Vigogo Uhamiaji wana utajiri wa kutisha

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Rais Jakaya Kikwete akifafanua jambo siku zilizopita
TUME YA KUWACHUNGUZA YAANZA KAZI LEO, WAHAMISHIWA MIKOANI KIAINA
Mwandishi Wetu

KASHFA nyingine imeibuliwa katika Idara ya Uhamiaji.Taarifa mpya yenye kurasa tano, imewataja vigogo hao saba wakidaiwa kuwa na utajiri wa kutisha.Taarifa hiyo ambayo tunayo nakala yake, imedai kuwa vigogo hao wanamiliki mali

na mamilioni ya shilingi katika akaunti zao binafsi.Maofisa saba wametajwa kwa majina na vituo vyao vya kazi ambavyo ni Lindi, Dar es Salaam, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) na Moshi.
Tuhuma hizo zimekuja wakati Tume Maalumu iliyoundwa kuchunguza tuhuma za ufisadi na utoaji wa vibali bandia kwa wageni, ikitajwa

kuanza kazi juzi. Hata hivyo, habari kutoka wizarani zinaeleza kuwa timu hiyo itaanza rasmi kazi zake leo.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Uhamiaji, zimedai kuwa baadhi ya wajumbe wa tume hiyo wamemhoji meneja wa benki moja kubwa ya Moshi ili kupata ukweli wa madai kuwa kigogo mmoja wa Uhamiaji mwenye cheo cha Naibu Kamishna (DCI), anamiliki akaunti ya fedha za kigeni.

Kigogo huyo anahusishwa pia na mtandao wa utoaji vibali bandia kwa raia wa kigeni wanaofanya kazi mkoani Kilimanjaro au kufanya kazi za kujitolea.

Ripoti hiyo imetaja taasisi 13, zikiwamo zisizo za kiserikali (NGO), hospitali na hoteli za kitalii zinazodaiwa wageni wake walipewa vibali bandia.

Mbali na kumhoji meneja huyo, inadaiwa pia walifanya mahojiano na uongozi wa kiwanda kimoja kinachodaiwa kukutwa na vibali bandia vya wageni 84.

Taarifa hizo zilidai kuwa maofisa wengine waandamizi wa Uhamiaji kutoka Makao Makuu, Dar es Salaam walitarajiwa kuwasili Moshi juzi kuungana na wenzao.

Baadhi ya maofisa waliotajwa katika ripoti hiyo kwamba wana utajiri ni wale waliokumbwa na uhamisho katika idara hiyo, Kia miezi mitatu iliyopita.

Katika ripoti hiyo, kigogo mmoja mwenye cheo cha DCI anadaiwa kukutwa na Sh700 milioni katika akaunti yake, achilia mbali kumiliki mali za mamilioni.

Mbali na maofisa hao kumiliki mamilioni ya fedha taslimu, pia wanadaiwa kufanya kufuru ya kununua magari ya kifahari, nyumba na viwanja.

Ripoti hiyo inayodaiwa kuandikwa na Maofisa Uhamiaji wazalendo, imepinga hatua ya kuhamishwa kutoka kituo kimoja kwenda kingine, maofisa wanaotuhumiwa kukutwa na utajiri ambao haulingani na vipato vyao.

Tunataka ufanyike ukaguzi wa kina wa vibali vyote vilivyotolewa kati ya 2009/2010, 2010/2011 hadi 2012 na taasisi zote zionyeshe nakala za vibali, imedai.

Pia taarifa hiyo imependekeza wenzao wote wanaotuhumiwa kuwa na utajiri wa kutisha wachunguzwe na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Haikuwa sahihi kuwahamisha na kuishia hapo, walipaswa wapelekwe Takukuru wachunguzwe chanzo cha utajiri wao.
Pia wametaka kigogo anayemiliki akaunti ya Dola, achunguzwe ili kujua alikuwa akifanya biashara gani nje ya utumishi wa umma na kama alilipa kodi kiasi gani.

Baadhi ya maofisa Uhamiaji wamependekeza kusimamishwa kazi kwa kigogo huyo katika kipindi hiki kwa hofu ya kuingilia na kuvuruga uchunguzi.

Wiki iliyopita, Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Magnus Ulungi aliwaambia waandishi wa habari kuwa imeundwa kwa tume ya kumchunguza kigogo huyo.

Hata hivyo, taarifa zilizopatikana jana zilisema tume hiyo imepanua wigo wa uchunguzi juu ya kuwapo kwa vibali bandia katika taasisi mbalimbali.

Kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Naodha alikaririwa akisema Kilimanjaro ni moja kati ya mikoa minane inayomtia kichefuchefu nchini.

Waziri huyo alisema baadhi ya watumishi wamekuwa wakijihusisha na mtandao wa uingiaji wahamiaji haramu nchini pia kutoa vibali bandia kwa wageni.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alipoulizwa juzi kuhusu sakata hilo alisema ni vyema Uhamiaji ikapewa nafasi ya kuchunguza suala hilo kwa kuwa tayari imeshateua tume ya uchunguzi.

Kamishna Mkuu wa Uhamiaji tayari amelifanyia kazi jambo hilo kwa uzito unaostahili. Tuwape nafasi walichunguze si vyema kuanza kuingilia katika hatua hii ya mwanzo, alisema.

Wahamiaji haramu

Serikali, bila mafanikio, imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kukomesha tatizo la wahamiaji haramu linalotajwa kuwa chanzo cha utajiri wa baadhi ya vigogo wa Idara ya Uhamiaji.

Miongoni mwa mikakati iliyowahi kutangazwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ni pamoja na idara hiyo kufanya utafiti kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Mzumbe kubaini chanzo cha ongezeko la wahamiaji haramu nchini.

Akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake bungeni mwaka 2007/2008 , aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wakati huo, Joseph Mungai alisema matokeo ya utafiti huo ni kuisaidia Serikali kujua chanzo cha tatizo hilo na jinsi ya kupambana nalo kwa ufanisi zaidi.

Hatua nyingine zinazochukuliwa ni pamoja na maofisa Uhamiaji kushiriki katika vikao mbalimbali kuanzia ngazi ya vijiji, ili kuwapa wananchi elimu juu ya masuala yanayohusu uraia na jinsi ya kukabiliana na wahamiaji haramu; Kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari; Kuweka mtandao wa kompyuta katika vituo vyote vya Uhamiaji ili kuviunganisha na makao makuu.

Pamoja na Serikali kutangaza mkakati huo miaka mitano iliyopita, wahamiaji haramu limeendelea kuwa tatizo sugu linalotia doa utendaji wa idara hiyo.

Tanzania yetu Kuna Mafisadi kila sehemu nchi inanuka kwa Rushwa,na Ufisadi Ewe Mungu Saidia nchi yetu ipate viongozi wazuri.
 
Huo utajiri wa wa hao vigogo ndio unafanya Wahabeshi na Wasomali wafie kwenye malori wakiwa wanavuka mipaka. Ninaamini mtandao huo wa usafirishaji wa wahamiaji haramu ni mkubwa sana, hauwezi kuishia kwa kigogo huyo tu wa uhamiaji! Polisi wa kwenye vizuizi pia wanahusika. Haiwezekani wahamiaji haramu wakamatiwe Mbeya ilhali kuna vizuizi kibao hapo katikati kati ya Moshi/Arusha/Tanga wanakoingilia hadi kufika Mbeya.
 
Sema hawa majamaa hawakamatiki bse wana mtandao ya hali ya juu sana..na dili hzo wanapga na wakubwa manake inasikitisha mtu kuwa na mln.700 mtumish wa umma kwenye akaunti.
 
Mchezo mwingine huo wa kuigiza hawatafanywa lolote mpaka JK au CCM itoke madarakani.. kwani wale walioiba billions kule kishapu walifanywa nini? zaidi ya maneno
 
Duh! kumbe uhamiaji nako watu wanapiga hela kiasi hiki? mimi nilijua ni maliasili, TRA, bandari n.k. kumbe na huku pia wapo? dah.
 
Mwananchi

TUME YA KUWACHUNGUZA YAANZA KAZI LEO, WAHAMISHIWA MIKOANI KIAINA

KASHFA nyingine imeibuliwa katika Idara ya Uhamiaji.Taarifa mpya yenye kurasa tano, imewataja vigogo hao saba wakidaiwa kuwa na utajiri wa kutisha.Taarifa hiyo ambayo tunayo nakala yake, imedai kuwa vigogo hao wanamiliki mali na mamilioni ya shilingi katika akaunti zao binafsi.

Maofisa saba wametajwa kwa majina na vituo vyao vya kazi ambavyo ni Lindi, Dar es Salaam, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) na Moshi.

Tuhuma hizo zimekuja wakati Tume Maalumu iliyoundwa kuchunguza tuhuma za ufisadi na utoaji wa vibali bandia kwa wageni, ikitajwa kuanza kazi juzi. Hata hivyo, habari kutoka wizarani zinaeleza kuwa timu hiyo itaanza rasmi kazi zake leo.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Uhamiaji, zimedai kuwa baadhi ya wajumbe wa tume hiyo wamemhoji meneja wa benki moja kubwa ya Moshi ili kupata ukweli wa madai kuwa kigogo mmoja wa Uhamiaji mwenye cheo cha Naibu Kamishna (DCI), anamiliki akaunti ya fedha za kigeni.

Kigogo huyo anahusishwa pia na mtandao wa utoaji vibali bandia kwa raia wa kigeni wanaofanya kazi mkoani Kilimanjaro au kufanya kazi za kujitolea.

Ripoti hiyo imetaja taasisi 13, zikiwamo zisizo za kiserikali (NGO), hospitali na hoteli za kitalii zinazodaiwa wageni wake walipewa vibali bandia.

Mbali na kumhoji meneja huyo, inadaiwa pia walifanya mahojiano na uongozi wa kiwanda kimoja kinachodaiwa kukutwa na vibali bandia vya wageni 84.

Taarifa hizo zilidai kuwa maofisa wengine waandamizi wa Uhamiaji kutoka Makao Makuu, Dar es Salaam walitarajiwa kuwasili Moshi juzi kuungana na wenzao.

Baadhi ya maofisa waliotajwa katika ripoti hiyo kwamba wana utajiri ni wale waliokumbwa na uhamisho katika idara hiyo, Kia miezi mitatu iliyopita.

Katika ripoti hiyo, kigogo mmoja mwenye cheo cha DCI anadaiwa kukutwa na Sh700 milioni katika akaunti yake, achilia mbali kumiliki mali za mamilioni.

Mbali na maofisa hao kumiliki mamilioni ya fedha taslimu, pia wanadaiwa kufanya kufuru ya kununua magari ya kifahari, nyumba na viwanja.

Ripoti hiyo inayodaiwa kuandikwa na Maofisa Uhamiaji wazalendo, imepinga hatua ya kuhamishwa kutoka kituo kimoja kwenda kingine, maofisa wanaotuhumiwa kukutwa na utajiri ambao haulingani na vipato vyao.

Tunataka ufanyike ukaguzi wa kina wa vibali vyote vilivyotolewa kati ya 2009/2010, 2010/2011 hadi 2012 na taasisi zote zionyeshe nakala za vibali, imedai.

Pia taarifa hiyo imependekeza wenzao wote wanaotuhumiwa kuwa na utajiri wa kutisha wachunguzwe na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Haikuwa sahihi kuwahamisha na kuishia hapo, walipaswa wapelekwe Takukuru wachunguzwe chanzo cha utajiri wao.

Pia wametaka kigogo anayemiliki akaunti ya Dola, achunguzwe ili kujua alikuwa akifanya biashara gani nje ya utumishi wa umma na kama alilipa kodi kiasi gani.

Baadhi ya maofisa Uhamiaji wamependekeza kusimamishwa kazi kwa kigogo huyo katika kipindi hiki kwa hofu ya kuingilia na kuvuruga uchunguzi.

Wiki iliyopita, Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Magnus Ulungi aliwaambia waandishi wa habari kuwa imeundwa kwa tume ya kumchunguza kigogo huyo.

Hata hivyo, taarifa zilizopatikana jana zilisema tume hiyo imepanua wigo wa uchunguzi juu ya kuwapo kwa vibali bandia katika taasisi mbalimbali.

Kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Naodha alikaririwa akisema Kilimanjaro ni moja kati ya mikoa minane inayomtia kichefuchefu nchini.
Waziri huyo alisema baadhi ya watumishi wamekuwa wakijihusisha na mtandao wa uingiaji wahamiaji haramu nchini pia kutoa vibali bandia kwa wageni.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alipoulizwa juzi kuhusu sakata hilo alisema ni vyema Uhamiaji ikapewa nafasi ya kuchunguza suala hilo kwa kuwa tayari imeshateua tume ya uchunguzi.

