(Video)Sultani wa Zanzibar alivyofurahia mauaji ya Karume; alitarajia kurudi Zanzibar?

Mimi nataka kujua tu, watu wa Zanzibar wanaonewa na nani na wanaonewa kivipi?
Vilevile mkishapewa Zanzibar ika nchi nini mtakachofanya ktk hiyo nchi yenu au mtakachodai tena(What next) ktk maisha yenu ya nchi yenu ya Zanzibar
 
Mimi nataka kujua tu, watu wa Zanzibar wanaonewa na nani na wanaonewa kivipi?
Vilevile mkishapewa Zanzibar ika nchi nini mtakachofanya ktk hiyo nchi yenu au mtakachodai tena(What next) ktk maisha yenu ya nchi yenu ya Zanzibar

HUYU NDIYE MR. NYERERE BAADA YA KUIVAMIA ZANZIBAR NA KUWAKAMATA VIONGOZI WALIOCHAGULIWA DEMOCRATICALLY AKAWAFUNGA KATIKA NCHI YAKE YA TANGANYIKA KABLA YA HUU UITWAO MUUNGANO 1964

MJUE NYERERE NA JELA ZAKE


Katika mwaka 1968 Hakimu Seaton, Hakimu wa Mahakama Kuu; alitembelea gereza la Mwanza.
Nilimuuliza kama kuna uhalali wowote juu ya kuwekwa kwetu kizuizini.

Mkuu wa gereza akamwambia Hakimu kuwa hakuna karatasi zozote zilizoletwa pamoja na mawaziri wa zamani wa Zanzibar.

Hakimu akaahidi kulifuatilia suala hili. Baada ya miaka minne tangu wakati huo, nikiwa katika gereza la Bukoba, Katibu wa Mkuu wa Mkoa alitoa shauri kuwa nimuombe Raisi anitoe kizuizini.

Nalimwambia kuwa kwa vile sijui nini kosa langu la kuwekewa kizuizini naona sina hoja za kimsingi juu ya ombi langu.


Alinijibu, "Hapana shaka ulipotiwa kizuizini ulisomewa amri ya kutiliwa kizuizini."

Nilimwambia kuwa, vile ninavyo kumbuka mimi hapakuwepo amri ya mimi kutiwa kizuizini.
Suprintendent wa magereza akanambia kuwa ilikuwepo amri, hapo akanisomea hio amri ambayo ikionesha kuwa inatokana na Raisi na ambayo imeandikwa kwa lugha ya kisharia.

Amri hio inasema kuwa Raisi baada ya kutoshelezeka kuwa, fulani na fulani; akiwataja mawaziri wote wa Serikali ya Muhammad Shamte, kuwa walikhusika na vitendo vya uchochezi wa kukhatarisha salama ya nchi, alitoa amri tutiwe kizuizini.

Nalipomuuliza amri hio ilitiwa sahihi lini, ilidhihiri ilikuwa ni mwaka wa 1968, baada ya muda mchache tangu pale nionane na yule Jaji Mkuu, Seaton kwenye gereza la Mwanza!


Sisi tulivamiwa nchi yetu na kutiwa vizuizini katika mwaka wa 1964. Najuwa kulikuwa na mapinduzi (mavamizi) huko Zanzibar, na hicho kitendo cha kiharamia iwe kimetokea huko.

Lakini tangu kati ya mwaka wa 1964 pale tulipotiwa vizuizini mpaka hii 1968 ambapo hii amri ya kutiwa kizuizini kutolewa na kutiwa sahihi; wakati huo wote - miaka minne - kuwekwa kwetu kizuizini na yeye Raisi Nyerere ambae ndie aliekuwa na hukumu yote huko Tanzania bara basi hakukuwa kisharia hata katika hio sharia ya kidhalimu ya Tanzania.

Kwa muda wa miaka minne kabla ya kutiwa sahihi hii amri ya kuwekwa vizuizini sisi tulikuwa basi ni wafungwa wake yeye Nyerere.

Je, ndio inayumkinika katika muda huo iwe yeyote miongoni mwetu sisi tuweze kufanya vitendo vya uchochezi wa kukhatarisha salama ya taifa?

