Vijana, msifanye makosa kama niliyofanya. Kujiunga na CHADEMA ni sawa na kucheza karata tatu!

Chris Lukosi

Naipenda Tanzania, nyumbani ni Tanzania CCM sio nyumbani na kamwe hapawezi kuwa nyumbani, wanaoiita CCM ni nyumbani ndio wanafanya ufisadi na kuuza meno ya Tembo, (Katibu Mkuu wa CCM anahusika) ndio wanaoiingiza Tanzania kwenye mikataba mibovu kama anayoingia Mwenyekiti wa CCM Taifa Jakaya Kikwete, ndio waliosababisha waTanzania wa Bulyanhulu wazikwe hai ili kunufaisha 'Nyumbani' CCM huku nyumbani kwangu mimi Tanzania kukiteketea

Kamwe sitakubali, na nitaunga mkono harakati zozote zitakazoiletea matumaini na neema Tanzania yangu, siko tayari kujiingiza kwenye mkenge wa CCM, CCM sio Tanzania

Ni roho za ajabu walizo nazo wana CCM, wengi wamejawa na roho za woga na kinafki,

1) Horace Kolimba - CCM inanuka na imeoza
2) JK Nyerere - CCM sio mama yangu

Huyu anayepaita 'CCM nyumbani' namsikitikia yeye na familia yake!

Joash R. Mussa
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Chris Lukosi,

Kila binadamu anafanya makosa na kujirudi pole sana kwa kupotea njia lakini nakupongeza pia kwa kujitambua.

Yupo wapi yule mwanajeshi wa Chadema kaenda jela kwa sababu ya Chadema kaacha familia yake siyo Lema wa Dr Slaa ambaye amejitokeza kuwasaidia japo chakula achilia mbali kuwasomesha watoto wa mwanajeshi wao.

Mpaka leo familia ya kamanda aliyepigwa risasi kwenye maandamano Arusha wameitelekeza mpaka mke wa marehemu kaamia CUF.

Sasa hivi Heche anatembea na DVD ya mauaji ya Mwangosi kuchangisha pesa Ulaya wakati familia ya marehemu hawapgati hata mia.
 
Last edited by a moderator:
Ha haaaaaaaa haaaaaaa, Lema akachukua mfuko wa pesa na kutokomea siyo?

Wajinga ndio waliwao.
 
Pipe minded man, sidhani kama unaishi uingereza wewe mtu mwenye mawazo mgando kiasi hicho. Si kwamba ulitoka Chadema kwa kuwa hukuona cha maana ila kwa sababu hukupata kile ambacho ulitegemea kukipata pale ulipokuwa unajiunga na CHADEMA yaani fedha ambazo ccm wanazigawa kama njugu kwa kuwa wanazipata kwa kutufisadi Watanzania. Sasa CHADEMA hatufanyi kitu kama hicho ninaomba uache kuwashawishi wengine kukihama chama na nina imani hakuna atakayeweza kukusikia kwani hata uwezo wako wa kufikiria ni mdogo sana. Naomba Kristu mfufuka akubadilishe, Amina.
 
Utaondoka kama ulivyo kuja, usitegemee kuna utakao mshawishi aondoke chadema. Hakuna kina asiye kuwa na msimamo na asiye jielewa labda wewe tu. isitoshe wewe ni kijana sura lakini akili zishazeeka kutokana na matendo yako. mia
 
Mvinyo wa Pasaka mbaya sana , hasa ukinywea kwenye pub iliyombali na nyumbani.

Hivi , kama huyo kijana anayemsema wa Iringa alikuwa hana hata nauli ya basi kurejea kwao, za mchango alitoa wapi? Ama alikuwa katumwa kazi maalum na alipobainika kafungiwa nje? Jambo hili linanifikirisha sana.

Dili , ni wewe na tenda yako ya bandarini dar, tutakufuatilia kama unalipia kodi zote halali ,maana CCM ni kichaka cha wezi.....

