimbali ya ufisadi dhidi ya serikali ni sehemu ya uhuru huo ambao umesaidia kwa kiasi kikubwa kukuza demokrasia nchini na kuleta mabadiliko ya mifumo ya maisha.

"Kwa upande wa siasa ninaipongeza serikali kwa kutoa mwanya wa uwazi na uhuru wa maoni kwani haya yamesaidia kwa kiasi kikubwa kubadilisha historia ya nchi katika nyanja ya demokrasia," alisema.

Hata hivyo, alisema mijadala ya kitaifa inatakiwa kuwa na maslahi kwa nchi na waanzilishi wa mijadala hiyo wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuonyesha njia ya ukweli kama alivyofanya Zitto Kabwe katika mjadala wa madini na kukubali kuteuliwa kuwa mmoja wa wajumbe wa kamati ya madini inayopitia mikabata ya uchimbaji wa rasilimali hiyo.

Alisema matokeo ya Redet kwamba serikali imeshuka katika utendaji wake wa kazi ni uhuru tosha wa kutoa maoni, hatua ambayo ni sifa kwa serikali iliyoandaa mazingira ya uhuru huo ingawa inatakiwa kupokea matokeo ya utafiti huo kama changamoto katika utandaji wake wa kazi

"Kushuka kwa utendaji wa serikali si ajabu kwani miaka yote hii imekuwapo Watanzania tumeona ajabu kwa kuwa miaka ya nyuma hakukuwa na uhuru wa kuichambua serikali. Kama ilivyotoa uhuru wa maoni, serikali inatakiwa kupokea utafiti wa Redet na kuufanyia kazi," alisema .

Askofu huyo alisema matatizo ya Tanzania ni mengi na akafafanua kwamba hakuna haja ya kumtafuta mchawi wa tatizo la umaskini nchini badala yake Watanzania waanze kupenda na kuthamini kazi.

"Watanzania wanakula wasichofanyia kazi, ni watu wanaoridhika na kipato chochote wanachopata na wako tayari kugawana kidogo walichonacho na wenzao. Mtu akiajiriwa anafanya kazi kidogo lakini siku zote anapigania kupanda kwa mshahara," alisema Kilaini.

Alisema suluhu ya ugumu wa maisha sio kuongezeka kwa kima cha mshahara bali utayari wa kufanya kazi, kwani hata kama mishahara ingeongezeka maradufu, bila uzalishaji gharama za maisha bado zingepanda.

Kwa mujibu wa Kilaini, kupanda kwa gharama za maisha kumetokana na uvivu wa kufanya kazi na si udogo wa mishahara kwani thamani ya fedha inategemea wingi wa bidhaa inayotaka kununua.

"Kuongeza mishahara bila kazi ni balaa, mishahara lazima iendane na ungezeko la juhudi za kazi na watu walipwe kwa kazi waliyoifanya sio kwa kuwa katika eneo la kazi" alisema.

"Kwa muda mrefu Watanzania wamekuwa wakiishi maisha ya ujamaa, maisha ambayo sasa yanatakiwa kubadilika na kuingia katika mfumo wa ubepari ili kila mtu ale alichofanyia kazi," alisema na kuongeza;

"Tumebweteka na urithi wa ujamaa ambao sasa haupo na hata mori ya maisha ya kibepari ya kila mtu kula analichofanyia kazi haipo lazima Watanzania tubadilike kama tunataka kujiletea maendeleo endelevu."

Kuhusu uhusiano wa Kanisa Katoliki na Kikundi cha Maombi kinachoongozwa na Padre Felician Nkwera, Kilaini alisema haupo kwa namna yoyote ile, ila Kanisa Katoliki limefanikiwa kuwarejesha kundini mapadre watano waliohama kanisa hilo na kujiunga na kikundi hicho katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Alisema kanisa linaendelea na msimamo wake wa kuwatenga wafuasi wa kikundi hicho ila hakiwazuii kurejea kundini ili mradi wafuate taratibu za Kanisa Katoliki.
 
12/25/2007

Maaskofu: Ufisadi ni janga la kitaifa
* Wasema unaipeleka nchi pabaya
* Washauri mikataba ya madini ifutwe
* Wasema haiwanufaishi Watanzania
* Wawahimiza wananchi kufanya kazi


Na Waandishi Wetu
Mwananchi


MAASKOFU wamesema ufisadi, rushwa, mikataba feki ya kuuza rasilimali za nchi na wimbi la wageni wanaoingia nchini na kuhodhi mali na ajira za wazawa ni janga linaloendekezwa na kuachwa likiwatafuna Watanzania.

Maaskofu hao walitoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti kwenye mkesha na ibada ya maadhimisho ya Sikukuu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo, katika makanisa tofauti nchini juzi na jana.

Akihubiri katika misa ya mkesha wa Krismasi juzi usiku, uliofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Albano, Askofu wa Kanisa la Anglikana Jimbo la Dar es Salaam, Valentino Mokiwa alisema utajiri wa madini wa nchi unasombwa na wageni huku raia wakibaki wanaogelea kwenye lindi la umaskini.

Askofu Mokiwa alisema alitembelea baadhi ya migodi na kushuhudia jinsi utajiri wa nchi hii unavyowanufaisha wageni, huku raia wakiendelea kutaabika.

Alisema suala hilo ni nyeti na linatakiwa kuangaliwa kwa jicho la pekee na viongozi wa kitaifa.

"Ningekuwa na uwezo, ukiniuliza leo kuhusu mikataba ya madini, nitakwambia ifutwe mara moja na iandikwe upya ili kuwanufaisha wazawa...," alisema.

Aliongeza kuwa hata kwenye Biblia imeandikwa kwamba, mgeni asinywe mvinyo kwenye shamba ambalo hajashiriki kulitayarisha, hivyo akahoji iweje, wageni wafaidike na madini ilhali wazawa wakiendelea kutaabika.

Askofu Mokiwa alisema suala la madini linatakiwa liangaliwe kwa jicho kali ili liweze kupatiwa ufumbuzi kusudi madini yawasaidie wananchi kuondokana na umaskini, badala ya kuwaacha wageni kuzoa utajiri huo.

Kuhusu kutelekeza watoto, Askofu Mokiwa alisema sio mafundisho ya Yesu Kristo, haiwezekani watoto wakaadhibiwa na kuitwa majina yasiyofaa kwa kosa la wazazi wao.

"Mara waitwe watoto wa mitaani na mengineyo mengi lakini mitaa haikuzaa! Watoto wanatakiwa kuangaliwa kwa jicho la huruma na hayo ndio mafundisho ya Yesu Kristo," alisema Askofu Mokiwa.

Naye Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Alex Malasusa alisema rushwa na ufisadi ni tatizo la kitaifa ambalo linahitaji watu kujikana ili kupambana nalo.

Malasusa alisema hayo wakati akihubiri kwenye ibada ya Krismasi iliyofanyika jana katika Kanisa la Azania Front, jijini Dar es Salaam,

Alisema ili kupambana na tatizo hilo, Watanzania hawana budi kushiriki kikamilifu katika kumaliza tatizo hilo.

Alisema sasa wakati umefika kwa wananchi kutimiza wajibu wao wa kupambana na tatizo hilo ili kuinusuru nchi kuendelea kupoteza rasilimali zake.

Ni lazima kila mmoja aone kuwa ni jukumu lake kupambana na rushwa na si kusubiri viongozi wawasukume, la sivyo tatizo hilo litaendelea kuwa sugu na kubadilishwa majina kila kukicha. Kwa mfano sasa hivi wameipa msamiati mwingine kwa kuiita ufisadi,� alisema Malasusa.

Alisema pamoja na kupambana na rushwa ili uchumi wa nchi uweze kukua ni lazima wananchi wajue umuhimu wao katika kuinua uchumi kwa kufanya kazi kwa bidii.

"Kazi ni uhai, suala hili linatakiwa kuingizwa kwenye mitaala ya shuleni ili kujenga vijana wenye moyo wa kupenda kazi," alisema Malasusa.

Aliyataka mataifa tajiri duniani kuacha utaratibu wa kuzinyonya na kuzikandamiza kiuchumi nchi maskini.

Alisema nchi tajiri za duniani zinazikandamiza nchi masikini kutokana na uwezo wao wa kiuchumi waliojiwekea tangu zamani, hivyo kutawala masoko na kuweka mfumo wa kuendelea kuzinyonya nchi zinazoendelea.

Pia aliwataka Watanzania wa dini zote kutumia muda huu kuombea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika kesho nchini Kenya.

Alisema uchaguzi huo ukifanyika kwa amani ni jambo la heri kwa Watanzania kutokana na ujirani uliopo baina ya nchi hizi mbili, kwani yatatokea machafuko nchini humo kutokana na matokeo ya uchaguzi huo, Watanzania pia wataathirika.

Imeshazoeleka kwa nchi za Kiafrika unaposikia uchaguzi, mara nyingi maana yake ni fujo, heka heka na machafuko. Sisi na Kenya ni watu wa nyumba moja, vyumba vinavyofuatana, lolote litalotokea kwa wenzetu linatuhusu pia. Tuwaombee ili wafanye uchaguzi wao kwa amani,� alisisitiza Askofu Malasusa.

Katika ibada hiyo, Askofu Malasusa alifanya maombi maalum kwa ajili ya uchaguzi huo na kuwaombea Watanzania waweze kubadilika na kusimama kikamilifu kwenye maadili ili waweze kupata neema ya Mungu wanapojiandaa kuingia mwaka mpya wa 2008.

Kutoka Geita, Mwanza, Askofu Mkuu Damian Denis Ndalu wa Kanisa Katoliki, akihubiri katika ibada ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo iliyofanyika kitaifa katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Mama Bikira wa Phatimo, Jimbo la Geita jana, aliwataka viongozi na wananchi kuacha vitendo vya ufisadi na rushwa.

Alisema vitendo vya ufisadi na rushwa vimekuwa vikiendelezwa na watu kutokana na ubinafsi ambao umewafanya walazimishe kuomba rushwa bila kuogopa.

Siku hizi watu hawaombi rushwa bali wanalazimisha rushwa, wanasema leta rushwa ili waweze kutoa huduma. Sasa sijui tunakwenda wapi?� alisema na kuhoji Askofu Ndalu.

Alisema ili taifa na watu wake waweze kuondokana na vitendo vya rushwa na ufisadi wanapaswa kusali na kuwa waaminifu katika sehemu zao za kazi.

Askofu huyo alisema mbali ya Wananchi na Serikali kupambana na rushwa, Watanzania wanapaswa kufanya kazi kwa bidii na kujenga tabia ya kujisimamia wenyewe kwa ajili ya kuongeza pato la taifa.

Alisema kufanya hivyo, Watanzania watakuwa na sauti ya kuitaka Serikali iwaongezee mishahara kwa kuwa pato la taifa litakuwa limeongezeka.

Watu wajijengee tabia ya kujisimamia wenyewe na wasichague kazi ya kufanya. Tupende kazi kwa sababu kwa kufanya kazi, Watanzania watakuwa na uwezo wa kuiambia serikali iwaongezee mishahara. Sasa unataka serikali ikuongezee mshahara wakati kazi hufanyi kwa bidii na uzalishaji unakuwa hafifu...,� alisema askofu huyo.

Akizungumzia ugonjwa wa ukimwi, Askofu Ndalu aliwataka Watanzania kuacha kufanya ngono kwa kuwa kufanya hivyo kutawasaidia kuepukana na maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) kwa asilimia 100.

Acheni ngono. ,Utasikia wanasema ngono zembe, acheni kabisa kufanya ngono, jiheshimuni muweze kuishi kwa amani. Kutokana na watu kutokuwa makini na watu wengi kuendeleza zinaa kumekuwa na ongezeko kubwa la watoto wengi wa mitaani, alisema askofu huyo.

Kutoka Zanzibar, Askofu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Zanzibar, Augustine Shao, alishutumu utandawazi usiokuwa na usimamizi wa dola kuwa unaua Utamaduni wa Mtanzania.

