Video: Jerry Muro apasua jipu la sakata lake la rushwa!

kwakweli inakua ngumu hata kutoa comment! coz kitu cha kuungaunga sometimz unaweza kwenda ndivyo sivyo!
 
polisi wa tanzania huwa awakubali kushindwa, na jambo kama hili iwapo itabainika JM hakuusika kwa namna yoyote kuomba rushwa inabidi watanzania tuandae kongamano la kumuomba mh Rais alivunje jeshi lote la polisi na aunde kikosi kingine cha kulinda raia ambacho kitaweza kushirikiana na jamii nzima
 
Kwa kazi anayoifanya ni wazi atakuwa na maadui wengi pia. Kama aliondoka IPP Media kwa mabaya, ni wazi pia alijipatia maadui. Yote haya kwa pamoja yanamtaka JM awe makini.
 
hii ndo Tanzania bwana, wanaofanya mema wote wanachukiwa na kuzimwa kwa style tofauti na wasio waadilifu wanasurvive tu. sorry, but sometimes i hate this country.
 
katika mazingira ya kawaida lazima Jerry ategemee kuwa na maadui wachache lakini wenye mbinu mbalimbali chafu.

Sudi Mnete nakushauri na wewe hiki si kipindi cha kupayuka payuka.kaa chini tafakari
 
ipp inahusika kumpa umaarufu jeri muro na hatimaye kuhamia tbc1,haiwezi kuhusika ila jeri anahusika kwa yaliyompata.
pia mwandishi hueleweki iwapo unauliza ipp media kuhusika kumpa rushwa jeri au kuhusika kwa namna gani hasa....................
kila mtu anavuna anachopanda..............
 
hii ndo Tanzania bwana, wanaofanya mema wote wanachukiwa na kuzimwa kwa style tofauti na wasio waadilifu wanasurvive tu. sorry, but sometimes i hate this country.

inaudhi Carmel (u r nt alone)!!!! ndo maana tutabaki hivi tulivyo!!!!!!!!!
 
katika mazingira ya kawaida lazima Jerry ategemee kuwa na maadui wachache lakini wenye mbinu mbalimbali chafu.

Sudi Mnete nakushauri na wewe hiki si kipindi cha kupayuka payuka.kaa chini tafakari

mwenzio akinyolewa wewe tia maji!!!!! wacha nireserve comments zangu kwa Sudi for the time being!!!!!!!!!!
 
Mr. Policeman, tunakudis kitaani, kama Ferouz alivyoimba kweli hawana cha kufanya zaidi ya kubambikia kesi wananchi. Kuna Binamu yangu yeye kasomea mambo ya electronics na ni fundi TV wakati huo, siku moja alipigiwa simu na jamaa anayemfahamu aende akachukue TV kwake imeharibika, kama saa 12 jioni hivi jamaa akaenda akaicheki akagundua ina hitilafu kwa hiyo inahitaji kwenda workshop ikafanyiwe kazi, akatoka pale alipo kaibeba kichwani na fundi mwenzie si mbali na home kwake mwendo kama wa dk tano tu hivi, njiani akakutana na Polisi wawili, wakamhoji unapeleka wapi TV usiku huu, jamaa akajitetea kuwa yeye ni fundi na anaipeleka ile TV workshop, polisi wakadai nyie ndo wezi wenyewe leta risiti ya kununulia TV, jamaa akasema kama vipi twendeni kwa mwenye TV mkadai hiyo risiti polisi hawakuhitaji maelelzo zaid wakamkamata na kwenda naye polisi post wakamweka 2days pale mpaka habari zilipotufikia jamaa tayari alikuwa keshabambikiwa kesi ya kuua ya mtu aliifanya songea huko na ilibaki siku moja tu angepandishwa kizimbani, ilibidi kutoa kilo nzima kuifuta ile kesi hiyo ilikuwa ni miaka ya 2000-2001. Jeshi hili limeoza SANA TUUU, hakuna anayesema ukweli huko
 
kwenye swala la jerry....!nitakisimamia ninachokiamini.na ninachoamini ni kwamba jerry wamemuundia scandal
tatizo sio kuundiwa scandal..............
yaani unaamini jerry hawezi kuchukua rushwa?????
kwa kuwa sio mtanzania?????
kwa kuwa yeye sio binadamu hivo unaamini hawezi kuwa na mapungufu????
KWA TAARIFA YAKO..............KELELE NYINGI ZOTE ZINZLENGA MASLAHI BINAFSI YA BAADAE NA ZINALENGA KUWAFUMBA MACHO WALE WENYE UPEO MDOGO WA KUAMINI KUWA ANAEKEMEA HAWEZI AKAFIKIA HATUA YA KUKEMEWA........
mwacheni awajibike kwa makosa yake...........kama sio kweli pia itajulikana ila huwezi kumtia mtu hatiani kabla ya mkondo wa sheria kuingilia na pia huwezi kumwondoa mtu hatiani kabla haijathibitika kutokuwa na kosa.............
 
