Uzuri wa magari ya automatic na manual...!!

aa mm naipenda Manual kwani muziki wake naupenda unaweza kwenda mpaka 4, halafu ukarudi 3, lakini ukapitia clutch na ress kama 2 hivi ni lazima utanyanyuka katika kiti kidogo basi usingizi hauji, unakaa kidogo unaitupia 4, halafu ress 2 unaingia over (5)
Lakini AT unalikanyagia weeee watu watadhani ww ni mDADA Du shit
 
Naomba mjiulize. Je kuna gari lolote la Serikali ya JMTz au SMZ ambalo ni automatic? Je mnaweza tujuza ni kwa nini?
 
Naomba mjiulize. Je kuna gari lolote la Serikali ya JMTz au SMZ ambalo ni automatic? Je mnaweza tujuza ni kwa nini?


Acheni utani kabisa gari la manual ukilifunga lile bomba la moshi lenye milio utaona raha yake, mita 20 umeshamaliza gea zote tano aftena unafuta unaanza wani huku watoto mtaani wanachangilia ureeee.....
 
Manual ni gari imara sana kuliko Automatc. Unabadili gia unapoona inahitajika kufanya hivyo. Matumizi mazuri ya mafuta. Ikikataa kuwaka hauna haja ya kutafuta gari nyingine ili kuboost betri. Change down inafanyika vizuri. In short i prefer manual to automatic
 
sina hoja wala ushauri, naosha kinywa tu jamani :hat: mi napenda Tiptronic a.k.a Manumatic gearbox :loco:
 
Mkuu gari ni Manual achana na automatic za kike.Nilikuwa na ka-automatic basi ilikuwa kila siku ugomvi na wife yaani gari ikiwepo home tu yeye keshapata safari sasa tangu ninunue automatic aaahh raha tu manake ni mimi tu ndo nayeweza kuizungusha yeye zake lawama tu.
 
Mkuu gari ni Manual achana na automatic za kike.Nilikuwa na ka-automatic basi ilikuwa kila siku ugomvi na wife yaani gari ikiwepo home tu yeye keshapata safari sasa tangu ninunue automatic aaahh raha tu manake ni mimi tu ndo nayeweza kuizungusha yeye zake lawama tu.

Mkuu hiyo kwenye blue nafikiri ulitaka kusema "manual" ukasahau tena
 
Habari wana JF??

Sie wengine magari ya manual tulijifunzia tu lakini tumekuwa tukitumia automatic kwa muda mwingi sana.

Ok, issue iko hivi...nimekuwa nikitumia gari yenye automatic transmission, sasa kuna jamaa yangu yupo Ulaya nikaomba aniangalizie gari ingine kutoka huko na kanitafutia gari nzuri sana ya 2008*ila ni manual. Kiukweli nimeipenda ila nilihofu kuhusu hiyo transmission yake na kila ninayemgusia ananiambia gari za manual si nzuri ukilinganisha na automatic. Swali ni je kwa nini bado zinatoka na Ulaya wanapenda manual zaidi kuliko Africa na Asia???

Tatizo ni kwamba sijapata mtaalam wa kunifafanulia hasa uzuri na ubaya wa gari za manual kushinda automatic.

Wataalam tumwagieni maujuzi kuhusu hii kitu ili niondoe hii conflict niweze kuchukua kitu nikiwa na raha kumoyo!!!!

Nawasilisha

Bila hata kusoma michango ya wengine, mimi nipo ulaya. Issue ni kwamba automatic ni bora kuliko manual. Ila Ulaya wanapenda hizo manual kukwepa gharama, maana yake ukinunua automatic bei inaongezeka kuliko manual na watu wengi wanakwepa hiyo gharama (kumbuka ongezeko kidogo lina imapact kwenye insurance n.k.).
 
Inategemea unaongelea uzuri gani. kama ni urahisi wa kuendesha sawa ni automatic. kama ni ubora automatic hamna kitu ndugu. Wamezitengeneza kibiashara tu. Ndio mana nchi zilizoendelea hawatengenezi wala hawanunui.

Hujui ndugu. It is too expensive in europe to buy automatic transmission car compard to manual
 
Hujui ndugu. It is too expensive in europe to buy automatic transmission car compard to manual

Hapa kuna contradictions kidogo mkuu. Unachosema nimewahi kumsikia dada mmoja wa Kijerumani akikisema pia. Lakini ni kinyume hake kwa Japani. Maana ukiingia hata kwenye mitandao ya wauza magari wote wa kijapani utakuta kuwa magari ya manual ni ghali kuliko automatic, hapa sasa sielewi.. Huenda Ulaya wamefanya hivyo ili kuwa-discourage watu kununua magari automatic ambayo wanajua matatizo yake (ni mawazo yangu tu haya).
 
Automatic ikizima wakati ipo kwenye gear utaoona joto lake, utatamani kulibeba, ila manual unaweza jaribu kulishtua hata kama chaji ya betri ipo chini, au unaweza acha silence bila ya kuwa na betri na ikaendelea kuwaka.

