Kwa kweli hali hii ya kujichukulia sheria mikononi inabidi idhibitiwe kabla maafa hayajawa makubwa. Kama leo wameru wamefanya hivi tukakaa kimya na kesho wakafanya wazigua kule Tanga si tutakuja jikuta watu wanafukuzwa katika mikoa ambayo si yao?
Mkuu WildCard, kumiliki shamba au mali yoyote si kosa. Liwe limeendelezwa na mmiliki wa awali au lilikuwa pori. Kinachohitajika ni uhalali wa umiliki wa shamba au mali hiyo.Utitiri na ukubwa wa mashamba haya wanayonunua viongozi wetu tena kwenye maeneo jirani na watu wetu masikini kabisa ndio inayonisikitisha mimi. Bado tuna mapori makubwa tu nchi hii yanayohitaji kuendelezwa. Viongozi wetu hawayaoni hayo. Wananunua ambayo tayari yameendelezwa pamoja na ukweli kuwa wanao uwezo mkubwa tu wa kufungua mashamba mapya kuliko hao wananchi. Tupunguze UROHO na UBINAFSI wa Viongozi wetu vinginevyo milipuko ya aina hii baadaye itageuka kuwa vita kamili. Kimaro hawezi kuililia KIWIRA ambayo haina hata eka 20 wakati yeye anamiliki maekari mengi kiasi hiki.
Mtanzania,Mbona wananchi walipojichukulia sheria kwa Ballali hamkulaani? Ndio maana wengine tunaipenda JF, rahisi kweli kweli kuona unafiki mkubwa ulioko hapa.
Kama tunalaani hizi tabia mbaya za wananchi kujichukulia madaraka mikononi mwao basi tulaani kwa kila mtu; tulaani hata pale hizo tabia zinapotumika kuchoma vibaka.
wananchi sio polisi, sio mahakama, hizi tabia za kuvamia na kuharibu mali za watu hazifai. Tusipoangalia tutaishia kuwa kama Zimbabwe.
Lakini pia wanasiasa nao waelewe kwamba kadri wanavyofanya deals mbalimbali za kuwaibia wananchi kwa kutumia system, kuna siku wananchi watashutuka na kuwafuata.
Makaayamawe nakubaliana kabisa na hoja yako ila bado nasisitiza kuwa walichokifanya si kitendo cha ujasiri na hata huyo aliyewatuma kama unavyosema ni kunguru mwoga ambaye hafai kuwa johari wa taifa letu changa. Kama wananchi hawa wanatatizo na Mh. Kimaro kuna njia nyingi tu za kutatua tatizo hili ikiwemo ya kumface na kumtamkia wazi kile wanachokitaka hata kama ni kuandamana na kumfungia njia asitoke ndani mwake.Mwanajamiione,
Sidhani kama hawa vijana wamejichukulia sheria mikononi mwao. Ni wazi kabisa kuwa kuna aliyewaamrisha kumshambulia Mbunge Kimaro.
- Hebu tujiulize, ni lini walalahoi wanathubutu kuharibu mali ya kiongozi wa juu serikalini kiasi hicho tena mchana mbele ya wanahabari?
- Viongozi kama EL, kwao vurugu zikitokea na watu wakachinjana, sidhani kama wao wanajali, ili mradi tu vurugu hizo ziwe zinawasaidia wao na familia zao kuendelea kuitafuna nchi.
Wananchi haohao wakimzomea Mkapa au wakipiga mawe msafara wa JK baadhi yetu tunawaona kama mashujaa wa aina fulani hivi. Wakichukua ardhi yao.....Kimaro anapinga ufisadi! Amiin nawambia hakuna ufisadi mbaya kama wa kujilundikia ARDHI huku ukiwaacha walio wengi kuwa wapangaji kwenye nchi yao. Moja Mambo ya msingi kabisa yaliyotufanya tudai UHURU wetu ni ARDHI. Mwalimu alilisimamia vizuri sana hili. Sasa limeanza kuvurugwa na akina Kimaro, Sumaye, Mkapa, Mramba, Yona,.....
