Maafisa Elimu Watoa Milioni 20 kwa Waathirika wa Mafuriko ya Hanang

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amekabidhi Sh.Milioni 20 kwa Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Mhe.Jenista Mhagama kutoka kwa Umoja wa Maafisa Elimu wa Mkoa na Halmashauri zote nchini kwa ajili ya waathirika wa mafuriko ya Hanang mkoani Manyara.

Mhe. Mchengerwa amekabidhi fedha hizo leo kwa Waziri Jenista Ofisi ndogo jijini Dar es salaam, ambapo amepokea fedha hizo kwa niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Waziri Mchengerwa amesema fedha hizo zilitolewa kwenye Mkutano wa Maafisa Elimu hao mwishoni uliofanyika Manispaa ya Morogoro ambapo Maafisa hao wametoa mchango wao kuunga mkono juhudi za serikali katika kuwahudumia wananchi wa Hanang waliopatwa na janga la mafuriko.

"Maafisa Elimu kwa ushirikiano wao waliona umuhimu wa kuchangishana na kusaidia waathirika wa maafa yaliyotokea Hanang na kunituma nikukabidhi wewe Mhe.Waziri mwenye dhamana,"amesema.

Naye, Waziri Mhagama amewashukuru kwa mchango huo na kuunga mkono serikali katika kuhudumia wananchi hao na kwamba fedha hizo zimewekwa kwenye Akaunti ya maalum ya maafa iliyoko Benki Kuu.

GDaZFdAWAAAnAVc.jpg
 
Back
Top Bottom