Nilicheka sana kwa tabia chafu aliyoonyesha baada ya kuja Bongo kutoka majuu na kulazimisha apewe vyeo.Alipojibiwa kwamba CHADEMA tunagawana majukumu na sio vyeo akaanza kutukana CHADEMA na kwa hasira akahamia kule kwa wapiga deal wa mjini wenye ujasiri wa kuunda vyeo hadi wizara maalumu bila potfolio

-Jamaa alipoambiwa kuna utaratibu yeye aliahindwa kuonyesha professionalism na courtesy ya kawaida tu aliyojaaliwa baada ya kuwa na exposure ya kuishi First World akatanguliza uroho wa madaraka na tamaa nyingine mbele

Kama aina ya vijana anaowatahadharisha ni vijana wa aina yake basi yupo sahihi maana anapunguza kazi nzito ya kuwachuja hawa.

Kwamba vijana wasiofuata katiba,taratibu na maadili ya chama katika kukosoa hawastahili kuingia CHADEMA au chama chochote makini,hilo ni sahihi na ninamuunga mkono.

Kwamba alikua hakijui CHADEMA vizuri inawezekana maana alizunguka UK nzima akisukumwa na tamaa na uroho wa cheo atajaporudi na hakujihangaisha kuisoma katiba ya CHADEMA na kuelewa Taratibu na kanuni.

Kwamba inawezekana tamaa na uroho wake umempunguzia uwezo wa kufikiri na kuingia CCM inawezekana.Pengine kwa kuwa hana dhamira ya dhati ya mabadiliko na kwamba hadi muda huu hawezi kujifunza na kuijua CCM kwa kuwa ni msomi asiyependa tafiti hilo liko wazi.

Huyu ni msomi aliyetanguliza Ideology ya vyeo,uroho wa madaraka na majungu badala ya sera iliyojengwa juu ya Itikadi.Ndiyo maana ukimuuliza hapa muda huu ataje uhusiano uliopo kati ya Itikadi ya CHADEMA na CCM ni upi hadi ahamie CCM badala ya kuingia CUF au chama cha UPDP cha Dovutwa hawezi kukuambia.Kama anabisha muulizeni hili alijibu kwa weledi

Huyu hakufaa hata kuwa mwenyekiti wa kitongoji au mtaa maanake hata kesi ndogo za kifamilia zitakapopelekwa kwake ataishia kutoa uamuzi kwa kulenga prism ya jinsi atakavyonufaika binafsi kutokana na mgogoro huo.Tamaa ni mbaya sana na nampa hongera kwa kuwatahadharisha vijana wenye tabia,hulka na fikra kama zake.Wataumbuka,maana kitawakuta kilichompata yeye

Ni kiongozi gani anashindwa kufikiria mtu ameleta mchango wa harambee kwa basi kutoka Iringa huku ikijulikana kuna MPESA ambazo zina-facilitate transaction.

Fikra mgando hizi hazina chembe ya creativity bali ni mambo yale yale ya fikra mgando tu kama jambo dogo kama hili mtu unashindwa kufanya uamuzi sahihi.

Hongera kwa kuwatahadharisha vijana wa aina yako.

Juvenile Gibberish ! ! !
 
Mwendelezo...teh..teh..teh...nangoja ingine tena.kweli kazi ipo.naomba LUKOSI KAMA SI MKOSI..unipe tafisri chama cha siasa nini manaake?...aahh..mwendelezo,poa mpe hi mtela,shonza nk...ukoko.
 
Kinachowafanya vijana wengi kutokuipenda CCM ni madhaifu, kinachowafanya baadhi ya vijana kuipenda CCM ni uoga wa maisha na ubinafsi wa kutokujali maslahi ya nchi na kufikiria kujinufaisha peke yao na familia zao.
 
