Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 877
- 4,106
Kilichojibiwa na Idara ya Uhamiaji ndicho kinachoitwa majibu katika macho ya sheria. Si kila bendera ya kijani ni bendera ya CCM na siyo kila bendera ya kijani yenye nembo ya CCM siyo mali ya CCM.
Kamishna wa Uhamiaji Manyara amepewa nguvu ya kufanya uchunguzi kwa mijubu wa sheria ya Uhamiaji. Kwa kweli mimi nimependa majibu yake kwa sababu amejibu kwa ufupi ila akizingatia sheria inayosimamia. Awali niliunga mkono kile kinachoshabikiwa katika mtandao wa X lakini nimelazimika kwenda kusoma sheria ya Uhamiaji.
Kifungu cha 46 cha sheria ya Uhamiaji ya mwaka 2016 kinasema ni kosa kusafirisha au kufanya ulanguzi wa binadamu. Faini yake ni kifungo kisichopungua miaka ishirini au faini isiyopungua milioni tano. Kifungu hicho kinasema pia kifaa kinachotumika kwenye magendo kutaifishwa.
Nakubaliana na Kamishna huyu kwamba lile gari siyo mali ya chama cha mapinduzi. Lakini pia hata wale waliotoa taarifa za umiliki wanakiri kwamba lile gari siyo mali ya chama cha mapinduzi bali ni la mwanachama na kiongozi wa chama cha mapinduzi. Kwa tafsiri nyingine mali za kiongozi wa chama siyo mali za chama na uhalifu wa kiongozi wa chama siyo uhalifu wa chama cha siasa.
Kuhusu Bendera; nakubaliana naye pia kwamba bendera ile siyo mali ya chama cha mapinduzi ila inafanana na bendera ya chama cha mapinduzi.
Kuhusu wito wa kutohusisha uhalifu ule na chama cha mapinduzi; nakubaliana naye kwamb uhalifu wa kijana yule siyo uhalifu wa chama na hakuna sheria inayoweza kuthibitisha chama kuhusika.
Pamoja na kukubaliana naye napenda kuwatahadharisha sana viongozi wa kisiasa kusoma kifungu hiki cha 46 cha sheria ya Uhamiaji.
Viongozi wa kisiasa wengi mnamiliki magari na hayo magari mnawapa madereva ambao nafsi zao zimeficha siri kubwa. Kumbukeni kesi ya kubumba ya Mbowe.
Kifungu hiki cha sheria ambacho Uhamiaji wanakwenda kukitumia kutaifisha ile gari kinatoa adhabu ya faini kwa Dreva aliyekamatwa na kwa aina ya kesi hii naamini yule kijana atalipa faini kwa kukiri makosa na gari itaitishwa.
Swali lakujiuliza, hakuna uwezekano wakawepo vijana kama huyu watakaotumika kutumia magari ya viongozi wa upinzani kisha wakikamatwa hayo magari yataifishwe? Siku likikamatwa gari lenye bendera ya chadema tutafurahia kusikia vyombo vya dola vikisema gari husika ni mali ya chadema? Tutafurahia kuona mali binafsi za kiongozi wa chadema zikiitwa mali za chadema?
Tukubali kujifunza yafuatayo
1. Mali ya mtu binafsi inapotumika kutenda uhalifu isihusishwe na taasisi
2. Viongozi wa vyama vya upinzani chukueni sana taadhari mnapowapa watu magari yenu kwani binadamu mwenye nia ovu hana alama
3. Wenye nyumba za kupanga na vyombo vya usafiri someni sheria hiyo ya uhamiaji msijejutia mtakapoambiwa mali zenu zimetumika kuhifadhi wahamiaji haramu.
Mwanagenzi
Soma Uhamiaji: Dereva na V8 Iliyobeba wahamiaji Haramu 20 wa Ethiopia Isihusishwe na CCM