Ni raha unapocheza na gear kwenye manual,
 
Dunia inakwenda inabadilika wandugu..kama una pesa nunua AT,maana bei yake imechangamka kuliko manual
AT hazina usumbufu kabisa kama watu wanavyosema,hata ukitaka ya masafa marefu we chukua engine kubwa....hapa UK magari yote ya police ni AT na mabus yote ya public transports ni AT.
 
Best choice buy manual. Ever asked yourself whether any of those drivers who died in USA after their cars were stuck in acceleration mode had a manual? it would not have happened since declutching would have neutralised any acceleration. Save for very recent automatic vehicles that have decent 0-60kph revving up to overtake in a highway is left at the mercy of slow gear changing autos while in a manual upshift or downshift is driver dependent.
My two cents
i) if the bulk of your driving will be spent cruising on a highway buy a manual
ii) if it will be spent stuck in traffic jams buy an auto
 
Dunia inakwenda inabadilika wandugu..kama una pesa nunua AT,maana bei yake imechangamka kuliko manual
AT hazina usumbufu kabisa kama watu wanavyosema,hata ukitaka ya masafa marefu we chukua engine kubwa....hapa UK magari yote ya police ni AT na mabus yote ya public transports ni AT.

Mkuu Polisi wanatumia AT kwa ajili ya urahisi wa kufukuza/kukimbiza wezi/wahalifu na hayo mabasi AT ni yale tu yanayofanya safari fupi za mjini ila yale ya safari ndefu ni Manual. Hilo la bei ni kwa Ulaya na Marekani tu ila Japan manual ni ghali kuliko AT. Check mawazo ya watu wengine hapa : http://manualversusautomatic.com/
 
Jambo wana jf.

Mimi nina zote na mara nyingi kwa safari fupi za hapa town na prefer auto ila kama ni long trip basi manual ndo best coz unakua bize muda. Fuel consumpt: manual is the best maana we ndo unaiendesha wakat auto inakuendesha. Kubwa zaidi auto service yake iko juu maana lazma ubadilishe hydrolic pia while manual ni engine oil tu na ofcoz filter.

Nafikiri cku zote kabla ya kununua kitu chochote ni bora uka fanya a very simple analysis kwa ku compare pros and cons hence decision, mf: ukubwa wa familia? Matumizi yako ni rough road au rami tu? 4wheels au 2wheels maana unaweza kua unaishi sehemu ambayo gari fupi haliwezi kuvumilia shida esp wakt wa masika au barabara ni mbaya sana labda mchanga mwingi au matipo so u must hv a 4x4 au unashuguri za offload eg shamba u need kubeba mbolea, miti etc lkn kubwa pia ni space maana huwezi kufikiria short chasis wakt familia yako ni zaidi ya watu watano.

Kingine ni kipato chako, maana unaweza kukuta gari linatumia zaidi yako wewe na hata ukashindwa kuliendesha labda wiki ya kwanza ya mwanzo au mwisho wa mwezi tu ( hapa nime wagusa wengi wetu) siku zingine mzee unawahi kituo cha basi. Kumbe ungeweza kuchukua stalet au vitz na Mambo yako yakawa shwari tena full mfindi aka kiyoyozi wenzetu wanasema air condotion maana wapo wenye fikra potofu kuwa a/c inakula mafuta hahaha, unakuta mtu anazima ac kisa mafuta wakat bar na guest house anatumia zaidi na mwenziwe au washikaji (hapa pia nimewa...wengi hahaha).

Anyways to make it short manual is more durable maana inatengenezeka wakati auto mara nyingi unatakiwa kunua complete componet eg ingine kumbe tatizo lilikua piston au sleeve tu. Nakaribisha maswali maana hii ndo field yangu.
 
Kwa mtazamo wangu manual cars ni mazuri zaidi ukilinganisha na automatic cars,ukizingatia vigezo vifuatavyo:-
1.Utumiaji wa mafuta-manua inatumia mafuta kidogo ukilinganisha na automatic katika hali ya kwamba dereva ndio unashift gia lakini kwenye automatic gia haiwezi kushift hadi ukanyage sana accelerator.na gia itachange kulingana na ilivyokuwa program mfano after 20km/h.Pia kwenye mteremko unaweza ukaiachia gari free(N) ikaweza kwenda kwa umbali mrefu NB: haishauriwi sana kufanya hivyo kwenye mteremko,wengi wanafanya hivi kupunguza fuel consumption.
2.Dereva anakuwa na full control ya gari, kwa maana kwamba anakuwa na clutch, brake na accelerator.wakati kwenye auto unakuwa na brake na accelerator tu.Kwenye manual hata kama gari iko kwenye gia na ukaapply mafuta hadi mwisho bila kuachia clutch gari haiwezi kuondoka hata iweje.while kwenye auto gari kama ipo kwenye D na ukaachia brake gari inawezakwenda.Na ndio hicho kinachowapaga watu jeuri anakata kilaji hadi anapitiliza anasema nikikaa kwenye usukani tu nitafika nyumbani wakati yuko bwii na hii mara nyingi inakuwa rahis kwwa automatic.
3.Ukiendesha manual unaenjoy kuendesha gari unahisi kabisa kuna kitu unafanya gia unavyoshift u feel it lol
4.Kwa ubora in terms ya durability uwa zinadumu ukilinganisha na automatic.
5.Kutoka na nature ya nchi yetu watu wengi wanapata leseni hata gari hajawahi kulugusa ni vigumu sana mtu kuendesha manual kwasababu wengi wanajua kulenga barabara lakini sio udereva hasa.pia na madereva wengi tz anaendesha gari huku anachat na simu,mara hivi so inapelekea kuprefer automatic zaid.Na hali ya foleni inachangia wengi kupenda kutumia automatic.
 