Lukosi, weye ni matokeo ya wote waingiao katika siasa kwa malengo binafsi.
Tuhuma zako juu ya cdm ni baada ya kushindwa kwako kutimiza malengo yako binafsi yaliyotawaliwa na tamaa, Ulipohamia ndo kukufahako maana huku kwafahamika kama chukua chako mapema, ungana vyema na wapiga porojo na wadhalimu ya kitaaluma akina Nchemba, Kigwangallah etc
 
Kichefuchefu,usipotoshe vijana ambao ni nguvu ya taifa lijalo,tafuta njia nyingine ya kujipatia kipato
 
ONLY A FOOLISH DOG BARKS AT THE FLYING BIRDS . Pole sana kaka Lukosi kwa mawazo yako mgando yasiyo na tija kwa mstakabali na masilahi mapana ya Tanzania tuitakayo. Bora uzee kuliko uzembe wa kufikiri .Mzigo wa mawazo haya ya kijinga na kipuuzi ni zaidi ya gunia la mchanga mbichi au mavi .

Naomba utafakari nukuu hii " MWANADAMU ANAPO ACHA KUTAFAKARI MAMBO MUHIMU ANAKUWA ANAJIWEKA KWENYE KUNDI LA WANYAMA WENGINE. ANAWEZA KUISHI NA KUTENDA KAMA WANYAMA WENGINE. MUNGU ALITUPATIA AKILI NA UTASHI NA KUTENDA KWA KUTAFAKARI . NDIYO MAANA TUNAFIKIA HATUA YA KUWA NA MAADILI, UTAMADUNI,MIIKO, MIONGOZO, MIFUMO NA FALSAFA YA KUTUONGOZA KATIKA MAISHA ." By Padre Privatus Karugendo , January 2 ,2013 kwenye makala yake Raia mwema. Hongera kujitia umbumbu wakati ukijua fika kuwa ccm ni kichaka cha kupigia dili zenu.
 
Nilicheka sana kwa tabia chafu aliyoonyesha baada ya kuja Bongo kutoka majuu na kulazimisha apewe vyeo.Alipojibiwa kwamba CHADEMA tunagawana majukumu na sio vyeo akaanza kutukana CHADEMA na kwa hasira akahamia kule kwa wapiga deal wa mjini wenye ujasiri wa kuunda vyeo hadi wizara maalumu bila potfolio

-Jamaa alipoambiwa kuna utaratibu yeye aliahindwa kuonyesha professionalism na courtesy ya kawaida tu aliyojaaliwa baada ya kuwa na exposure ya kuishi First World akatanguliza uroho wa madaraka na tamaa nyingine mbele

Kama aina ya vijana anaowatahadharisha ni vijana wa aina yake basi yupo sahihi maana anapunguza kazi nzito ya kuwachuja hawa.

Kwamba vijana wasiofuata katiba,taratibu na maadili ya chama katika kukosoa hawastahili kuingia CHADEMA au chama chochote makini,hilo ni sahihi na ninamuunga mkono.

Kwamba alikua hakijui CHADEMA vizuri inawezekana maana alizunguka UK nzima akisukumwa na tamaa na uroho wa cheo atajaporudi na hakujihangaisha kuisoma katiba ya CHADEMA na kuelewa Taratibu na kanuni.

Kwamba inawezekana tamaa na uroho wake umempunguzia uwezo wa kufikiri na kuingia CCM inawezekana.Pengine kwa kuwa hana dhamira ya dhati ya mabadiliko na kwamba hadi muda huu hawezi kujifunza na kuijua CCM kwa kuwa ni msomi asiyependa tafiti hilo liko wazi.

Huyu ni msomi aliyetanguliza Ideology ya vyeo,uroho wa madaraka na majungu badala ya sera iliyojengwa juu ya Itikadi.Ndiyo maana ukimuuliza hapa muda huu ataje uhusiano uliopo kati ya Itikadi ya CHADEMA na CCM ni upi hadi ahamie CCM badala ya kuingia CUF au chama cha UPDP cha Dovutwa hawezi kukuambia.Kama anabisha muulizeni hili alijibu kwa weledi
Ben habari yako kamanda,
Cheo tayari nilikuwa nacho.
Mimi sio tu nilikuwa mwenyekiti wa Chadema UK, bali nilikuwa kiongozi wa M4C.
Hiyo single unayotaka kuleta usiirekodi haitauza
 
Jamaa kweli Chadema hawampi usingizi.muulizeni wanachama wa chadema wangapi ameondoka nao tokea atimuliwe
Hata hilo tawi la CCM hapa Uk hawamfahamu.Tuko kwenye pasaka tunamkubuka sana Yuda ambaye
hana tofauti na Chris
 
Inasikitisha sana kusoma Utumbo mchafu ulioandikwa na Chris Lukosi, kwa ujumla hakuna hoja ya msingi zaidi ya blah blah za Lumumba.

*Nimejaribu kutafuta sababu za msingi zilizomfanya ahame CHADEMA lakini sijaziona, zaidi ni zile zile propaganda za muda mrefu sana za CCM ambazo hata yeye anazijua kabla hajahamia CCM na vitu vya kufikirika tu.

*Tulitegemea atuambie zile kasoro za msingi zilizopo CCM(Rushwa, Ufisadi, Uuaji, Uchakachuaji, Usanii, Wizi, Usultani, Hila nk) ambazo alikuwa akizisema humu JF wakati akiwa mpinzani zimekwenda wapi mpaka arudi CCM?

*Sote tunajua alikuja CCM baada ya kupewa vitisho vya kibiashara na pia kupewa ahadi ya kupewa tender ya TBS ya ukaguzi wa magari nje ya nchi lakini akachezewa KARATA TATU na tender akaikosa mazima, na sasa anatuambia anataka kuja Iringa mjini 2015 kuja kugombea Ubunge kupitia CCM, nafikiri wakati ukifika hasa baada ya kura za maoni atakuja humu mtandaoni kutupa feedback kuhusu CCM.
 
Last edited by a moderator:
Ben habari yako kamanda,
Cheo tayari nilikuwa nacho.
Mimi sio tu nilikuwa mwenyekiti wa Chadema UK, bali nilikuwa kiongozi wa M4C.
Hiyo single unayotaka kuleta usiirekodi haitauza

Kamanda hilo la kutaka kuwapangia watu wakuahidi watakupa cheo gani huko baadae lilikushusha sana mkuu.Ni tabia mbaya sana sana kukasirika unapojibiwa kistaarabu kwamba utaratibu wetu si kupeana vyeo bali kugawana majukumu.

Jibu swali la ideologies hapo juu kati ya CCM na CHADEMA.Je ulihamia huko kwa kuwa.walibadilika au wewe ndiye uliyebadilika kiitikadi?
 
Rafiki unaweza kupunguza kasi ya maneno yako.
inawezekana wengi hawakujui.
unakumbuka ulipokuja nyumbani kwetu,Japo sikuwapo lakini kamera ilikuchukua pamoja na mazungumzo yote.hivyo najua.

Umasikini wa Roho na akili ni janga linalowatesa vijana kama wewe.Shida ndizo zinazokufanya uandike hapa na pale.
nisinge penda kuongea mengi,kilichonikwaza ni baada ya kutazama mkanda,nakujua nini kilikusibu mpaka kwenda ccm,halafu unakuja kuwadanganya watu hapa.

Waambie basi ulikuwa unataka tenda serikalini na namna ulivyosumbuliwa,tueleze makubaliano baada ya usumbufu huo wa mda mrefu na jinsi ulivyokuja kuongwa kadi ya ccm.
Tuambie kwanini serikali ilikuwa inakusumbua na mwisho uje uongee pumba zako.

Nakupa pole sana.Unafikiri umepata kumbe umepatikana,unakula matapishi yako tukuitaje wewe?
 
Back
Top Bottom