Wananchi haohao wakimzomea Mkapa au wakipiga mawe msafara wa JK baadhi yetu tunawaona kama mashujaa wa aina fulani hivi. Wakichukua ardhi yao.....Kimaro anapinga ufisadi! Amiin nawambia hakuna ufisadi mbaya kama wa kujilundikia ARDHI huku ukiwaacha walio wengi kuwa wapangaji kwenye nchi yao. Moja Mambo ya msingi kabisa yaliyotufanya tudai UHURU wetu ni ARDHI. Mwalimu alilisimamia vizuri sana hili. Sasa limeanza kuvurugwa na akina Kimaro, Sumaye, Mkapa, Mramba, Yona,.....
Mbona wananchi walipojichukulia sheria kwa Ballali hamkulaani? Ndio maana wengine tunaipenda JF, rahisi kweli kweli kuona unafiki mkubwa ulioko hapa.
Kama tunalaani hizi tabia mbaya za wananchi kujichukulia madaraka mikononi mwao basi tulaani kwa kila mtu; tulaani hata pale hizo tabia zinapotumika kuchoma vibaka.
wananchi sio polisi, sio mahakama, hizi tabia za kuvamia na kuharibu mali za watu hazifai. Tusipoangalia tutaishia kuwa kama Zimbabwe.
Lakini pia wanasiasa nao waelewe kwamba kadri wanavyofanya deals mbalimbali za kuwaibia wananchi kwa kutumia system, kuna siku wananchi watashutuka na kuwafuata.
Ni kweli kabisa WildCard unayoyasema yana ujumbe mzito but kuzomea si sawa na kuharibu mali!! Ni njia moja wapo ya kuonyesha kuwa umekerwa kupita kiasi!! Kitendo chao wameru kimeweza kikasababisha maafa kama angetokea mtu wa kupingana nao shambani mule!! Isitoshe mtu kuwa na ardhi si kosa unless ardhi hiyo awe ameipata kwa njia za panya kitu ambacho hatuna uhakika nacho kwa Mh. Kimaro.
Sijui utaelezea vipi wale wakazi wa Lindi, Mtwara na hata maeneo ya Kisarawe wanaouza maeneo ya mashamba yao kwa wageni. Nao ikifika muda waje waharibu mali na mazao yaliyomo katika maeneo hayo?.
Wajumbe,
Napenda kutoa mchango wangu kama ifuatavyo.
Wabilah Tawfiq!
- Kwa mtazamo wangu, kinachotokea leo, suala la wananchi (soma "fukara") kujichukulia sheria mikononi, haswa kwenye migogoro ya ardhi, ni mwendelelezo wa mlolongo mrefu ambao umetokana na kuwepo kwa mazingira tatanishi kwenye uwekezaji unaotumia ardhi. Wananchi wanaona kwamba wao wametelekezwa na ardhi wanayoihitaji (ni mtaji mkubwa kwao) kwa ajili ya kilimo, n.k., kupewa kwa watu ambao TAYARI WANA UWEZO. Je, tumejiuliza iwapo wananchi hao wa Arumeru hawakuandika barua za maombi kwa Serikali yao, wakitaka (si kuomba) kupewa ardhi hiyo ili waitumie kujiendeleza kwa shughuli za kilimo, elimu, n.k.? Je, kwa nini walikataliwa na ardhi hiyo kupewa mtu mwingine, MWENYE UWEZO MKUBWA, Mbunge wa CCM, Aloyce Kimaro?
- Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kutabiri kwamba, itafika siku wale ambao hawana watashika mapanga, sime na mikuki na kuwatafuta wale walio-nacho, na kuwataka wawape sehemu ya kile walichonacho, ama kwa hiari yao au kwa nguvu. Kilichotokea kwa shamba la Kimaro ni dhihirisho na utimilifu wa utabiri huu.