Akihubiri kwenye ibada ya mkesha wa kuzaliwa kwa Yesu Kristo katika Kanisa Katoliki la Minara Miwili Unguja, alisema ni ukweli usiopingika kwamba Tanzania haiwezi kuwa kisiwa bila ya kuingia kwenye utandawazi, lakini akaonya kuwa utandawazi usiokuwa na usimamizi unaleta matatizo kwa jamii

Siamini kwamba tunahitaji wageni kuwa wauza maduka, kioski, wapishi na watandika vitanda katika mahoteli yetu. Ndugu zangu Watanzania, hivi sasa wapo wageni wengi nchini kihalali, kwa sababu ya ndugu zetu tuliowakabidhi ofisi za uhamiaji wameshindwa kusimamia ipasavyo wajibu wao,� alisema.

Askofu Shao alisema ubinafsishaji wa sehemu muhimu za uchumi ni jambo linalowasononesha wananchi kwani hakuna manufaa yoyote wanayopata zaidi ya kushuhudia bidhaa nyingi zikitoka nje na kuletwa hapa nchini na mali zao kupelekwa nje kinyemela.

Askofu Shao pia alizungumzia tatizo la uwajibikaji katika jamii kwani shida nyingi katika taifa hili ni watu kupenda vyeo na madaraka bila ya kuwajibika.

Dhambi kubwa iko kwenye mikataba feki ya kuuza rasilimali za nchi. Hii ni dhambi kubwa ambayo itazaa mateso kwa vizazi vingi vijavyo kwa hiyo lazima ipigwe vita kikamilifu,� alionya Askofu Shao.

Aidha, aliwasihi viongozi kuwa makini katika kushughulikia kero mbali mbali za wananchi hasa katika suala la uwekezaji na ukosefu wa ajira.

Alisema mara nyingi mishahara na marupurupu ya watu kutoka nje ya nchi ni makubwa zaidi ya mishahara ya Watanzania wanaotumikishwa katika kazi ngumu zaidi ya zao za usimamizi.

Alitoa mfano kuwa kwenye hoteli zote za kitalii Zanzibar hakuna chumba kinachotozwa chini ya dola za Marekani 50 kwa siku, lakini Mtanzania anayefanya kazi katika hoteli hizo hulipwa mshahara wa kati ya dola 50 na 80 kwa mwezi.

Naye Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo, akihubiri katika ibada ya Krismasi jana, alikemea uzinzi na kuitaka jamii kuachana na uasherati na utoaji mimba kwa kuwa vitendo hivyo ni vya aibu na vinamkasirisha Mungu.

Kwetu sisi tunaotambua kuwa Neno (Yesu) alifanyika mwili na akakaa katikati yetu, tusiidhalilishe miili yetu kwa uasherati, uzinzi na kutoa mimba kwani huko ni kumdhalilisha Mungu, alisema Kadinali Pengo.

Alisema waumini wa dini ya Kikristo wanatakiwa kumuenzi Mungu kwa kuthamini miili yao na kuepuka vitendo vya kuidhalilisha kwani ndani ya mwili wa mwanadamu ipo roho inayoungana na Mungu.

Kwa mujibu wa Kadinali Pengo jamii inatakiwa kulitangaza fumbo la sherehe za Krismasi kwa kuishi maisha ya kuheshimu miili yao na kuwa chachu ya mema badala ya kutumia sherehe hizo kufanya anasa na kumkosea Mungu.

Alisema tofauti na imani za watu wa kale kwamba mwili ni tunda la shetani hivyo kuamua kuidhalilisha kwa lengo la kumkomoa, lakini kwa Mkristo mwili ni hekalu la Mungu linapaswa kuheshimiwa na kulindwa wakati wote.

Alisema roho na mwili siku zote vinashirikiana katika kumjengea mtu utakatifu hivyo aliwataka Wakristo kuwa safi roho na mwili ili kuweza kuwa karibu na Mungu.

Imeandaliwa na Salma Said kutoka Zanzibar, Andrew Msechu, John Stephen, Midraji Ibrahim na Kizitto Noya.
 
