Niliandika Mwaka 2022 kuhusu vigogo Kutumia Bendera ya CCM Kusafirisha Wahamiaji

Mdude_Nyagali

Member
Dec 11, 2022
60
1,237
16 Novemba 2022 niliandika katika mtandao wa Twitter au X kama unavyoitwa kwa sasa kwamba vigogo wengi ndani ya CCM wanatumia bendera za CCM hasa wakati wa chaguzi kusafirisha wahamiaji haramu. Miezi 16 baadaye yani March 24, 2024 linakamatwa gari lenye bendera ya CCM likisafirisha wahamiaji haramu.

Watu wengi wako CCM sio kwa ajili ya maslahi ya nchi isipokuwa wengi wako huko kwa ajili ya maslahi binafsi. Bendera ya CCM inatumika kama kichaka cha kuficha wezi na kuliumiza taifa.

Mtandao huu wa kusafirisha wahamiaji haramu ni mkubwa sana unahitaji vyombo vya kimataifa kuudhibiti. Nikiwa gerezani nilifanya uchunguzi kiasi kuhusu biashara hii ya human trafficking kilichonisikitisha ni kwamba wengi wanaofanya biashara hii ni vigogo wa ccm na polisi. Mmoja wa vigogo wa polisi nilimuonya wakati wa kikao cha wiki ya sheria kilichowashirikisha wafungwa, mahabusu na wadau wa sheria wakiwepo polisi pale gerezani. Nilimuambia ajichunge kuna mafaili yake mabaya. Mwaka mmoja baadaye 2022 vigogo wawili wa polisi akiwemo yule mmoja niliyemuonya walikamatwa Mbeya wakisafirisha wahamiaji haramu wakawekwa lock up kisha baadaye wakahamishwa vituo vya kazi kama adhabu bila kufikishwa mahakamani wala kufukuzwa kazi. Hii inadhihilisha kwamba biashara hii ina mtandao mkubwa.

Huko Iringa kada, mfadhili na kiongozi wa CCM magari yake yalikamatwa yakisafirisha wahamiaji haramu. Kilichotokea ni kwamba magari hayo yaliachiwa na baadaye madereva wake waliachiwa huku afisa uhamiaji aliyeonyesha uzalendo wa kuhakikisha kesi hiyo inafika mahakamani alijikuta kwenye matatizo. Kumbuka sheria ya kusafirisha wahamiaji haramu ni kifungo cha miaka isiyopungua 20 jela na kutaifisha gari zilizokamatwa katika biashara hiyo.

Kwa kumalizia ni kwamba wanaCCM wa kweli ni mzee Warioba na Mzee Butiku hawa wengine ni vibaka tu wanaotumia CCM kwa maslahi yao bianafsi.

Mdude Mpaluka Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.

Pia soma > Asafirisha wahamiaji 20 kwa V8 yenye bendera ya CCM

GridArt_20240325_81514477.jpg
 
View attachment 2944066
Siyo Siri, Waovu na Wahalifu wengi hapa nchini (na hata ktk baadhi ya nchi zingine) huwa wanaficha uovu wao kwa kujiunga au kushabikia chama kinachotawala ktk nchi. Ukifuatilia au ukiwachunguza kwa undani sana hao Viongozi wa Serikali au wa Chama Tawala ambao wanaojifanya kuwa ni watu safi sana katika jamii au kujionyesha kwa watu kuwa ni watu wema, kiuhalisia utagundua kuwa ni watu wabaya sana, ni watu waovu na wahalifu wakubwa sana. Wengi wao mikono yao imejaa damu za watu. Kwa kifupi hao ni watu waovu wabaya sana kuwazidi hata Mashetani kwa uovu, 'The Snakes in Suits,' na Chama Tawala huwa ni mtetezi wao mkuu wakati uovu wao unapofichuka.
 
Wananchi ndio wanaibebaga ccm japo haifai kuwepo madarakani
Wananchi gani hao ambao wamekuwa wanaibeba CCM???? Usione ukadhani!
Hata hao wananchi au watu unaowaona huko mitaani ambao wanaishabikia CCM usidhani kwamba kweli Wana upendo wa dhati na CCM, wengi wao ni wanafiki tu, wanafanya hivyo kinafiki ili mambo yao yaende au kwa kuogopa kwamba watashughulikiwa na Watawala waovu waliopo endapo kama watabainika kwamba wanakwenda kinyume na matakwa ya CCM. Je, haujawahi kusikia msemo huko mtaani uliko unaosema kwamba 'wataku-Kolimba'?Haujawahi kusikia???
Kumbuka kwamba CCM ni Chama-Dola,
 
Umelidandia na hili baada la Mgodi wa Kitunda kubuma. La DAS na mafuta kudunda sasa unatafutia Kiki hili.

Mi sio mwana CCM ila kutumia bendera ya CCM hakujustify kuwa katumwa na CCM. Hili nalo sio la kutumia nguvu kufikiria wala kulishupalia mkuu. Bendeara za CCM au CDM zipo tu mtaani. Hata mi naweza nunua za CDM na kukutwa navutia nazo bangi, haitajustify kuwa nimetumwa na CDM mkuu.
 
Back
Top Bottom