Kamishna Mkuu wa Uhamiaji tayari amelifanyia kazi jambo hilo kwa uzito unaostahili. Tuwape nafasi walichunguze si vyema kuanza kuingilia katika hatua hii ya mwanzo, alisema.

Wahamiaji haramu
Serikali, bila mafanikio, imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kukomesha tatizo la wahamiaji haramu linalotajwa kuwa chanzo cha utajiri wa baadhi ya vigogo wa Idara ya Uhamiaji.

Miongoni mwa mikakati iliyowahi kutangazwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ni pamoja na idara hiyo kufanya utafiti kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Mzumbe kubaini chanzo cha ongezeko la wahamiaji haramu nchini.
Akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake bungeni mwaka 2007/2008 , aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wakati huo, Joseph Mungai alisema matokeo ya utafiti huo ni kuisaidia Serikali kujua chanzo cha tatizo hilo na jinsi ya kupambana nalo kwa ufanisi zaidi.

Hatua nyingine zinazochukuliwa ni pamoja na maofisa Uhamiaji kushiriki katika vikao mbalimbali kuanzia ngazi ya vijiji, ili kuwapa wananchi elimu juu ya masuala yanayohusu uraia na jinsi ya kukabiliana na wahamiaji haramu; Kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari; Kuweka mtandao wa kompyuta katika vituo vyote vya Uhamiaji ili kuviunganisha na makao makuu.

Pamoja na Serikali kutangaza mkakati huo miaka mitano iliyopita, wahamiaji haramu limeendelea kuwa tatizo sugu linalotia doa utendaji wa idara hiyo.
 
Kama wanakwiba na kuwekeza nchini itakuwa njema!
Maana siku izi wizi ni kila mahara wanachotofautiana ni kiasi cha fedha tuu.
Mbaya zaidi tumehama toka kwenye TSHS sasa watu wanajilipua na maUSD
 
Niliisikiaga hii kitambo tu mara yule afisa uhamiaji KIA alipohamishiwa Lindi/Ntwara kama sikosei, wonders will never end here in TZ
 
hii nchi kila mtu ni mwizi . mi namfaham traffic mmoja ana miliki dala dala 8 na tax 4 pamoja na nyumba tatu zilizoenda shule , nikajiuliza amepata kwa mshahara gani?
 
It is Another Episode here in Bongo land. Hakuna kitu hapo wakuu hii kitu ni Upepo tu. Hivi wale askari waliobainika na NIDA kwamba wamefoji vyeti issue yao imeishia wapi vile!
 
Kama wanakwiba na kuwekeza nchini itakuwa njema!
Maana siku izi wizi ni kila mahara wanachotofautiana ni kiasi cha fedha tuu.
Mbaya zaidi tumehama toka kwenye TSHS sasa watu wanajilipua na maUSD

Huwezi iba halafu ukawekeza maana watu watahoji umehodhi vipi mali zote hizo na huku unafanya kazi serikalini tena wizara ya mambo ya ndani ambapo kwa cheo chake cha DCI mshahara ni kama milioni 2 hivi.

Kwa hiyo mkuu huu si uwekezaji kwa kujinunulia magari, kujenga nyumba na kuhifadhi mshiko mwingine benki.

Uhamiaji kuna watumishi ni mafisadi kuliko hata ufisadi wenyewe.
 
heshima wadau.

acha tutafune tu, kwani nani wa kumuogopa? kila mtu yupo katika nafasi fulani ili apige hela.
mishahara midogo, mzungu analeta dola utaacha kuzipiga?

nchi imeuzwa hii, tuiondoe ccm madarakani kwanza, tuanze upya, ili serikali itakayokuja ianze upya.
maana waliopo madarakani wote ni wapigaji pesa, nani anaejua kuhusu Jairo? Kelege? na hata wakina Maige ndio imetoka hiyo,

wasalaam
 
Kuna tetesi kuwa hao "maafisa uhamiaji" baadhi yao nao sio raia halali wa Tz.

Kwa vile bado Tz haitambui (rasmi) uraia wa nchi zaidi ya moja ni ajabu kuwa baadhi ya hao maafisa wana uraia wa nchi zaidi ya moja, so kwa mantiki hiyo lazima hakitawasumbua kugawa uraia kwa urahisi.

Pia hawataumwa na uzalendo kama nchi hii ikaharibika wataenda/watarudi makwao.
It's a loose loose situation kwa Tz.
 
Hivi kuna department yoyote ya serikali ya hii nchi ambayo hakuna rushwa?? dah yaani nchi hii kila kiongozi ni dalali (meaning akifanya kazi anataka apewe commission) mpaka Rais wetu nae ni dalali...
 
Hivi huyo Kamishna wao anavyo sema ameunda tume na wapewe nafasi mibinafsi haiingii akilini sababu kama nitume ilisha toa majibu ya yote waliyo yaona pale KIA-Kilimanjaro, Pamoja na hao wote wanao watuhumu kukutwa na huo Utajiri wengi wao ni watoto wao na walio karibu nao

Hivyo wakaona bora kuwahamisha baadhi wapo Waliokwenda Lindi, Mtwara na Morogoro: Kwa Vibali bandia hilo nikawaida na ndio dili kubwa sana linalo wapa maafisa wengi kiburi hasa Makao makuu, Arusha, Moshi Mwanza nasehemu zote zile zenye wakandarasi wa Kichina wengi wao wanavibali Bandia hili liko wazi Kabisaaa:

Hapa ni yeye mwenyewe Kamishna wao apime upepo na kukimbilia kuwahamisha watu sio ufumbuzi, kama ulikuwa unatoa Vibali Bandia Singida hata Tanga unakokwenda utatoa tu. Waziri husika chukua hatua Kampuni imeoza hiyooo.
 
Vigogo Uhamiaji wana utajiri wa kutisha
Monday, 21 May 2012 07:57

TUME YA KUWACHUNGUZA YAANZA KAZI LEO, WAHAMISHIWA MIKOANI KIAINA
Mwandishi Wetu
Mwananchi

KASHFA nyingine imeibuliwa katika Idara ya Uhamiaji.Taarifa mpya yenye kurasa tano, imewataja vigogo hao saba wakidaiwa kuwa na utajiri wa kutisha.Taarifa hiyo ambayo tunayo nakala yake, imedai kuwa vigogo hao wanamiliki mali na mamilioni ya shilingi katika akaunti zao binafsi.

Maofisa saba wametajwa kwa majina na vituo vyao vya kazi ambavyo ni Lindi, Dar es Salaam, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) na Moshi.
Tuhuma hizo zimekuja wakati Tume Maalumu iliyoundwa kuchunguza tuhuma za ufisadi na utoaji wa vibali bandia kwa wageni, ikitajwa kuanza kazi juzi. Hata hivyo, habari kutoka wizarani zinaeleza kuwa timu hiyo itaanza rasmi kazi zake leo.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Uhamiaji, zimedai kuwa baadhi ya wajumbe wa tume hiyo wamemhoji meneja wa benki moja kubwa ya Moshi ili kupata ukweli wa madai kuwa kigogo mmoja wa Uhamiaji mwenye cheo cha Naibu Kamishna (DCI), anamiliki akaunti ya fedha za kigeni.

Kigogo huyo anahusishwa pia na mtandao wa utoaji vibali bandia kwa raia wa kigeni wanaofanya kazi mkoani Kilimanjaro au kufanya kazi za kujitolea.
Ripoti hiyo imetaja taasisi 13, zikiwamo zisizo za kiserikali (NGO), hospitali na hoteli za kitalii zinazodaiwa wageni wake walipewa vibali bandia.
Mbali na kumhoji meneja huyo, inadaiwa pia walifanya mahojiano na uongozi wa kiwanda kimoja kinachodaiwa kukutwa na vibali bandia vya wageni 84.

Taarifa hizo zilidai kuwa maofisa wengine waandamizi wa Uhamiaji kutoka Makao Makuu, Dar es Salaam walitarajiwa kuwasili Moshi juzi kuungana na wenzao.
Baadhi ya maofisa waliotajwa katika ripoti hiyo kwamba wana utajiri ni wale waliokumbwa na uhamisho katika idara hiyo, Kia miezi mitatu iliyopita.
Katika ripoti hiyo, kigogo mmoja mwenye cheo cha DCI anadaiwa kukutwa na Sh700 milioni katika akaunti yake, achilia mbali kumiliki mali za mamilioni.
Mbali na maofisa hao kumiliki mamilioni ya fedha taslimu, pia wanadaiwa ‘kufanya kufuru' ya kununua magari ya kifahari, nyumba na viwanja.