Tujaalie kuwa inakusudiwa ule muda kabla ya kukamatwa na kutiwa kizuizini.

Wakati huo sisi tulikuwa ni mawaziri wenye mas-ulia kwa vile tulichaguliwa kulingana na sharia ya kikatiba iliokuwepo nchini - Zanzibar - wakati huo.

Je, sisi wakati huo tutaweza kuwa tutende kama vile ilivyoelezwa katika hio amri iliotiwa sahihi na Julius Nyerere?

Kama itakavyokuwa, hilo taifa linalo elezwa kuwa ni Tanzania; halikuwepo kabla ya sisi kukamatwa na kutiwa vizuizini.

Huyo ndio mkuu wa nchi, anaejigamba kuwa yeye ni mwenye kuweka haqi, anafika kuzuwa na kupanga uwongo kama huo; ni jambo la kushangaza sana; lakini kwa watu kama yeye sio ajabu kulitenda.

Baada ya kupata hoja hizi ndipo nilipomwandikia Raisi, bila shaka maandishi yangu yalikuwa ni ya upole na kweli za hakika.

Sikupata majibu. Kwa hakika sikupata hata mara moja jawabu au hata kuarifiwa kuwa zimefika, baruwa zangu kadhaa wa kadhaa nilizompelekea Nyerere, tangu niko kizuizini na hata baada ya kutoka. Utaritibu wa hishima kama hio Tanzania inaonekana ni mpango wa kikoloni uliokwisha pitwa na wakati.


Dr. Kleru alikuwa ni Mkuu wa Mkoa aliepigwa risasi na mkulima, Abdulla Saidi Mwamindi; siku ya krismasi mwaka 1971. Mkulima huyu, Abdulla Saidi, alikuwa ni miongoni mwa watu kadhaa wa kadhaa walionyang'anywa mashamba yao kwa kuwanzishia vile vijiji vya ujamaa. Jeuri ya Mkuu wa Mkoa huyu ilifurutu ada.

Waliokuwa wakiteswa na kudhulumiwa na Mkuu wa Mkoa huyu walishitaki kwa wakuu wa chama.
Kila wakishitaki huambiwa wakashitaki polisi; na wakifanya hivyo.

Kamanda wa Polisi, Abubakar aliwaonya wakuu huko Dar es Salaam juu ya vitendo viovu na vya kuudhi vya Mkuu wa Mkoa huyu na juu ya ile tabia yake ya ulevi kufika kuanguka na kuingiliwa na wahuni.

Baada ya kupigwa marisasi na kuuliwa, wale jamaa wote waliokuwa wakipeleka mashtaka yao Polisi walikamatwa na kuwekwa kizuizini mpaka Abdulla Saidi Mwamindi ahukumiwe na kunyongwa. Hata kabla ya kesi kumalizika, magazeti na vyombo vyote vya khabari vya Serikali na vya Chama, vyote vilianza shutuma zao, sio tu dhidi ya Mwamindi, bali dhidi ya wakulima wote, huku wakisemwa, "mabepari", "wanyonyaji", "wakoloni" na makhaini".

Mudhahara uliopangwa na Sirikali ukaingia njiani kupita kuwashutumu na kuwalaani watu hawa. Kwa hali hii ikawa Mwamindi kesha hukumiwa na vibaraka vya Sirikali hata kabla ya kufikishwa mahakamani.

Mashahidi wote wale ambao wangeliweza kutowa ushahidi japo kuthibitisha juu ya vitendo vya uchokozi vya yule Mkuu wa Mkoa walizuiliwa mpaka pale kesi kumalizika.

Khatuwa hii ilikusudiwa kumtia khofu yeyote yule aliekuwa na fikra ya kutaka kutowa ushahidi upande wa mshitakiwa.

Hivi ndivyo sharia inavyo firigiswa katika nchi kama hivi Tanzania wakati ambapo sharia ya kumtia mtu kizuizini bila ya kupelekwa mahakama inatumika.