Hawa nao wamekaa kinafiki nafiki tu

Paomoja na unafiki wao,
Siku hizi naona wana ka mwamko fulani, taratiiiiibu nuru ya kumkoma nyani ina ingia.

Kumbuka hawa nguvu yao ni kubwa, wakitoa mwamko wa kwamba ufisadi ni mbaya huko makanisani, na misikitini, huku nje akina Slaa wakagongomela misumari kwa kuanika chanzo cha ufisadi, na njia pekee ya kuepukana nao... kitaeleweka. Tuwape motisha kwa sasa walau kwa ujasiri wao wa kuanza kusema wazi wazi.
 
Askofu atamani kufuta mkataba wa Buzwagi

na Mkolo Kimenya na Safina Tibanyindela
Tanzania Daima


VIONGOZI wengi wa dini waliyatumia mahubiri yao katika maadhimisho ya Sikukuu ya Krismasi kukemea maovu yanayoshamiri katika jamii, wakiyataja masuala ya rushwa na ufisadi kama yanayopaswa kupigwa vita sasa kwa nguvu zote.

Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam, Kanisa Kuu la Anglikana, Valentine Mokiwa, amesema kuwa, mikataba inayosainiwa nje ya nchi ina harufu ya rushwa na inamuweka hatarini mtoto wa kizazi cha sasa, kwa sababu rasilimali zote zinamilikishwa mikononi mwa watu ambao hawalinufaishi taifa.

Alisema hayo kupitia mahubiri aliyoyatoa katika misa ya mkesha wa Krismasi iliyofanyika kitaifa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Albano, Dar es Salaam.

“Mikataba inampa mgeni haki kuliko mzawa, mikataba hii inawafikiriaje watoto, kila rasilimali za watoto wetu zinamilikishwa, kama angekuwa mimi ningefuta mikataba yote ambayo imejaa unyanyasaji hasa kwa watoto ambao wakikua na kukuta rasilimali zote zimemilikishwa watashindwa kuutetea utaifa wao hapo baadaye,” alisema.

Ingawa hakutaja waziwazi, lakini mkataba wa madini hapa nchini ambao umesainiwa nje ya nchi unaofahamika na wengi ni wa mradi wa Buzwagi mkoani Shinyanga.

Sakata la mkataba huo kusainiwa nje ya nchi lilisababisha Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, kusimamishwa kwa muda bungeni, kufuatia kuhoji uhalali wa mkataba huo kusainiwa nje ya nchi.

Aidha, katika mahubiri yake Askofu Mokiwa alionyesha kusikitishwa na unyanyasaji unaofanywa na wawekezaji katika sekta ya madini dhidi ya wananchi.

Akitoa mfano wa unyanyasaji unaofanywa na watu wanaomilikishwa maeneo mbalimbali, hasa yanayosadikika kuwa na madini, alizungumzia sakata la wakazi kadhaa wa Kijiji cha Mtakuja wilayani Geita mkoani Mwanza, ambao wameondolewa katika ardhi yao kumpisha mwekezaji.

Alisema wakazi wa kijiji hicho walikuwa wakilazimishwa kuondoka haraka na matokeo yake waliondoka na kwenda kukaa katika eneo lisilokuwa na huduma muhimu.

Askofu huyo alisema hali ya wakazi hao bado ni mbaya hadi hivi sasa na kusema kuwa hiyo inahatarisha hali ya mtoto ambaye baadaye atataka kuwa na rasilimali ya kumletea maendeleo.

“Watoto imekuwa ni taasisi moja isiyoweza kujitetea yenyewe na kuonewa na kila mtu, watoto wananyanyaswa, wanatendewa vitendo viovu, inabidi jamii ya watoto waweze kujisemea wenyewe au wafundishwe kuwaweka hadharani watu hao ambao wanawafanyia vitendo viovu,” alisema.

Askofu Mokiwa alisema sasa hivi kuna roho chafu za kuharibu watoto wa kike na kiume, hivyo aliwataka wazazi wasiziachie televisheni na redio kuwalelea watoto wao, bali wawe waangalifu na watoto wao na kuwakanya bila kukata tamaa.

