Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 14,047
- 20,411
Nyimbo za bongo fleva, kwa asilimia 96% ni matusi, chache ni matusi ya mafumbo lakini mafumbo ya wazi na za mapenzi, zile zenye maadili za kina Afande Sele, na wengine hazipendwi, za matusi zinaimbika na pia zina amsha hisia hivyo hupendwa , ndicho kitu naibu waziri ameona Watanzania wanakitaka kwa sasa badala ya viwanja vua michezo kwa kila shule, apambanie tupate timu za vijana kila Mtaa n a Kata, tupate maeneno ya wazi ambayo CCM imeyateka na kuweka makontena ya kulaza magari na baa za kuuza konyagi za kupima na kitimoto!
Nyimbo za Wanamuziki wa Kitanzania zinatarajiwa kuanza kupigwa kwa asilimia 100 kwenye viwanja vya ndege hapa nchini ili kuendelea kuutangaza muziki wa kitanzania.
Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya kikao cha Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma maarufu Mwana FA ambaye amekutana na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini katika kikao kilichofanyika Jijini Dar es salaam.
Katika kikao kazi hicho, Naibu Waziri Mwinjuma ametoa rai kupitia kwa Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Musa Mbura kufanya hivyo ili kutangaza muziki wa kitanzania kwa wageni wanaoingia na kutoka nchini.Kikao hicho kimehudhuriwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa, Dkt. Emmanuel Ishengoma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa, (BASATA) Dkt. Kedmon Mapana, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu, Dkt. Kiago Kilonzo na Kaimu Mtendaji Mkuu wa COSOTA, Baraka Katemba.
WADAU wanajiuliza, nyimbo hizi za matusi za Diamond, Zuchu , Harmoniser ndio zitapigwa au itakuwa kwaya na kaswida?
Video za wanawake wa kislamu wakiwa uchi kama steji shoo ndio mnataka kutuwekea Pale DIa, KIA na kwengineko tukiwa tunasubiri check-in tuangalie na wanetu tukiwa tunasubiri ndege za kwenda likizo?
Mauno na mabusu ya kina Diamond na video zao wakila shisha zilizochanganywa na madawa ya kulevya ndio mtuonyeshee watoto wetu?
Huo muziki wewe Mwana FA tukiweka wanao waangalie kwa masaa 2 mfulilizo utakubali?
MWANA FA umetuchoka, kuongoza si shurti, achia wizara uwe back bencher!