King Kong III
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 51,672
- 68,636
Majina mbona siyaoni? Au Vigogo alimaanisha Wakazi wa kigogo
"Eti wanaiuliza serikali waende wapi? kwani sisi ndio tuliwapeleka mabondeni?" mh.mkuu wa mkoa.
Gazeti la mtanzania ni gazeti majeruhi la Rostam Aziz na Hussein Bashe tuwe makini kulifanya chanzo chetu makini cha taarifa. magazeti majeruhi wakati mwingine yanaumba taarifa bandia ili kukidhi haja ya kuwasafisha majeruhi wa kisiasa au kututoa kwenye agenda za msingi za kujadili madhambi ya waliohujumu uchumi wetu na kutufikisha hapa tulipo.
Ili kuwe na uwazi inabidi majina ya walioathirika na kugawiwa viwanja yawekwe hadharani. vinginevyo kweli tutakuta waathirika wa narudi jangwani na viwanja vya mabwe pande wanapewa vigogo. Tumeyaona haya kumbuka miaka ya 90 waathirika wa Jangwani waliambiwa wanapewa viwanja kinyerezi lakini waliovipata ni wachache vingine vikaenda kwa vigogo! Nchi hii bwana kila kitu deal!
Wewe kama sio dalali basi ni bepari mmojawapo mwenye nyumba nyingi hapa dar, hivyo unaogopa kukosa wapangaji. kwanini wasipewe viwanja? kwani wapangaji hawana haki ya kupata viwanja? wakirudi mabonddeni mtawalaumu?
Viongozi wa serikali wapo kwaajili ya matumbo yao na wala si kwaajili ya kutumikia wananchi, so kila dili lolote litakalo tokea lazima wao wawe wa kwanza kunufaika. Nawapongeza CDM misaada waliyotowa waliwapa waathirika moja kwa moja.
Enzi za Jenelali Ulimwengu magazeti hayo yalikuwa maarufu sana lakini sasa ni magazeti ya fisadi namba moja hapa nchini na wakati mwingine yanataka kutuonyesha kwamba fisadi sio yeye tu bali wapo na wengine. Mbona wao hawataki kuandika mabaya yaoi? lini uliwahi kuona magazeti haya yakiandika kuhusu mmiliki wake yule mwizi mkuu?
viongozi wa serikali wapo kwaajili ya matumbo yao na wala si kwaajili ya kutumikia wananchi, so kila dili lolote litakalo tokea lazima wao wawe wa kwanza kunufaika. nawapongeza cdm misaada waliyotowa waliwapa waathirika moja kwa moja.
afadhali umewaambiaMbona hamuwataji majina kama sio UDAKU?
Mimi hili la wapangaji nao kudai viwanja sili support ... Wapewe wenye nyumba tu ... Wapangaji wakatafute mahala pengine "sio bondeni kupanga "