Alisema vitendo vya rushwa ndivyo vinavyochangia kuendelea kuwepo kwa uharibifu wa maadili kwa watoto na vijana, akitolea mfano madanguro ambayo yamekuwa yakitumika kwa ajili ya mabinti kujiuza na kusema kuwa maeneo hayo askari wanayajua, lakini wakifika wanapewa fedha na kuondoka huku watoto wakiendelea kuuza miili yao.

Kwa upande wake, akihubiri katika misa ya kitaifa iliyofanyika jana asubuhi wilayani Geita, Askofu wa Jimbo Katoliki la Mwanza, Mhashamu Damian Dallu, alisema ubinafsi na chuki miongoni mwa wanajamii ndio chanzo cha ufisadi na rushwa inayoshuhudiwa nchini hivi sasa.

Katika mahubiri yake yaliyotangazwa moja kwa moja na Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD), Askofu Dallu alisema ubinafsi uliojengeka ndani ya mioyo ya baadhi ya watu, unasababisha baadhi ya viongozi kujinufaisha bila kujali maslahi ya wengine, jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya nchi.

“Tukitaka kufanikiwa kuondoa ufisadi na rushwa iliyotawala, hatuna budi kuondoa ubinafsi tuliojijengea ndani ya mioyo kwa kutaka kujinufaisha wenyewe bila kufikiria mwingine.

“Hili ndio tatizo kubwa na kama tutafanikiwa kuzimudu nafsi zetu, hakika vitu hivi hatutavipigia kelele tena kama ilivyo sasa,” alisema Askofu Dallu.

Alisema hivi sasa dunia inatawaliwa na utamaduni wa vifo ambavyo vinasababishwa na uzembe au kwenda kinyume cha maagizo ya Mwenyezi Mungu.

Askofu huyo alisema utamaduni huo ndio ambao unawafanya watu wengi kujitumbukiza katika ubinafsi, hivyo kuwa na tabia za ufisadi ambazo zinaliangamiza taifa.

“Wote huo ni ubinafsi ambao umeleta ufisadi ndani ya jamii pamoja na tabia mbaya ya kudai rushwa,” alisema na kuongeza kuwa rushwa hivi sasa inadaiwa na si kuombwa kama ilivyokuwa awali.

Askofu huyo alieleza hali ya kusikitisha inayoshuhudiwa katika jamii hivi sasa, ambapo viongozi wenye madaraka au uwezo katika maamuzi wanadai rushwa huku kundi jingine la vijana linakaa vijiweni bila ya kufanya kazi na kujihusisha na kuvuta bangi na kukaba watu bila kujali taifa linaathirikaje.

Mbali na hilo, askofu huyo, aliikumbusha jamii umuhimu wa kujijengea utamaduni utakaoweza kutibu mmomonyoko wa maadili ambao unaonekana kwa baadhi ya wanajamii, ili kujenga taifa lenye amani na upendo.

“Tuondokane na fikra za kuiga tamaduni za kigeni ambazo ndio chachu ya kumomonyoka kwa maadili na hata kubadilika kwa mfumo wa kuishi katika nchi yetu, tunachotakiwa ni kutengeneza utamaduni ambao utakuwa kielelezo na chanzo cha amani na upendo miongoni mwetu,” alisema.

Akizungmzia ugonjwa wa ukimwi, Askofu Dallu aliishauri jamii kutumia njia ambayo ina uhakika wa asilimia 100 kukabiliana na maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo badala ya ile isiyo na uhakika ambayo huwaacha na asilimia kadhaa ambazo zinaweza kuwaweka katika maambukizi zaidi.

Alisema kinachotakiwa ni watu kuishi kwa uadilifu na kuachana na matendo ambayo yanaweza kuwatumbukiza katika maambukizi ya ugonjwa huo.

Hata hivyo, alisema: “Si watu wote wanapata maambukizi kutokana na ngono zembe, bali wapo ambapo wanapata kutokana na majukumu yao kama wakati wa kuhudumia wagonjwa na vitu vingine vya namna hiyo.”
Askofu Dallu alisema hata baadhi ya viongozi wa dini wamejikuta wakitumbukia katika kitu kinachoitwa ngono zembe, ambacho wanadai inatokana na walio wengi kushindwa kutekeleza amri ya sita ambayo inakataza watu kuzini.

Aidha, Askofu Dallu aliitaka jamii kuitumia Krismasi kubadilika na kuwa nyota ya kweli kama alivyokuwa Yesu Kristo, kutokana na ukweli kuwa nabii huyo alikuja kwa ajili ya watu wote wenye dhambi na wale waliokuwa safi.

 
1/2/2008
Maaskofu waitaka serikali kunusuru uchumi wa nchi

Na Waandishi Wetu
Mwananchi


MAASKOFU wamewataka viongozi wa serikali kuchukua hatua za haraka kunusuru hali ya kiuchumi mwaka huu wa 2008 ili kudhibiti mabadiliko yalisababisha uchumi wa nchi kupoteza mwelekeo mwaka jana.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye mkesha wa kuuaga mwaka 2007 na kuukaribisha mwaka 2008 juzi, Mkuu wa Kanisa Katoliki nchini Polycarp Kadinali Pengo na Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Dar es Salaam Valentino Mokiwa walisema uchumi kiimarishwa utapungua makali ya maisha ya waananchi hivyo kumisha umoja na amani nchini.

Askofu Mokiwa aliitaka serikali kuchukuwa hatua za haraka mwaka huu wa 2008 dhidi ya mabadiliko makubwa ya uchumi yanaoyendelea kupoteza muelekeo wa watanzania kwa kujenga matabaka matatu ya matajiri, watu wenye hali nafuu na maskini ambao wanazidi kuongezeka kwa kasi.

Jambo la kusikitisha ni kwamba mwaka uliopita uchumi wa nchi umeporomoka, watu wenye hali duni wameendelea kuteseka, hivyo serikali inatakiwa kuchukua hatua madhubuti kunusuru hali hiyo, alisema Askofu Mokiwa.

Alisema ugumu wa maisha unaowakabili Watanzania baadhi ya watu na hasa vijana kujiingiza kwenye vitendo viovu huku wengine wakipoteza maisha yao kwa kujinyonga kwa kukata tamaa.

Alisema hali hiyo ni kikwazo katika harakati za kupambana na rushwa nchini kwa kuwa umaskini uliokithiri ni moja ya sababu zinazowasukuma watu kupokea na kutoa rushwa.

Naye Kadinali Pengo wa Kanisa Katoliki alisema kuwa viongozi wasiowasaidia watu wao kuweza kujinasua kiuchumi ni viongozi wasiofaa, hivyo kuwataka wajichunguze upya.

Akiwakilisha salamu za Papa Benedict (XVI) zilizokuwa zikilenga familia kama nguzo ya kujenga upendo na amani, Pengo alisema ni jukumu la viongozi wa serikali kuhakikisha kuwa watu wao wanapata maslahi ya kutosha ili kuonyesha upendo kwa familia zao na kujenga taifa lenye amani.

Hatuwezi kuzungumzia taifa au dunia yenye amani bila kuwa na familia zenye upendo uliosimama, wazazi ambao ndiyo wajenzi wakuu wa upendo kwenye familia wanatakiwa wawezeshwe kiuchumi ili waweze kuonyesha upendo kwa kuendeleza familia zao," alisema na kuongeza kuwa viongozi wa watu au jumuia yoyote wasiyowawezesha watu wao kujinasua kiuchumi na kuzisaidia familia zao hawafai kuwa viongozi.

Alisema nchi haiwezi kuzungumzia suala la amani bila kuwa na misingi ya kujenga upendo kwa familia kupitia ujenzi familia takatifu, ambayo ndiyo nguzo ya amani popote duniani.

Aliongeza kuwa sasa hivi dunia imejikuta katika tatizo kubwa la ugaidi na wanaotumika kufanikisha vitendo hivyo ni viajana wasio na ndugu ambao huokotwa mitaani baada ya kutelekezwa au kukosa ajira na shughuli za kufanya pamoja na malezio sahihi kutoka kwa wazazi wao kutokana na umasikini.

 
Back
Top Bottom