Uvamizi wa Eneo Meru na Mahojiano na Aloyce Kimaro (MB)

1.Nani alibaini balali ni mwizi?

2.Aliiba shilingi ngapi?

3.Kwanini hawakumfungulia Kesi?

Vitu vingine muwe mnakaa kimya kama haujui kuhusiana na hilo,kwa taarifa yako Balali ndiyo alikuwa wa kwanza kuachia ngazi na mambo mengine yalikuw ani zuga tu ila Balali alijiuzuru kabla hajafutwa kazi!

Suala la Kimaro siyo njama za Mafisadi.Tutajie ni mafisadi gani hao siyo kubwabwaja tu...


kwa nini rais alimfukuza kazi.....?
 
Endeleeni kumiliki pesa kiasi mnachotaka hata kama ni kwa njia ya UFISADI, WIZI, UBADHIRIFU.... lakini sio ARDHI. Ardhi ni bidhaa ya aina yake. Tangu mwaka 1967, Watanzania tunajua ardhi ni mali yetu sote. Tugawane hii ardhi yetu kwa utaratibu unaokubalika, unaozingatia maslahi ya WENGI. Sio Kimaro peke yake.

Mkuu unajua fika kwene post zote nimesema kuwa kumiliki kiasi chochote cha mali ina ruhusiwa ili mradi iwe kwa njia halali sasa hapo pekundu sijui pame kujaje. Kubali to hoja yangu ni sawa kuwa si kinyume cha Mtanzania kumiliki kiasi chochote cha mali ili mradi iwe halali. Kwani Kimaro kamiliki ardhi nzima ya Tanzania mkuu? kama una ushahidi kaipata kifisadi sawa ila kama kaipata kihalali ni haki yake. Hata wewe kwa kulinganana uwezo wako waweza nunua kiasi chochote cha ardhi unacho kitaka. Hii ya kukimbilia kusema kila mwenye mali ni fisadi haina hoja. Labda utuambie wewe Watanzania wata milikije kiasi sawa cha ardhi tushauri serikali ifanye hivyo. Point ina rudi pale pale kwamba we are a capitalist economy labda useme turudi kwenye ujamaa.
 
Nimeshasikiliza nakula sebene hapa la mwisho wa clip!

dah!
maisha bwana!dah
 
Ekari 1000 za nini kwa mtu mmoja? Mbaya zaidi karibu kabisa na makazi ya watu wa kawaida. Yapo mapori Nchi hii yanahitaji kuendelezwa waende huko akina Kimaro.

Wildcard,
Hii ni changamoto kwa matajiri/wenye nacho wa nchi yetu. Pamoja na kwamba siafikiani na kitendo cha wananchi kuvamia shamba la Mhe. Kimaro bado tunapaswa kuwaangalia na kuwadadisi wenzetu 'waliobarikiwa'. Je ni kwa kiwango gani katika kujitwalia ardhi na kupata mali waliyonayo kutoka nchini mwetu wameweza kuwafikiria wananchi wenzao na kuwasaidia ipasavyo?

Kijijini kwetu enzi hizo alikuwepo Mgiriki mmoja aliyekuwa na shamba kubwaaaaaa la mkonge. Mgiriki huyo alizungukwa na wananchi wa kawaida na wale waliokuwa wafanyakazi kwenye shamba lake. Tulipopata Uhuru, wapo Wagiriki ambao hawakupenda kutawaliwa na ngozi nyeusi na ambao hawakukubaliana na siasa ya Ujamaa waliondoka kurudi makwao. Mashamba yao yalichukuliwa na Serikali. Mgiriki ninayemzungumzia hakuondoka alibaki nchini na akafia hapahapa nchini. Kwa kipindi chote alichokuwa akimiliki shamba lile alitoa ruksa kwa wananchi kulima mazao yao katikati ya mistari ya mkonge. Hatimaye hata Mameneja wa mashamba ambayo yalitaifishwa na Serikali walifuata nyayo za Mgiriki na kuwaruhusu wananchi wanaozunguka mashamba hayo kulima ndani yake. Huyo alikuwa Mgiriki mwenye utu aliyejali majirani na wafanyakazi wake!

