Vigogo Uhamiaji wana utajiri wa kutisha

Kaka twnsend mimi nipo shytwn walokwapua kodi zetu wapo gelezan had sasa hv kwa kukosa dhamana, but je mahakama itawafunga au nh danganya toto tu kwa watz il wasahau?
mchezo mwingine huo wa kuigiza hawatafanywa lolote mpaka jk au ccm itoke madarakani..kwani wale walioiba billions kule kishapu walifanywa nini? zaidi ya maneno
 
Tatizo huwa serikali katika kufuatilia ishu kama hii, huwa inakurupuka na haichunguzi kwanza. Itafuata upepo a vyombo vya habari, na presha ya mambo haya kuwekwa hadharani badaye itapoa na kuishia kuwaadhibu tu watumishi wa serikali walio husika na kuuacha mtandao kama ulivyo.

Miaka mingi ya nyuma nilishafanyaga hiyo biashara, hivyo naijua mwanzo mwisho, hadi nilipoiacha! Kama ilivyo kwa madawa ya kulevya ambayo hayanyeshi kama mvua (yaani, yanapita through vizuizi vyenye vyombo vya dola) ndiyo ilivyo kwa wahamiaji haramu, au wanaopita TZ kwnda nchi nyingine. Ni lazima ufanikishaji wake uhusishe maafisa wa uhamiji na kiasi kikubwa sana cha fedha. Na ushawishi kwa maafisa hawa wanaopewa ni mkubwa sana kwa wao ku-resist, such kwamba hata mkimtoa huyu, atakayekuja naye lazima afanye. Kikawaida, maafisa wa uhamiaji wanabidi wawe wanazungushwa katika vituo mbalimbali kila baada ya muda fulani, ili kuepuka kuzoea na kuzoeana, lakini utakuta afisa yupo kituo kimoja labda cha KIA kwa miaka mitatu......, jiulize, yule anayetakiwa kumbadilisha anafaidika na nini hadi amwache mtumishi huyo kwa kipindi chote hicho? Chain ni kubwa ya wanao faidika tangia makao makuu...!

Katika mtandao huu, kuna wenye connection ya wahamiaji haramu au wageni wanao pita tu tanzania. Kuna wenye connection ya kupata documents fake zinazo lingana na document original, hapa ikiwapo na mihuri ya boda na makao makuu, ambayo hubadilishwa kila mara pamoja na jinsi ya kuandika na codes mpya za uhamiaji kila mara zinapo badilishwa n.k!

Natoa mfano wa ukweli;- Zaidi ya miaka mitano iliyopita, Msomali alikuwa natoa sio chini ya dola elfu tatu kwa afisa atakaye mpandisha kwenye ndege ya kwenda ulaya au amerika, na mara nyingi huwa wawili au watatu kwa mkupuo. Mbali na fedha hizo ni kuwa atakuwa amenunua tiketi ya ndege, amegongewa residence permit ya Tz ili impe uhalali wa kuanzia safari Tz, na kwenye Ppt yake hana haja ya kuwa na viza original zaidi ya scaned visa ambavyo vyote amelipia. Shida yao kuu ni kuingia kwenye ndge, wakiwa angani kwenye ndege has KLM au SWISS, huchana ppt na docs zao zote na kudumbukiza vyooni wakiwa angani, wakiteremka husema wao ni wakimbizi na kujifanya wanachokiweza kusema ni neno "refugee" tu, na hawasemi wamekuja kutokea wapi. Wasomali walikuwa wanatoa sio chini ya dola elfu moja kwa kuwawezesha kufika South Africa, usafiri wanalipa wenyewe na mahali pa kuishi, wanachotaka ni documents za tanzania hata ziwe fake ili waweze kuzitumia nje ya tanzania to south afrika, weka maanani kuwa nchi ambazo wageni hao wanapitia nchi hizo hawawezi kuthibitisha uhalisi wa travelling docs hizo, mara nyingi hutumia temporay travelling docs nk.

Kwa wanaoishi hapa nchini kinyume na taratibu, huwa wanawezeshwa na maafisa fulani wa uhamiaji ambao hulipwa kila mda fulani na wageni hao, na hata vitengo vya uhamiaji "investigation departmnt" vilivyopo kila wilaya wakati vinaenda kukagua lets say Murza, sasa kabla hawajafika tayari Murza ana taarifa kuwa uhamijai wanakuja na anachofanya ni kuwaficha wahamiaji haramu au kuwaambia wasije kazini siku hiyo.

Mambo ni mengi na makubwa sana....lakini serikali haitakiwi kukurupuka kwakuwa fulani katajwa au ana kiasi kibwa cha fedha.....sawa imchukulie hatua stahiki.....lakini ni lazima serikali iingizwe darasani kujua ni jinsi gani itapambana na mtandao. Ina maana serikali haijui kuwa wasomali woote wanaoenda nje kupitia TZ, lazima wa'camp temeke kwanza wakati mambo yao yanashughulikiwa?

Kibanga Msese
 
Back
Top Bottom