Uza bidhaa nchini Marekani ukiwa Tanzania

The Tai

Member
Dec 9, 2019
6
14
IFAHAMU BIASHARA YA AMAZON FBA.

Fulfilment By Amazon (FBA).

1.AMAZON ni nini?
AMAZON ni kampuni inayohihusisha na uuzaji wa bidhaa kwa njia ya mtandao yaani mteja atachagua bidhaa anayoiitaji kisha atalipia baada ya malipo AMAZON watamletea mteja bidhaa hiyo mpaka mahali alipo nchi yoyote.makao makuu ya kampuni hii yapo nchini marekani.

2. AMAZON FBA ni nini?
Hii ni huduma inayowawezesha wamiliki wa biashara kuweza kuunganishwa na mtandao wa usafirishaji bidhaa ulioanzishwa na AMAZON.

hii inafanyikaje?

Amazon itapokea bidhaa ambazo unaziuza kutoka kwa mtengenezaji wako itadhiifadhi bidhaa hizo na itakuwa inapokea oda ya bidhaa zako kwa njia ya mtandao wao (app au website) kisha Amazon wao watazipaki na kumfikishia mteja huyo.Amazon FBA inafanyika mahali popote duniani muhimu uwe na na simu au laptop iliyounganishwa na internet .


3.Namna ya kuanza biashara hii

Kama zilivyo biashara zingine pia biashara hii inahitaji uweze kujitoa vilivyo.

-Inatakiwa ujisajiri amazon kama muuzaji kupitia app ya Amazon seller ambayo utakuwa unalipia $39.99 kwa mwezi.

Sasa utajuaje bidhaa zenye uhitaji nchini marekani?

-Zipo site mbalimbali ambazo zinaonesha bidhaa zenye uhitaji zipo za bure na za kulipia ila za kulipia ndio zinashauriwa utumia zaidi mfano wa site hizo ni Hellium 10 ambayo wanatoza $29-$34 kwa mwezi na junglescout ambao wanatoza $39-$249 kwa mwezi ili kupunguza gharama tunashauriwa kutumia helium 10.

-Baada ya kujua bidhaa zenye uhitaji nchini marekani unachotakiwa kufanya ni kwenda katika app ya uuzaji bidhaa mtandaoni kama vike Alibaba au AliExpress ambapo utazitafuta hizo bidhaa zenye uhitaji baada ya hapo utawasiliana na mtengenezaji (manufacturer) wa bidhaa hizo (hapa lugha ya mawasiliano ni kiingereza 😂😂) kisha utalipia atakuandalia mzigo wako halafu atautuma kwenda Amazon baada ya hapo wataupokea na kuuhifadhi katika store zao kusubiri wateja watakao weka oda.

-Amazon FBA hufanywa na watu wengi duniani japo Africa haijasambaa sana hivyo bidhaa zenye uhitaji marekani kila mtu anakuwa anaziona hivyo basi unashauriwa kufanya yafuatayo.

-kutengeza brand yako mwenyewe yaani baada ya kugundua bidhaa zenye uhitaji nchini marekani unachotakiwa kufanya ni kuchukua picha za bidhaa hizo kutoka kwa mtengenezaji kumbuka mtengenezaji anatoa picha kwa kila mteja wake hivyo basi chukua zile picha zioengezee manjonjo ili zivutie,weka logo yako pamoja na barcode halafu mwambie manufacturer akuwekee kwenye aina ya bidhaa ulizochukua hii itasaidia bidhaa zako kuwa na muonekano wa tofauti hivyo kununuliwa na watu kwa haraka.

-Mzigo wako unapokuwa tayari unaweza kukaguliwa na Amazon kama upo sahihi hivyo kama utataka Amazon wakague mizigo yako kutoka kwa mtengenezaji wa Alibaba itakiwa ulipie kiasi cha $150-$300 kutegemeana na ukubwa wa mzigo.Ila sio lazima mzigo wako Amazon waukague wanaweza uchukua moja kwa moja bila kuukagua kama hutohitaji.

-Kwa kila bidhaa utakayouza kupitia Amazon wao kama Amazon watachukua kiasi cha 25% ya faida ya bidhaa hiyo.

-Kumbuka gharama za kuweka barcode/UPC code kwenye bidhaa zako ni kuanzia kiasi cha $5-$10 kwa bidhaa zote.

-Unashauriwa unapoanza kuuza bidhaa hizi wakati wa kupnga bei tumia formula ya ×3 au ×4 yaani mara tatu au nne ya gharama ulitumia kutengeneza bidhaa hiyo mfano umenunua kalamu kutoka Alibaba na kalamu moja imegharimu $1 hivyo bidhaa ikifika Amazon nenda kaiuze $3 au $4.

-Viu kama logo na mwonekano wa bidhaa yako baada ya kutengeneza itatakiwa umtumie mtengenezaji wa bidhaa zako ili akuwekee kwenye kila bidhaa ya aina hiyo uliyo agiza.

-kwa kuanza biashara hii inashauriwa uanze na angalau kiasi cha pesa kisichopungua $5000 sawa na Tsh 11,500,000 ili uweze kuona faida nzuri.

-Wakati wa kufanya mazungumzo na mtengenezaji wa Alibaba au AliExpress unaweza zungumza nae akakupunguzia bei na akakuwekea bidhaa muonekano ambao utauhitaji wewe.

Do your own research

Je kuna biashara unapenda tuijadili ? Basi tuwasiliane kupitia WhatsApp number
+255768796276
 
Kwa biashara zetu za bongo magumashi/feki na uswahiliswahili mwingi hapa tutaaibisha taifa hadi vizazi vijavyo vitapata laana ya milenia.
 
Hapa ni kuwauzia wazungu sildenafil naichanganya na unga wa karafuu nawaambia ni African ginger
 
Mkuu nimemaliza process zote za kufungua amazon seller acc..huwa ninaenda china na ninafahamiana na viwanda lakini nakwama kwenye bank account maana wamereject card yangu sasa je ni account gani wanazohitaji?
 
Mkuu nimemaliza process zote za kufungua amazon seller acc..huwa ninaenda china na ninafahamiana na viwanda lakini nakwama kwenye bank account maana wamereject card yangu sasa je ni account gani wanazohitaji?
Nadhani hapo fungua "SKRIL" account itakusaidia kutumiwa Hela kutoka Amazon Kisha wewe utakuwa unaileta kwenye account yako kama kawaida.
 
Nadhani hapo fungua "SKRIL" account itakusaidia kutumiwa Hela kutoka Amazon Kisha wewe utakuwa unaileta kwenye account yako kama kawaida.
Kwa sasa amazon hawaruhusu namna yoyote ya transaction zaidi ya bank account na credit cards
 
Umetumia bank Gani ?
Screenshot_20240403-185117_Chrome.jpg
 
Nadhani hapo fungua "SKRIL" account itakusaidia kutumiwa Hela kutoka Amazon Kisha wewe utakuwa unaileta kwenye account yako kama kawaida.
Inchi ina viongozi washenzi hii, majitu yana laana za ukoo sijui yanakuja kutuletea nuksi zao kwenye maisha yetu. Sasa mambo madogo kama kurusha pesa tu yameweka ngumu ili raia wasiwe na access ili sijui iweje matako yao hawa takataka.
 
Back
Top Bottom