Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 16,066
- 10,567
Ndugu zangu Watanzania,
Wema ni Akiba,Ni akiba isiyooza ,ni akiba ya kudumu,.Ukitenda wema Tegemea kulipwa Mema ,inaweza isiwe leo au kesho lakini fahamu ya kuwa Wema una Tabia ya kumrudia mhusika kwa njia Tofauti Tofauti,wema una desturi ya kurudi ulipotoka.
Sasa kwa Jimbo la Mbeya mjini wema umeanza kumtafuta Daktari na Nguli wa sheria Mh Tulia Acksoni mwansasu, unamtafuta kila kona ya jiji la Mbeya,Unatembea kwa magoti na kutambaa kumtafuta popote alipo ili umpate,Una haha kila mahali ,kila kijiwe,kila kilinge na kila kijiwe. Dkt Tulia amekuwa ni gumzo kwa namna anavyotafutwa na wema wake alioutenda kwa maelfu ya vijana mkoani Mbeya katika kutaka kumrudia na kumlipa wema wake alioutoa kwa upendo na huruma ya hali ya juu kwa vijana mkoani Mbeya pasipo ubaguzi wa aina yoyote ile.
Vijana katika vijiwe mbalimbali na maeneo mbalimbali mkoani Mbeya wamejiapiza kumpigania ,kumkapenia na kumuombea kura Nyumba kwa nyumba katika jimbo la Mbeya mjini uchaguzi ujao.Hii ni baada ya kutendewa wema na Dr Tulia,kama vile kuwasaidia mitaji vijana iliyowasaidia kuanzisha na kufungua biashara zilizowasaidia kuondokana na utegemezi wa kipato na kuanza kujitegemea na kuinuka kiuchumi,kuwa saidia na kuwapa bure pikipiki pamoja na bajaji ambazo sasa zinawasaidia katika kujipatia fedha kila siku iendayo kwa Mwenyezi Mungu,hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa jiji la Mbeya ni Eneo lenye abiria wengi sana kila kona ya jiji kunakotokana na kuchangiwa na uwepo wa shule na vyuo mbalimbali na vya ngazi Tofauti Tofauti.
Huruma na upendo huo wa Dr Tulia katika kuwainua kiuchumi umewagusa sana vijana,kwa kuwa umewaletea matumaini,Tabasamu,furaha ,nuru na faraja katika mioyo na maisha yao.wanamuona Dkt Tulia kama mkombozi wao kiuchumi. Hawapo Tayari kumsaliti au kumuangusha uchaguzi ujao,wapo Tayari kutembea nyumba kwa nyumba kwa miguu katika adhima ya kumuombea kura za ushindi ili arejee Bungeni na kuendelea kuwasaidia na kuwaletea maendeleo na kugusa maisha yao.
Wanamuona kama Dada yao wa Tumbo moja kutoka kwa mama mmoja kwa namna anavyo wasaidia bila kikomo wala ubaguzi wala masharti wala mipaka. Moyo wa Dr Tulia ni wa kipekee sana kwa kuwa Anamsaidia na amesaidia vijana wengi sana mkoani Mbeya ambao sasa Wanatamka waziwazi bila kificho kuwa hawapo Tayari kupoteza kura zao kwa kumpigia mwingine yoyote nje ya Dr Tulia ambaye Ndiye chaguo la wana Mbeya wote.
Ni funzo kwa wabunge wengine kuwa ukitaka ukumbukwe,kukubalika ,kuungwa mkono na kupendwa na wapiga kura wako basi jitahidi kuacha alama katika mioyo ya wananchi wako,uwe karibu nao, kusikiliza kero zao na kuwapa majibu, kuwa mwenye huruma,upendo na unyenyekevu kwa watu wote wa rika zote na makundi yote pasipo ubaguzi, kutambua kuwa wapiga kura ndio waliokufikisha hapo ulipo Bungeni na ndio maboss wako unaopaswa kuwasikiliza na kuwatumikia. Lakini pia kuzungumza lugha za wapiga kura au wananchi wako juu ya changamoto mbalimbali zinazowasumbua na kuzitafutia majibu sehemu husika.
Siyo mtu anachaguliwa ubunge leo anaanza kujiona ana akili kuliko wananchi wote,anaanza kuwaona wapiga kura kama Takataka wasio faa hata kumsalimia kwa mikono,muda wote amepandisha vioo vya Gari lake huku akikimbia utafikiri yupo kwenye mashindano ya magari na hata kuonekana tu jimboni ni kwa nadra sana,Hasikilizi la mtu wala kushauliwa na mtu ,Hakai na wananchi wake wala kusikiliza wanasema nini juu ya jimbo lao. lakini dkt Tulia licha ya elimu yake kubwa wadhifa wake mkubwa ndani ya Bunge na ndani ya chama bado ameonekana muda mwingi na wote akiwa pamoja na wapiga kura wake kipindi chote ambapo vikao vya Bunge vinakuwa vimesimama.
Sasa kiongozi wa aina hiyo ya dkt Tulia kwanini asiungwe mkono? Kwanini asipendwe jimboni kwake? Kwanini asipitee tena uchaguzi ujao? Kwanini asipigiwe kura za kishindoo? Sasa mwingine siyo waziri wala naibu waziri wala spika wa bunge au naibu spika au mwenyekiti wa kamati yoyote ile lakini anajifanya yupo Bize muda wote na yupo nje ya jimbo muda wote Haitishi mikutano kuwapa mrejesho na kusikiliza changamoto zao wala kuwa nao karibu .sasa wa hivi nani anaweza muunga mkono au kumpigia kura? Nani anayeweza kumpigania au kumtetea popote pale? Nani anayeweza kutamani mtu wa aina hiyo arudi Bungeni Tena uchaguzi ujao?
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel mwashambwa,kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.