Zijue mbinu zinazotumiwa na wezi wa magari, kisha chukua tahadhari

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,718
10,214
1. Wizi wa kutumia mfumo wa Keyless. Wizi wa keyless au wizi wa relay ni wizi ambao huusisha watu wawili ambao hufanya uhalifu huu kwenye magari ambayo yameegeshwa nyumbani. Wizi huu huusisha vifaa viwili ambavyo ni "relay transmitter" na "amplifier", hivyo wanatumia vifaa hivi kuidanganya gari na kuifanya ifikiri kuwa funguo ipo karibu na hivyo automatically gari inajifungua(unlock) na wezi wanapata nafasi kusepa na ndinga.

Kujilinda na wizi huu wa kutumia mfumo wa keyless ni bora kuzima signals baada ya kuegesha gari lako. Baadhi ya funguo huwa na "sleep mode" au unaweza kuweka ufunguo wako kwenye kifaa cha chuma chenye kublock signals, na kuna baadhi husema foili huziba signal ila sijaprove kwa hilo.

2. Wizi wa kuvamia. Wizi huu ni ule ambao wezi huvamia nyumbani kwako kwa kutumia nguvu na kisha kukupora funguo za gari na kuondoka. Kujilinda na wizi huu hakikisha milango yako ya nyumba imefungwa vema au tunza funguo yako sehemu ambayo sio rahisi kufikiwa kama vile kwenye droo zenye lock.

3. Wizi wa turbo decoder. Huu ni wizi ambao mwizi huchokonoa kwenye tundu la lock. Hichi kifaa akikiingiza kwenye tundu la mlango wa gari lako huwa kinatengeneza umbo la funguo ya gari lako na kufanikiwa kufungua(funguo mal*ya wa kisasa). Huu wizi hufanyika sana sehemu zenye kuegeshwa magari mengi.
Kujilinda na huu wizi, yakupasa uongeze ulinzi zaidi kwenye gari lako kama vile kufunga alarm au kutumia steering wheel lock. Vilevile hata mfumo wa tracking huweza kusaidia pia.

4. Transponder key cloning. Huu ni wizi ambao mwizi huchukua funguo wako na kuufanyia copy. Hii hutokea sanasana labda umeacha gari garage au car wash, hivyo mwizi hupata nafasi ya kucopy code za funguo na kuhamishia kwenye funguo empty ambazo hununuliwa zikiwa hazina code yoyote na baadae kukurudishia funguo, hivyo kusubiri siku zisogee akuibie gari kwa ule ufunguo aliotumia kucopy code muhimu.
Kuepuka wizi huu fanya uchunguzi kwa utakao wakabidhi ufunguo iwe gereji au car wash maana wizi huu hufanyika baada ya muda. Hata hivyo kuepuka na wizi huu unaweza kufunga ulinzi zaidi kama vile steeling wheel lock na gear stick lock.

5 On- board diagnostic(OBD). Huu mfumo wa OBD huwa na taarifa zote za mifumo ya gari. Kawaida fundi akitaka kutengeneza gari lako atatumia hichi kifaa kuchunguza afya ya gari lako. Hivyo kama fundi ni mwizi atatumia kifaa hichi kuiba mifumo ya gari lako. Sasa kama ni mwizi anayetumia huu mfumo ana urahisi zaidi wa kuiba taarifa za gari lako. Baada ya kuiba taarifa za gari, kwa kutumia turbo decoder au kwa njia nyingine, atachomeka kifaa hicho kwenye kishimo(port) cha OBD ambacho kipo chini ya dashboard na anakuwa na uwezo wa kudownload information zote za gari na code maalumu atakazotumia kutengeneza funguo bandia au copy. Kujilinda na wizi huu ongeza ulinzi wa steering wheel lock na handbrake lock ambayo ni ngumu kuitoa.

6. Electronic Control Unit (ECU). Huu ni wizi unaotumia laptop na computer ambao hucontrol mfumo wa injini na sehemu zingine za gari. Hii teknolojia huweza kutumiwa na wezi kuiba gari wakiwa mbali na sehemu husika. Huu wizi hutumia muda sana, hivyo mwizi hulenga sanasana magari ya biashara yanayoegeshwa usiku mzima bila kufanya kazi.
Mwizi atatumia ECU empty akitumia pia njia ya turbo decoder na kuhamisha ECU yote ya gari. Kujilinda na wizi huu inapaswa mlinzi awe anakagua kagua kila muda kwenye sehemu ilipoachwa na pia unaweza kutumia usaidizi wa CCTV.

7. Car key code grabbing. Huu ni wizi ambao mwizi hujifanya akisubiria kitu sanasana kwenye sehemu za maegesho au supermarket akivizia code za funguo ya umeme kupitia mawimbi akiwa na kifaa maalumu cha umeme cha kunasa code hizo.Baada ya kufanikiwa kunasa code huzidownload code hizo na kuzihamisha kwenye funguo yake. Kujilinda na wizi huu angaliaangalia sehemu ulipoacha gari lako na kuwa makini na mtu ambaye haeleweki akizungukazunguka sehemu ulipoacha gari, vilevile steering lock inasaidia.

8. GPS jamming device. Hichi kifaa hukitumia kujam gps ya gari ili isionekane inapopelekwa au ilipopelekwa baada ya kuibwa. Huu wizi hufanya kazi kwa zile gari zilizonunuliwa zikiwa na tracker ya nyongeza kama security ila huwa ni ngumu sana kufanya kazi kwa tracker zilizowekwa(VHF Technology).
 
Asante kwa elimu.
Lakini nina swali nje ya mada.

Hivi kwa nini wastaafu wengi kwenye kada mbalimbali ndio mara nyingi hutumika kama wakufunzi mashuleni.
 
Asante kwa Elimu

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom