VIDEO - Vimombo Vya Wasanii Wabongo

jamani jamani, mimi sipendi kuwacheka hao wasanii kwani ninaamini kabisa hicho kingereza walichoongea ndio wanachokifahamu. pia muelewe kuna presha ya kujua unahojiwa mbele ya kamera tena katika lugha ambayo si yako ulikokulia zaidi ya kujifunzia ukubwani nayo inachangia kidogo kusahau hata maneno wanayoyafahamu.

pili baadhi yao kiwango cha elimu walichonacho kinachangia, tutambue fika si Watanzania wote waliopita katika shule za English Medium, na baadhi tuliosoma shule ya chini ya mwembe na madarasa ya nyasi, hakuna vitabu, kuna upungufu wa walimu, matatizo ya ada na matatizo mengine ya kifamilia aliyokumbana nayo huyo msanii mpaka kufikia hatua hiyo ya kujikomboa kwa kutumia kipaji alichopewa na Mungu kufikia hapo leo. la msingi ni kuwahimiza hao vijana (wasanii) kujiendeleza kielimu hata kwa kwenda katika madarasa ya jioni ya kujifunza lugha za kigeni mfano kiingereza ama kifaransa ili usanii waweze kuuza kazi zao kwa kiwango cha kimataifa, ninaamini tukiwapa muda wakajiendeleza baada ya miaka kama miwili ninahakika tukija kukutana nao katika hayo mahojiano ya kimombo nao watakuwa wanaelewa na kuongea kiufasaha tena huenda kuliko hao wanavyoongea leo hii.

aidha, tutambue si wasanii pekee ambao lugha za kigeni zinawapa shida jamani ni kila kada kuna tatizo hilo kwahiyo leo wakianza kunyolewa hao wengine twendeni shule sio kuwashikia mabango kama wametenda kosa la jinai, ongeeni nao kwa kiswahi ama lugha zao za asili mtawaona kama watababaika.

mwisho mimi ninawapongeza sana wasanii wote wanaojituma na hata kufikia mafanikio ya kuitangaza nchi yetu ya Tanzania katika ngazi ya kimataifa ial wajue umaarufu una gharama zake na ili kweli udumu katika huo umaarufu na usiwe mbabaishaji basi warudi shule kama wafanyavyo baadhi ya wasanii wenzao jamani dunia ya leo si ya kutumia vipaji na ujanjaujanja tu tutaporomoka ni shule na hayo mengine ni ya ziada kaka na dada zangu.
 
bora hata kanumba form four mbona jk huwa anachemka chuo kikuu?ohoo nyie mnaomponda kanumba hamjawahi kuchemka?ohho then kwani hata kama anaongea kibovu kwani hamkuelewa msg?
 
bora hata kanumba form four mbona jk huwa anachemka chuo kikuu?ohoo nyie mnaomponda kanumba hamjawahi kuchemka?ohho then kwani hata kama anaongea kibovu kwani hamkuelewa msg?

Mama 5J's,

Hapa watu wa makundi mawili. Moja ni wale wanaosaga na kufurahia jamaa kuteleza. La pili ambalo na mie nimo ni hili linaloona kuwa "Kanumba katereza, ila anaweza kusimama imara zaidi ya hiyo ANAJITAHIDI". Kama ningelikutana naye basi ningelimsisitiza afanye kozi za kuongea Kiingereza hadi awe muongeaji safi kabisa wa Kiingereza. Jamaa kweli anafahamu Kiingereza ila mazoezi ya kuongea hana. Nilishaona mhandisi mmoja akijikanyaga mbele ya vijana wa UDSM kwa sababu tu, wengine walikuwa wanatoka nje ya Tanzania.

Mie hilo tatizo pia nilikuwa nalo. Nilikuwa nikimkimbia jamaa mmoja wa Ghana hasa ukichukulia ile semaje yao ya Ohh mai braza........ Ikatokea tukawa tunakaa wote nikawa sina njia. Mwaka mmoja baadaye nikawa nashindwa kuelewa ni kitu gani hasa nilikuwa simuelewi.

Watanzania tunafahamu Kiingereza safi tu ila kwa kuwa hatufanyi mazoezi ya kuongea basi huwa ni kasheshe. Ndiyo maana watoto wanaosoma SHULE za Kimataifa, wanaongea safi sana kwa sababu huko huna ujanja, lazima useme Kiingereza na si SWAHI-ENGLISH........
 
Vienglish vyao ni vile vya waTZ tulio wengi inaonesha kabisa kuwa hawa vijana wameso hii lugha kwenye vitabu ila hawajapata chance ya kuzungumza mara nyingi achilia mbali kwa ufasaha!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom