Uzi wa kupeana machimbo mbalimbali ya vifaa vya ujenzi na bei zake

Naanza na Mimi
Nilipata mbao kutoka kwa Ustaadhi mmoja hivi pale Buguruni. Fundi wangu aliniambia nimtume yeye akachukue yeye kwa TZS 450/futi 2x2 na TZS 900/ft Kwa 4x2. Alisema nikienda mimi nitapewa mbao mbichi, zisizo na dawa au zenye vidonda.

Nilivyoenda mwenyewe nilipata kwa TZS 350 mbao za 2x2 na TZS 700 mbao za 4x2. Yawezekana najiona cheaper kumbe nami nimepigwa bado ila ni angalau kuliko hardware za hapo napojenga.

Bati geji 30 nilipata kwa TZS 11,500/mita kiwandani Dragon.
Bati ulinunua za aina gani ?
 
Kwa mfano wa reject ni iyo nimezungushia duara apo
20230507_131218.jpg
 
60*60 za box 35,000
60*60 reject 25,000

Wall tiles size 25*40 bei 20500 za box, reject 17000
Chini chooni 30*30 bei 22000/17000
sawa 60*60 zinatoshea kwa mita ngapi za mraba? na kama kuna sampuli ile kama mbao naomba uweke tafadhali.
 
Back
Top Bottom