[*]Wananchi wametambua hadaa kubwa waliyotendewa na watawala. Sasa wameamua kudai mapema haki yao. Suala ni, je, watawala watakuwa tayari kuwa waadilifu na wakweli kwa wananchi ambao ndio wamewapa dhamana ya kuitawala nchi hii, au wananchi wataamua kuitwaa (kwa njia ya demokrasia ama - God forbid - kwa njia ya silaha) na kuirejesha mikononi mwao?- Yaliyotokea Busanda na yanayotarajiwa kutokea Biharamulo yanatudhihirishia kwamba watawala hawako tayari kuiachia nchi hii itawaliwe na wananchi wengine zaidi yao wenyewe. Watawala wamejimilikisha nchi hii yenye utajiri lukuki, si kwa maendeleo ya wananchi wote ila kwa ajili yao wenyewe, at least kwa kiwango kikubwa.
- Ndio, wapo baadhi ya viongozi wa chama tawala ambao ni waadilifu na wenye kutimiza wajibu wao. Lakini hawa wanaharibiwa na wengi walio wachafuzi. Hali ikiendelea, vita itatokea, whether or not we want the situation. Je, nani ataanza kumvika paka kengele kwenye suala hili la uadilifu na kupiga vita ya UKWELI dhidi ya ufisadi?
- Nisiwe quoted vibaya kwamba watu wote WENYE UWEZO ni mafisadi, ila, wawaachie wananchi ardhi yao, waiendeleze.
- Kimaro, hujatosheka?
./Mwana wa Haki
Ekari 1000 za nini kwa mtu mmoja? Mbaya zaidi karibu kabisa na makazi ya watu wa kawaida. Yapo mapori Nchi hii yanahitaji kuendelezwa waende huko akina Kimaro.Tatizo isiwe ukubwa wa ardhi mtu anayo miliki tatizo iwe kama kapata kihalali au la. Ardhi nayo ni uwekezaji. Kama mtu ana uwezo wa kununua ekari 1000 au zaidi na akaendeleza hiyo ardhi asi nunue? Ardhi ni kama mali yoyote ile na kamwe watu hawawezi kumiliki kiwango sawa. Kama bwana Kimaro haku jipatia hiyo ardhi kihalali basi hilo ni swala jingine ila kama kaipata kihalali basi hana kosa.
Ekari 1000 za nini kwa mtu mmoja? Mbaya zaidi karibu kabisa na makazi ya watu wa kawaida. Yapo mapori Nchi hii yanahitaji kuendelezwa waende huko akina Kimaro.
Balali alisha bainika ni mwizi na rais alikwisha mfukuza kazi lakini kwa kimaro ni njama tu za mafisadi wamewachochea wananchi (wahuni).
lol nitafute nini? wananchi kujichukulia sheria mikononi dhidi ya balalli? kuna thread nyingi za balalli.....
Endeleeni kumiliki pesa kiasi mnachotaka hata kama ni kwa njia ya UFISADI, WIZI, UBADHIRIFU.... lakini sio ARDHI. Ardhi ni bidhaa ya aina yake. Tangu mwaka 1967, Watanzania tunajua ardhi ni mali yetu sote. Tugawane hii ardhi yetu kwa utaratibu unaokubalika, unaozingatia maslahi ya WENGI. Sio Kimaro peke yake.Kwa nini mtu asiwe na ekari 1000? Mtu kama una pesa yako kwa nini usi nunue kitu unacho taka? Kwa hiyo una taka kusema iwekwe limit ya kiasi cha ardhi mtu anayo weza kumiliki? una taka kusema iwekwe limit ya kiasi cha mali mtu anacho weza kumiliki? Watu kama wakina Bill Gates wana net worth zaidi ya $50 billion jiulize zote hizo za nini. We are a capitalist economy and everyone is guaranteed by law to own any amount of property as long as it is legal.