Watu kumi na mbili wa Iringa pamoja na yeye Mwamindi mwenyewe walikuwa pamoja na mimi gerezani Dodoma.
Kamanda wa Polisi Abubakar, na yeye vilevile aliwekwa na sisi siku mbili gerezani akiwa yumo katika pirika za kuhamishwa kutoka gereza hii na kupelekwa gereza jengine.


Ilani nyingi zilitolewa na kutangazwa ulimwenguni juu ya maafa na mateso katika magereza ya Zanzibar na Pemba.

Lakini hapana lililosemwa na kuelezwa walimwengu kukhusu mateso yanayowapata wazuiwa katika magereza ya Tanzania bara.

Sio kuwa uwovu na mateso wanayotendewa wazuiwa magerezani huko Tanzania bara hayajuulikani; mengi yake hayafiki ulimwenguni basi kwa sababu ya kukosekana demokrasia na heshima ya haki za binadamu juu ya haki ya kueleza na kujieleza.

Kutokana na hali hii, mateso na vitendo vya kikhabithi havielezwi nje kwa walimwengu kukhofia hao watakaoeleza kuadhibiwa na utawala wa kidikteta. Niliona kwa macho yangu nilipokuwa gereza la Mwanza, wakati ambapo Superintendent Odenyo ndie aliekuwa mkuu wa gereza wakati huo; niliona wafungwa walipozuiliwa chakula na maji kwa muda wa siku nne, kisha wakapelekwa hospitali (nusu maiti) na ripoti kuwa (ati) walikuwa wamegoma kula.

Nilipokuwa Dodoma nilikuwa nikisikia kadhia kama hizo.
Nikisikia, kwani baina yetu ilikuwa ni kuta, baina ya chumba niliokuwemo na vile vyumba vya mateso.

Katika gereza la Dodoma aliekuwa katili hivyo ni Ofisa Mkuu, aliepangwa jina "Iron Face" (Uso wa Chuma), kwa vile akijuulika kuwa hajapata kuwa na huruma.

Mkuu wa magereza hapa, alifika kuwa hajishughulishi tena na kazi yake; hivi ni kwa sababu kwa hichi cheo chake cha juu na daima kuwemo katika vikao na sherehe za kisiyasa, takribani alimuachilia uendeshaji wote wa gereza mikononi mwa msaidizi wake - huyu Ofisa Mkuu. Mabwana wawili hawa waliyafanya maisha ya gerezani hapa hayastahamiliki hata kidogo.


Ile mikutano ya kawaida ya kila Jumamosi ambapo ofisa mas-uli hutarajiwa asikilize malalamiko ya wafungwa ikawa haifanywi tena.

Ziara za kila mwezi gerezani za Mahakimu mbalimbali nazo pia zikasita. Wafungwa hutiwa gerezani na kufika kutolewa bila ya kujuwa kuwa wanahaki ya kuwasiliana na watu wao.

Inafaa ifahamike kuwa hivi kuharibika hali kiwango hichi, sio tu katika gereza la Dodoma. Niliiona hali kama hiyo katika gereza la Mwanza.

Gereza la Bukoba ilikuwa haijambo pale nilipoondoka.
Lakini, wakuu wa kisiasa; kama vile Mkuu wa Mkoa na Mawaziri dhahiri shaahir walikuwa wakijiepusha kuyazuru magereza na kujuwa hali za wafungwa na wazuiwa waliomo humo magerezani.

Ama Raisi na Makamu wa Raisi, si dhani kama iko siku wamewahi kuzuru gereza lolote lile katika Tanzania bara, licha kuzungumza na mabwana au mabibi waliowatia humo magerezani.

Hali katika gereza la Dodoma ilizidi kufanywa kuwa mbaya kwa ukhabithi wa huyu "Uso wa Chuma" na kulemaa kwa ulevi wa marungi Msaidizi wa Superintendent.


Mpango ulifanywa kumuuwa "Uso wa Chuma". Mmoja wa wafungwa aliweza kupata kisu na akataka kumpiga nacho huyo "Uso wa Chuma", kwa bahati akaanguka kifudifudi, kichwa chake mbali na yule mfungwa ambae alikuwa na pingu za chuma miguuni mwake na yeye vilevile akaanguka upande wake.

Wakati huo mfungwa aliweza basi kuipata miguu ya "Uso wa Chuma" na kuanza kumpiga visu vya miguuni mpaka pale ilipowezekana kuzidiwa nguvu akanyang'anywa hicho kisu.

Hapo tena akaingiliwa mfungwa huyo kupigwa marungu mpaka akawahijiwezi ndipo alipotiwa pingu za mikono. Askari wa gereza akaamrishwa kumpiga marisasi ya miguu.

Hivyo ikawa kafungwa kila upande na marisasi miguuni mwake, hapo tena akasukumizwa katika chumba cha adhabu.
Baadae kidogo msaidizi wa superintendent akaja na yeye akaanza kumpiga vile alivyopenda.

Vilio vyake tukivisikia kutokea katika hicho chumba cha adhabu alimokuwemo na tukamuona askari aliekuwa zamu kwenye kidungu akigeuza uso na kupiga ukelele: "Wanamuuwa huyu mtu!" Binadamu huyu akavurumishwa tena humo chumbani kisha bomu la kutowa machozi likatupwa katika hicho chumba ambacho sehemu yake ya kupitia upepo ni ndogo kabisa. Usiku uleule akajifia.


Asubuhi yake wafungwa wote wakasimamishwa kwenye uwanja na maiti ikaletwa mbele yao uchi kama alivyozaliwa. Hapo tena msaidizi wa superintendent akawa anamchocha maiti kwa gongo huku akimwambia yule maiti: "Inuka uwaambie wenzio vipi ulivyokuwa hodari, na nini mwisho wa uhodari wako?"

Baada ya hivyo tena akawahutubia wafungwa kwa kuwaambia kuwa hivihivi ndivyo tutakavyomfanya yeyote yule miongoni mwenu asiposhika adabu yake.
Hapo tena wafungwa wote wakafungiwa vyumbani mwao kisha mabomu ya kutowa machozi yakatupwa humo vyumbani mwao.

Haya yalifanywa kwa makusudio ya kuwataka watajane wale waliokhusika na mpango huu. Haukupita muda isipokuwa wengi wakatajana na kukiri makosa yao.

Lakini adhabu na mateso yaliendelea kwa wiki kadhaa wa kadhaa. Chakula kikapunguzwa, hata kwetu sisi wazuiwa. Kila mtu alitaraji mauwaji haya yatafanyiwa uchunguzi na hukumu ya haki kupitishwa. Askari wa gereza ikawa wanasema hadharani kuwa ukifanywa uchunguzi watawaambia askari Polisi hakika ya mambo ilivyo. Lakini hapana lilokuwa.

Tulisikia katika redio, kama maneno ya kupita tu yaliosemwa Bungeni - kwa woga - na mmoja wa Wabunge kuwa kulikuwa na askari makhabithi walio waadhibisha wafungwa mpaka kufika kuwauwa.

Kubwa lililotokea ni uhamisho wa kawaida wa maofisa wa magereza wa vyeo vya juu kutoka magereza mbali mbali nchini. Khabari ikamalizikia hapo.

Katika nchi yenye sheria ya kutiwa watu vizuizini bila ya kupelekwa mahakamani, kelele zozote zile ni sawa na mbwa mwenye kubweka hazina athari yoyote ile, na sharia basi ni kwa kumtumikia bwana mtawala aendelee katika utawala wake na atende vile anavyopenda.
 
Comments za hawa wanaotaka muungano uvunjike hapa ni sawa kabisa na Mr Jacobo katika kitabu "Weep Not Child" ambaye alikuwa anaamini katika "uwezo uliotukuka wa mkoloni kwamba bila watu kama Mr Howlands future ilikuwa nyeusi". Nanyi mwaona bila mkoloni mwarabu Zanzibar haina future
 
Well said, namkubali kikamilifu Nyerere, namkubali pia Mzee Karume the supergenious who didn't go to school but left historic achievements that the so called "modern" scholars want to destroy. Tusidanganyane, madhara ya kuuvvnja muungano yatakuwa na impact kubwa na ya muda mrefu kabisa kwa bara na visiwani. Wazanzibari wanatumiwa kisiasa na maajenti wa Jamshid bila kujua. Tatizo ni vyombo vya inteligensia kuchakachuliwa hadi yote haya kutokea bila hata ya serikali kujua. CCM ya sasa itabeba lawama kwa yote yanayojiri.