binafsi nafagilia sana MANUAL haswa huku mikoani kusiko kua na foleni utaipenda.
1. wese inakula kidogo coz inakupa great control kwenye gia. mfano kwenye kilima kikubwa unapanda na namba 2 na manual lakini ikiwa AT lazma ijiset kwenye gea namba 1 ambayo ina nguvu zaidi na inakula wese.
2. manual ni nzuri kwa sehemu zisizo na foleni kama dar, wakati AT ni nzuri kwenye foleni kali, haupati maumivu ya kucheza na clutch, accelerator na breki kwa wakati mmoja.
3. vyuma vya mjapani vya manual ni cheap kuliko ATs!
4. manual ukiendesha kweli unajiona unaendesha gari na sio AT (kwa kina mama, wadada na watoto!)

Unapiga hand brake tu alafu wakati wa kuondoka unakanyaga accelerator kwanza ikishitua kuondoka unaitoa handbrake maana ku-balance clutch na accelerator kwa sie madereva wa kichina hukawii kuunguza clutch
hahahaaa, kweli wewe sio dereva!.
kama mlima ni mkali kama ile ya kule kimara bonyokwa au kilungule lazma likushinde, kubalance clutch na accerator its too simple than using the handbrake, maana ukicheza kidogo ikakushinda wakati wa kuachia handbrake lazma gari litazima. sasa pata picha gari ndio limeshazima linaanza kurudi nyuma halafu linatumia hydraulic, means breki hazikamati, stering inakua ngumu vibaya mno!.


Manual au automatic inategemea na matumizi ya mtu anayenunua , na zote zina umuhimu wake katika matumizi, kama unahitaji gari kwa matumizi ya safari zenye kuhitaji max power output kama vile milima matope au racing nunua manual ,kama unatcumia kwenye barabara zenye foleni safari fupi fupi automatic ni chaguo sahihi.
uko sawa kabisa mkuu!, foleni za dar ni nuksi, ukifika home mguu wa kushoto unauma balaa kwa kucheza na clutch na breki always si unajua zile daladala linataka kukuchomekea na wewe unalibania kwa hiyo hapo lazma ufanye kazi ya ziada kucheza na clutch na breki!, lakini ukiwa na AT aaah wala haikupi shida.
kuna siku bwana nilikua naendesha manual, sasa kumbe brake fluid ilikua imevuja na ikawa imepungua sana halafu mbele yangu ndio foleni imeanza kila nikikanyaga breki nakuta holaaaa, kilichonisaidia ni kupunguza mwendo kwa kutumia gea, assume ingekua AT hapo nini kingetokea kwa gari ilokua mbele yangu.

Naomba mjiulize. Je kuna gari lolote la Serikali ya JMTz au SMZ ambalo ni automatic? Je mnaweza tujuza ni kwa nini?
karibu asilimia 99 ya magari ya serikali ya JMTz ni MANUAL especially kama limenunuliwa likiwa jipya kabisa!. si unajua lazma wafuate mchakato wa manunuzi, so lazma mzabuni anaeiuzia ataambiwa apeleke kitu cha manual wakijua kuna kukabiliana na barabara mbovu.
mengine yanayotolewa kama misaada au yaliyotumika kwenye miradi ndio wakati mwingine huwa AT

Acheni utani kabisa gari la manual ukilifunga lile bomba la moshi lenye milio utaona raha yake, mita 20 umeshamaliza gea zote tano aftena unafuta unaanza wani huku watoto mtaani wanachangilia ureeee.....
aaah wewe utaua gear box, yani kutoka gea namba tano uingize gea namba wani kweli!??.
unapoingiza gea lazma uingize moja baada ya nyingine KIUSALAMA na UTUNZAJI wa gearbox, hata kushusha gea pia lazma ushushe moja baada ya nyingine (labda kama una dharura endapo breki zitafeli unaweza toa 5 ukashusha mpaka moja kupunguza kasi ya injini ingawa gea itakua NGUMU sana kuingia!).
 
Mimi watoto wangu wote nimewafundisha kuendesha manual. Hata wakinunua automatic lakini wanaweza kuendesha manual. Huwezi kuwa dreva mahiri kama huwezi kuendesha gari ya manual gear.
 
Back
Top Bottom