Vigogo walioenda kunywa dawa kwa mchungaji loliondo

mi mbona nilienda hujaniandika una ubaguzi sio? Afu hawa viongozi nao si ni bin adam wanaugua pia we vp? Surely hii jf imevamiwa!!!!!!!!!!!
 
Habari za Kiinteligensia na za kuaminika zinasema viongozi wafuatao walienda mapema sana kwa Mch. Loliondo kunywa dawa,

1. JK na first lady, ndo maana siku hizi haanguki, alienda January,
2. Edward Lowasa.
3. Generali Mwamunyange
4. Bernard Membe

5. Magufuli
6. Mizengo Pinda,
Na wengine wengi tu.

SWALA kubwa hapa ni kwamba, hawa viongozi wote wametibiwa, na kuna waliotoa ushuhuda kuwa wamepona, sasa kwanini wizara ya afya inamkataza mch. asitoe huduma, wakati huduma yake inaponyesha kweli, hawa viongozi wakuu kwanini wasimsaidie mzee kurekebisha mazingira ya kufanyia kazi yake vizuri ili na wengine wapate huduma yake kama wao walivopata. Badala yake wizara ya afya imesimamisha huduma bila kujali kwamba wanawanyima watu wengine huduma ya kupona pia.


Hao uliowataja huenda wametibiwa kabla ya sasa ambapo kumefurika watu ile mbaya na hakuna huduma nzuri za Afya hivyo panaweza kutokea magonjwa ya kuharisha na kutapika au kipindipindu na kuleta madhara makuwa zaidi!!! hivyo ni sawa Wizara husika kusimamisha huduma hiyo huko porini!!!

Jamani issue zingine tutumie akili zetu na tuache ushabiki na chuki binafsi!!!!
 
Imani za ile dawa zinasema endapo serikali itapiga marufuku dawa hiyo basi wale wote watakaohusika kwa njia moja au nyingine kufanikisha hilo hata kama waliwahi kunywa ile dawa itaacha kufanya kazi na magonjwa yao yatawarudia vibaya sana.

Kwa hiyo nawaonya tu watu wa serikali wasizuie chochote kuhusu dawa hii ila waweke utaratibu mzuri watu waende kule, haya mambo ya kupima ubora wa dawa kwenye maabala hautasaidia kitu mtapima taona ni sumu na haifai kwa matumizi ya binadamu je mtasemaje? na kwa nini mnataka babu hadi apate cheti cha huduma? haya yote ni kumdhihaki mwenyezi Mungu, hatapenda.

Kwa akili ya kawaida hivi unaweza kupona KANSA, UKIMWI, SUKARI, PUMU, KIFUA KIKUU kwa kunywa glass ya moja ya maji ya dawa na kisha dawa kuanza kufanya kazi mara moja? Kama hupati jibu basi fahamu ya kwamba mwenyezi Mungu ameshusha neema yake kupitia kwa huyu mchungaji.
Waziri wa afya na nyie vyombo vya usalama please kwekeni mchakato mzuri tu wote wenye shida twende kwa babu.
 
Lets respect one"s privacy they have the right not to disclose their identity
Tusiende mbali tuheshimiane katika mambo mengine ila inashangaza kwa nini hawatoi supprt taifa lipate tiba?????
 
Kuna habari kwamba kuna meli ya wahindi na waarabu wanakuja kwa Babu kutibiwa, sasa si ingelikuwa ndia wakati mzuri kwa Waziri wa Utalii kumuwezesha Babu, kwani kutalii sio kuona wanyama pori tuu, masomo na matibabu is part of it.

Is this a cynical or racist remark??or these people human being like others seeking medical treatment...
 
wao wameshapona hawaoni umuhimu wa mchungaji tena!! hiii nji hiii hiii nji MUNGU ndo anaijua peke yake
 
ha ha ha ha God made man, Man made money, money made man mad. Mi ninivojua hamna tiba pale sema watu wanapata releaf tu afu si mnajua haya mambo ynaendana na imani?

Na jinsi watu tulivoisha mboa sir God hamna tiba pale. Mvua tu katubania ije iwe dawa ya haya maginjwa?

Sijui ........ Let us pray oooh jizuz di shuu...........
 
kupindua hii nchi ni rahisi sanaa imagine kama Mkulu alienda halafu ananyweshwa sumu...na btw hiyo dawa inahitaji imani ina maana Mkulu ashabatizwa!
 
mchungaji anatakiwa kusajili maombi, kazi itaendelea tu . . .

Mchungaji Mwasapile hapaswi kusajili kwani ni Mchungaji aliyebarikiwa (ordained) labda avae mavazi ya kichungaji wakati wa kushirikisha (kugawa) dawa na anapofanya maombi. Maaskofu (wasimamizi) wa KKKT wanaitambua huduma yake kwamba ni ya kichungaji.
 
BAADA ya kutumia musuli wa fedha na kuweza kuonana na Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila wilayani Loliondo mkoani Arusha, na kuwaacha wanyonge wakisota, sasa vigogo hao huenda mambo yakawatumbukia nyongo.

Mchungaji Masapila ameapa kuwa vigogo waliofanya hivyo kwa kutumia njia za mkato na kufanikiwa kumwona na kunywa dawa, hawatapona magonjwa sugu yanayowakabili.

Mchungaji huyo mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) amesema hali hiyo imesababishwa na kitendo chao cha kukiuka baadhi ya masharti ya tiba yake ambayo inakataza kufanyiwa biashara na wala kupewa upendeleo.

Hivi karibuni, baadhi ya maofisa wenye vyeo katika sekta mbalimbali nchini,
walidaiwa kutumia nafasi zao kushawishi askari wanaolinda usalama katika makazi ya Mchungaji Masapila, ili kuwavusha foleni na kupata tiba haraka.

Polisi walio eneo hilo kijijini Samunge, tarafa Sale, pia wamedaiwa kutumia nafasi zao kupitisha ndugu, jamaa na marafiki zao, jambo ambalo Mchungaji Masapila alionya kuwa halitawasaidia kwani dawa hiyo haifanyi kazi katika mazingira hayo.

"Huu ni uponyaji wa Mungu na Mungu huwa hatambui cheo au nafasi ya mtu, ukikosea utaratibu dawa inabaki kuwa maji ya kawaida," alifafanua Masapila.

Maelfu ya watu kutoka pande zote za nchi na nchi jirani wako katika kijiji hicho kwenye mbuga ya Sonjo, kata ya Digo-digo, Ngorongoro wakitumaini kupata tiba hiyo ya ajabu.

Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali, alisema jana kuwa ofisi yake inafikiria kutenga siku maalumu na hasa Jumamosi, kwa watumishi wa umma na Serikali kwenda kupata tiba hiyo ili kupunguza msongamano na kuwawezesha kurudi mapema kwenye kazi zao za utumishi kwa Taifa.

Hata hivyo, haijulikani kama Mchungaji Masapila atakubaliana na wazo hilo, kwa maana alisisitiza kuwa mtoaji huyo wa dawa anazingatia kutokuwapo kwa upendeleo katika utoaji tiba hiyo.

Katikati ya wiki hii, vurugu zilidaiwa kuzuka karibu na eneo la tiba, baada ya watu wanaodhaniwa kuwa vigogo kulazimisha kuwapita wananchi wengine waliopanga foleni kwa ajili ya kupata tiba.

Hivi sasa watu wanalazimika kukesha kwa siku nne wakisubiri zamu ya kupewa dawa na Mchungaji Masapila ambaye sasa amepata usaidizi wa wachungaji wengine watatu wanaomsaidia kuchota dawa.

Hata hivyo, Masapila analazimika kugawa dawa hiyo kwa mkono wake mwenyewe, maana bila hivyo, tiba hiyo inayotokana na mizizi iliyochemshwa na maji, haitafanya kazi.

Mkazi wa Sonjo aliyevamia moja ya masufuria na kujichotea dawa na kuinywa Jumatatu alipata msukosuko mkubwa kwani tumbo lilipata maumivu makali na kulazimisha ‘Babu’ Masapila kuingilia kati kumsaidia.

Wakati hayo yakiendelea, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Akili Mpwapwa, alisema Jeshi bado halijapokea taarifa rasmi za vifo vinavyodaiwa kutokea katika mbuga ya Sonjo ambako maelfu wamepiga kambi wakisubiri tiba.

Hata hivyo Lali juzi alithibitisha vifo sita kati ya 14 vinavyodaiwa kutokea katika eneo la Samunge.

Lali alipozungumza jana na gazeti hili, alisema misururu ya watu wanaofuata matibabu imepungua na kubaki umbali wa kilometa 15 huku magari yakibaki kati ya 1,000 na 1,500 kutoka ya awali 3,000.

Alisema katika magari hayo yakiwamo malori na mabasi na magari madogo kila gari lina watu wasiopungua watano.

Kwa mujibu wa Lali, mtu mmoja alifariki dunia wakati akisubiri matibabu na alikutwa jana walipotembelea eneo hilo.

Mkuu wa Wilaya alisema watu wamekuwa wabishi kwa kutoa wagonjwa hospitalini wakiwa mahututi na kuwaweka mistarini kwa ajili ya kupata dawa na hivyo kuzidiwa na kufariki dunia.

Mchungaji Masapila hutoa dawa hizo anazodai kuoteshwa na Mungu kwa Sh. 500 huku akidai kutibu magonjwa sugu yakiwamo ya Ukimwi, pumu, kisukari na mengineyo huku dozi yake ikiwa kikombe kimoja tu cha dawa hiyo.

Inadaiwa kuwa kutokana na misururu hiyo, gharama za magari zimeendelea kupanda kwani sasa wanaokwenda kwa magari ya kitalii wanalazimika kulipa kati ya Sh. 120,000 na Sh 150,000 na mabasi ni kati ya Sh 30,000 na Sh 50,000.
 
jesuit wewe ni shoga na ndio maana kila chenye maana kwa jamii unapinga sasa 2takutongoza ili 2one kama utakataa au utakubali.?

Bora umwambie maana watu wengine sijui vipi, kila kitu anapinga bila hata kufikiri, vitu vingine viko wazi kabisa
 
Kuna Nesi.muuguzi wa Afya katoa ushuhuda leo asubuhi.Pia wako wafanyakazi wa serikali kadhaa wametoroka makazini kufuata dawa Loliondo.

Babu Mchungaji angesaidiwa kwa kuwekewa mazingira mazuri ili afidie pengo lililopo kwenye huduma za Afya nchini.
wewe nitakuamini
 
Hao uliowataja huenda wametibiwa kabla ya sasa ambapo kumefurika watu ile mbaya na hakuna huduma nzuri za Afya hivyo panaweza kutokea magonjwa ya kuharisha na kutapika au kipindipindu na kuleta madhara makuwa zaidi!!! hivyo ni sawa Wizara husika kusimamisha huduma hiyo huko porini!!!

Jamani issue zingine tutumie akili zetu na tuache ushabiki na chuki binafsi!!!!
Badala ya kusimamisha huduma, kwa nini wizara ya afya isimsaidie Babu kwa kuweka mazingira mazuri ili kuepusha magonjwa ya kuripuka? Kusimamisha huduma ndiyo solution?
 
Nilimuona Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro mama Nsilo Swai akipata kikombe, soo Viongozi wote wa CCM wagonjwa? tunangoja mkuu makamba nae akapate kikombe anaweza akapunguza kuropoka.
 
Huu ni utoto wa hali ya juu na kusema ukweli ni kushu sha hadhi ya hii forum. Let's put politics aside and respect other's privacy, period! Afterall, they have done the right thing.

What respect, mkuu??
 
Hapo ndio mtu utajiuliza unafiki wa viongozi wetu ! Wanajijali wao wanasahau wengine! Yaani baada ya wao kwenda na kufanikiwa sasa wamezuia wengine wasipate huduma hiyo muhimu.

Hii inasikitisha sana, mimi nazani kama kweli wataendelea kuzuia watu wasihudumiwe na mchungaji, itabidi tuombe mungu magonjwa yao yawarudie, maana kama hawajali utu wa wengine au maisha ya wengine iweje wao?!
 
Back
Top Bottom