Kweli ?
 
Ushahidi wa harakati hizi unafifisha ile dhana kongwe kwamba Muungano wa Tanzania ulifikiwa kwa hiari (bila shinikizo), ambapo inadaiwa kwa kupotosha kwamba Rais wa Tanganyika, Julius Kambarage Nyerere alipendekeza suala la Muungano kwa Rais wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume, naye bila kusita, akakubali na akapendekeza Mwalimu Nyerere awe Rais wa Muungano huo.


Dhana hii inapingana pia na ukweli kwamba, wiki chache tu baada ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964, Serikali ya Tanganyika iliwatuma Waziri wake wa Mambo ya Nje na Ulinzi, Oscar Kambona na Bibi Titi Mohamed, Naibu Waziri na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama tawala cha "Tanganyika African National Union" (TANU), kumshawishi Karume akubali Muungano kati ya nchi zao mbili, lakini Karume alidai alihitaji muda zaidi kufikiri juu ya jambo hilo.

Kama ni kweli kwamba Karume ndiye aliyependekeza Muungano, ilikuwaje awagomee mawaziri hao wawili waliotumwa na Mwalimu, na TANU?


Hata ule ujumbe wa pili uliowahusisha Mawaziri wa Tanganyika, Tewa Said Tewa na Job Lusinde, Februari 9, 1964, haukuweza kumgeuza mawazo Karume akubali haraka suala la Muungano, ulipokwenda Zanzibar kuwasilisha ujumbe wa Nyerere siku hiyo.

Duh! kumbe Karume sie aliyeomba Muungano ili alindwe na kupinduliwa na Sultani?!
 
HIvi inawezekana kulikuwa na mkono wa Sultani katika mauaji ya Karume?

Sidhani kama alikuwa bado na INFLUENCE YA KUWEZESHA TUKIO KUBWA NAMNA HIYO NDANI YA ZANZIBAR baada ya kupinduliwa.

Kama nakumbuka historia sawasawa alikuwa Uingereza alikopewa hifadhi na mchango wake katika masuala ya ZANZIBAR kutokana na maandiko niliyosoma, haukuwa na uwezo wa kufanya tukio hilo.

Pamoja na yote; katika masuala ya VISASI na UGOMVI JUUYA MADARAKA lolote linaweza kuwa kweli.....NI MAWAZO YANGU...
 
Kamwemwe hujanipa jibu zaidi za kunipa historia ya gereza la Mwanza na Dodoma, uso wa chuma enzi hizo.
Kipindi kile kila mtu alikuwa anakamatwa wengine mpaka wakakimbia nchi kina Kambona, watanzania wengi walifungwa. Switch to the point please
 
Mzee sasa naona unapotea! Yani unajifanya hujui kuwa siasa za bara kuikamata Znz ndio kumeleteleza haya mauchafu? Mnalazimisha muungano ili dola ya kiislam isisimame Znz na sheria za kuzuia upumbavu kama huo kutumika. Mnang'ang'ania znz ili uislam usiendelee kwani ukiendelea ukristo hautakuwa na nafasi.

Jibu zuri, ahsante. Upo sahihi mkuu
 
Kamwemwe hujanipa jibu zaidi za kunipa historia ya gereza la Mwanza na Dodoma, uso wa chuma enzi hizo.
Kipindi kile kila mtu alikuwa anakamatwa wengine mpaka wakakimbia nchi kina Kambona, watanzania wengi walifungwa. Switch to the point please
 
HIvi inawezekana kulikuwa na mkono wa Sultani katika mauaji ya Karume?
Sehemu ya ukweli ni kuwa Karume aliuliwa na Luteni Humud, shemeji yake mwenyewe, kwa madai kuwa Karume alishiriki katika mauaji ya baba yake Humud. Sasa ikiwa Humud alitumiwa na Nyerere au Jamshid hilo ni suala jengine.

Kuhusu suala la Jamshid na "watu wake", tukumbuke kuwa hawa walikuwa (na waliopo hai bado) ni wazaliwa wa Zanzibar tangu mababu wa mababu zao. Wale waliondoka na kukimbilia uhamishoni waliondoka kwa sababu mazingira yaliwafanya wakimbie kwao,sawa na wahindi wa Uganda walivyolazmiikakuondoka Uganda.

Mtu wa pwani
;
wazanzibari toke asili hadi leo ni mchanganyiko wa watu na makabila mbali mbali. ikiwemo damu ya kiarabu na kimanaga ambayo unataka kuwaaaminisha watu kuwa hawana haki ya kupigania nchi yao
Hapa isisahauliwe kuwa kuna Watumbatu, Wadonge, Wamakunduchi, Wakojani, Wamicheweni...bila kusahau Wanyakyusa, Wamakonde, Wangazija, Wahindi....miongoni mwa wengine.
 
Mzee Mwanakijiji.

Siku za hivi karibuni umekuwa unafanya siasa kama CCM, tena kwa ustadi na weledi.

Siku umma wa Tz utakapochoka kusikiliza propaganda za ki-CCM na kuzikubali kiulani watagundua kuwa unachokifanya sasa katika makala za karibuni kuhusu Muungano ni sawa na Mwalimu Nyerere kulia, kudondosha machozi kwa "huzuni" baada ya kuapata taarifa za kifo cha Sokoine.

Matukio ya Zanzibar yamekuparaganya na sasa unajaribu kuwababaisha wasomaji wako. MMJ una wafuasi wengi, wafuatiliaji wengi wa makala na michango yako watendee haki.

Analaumiwa au kupata mkwala wa nguvu Malecela Willy anapouliza masuali au kuleta uzi kama ule "ilikuwa lazima kumtoa Idi Amini?" lakini mkuu wewe unapata upenyo.

Ni nini lengo lako hasa kwa makala zako za hivi karibuni?

Je siku utakapopata ushahidi kuwa yale matukio ya Zanzibar yana mkono wa makada wa "Chai, Chapati, Maharage" na pia kuwa Polisi walisheheni uongo katika taarifa zao utarudi jukwaani na kuipa "tough" UAMSHO?

Mkuu Katiba mpya ambayo haitoi nafasi kuujadili Muungano kwa upana wake inatuletea madhara ya kimsongo wa mawazo hata sisi ambao tunaombea amani Jamhuri yetu ya Muungano wa Kero.

Tuna mjadala wa katiba mpya hili ni muhimu sana sasa hizi makala nyingite tena mkuu zinakusudia kuibua nini? Huyo Sultani bado yuko hai? Kama yuko hai ana umri wa miaka mingapi?

Kwa nini alikimbilia UK badala ya Oman?
Je Oman hawamtaki Mwarabu mwezao?
 
Haaahaaa! Kuna watu wanataka tena wafanye kazi kwa viboko. Kama wanafikiri kuna siri basi wajue sio siri tena.
 
MM Toka sakata la Uamsho lianze Viongozi walio mstari wa mbele hasa MA AMIRI/MAJEMEDARI ni wale wenye asili ya Kiarabu. Hao ndio wasemaji wakuu na ndio wenye Amri. Mmoja wao leo hii karudi toka Oman kwa kisingizio cha kutoka Hospitali! Mimi ninamashaka kuna makala hapa pia inatilia mashaka uhusiano wa Waarabu hawa (MA AMIRI) na conection ya Arabuni kwa jumla na Clip hiyo inamrudisha X Sultan Kwenye picha. Labda Vichwani mwao wanasema: Zimwi Likujualo..............! Time will tell.

" connection gani hiyo ya arabuni na zanzibar? hata viongozi wetu wa leo wanaenda sana tu huko arabuni. ndugu na jamaa zetu pamoja na WENU wengi wapo huko wanahangaika na maisha. sultan umesemaye si raia wa oman. yeye anaishi ukimbizini hadi leo huko UK - portsmouth, ni raia wa zanzibar (ambaye damu ya kimanyema inatembea kwenye mwili wake). hata enzi za dr salmin amour aliwahi kumwambia anaweza kurudi zanzibar kama raia mwengine yeyote"

 
Back
Top Bottom