Ripoti hiyo inayodaiwa kuandikwa na Maofisa Uhamiaji wazalendo, imepinga hatua ya kuhamishwa kutoka kituo kimoja kwenda kingine, maofisa wanaotuhumiwa kukutwa na utajiri ambao haulingani na vipato vyao.
"Tunataka ufanyike ukaguzi wa kina wa vibali vyote vilivyotolewa kati ya 2009/2010, 2010/2011 hadi 2012 na taasisi zote zionyeshe nakala za vibali," imedai.

Pia taarifa hiyo imependekeza wenzao wote wanaotuhumiwa kuwa na utajiri wa kutisha wachunguzwe na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
"Haikuwa sahihi kuwahamisha na kuishia hapo, walipaswa wapelekwe Takukuru wachunguzwe chanzo cha utajiri wao."

Pia wametaka kigogo anayemiliki akaunti ya Dola, achunguzwe ili kujua alikuwa akifanya biashara gani nje ya utumishi wa umma na kama alilipa kodi kiasi gani.
Baadhi ya maofisa Uhamiaji wamependekeza kusimamishwa kazi kwa kigogo huyo katika kipindi hiki kwa hofu ya kuingilia na kuvuruga uchunguzi.

Wiki iliyopita, Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Magnus Ulungi aliwaambia waandishi wa habari kuwa imeundwa kwa tume ya kumchunguza kigogo huyo.
Hata hivyo, taarifa zilizopatikana jana zilisema tume hiyo imepanua wigo wa uchunguzi juu ya kuwapo kwa vibali bandia katika taasisi mbalimbali.
Kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Naodha alikaririwa akisema Kilimanjaro ni moja kati ya mikoa minane inayomtia kichefuchefu nchini.

Waziri huyo alisema baadhi ya watumishi wamekuwa wakijihusisha na mtandao wa uingiaji wahamiaji haramu nchini pia kutoa vibali bandia kwa wageni.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alipoulizwa juzi kuhusu sakata hilo alisema ni vyema Uhamiaji ikapewa nafasi ya kuchunguza suala hilo kwa kuwa tayari imeshateua tume ya uchunguzi.

"Kamishna Mkuu wa Uhamiaji tayari amelifanyia kazi jambo hilo kwa uzito unaostahili. Tuwape nafasi walichunguze si vyema kuanza kuingilia katika hatua hii ya mwanzo," alisema.

Wahamiaji haramu
Serikali, bila mafanikio, imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kukomesha tatizo la wahamiaji haramu linalotajwa kuwa chanzo cha utajiri wa baadhi ya vigogo wa Idara ya Uhamiaji.
Miongoni mwa mikakati iliyowahi kutangazwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ni pamoja na idara hiyo kufanya utafiti kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Mzumbe kubaini chanzo cha ongezeko la wahamiaji haramu nchini.

Akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake bungeni mwaka 2007/2008 , aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wakati huo, Joseph Mungai alisema matokeo ya utafiti huo ni kuisaidia Serikali kujua chanzo cha tatizo hilo na jinsi ya kupambana nalo kwa ufanisi zaidi.

Hatua nyingine zinazochukuliwa ni pamoja na maofisa Uhamiaji kushiriki katika vikao mbalimbali kuanzia ngazi ya vijiji, ili kuwapa wananchi elimu juu ya masuala yanayohusu uraia na jinsi ya kukabiliana na wahamiaji haramu; Kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari; Kuweka mtandao wa kompyuta katika vituo vyote vya Uhamiaji ili kuviunganisha na makao makuu.

Pamoja na Serikali kutangaza mkakati huo miaka mitano iliyopita, wahamiaji haramu limeendelea kuwa tatizo sugu linalotia doa utendaji wa idara hiyo.
 
Watatajwa tu maana hiyo tume itafungua mambo yoote na wakikabidhiwa takukuru wanavyotaka sifa wakiletewa kazi kama hizo zisizo na vimemo utajuta kuwajua!!
 
Back
Top Bottom