VAT registration upatikanaji wa electronic fiscal device (efd)

Jun 26, 2012
39
10
nahitaji kujua njia rahisi (kama ipo) kwa ajiri ya upatikanaji wa hiki kifaa (efd), na VAT registration.
Kwa habari nilizonazo ni kwamba hiki kifaa kinauzwa usd 2000.
 
nahitaji kujua njia rahisi (kama ipo) kwa ajiri ya upatikanaji wa hiki kifaa (efd), na VAT registration.
Kwa habari nilizonazo ni kwamba hiki kifaa kinauzwa usd 2000.

je unafanya mauzo ya bidha zinazotozwa vat?
je turnover(mauzo ya bidha zinazotozwa vat) yako kwa mwaka unafikisha 40m au 10m katika three consecutive month?
Hivi ni vgezo vikuu ambavyo mtu yeyote yule anayetaka kujisajili kama wakala wa VAT lazima awe navyo.
Kama una hivyo vigezo una uhalali wa kusajiliwa kama wakala wa VAT hivyo fika ofisi za TRA ktk eneo ulilopo watakupa taratibu za kuapply 4 VAT reg.
Kuhusu bei za electronic Fisical Device(EFD) sina uhakika nazo ila kama upo dar waweza kufika victoria BMTL au mlimani city kwa maelezo zaidi kwani hawa ni agent waliosajiliwa na TRA kwa uuzaji wa EFD.
Kama kuna wenye taarifa zaidi watakupa wakifika hapa.
Kumbuka huwezi na huruhusiwi kutumia EFD za VAT kama hujasajiliwa na TRA kama agent wa VAT na ukapewa VRN(VAT Reg No)
 
nahitaji kujua njia rahisi (kama ipo) kwa ajiri ya upatikanaji wa hiki kifaa (efd), na VAT registration.
Kwa habari nilizonazo ni kwamba hiki kifaa kinauzwa usd 2000.
1. Kwanza unaenda TRA kufanya VAT Registration ni bure ali mradi biashara yako iwe na turn over ya zaidi ya milioni 40 kwa mwaka.

2. Ukishapata VAT Reg certificate yako, unakwenye kwenye makampuni approved na TRA kuuza hizo EFD, yote ni ya wahindi isipokuwa Peganon iko pale Msasani kwa Mwalimu hii ni ya wazawa japo bei zao nao zimesimama.

3. Mashine ndogo kabisa ya kutoa risiti ni $ 800 tuu, ila ukitaka ile kubwa ya kutoa invoice ndio $ 2000 ukikomaa nao watakupa kwa $ 1,600!.
 
Back
Top Bottom