Vijitabia vipi "unique" ambavyo ukivifanya vinakupa amani moyoni na "relaxation" ?

Hyo namba 1 kuna siku utapigwa radi ufe hautaamin utakapotuona tunakuosha ili tukutie kwenye jeneza

Mvua ndogo ndogo huwa zinaambatana na radi zenye madhara
 
Nilikuwa nakaa karibu na nimpendae ni mwangalie tu Ata kama sina cha kumwambia (bahati mbaya sahv hayupo tena)

Najiongelesha naweza kujiuliza maswali na kujijibu mwenyewe au kujipigisha story kama vile tupo wengi kumbe nipo peke yangu.

Natengeneza picha kichwani ya maisha niliyo/ninayo Taman siku moja kuwa nayo kuanzia nina mke, watoto had ninapo kufa. Najionaga nipo kwenye ulimwengu mwingine kabisa
Kutengeneza picha ya vitu navyotamani kuwa navyo au maisha.. Hali hii hata Mimi hunifariji sana
 
Kuvuja vyombo jamii ya glass nikiwa na hasira huwa nina chupa zangu hapa nazivunjaa na hasira huisha, pia kukaa baharini mida ya usiku hasa ninapokua na stress
Duuh
Very rare mkuu
Ila angalia usivunje vyote siku nikija ukatumia kikombe cha plastic hahah

Goodluck.
 
1. Kutembelea eneo kama mlimani city wale watu naowaona pale huwa najipa hope kwamba ipo siku soon na mimi ntatoboa ni suala la kukaza tu

2. Kusikiliza ala hasa za piano, guitar, violin, trumpet nk zile huwa huwa zinahamisha kabisa akili

3. Kwenda eneo la umma hasa sokoni kuona hustling za watu mbali mbali..
Inspirational
 
Nilikuwa nakaa karibu na nimpendae ni mwangalie tu Ata kama sina cha kumwambia (bahati mbaya sahv hayupo tena)

Najiongelesha naweza kujiuliza maswali na kujijibu mwenyewe au kujipigisha story kama vile tupo wengi kumbe nipo peke yangu.

Natengeneza picha kichwani ya maisha niliyo/ninayo Taman siku moja kuwa nayo kuanzia nina mke, watoto had ninapo kufa. Najionaga nipo kwenye ulimwengu mwingine kabisa
Motivational
 
1.napenda kusafiri huku nikiwa nimeshika simu nacheck jf
2.Napenda kutembelea sana sehemu zenye pori na wanyama muda mwingine

Mkuu, japo ni nje ya mada huwa kuna komentsi zako unaamuaga kujichomoa akili, zinanichekeshaga sana.

Nakumbuka kuna uzi wa Walimu walilalamika, shule yao haina vyoo na inawalazimu wakae chini ya miti kufanya shughuli zao za kiofisi.

Hahaha, ukaumiza akili sana na kuja na komenti ya kiintelijensia kwamba kutokuwa na vyoo hakuhusiani na kukaa chini ya miti, ukasema walimu waseme ukweli kwamba hawakai chini ya miti bali wana ku ....

Kila nikiwa Mbeya kwenye majukumu ya ujenzi wa Taifa, kuna type ya wadada nikiwaona huwa nahisi ni wewe.
 
1-napenda kukaa sehemu pekee yangu palipotulia penye upepo mnzuri,ukijani mnzuri hukuu nikisikiliza reggae na kuvuta weed

2-napendelea kulima lima vimboga,matnda home,huku nikimwagilia vibustani nakusikiliza sauti za ndege zikilia yani najisikia burudani sana

3-napenda kuangalia mifugo yangu wanavyokula,kuku wanavyonipita miguuni huku wakidonoana,huwa naona mkuu wa Mungu sana

4-napenda sana kukaa mtoni kusikiliza sauti za maji,huku nikiyaangalia yanavyotembea kutoka uelekeo mmoja kwenda mwingine

5- napenda sana kupika mwenyewe vyakula natural,sipendi mtu anipikie
 
Hakuna kitu ninacho kipenda kama kukaa peke yangu, kulala na lala peke yangu yapo nimeoa, napenda kula na kunywa peke yangu, kazi hata iwe ngumu kiasi gani huwa naenda kufanya peke yangu, nilisha wahi kuezeka majengo mengi peke yangu, nilisha wahi kuchimba shimo la choo peke yangu, nilijenga peke yangu , nilifyatua tofali peke yangu, zege nilichanganya na kumwaga peke yangu, hata maji ya kujengea nilibeba peke yangu na baiskeli.

Yaani amani ninayopata nikiwa peke yangu au kufanya kitu chochote peke yangu ni kubwa mno, sijui ni kwa vile nimezaliwa peke yangu ?
True To Self.

Nice.
 
1. Kuangalia Maji ya mto yanavyotiririka Samaki au Dagaa wakiogelea.

2. Kunyeshewa na mvua.
Hii nilikuwa napenda wakati nasoma nikirudi kutoka Chuo.

3. Kaundika andika,
Iwe wazo zuri au baya, Kwa siku sio ajabu nikaandika kurasa hamsini.

4. Kuongea na wanyama na kujiongelesha
Tunashare dna
 
Hakuna kitu ninacho kipenda kama kukaa peke yangu, kulala na lala peke yangu yapo nimeoa, napenda kula na kunywa peke yangu, kazi hata iwe ngumu kiasi gani huwa naenda kufanya peke yangu, nilisha wahi kuezeka majengo mengi peke yangu, nilisha wahi kuchimba shimo la choo peke yangu, nilijenga peke yangu , nilifyatua tofali peke yangu, zege nilichanganya na kumwaga peke yangu, hata maji ya kujengea nilibeba peke yangu na baiskeli.

Yaani amani ninayopata nikiwa peke yangu au kufanya kitu chochote peke yangu ni kubwa mno, sijui ni kwa vile nimezaliwa peke yangu ?
Mzee unanikumbusha 2016 nikichimba kisima cha futi 40 peke yangu,nilipiga plast nyumba nzima pekee yangu,napenda kujenga jenga ovyo tuna fanana mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom