Hivi kweli, inakuja akilini kweli. Ninavyojua mawakala wote wanakagua maboksi yote kabla ya watu kuanza kupiga kura. Hizo kura bandia si wataziona?
Hizi kelele zinatuchosha, wajaribu kufikirisha ubongo.
Wana JF habari;
Leo asubuhi nimeamka vibaya hasa kwa kutune redio ya CCM (Uhuru FM) habari ya kwanza kusikia ni kua basi nne zenye watu waliobeba silaha kama Marungu, Panga na Bunduki madawa ya kulevya kama Bangi toka Mara zimekamatwa Tinde zikielekea Igunga kama maandalizi ya kufanya vurugu j2 kwenye uchaguzi.
Kwa mjibu wa redio CCM wanasemekana ni Vijana wa CDM waliosafirishwa kufanya vurugu hizo. Wadau mlioko maeneo husika Habari hiz ni za Ukweli? Au ni visingizio tu, manake siamini kama kweli hii ikitu inaweza kutokea, na sijui wamewajuaje kama ni watu wa CDM.
Naombeni kwa mwenye taarifa zaid atujuze!
Hii habari haina ukweli ndani yake labda uwe umeishia madrasa
......(hivi) Chadema ina mawakala kwenye kila kituo?
hapo kwenye nyekundu ni kwamba taarifa za uhakika huwa hazina kawaida ya kudai bali huwa zinaeleza kwa kuwa tayari zina uhakika! pili si mara ya kwanza kwa chadema kudai kuna kura za wizi, rejea mwaka jana kule tunduma mlipodai masanduku ya kura yameingizwa nchini kumbe vipodozi na msivyo waungwana mpaka leo mmeshindwa hata kuomba radhi wakati ile ilikuwa ni fitna ambayo ingeweza kuligawa taifa vipande,tatu,msipoanza kusema uongo kama huu hamtaonewa huruma na mengi na akina sabodo tena make wamekufadhilini magari na helkopta so mnatengeneza mazingiira ya kuwa pleased! bye,tarehe 2 october kichapo kikali igunga
Jamani wa TZ kuna haja sasa ya kuingia msituni kwa ajili ya kuikomboa nchi yetu kutoka mikononi kwa MAGAMBA serius...!Without doing so hayo mabadiliko tunayohubiri kila siku kua tunayataka yatakua ni ndoto
Mbowe si kasema washapeleka vijana wao Nzega, we kazee vipi...!!Kama wanajua yalipo na yanavyopangwa kutumiwa kwanini wasitumie muda kupanga kuyakamata "live"? Ingekuwa ndio ushahidi mzuri kweli hasa kwenye mazingira ya digital camera na internet.. sasa yasipotokea Jumapili tutaamini kuwa yamedhibitiwa siyo? Na kama hayakuwepo? Chadema ina mawakala kwenye kila kituo?
Hivi kweli, inakuja akilini kweli. Ninavyojua mawakala wote wanakagua maboksi yote kabla ya watu kuanza kupiga kura. Hizo kura bandia si wataziona?
Hizi kelele zinatuchosha, wajaribu kufikirisha ubongo.
Mchezo huwa hivi,kura sikisha pigwa vituoni na kuhesabiwa vinapelekwa kwa msimamizi wa uchaguzi [mkurugenzi ] hapo ndipo wanapochakachuwa kuingiza hizo kura hewa...swali langu kama zimehesabiwa kituoni wanahesabu nini tena ? mara nyingi matokeo ya vituo yanakuwa tafauti na ya mkurugenzi
..Na kale kazee Wilson Mkama sioni tofauti yake na Makamba...Sijui CCM hawa watu huwa wanawatoa wapi?Yale yale ya MKAMA aliyesema kuwa kuna makomandooooo, yaani siasa za Bongo inabidi Mungu aingilie sana
Asante sana kwa taarifa!Bukijo,Pole kwa kuharibiwa moody yako asubuhi.
Naomba nikupe taarifa kamili:
Kuna wadau na wapenzi wa mageuzi au washabiki wa chama cha chadema ambao waliamua wao wenyewe kwenda kuwapa moyo na kutia hamasa kwa wanaIgunga,watu hao wametokea mwanza na walikuwa ndani ya Costa 4 idadi yao inafikia 120 hivi.watu hao walikamatwa jana saa tano usiku.Nikweli polisi wamewakagua na kuchukua maelezo yao,watu hao hawakukutwa na silaha zozote wala aina yoyote ya rungu inasemekana walitaka kuwabambikia vitu hivyo,lakini vijana hao wakawa wajanja baada ya kukataa kuondoka usiku walipoachiwa.wameondoka asubuhi na hakuna tatizo.
Ukitaka kujua hili ibeni kura Igunga muone kazi itakayofanyika.Ww kweli upo tayari kufa ? pambana kwanza kuikoa familia yako ambayo iko hali mbaya na kutaabika !
Mchezo huwa hivi,
Kura zitahesabiwa vituoni lets say chama pinzani mnapata 250 na CCM 200, mnaanza kushangilia, masanduku yanakusanywa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ambapo kura bandia zinaingizwa, mgombea wa CCM au chama kidogo kilichoandaliwa na CCM kinajidai kulalamika turudie kuhesabu, huku nje wapinzani tayari wanashangilia, baada ya kurudia kuhesabu inaonekana kumbe CCM wana kura 300 hapo kura 100 zimeongezwa na mchezo unakwisha. Mara nyingi unapoona sehemu wanachelewa kutangaza juwa zoezi hili linafanyika kwa usiri mkubwa. Ilitokea Busanda CDM wakaanza kushangilia baadae wakaambiwa kura za vijijini zilikuwa hazijafika, ilitokea pia Shinyanga, Segerea na sehemu zingine, safari hii Ubungo ilishindikana kutokana na uimara wa mawakala kila kituo kilikuwa na mawakala wa CDM zaidi ya wawili.
Kitu cha kufanya kwa sababu wanaofanya biashara hii ni binabamu kama sisi ni kuweka waangalizi sehemu yalipo masanduku kuanzia siku ya kuletwa yakiwa matupu, mbali ya mawakala kuwepo kila kituo kuwe na watu tofauti wakufatilia mienendo ya masanduku usiku na mchana toka yalipohifadhiwa, usafirishwaji, upigaji kura, kuhesabu kura na utunzwaji baada ya kuhesabu hadi matokeo yatangazwe na wawe na mawasiliano ya haraka linapotokea tukio lolote lisilo la kawaida.
Mwisho njia zote za kuingia na kutoka Igunga na kwenye Halmashauri zijulikane na wawe na waangalizi usiku na mchana, wakidhibiti mianya hiyo nina uhakika matokeo yatakayotangazwa yatakuwa halali.
You are sinking. Vatican ilisifia lini?