hii ndo Tanzania bwana, wanaofanya mema wote wanachukiwa na kuzimwa kwa style tofauti na wasio waadilifu wanasurvive tu. sorry, but sometimes i hate this country.[/QUOTE]

TAFAKARI CHUKUA HATUA;HAKUNA MTZ ASIPENDA MTEREMKO/SLOPE YOTE HAYA SABABU YA MAISHA MAGUMU!!!!!!! :confused:
 
Baada ya sakata la Jerry muro na polisi kuripotiwa umaarufu wake umeongezeka kwa zaidi ya 100%
Vyombo vyote vya habari vinamuongelea yeye, forums mbalimbali zinamuongelea yeye, kwenye blogz ni yeye tu, mitaani ndio usiseme, hadi watoto wanajadili ishu yake.
 
yes....................
hata ccj pia imekuwa hivo.......umaarufu umekuja ghafla na bila gharama yoyote..........habari ndio hiyo.
 
Huyo dogo anaweza kuwa Jambazi.....ngoja tuchambue Singles zake kwanza.Amenikumbusha wale vijana wa kirusi
 
tatizo sio kuundiwa scandal..............
yaani unaamini jerry hawezi kuchukua rushwa?????
kwa kuwa sio mtanzania?????
kwa kuwa yeye sio binadamu hivo unaamini hawezi kuwa na mapungufu????
KWA TAARIFA YAKO..............KELELE NYINGI ZOTE ZINZLENGA MASLAHI BINAFSI YA BAADAE NA ZINALENGA KUWAFUMBA MACHO WALE WENYE UPEO MDOGO WA KUAMINI KUWA ANAEKEMEA HAWEZI AKAFIKIA HATUA YA KUKEMEWA........
mwacheni awajibike kwa makosa yake...........kama sio kweli pia itajulikana ila huwezi kumtia mtu hatiani kabla ya mkondo wa sheria kuingilia na pia huwezi kumwondoa mtu hatiani kabla haijathibitika kutokuwa na kosa.............

Napenda watu wenye misimamo katika issues na wala si emotions. Mimi si mtazami Jerry kama anaonewa bali ninamtazama kama mtuhumiwa.
Sheria haitambui kwamba wewe unaifanyia jamii mazuri basi ukituhumiwa mabaya ni uonevu.
Jerry tumekusikia, lakini hata hivyo tuhuma ni tuhuma hazibagui, sasa hivi ni wakati wako na wewe kujinasua dhidi ya tuhuma hizo.

Ushauri:
Kaa chini utafute namna ya kujibu tuhuma hizo na huu si wakati wa kutaka huruma au kufikiri umeonewa.
Achana na media tatua tatizo lako.
Mwisho, kwa vile kuna madai ya kwamba ulimfunga mtu pingu, basi ni vema bila ya kumung'unya ieleze jamii hizo pingu umezipata wapi na unazitumia kwa kazi gani?
 
Mkuu kunaushabiki hapa unaendelea wa hali ya juu nimeshangaa sana Muro kusema Kova siyo jeshi la police, nadhani Muro amepandwa na jazba ambayo haimsaidii sana.

Kuna jambo ambalo Polisi wanalijua juu ya Muro na ninahisi hiyo ya kusema kuwa aliitwa kuombwa rushwa ilikuwa ni sababu ya kumpata akiwa na Bastola na Pingu.
Muro inabidi aeleze kinagaubaga matumizi ya Pingu hizo. Kwani tayari analalamikiwa kuzitumia.
Nimeziangalia clips zote 2, Jerry kuna mambo halisi kabisa lakini hawezi kuyasema juu ya sakata hili.
Kwa vile binadamu si malaika, si wezi kumchulia dhamana Jerry kwa lolote bila ya kutoa maelezo ya matumizi ya pingu.
Ninaamini, kitendo chochote cha kutumia pingu kwa mtu ambaye si mlinzi wa usalama, ni kitendo cha kutumia nguvu na kujichulia sheria kutoka mikononi mwako.
 
Hivi TBC hawajatoa tamko hadi sasa au wanasubiri kesi ifike mahakamani? At least baraza la waandishi wa habari wamesema kitu nimemsikia Kajubi Mukajanga akizungumzia suala hili. TBC vipi?
 
Baada ya sakata la Jerry muro na polisi kuripotiwa umaarufu wake umeongezeka kwa zaidi ya 100%
Vyombo vyote vya habari vinamuongelea yeye, forums mbalimbali zinamuongelea yeye, kwenye blogz ni yeye tu, mitaani ndio usiseme, hadi watoto wanajadili ishu yake.
Muro Gombea Ubunge ule ulaji maana umaarufu umepanda ongera na pole na matatizo
 
Back
Top Bottom