Na sisi tunaojiita Wazalendo lakini matajiri tuliohodhi mamia ya ekari wakati wananchi wenzetu hawana hata kipande cha ardhi, hilo la kuamua kuwasaidia wenzetu kwa kuwagawia eneo la kulima bila masharti tunaliweza?

Pamoja na hayo yote, Tanzania yetu ni kubwa, ina ardhi kubwa ya kutosha. Nakumbuka enzi hizo, watu wa Kilimanjaro waliwahi kudai mbele ya Mwalimu Nyerere kwamba baadhi yao hawana ardhi. Mwalimu akawaambia Tanzania ni kubwa mno akawashauri wahame waende mikoa mingine yenye ardhi ya kutosha. Leo hii kila kona ya nchi huwezi kumkosa Mchagga aliyeridhika kuishi mkoa mwingine na kuendesha maisha yake kwa mafanikio badala ya kushawishika kwenda kumvamia Mhe. Kimaro!
 
Nionavyo mimi wananchi wamechoka na wamechoshwa na tabia za viongozi wetu, jamani hivi vilio vya mafisadi kila siku tunavisikia si mitaani si JF lakini hakuna hatua hakuna sheria, na wananchi wamechoshwa na wamekosa imani na viongozi hivyo kila mmoja anaonekana fisadi na ndio hapo sheria mkononi msije tu sikia siku kiongfozi kachomwa moto..tulisikia mkapa kuzomewa, kikwete kupigwa mawe, balali kuvamiwa leo hii kimaro bado mengi yatakuja, serikali na viongozi wetu wabadilike, hakuna kiongozi asiyejilimbikizia mali wakati mwananchi anaishi kwa chini ya dola moja na hana hata nusu eka wakati tunadanganywa eti ardhi ni mali ya serikali!!! unakuta mheshimiwa ana ekari 1000 amezungusha senyenge au ukuta hakuna maedeleo yoyote hata umeme unashindwa kuwafikia wananchi waliopo maeneo ya mbele yake kwa kuangalia gharama za nguzo amabzo zitapita kwenye hilo eneo na kama tujuavyo nguzo wananchi mnanunua au kuchangia ili muwekewe umeme, kwani watu wasivamie kupunguza!!! na je

tujiulize kwanini wananchi hao waende hapo tu hakuna wawekezaji wengine hapo, kipo kilichowasibu wanatakiwe wasikilizwe sio kuchukuliwa hatua, na pia kama serikali inajua kuchukua hatua ianze na mafisadi wanaofanya wananchi kukosa amani na kuikiria vitendo vya namna hiyo,

Lakini wananchi hao hao wanaendelea kupigia kura mafisadi. Tuna lalamika sana wakati njia pekee ni kuwaondoa kwa kutumia kura. hata kama wanaiba they can only steal up to a certain extent. Hauwezi kuendelea kulalamikia viongozi wakati wa uchaguzi ukifika una wapigia kura tena au hauendi kupiga kura ya kuwa pinga. Njia tunayo ambayo ni kura lakini hatuitumii tuna zidi kulalamika. Angalia chaguzi ndogo tu iliyo pita hapa juzi juzi, watu wameambiwa kuhusu ufisadi na madhambi yote ya uongozi lakini wame kichagua chama kile kile wanacho kilalamikia.
 
Lakini wananchi hao hao wanaendelea kupigia kura mafisadi. Tuna lalamika sana wakati njia pekee ni kuwaondoa kwa kutumia kura. hata kama wanaiba they can only steal up to a certain extent. Hauwezi kuendelea kulalamikia viongozi wakati wa uchaguzi ukifika una wapigia kura tena au hauendi kupiga kura ya kuwa pinga. Njia tunayo ambayo ni kura lakini hatuitumii tuna zidi kulalamika. Angalia chaguzi ndogo tu iliyo pita hapa juzi juzi, watu wameambiwa kuhusu ufisadi na madhambi yote ya uongozi lakini wame kichagua chama kile kile wanacho kilalamikia.

nimekupata MF1 lakini suala la kura ni suala gumu kulisemea lina utata mwingi binafsi siamini kama viongozi wote wanapigiwa kura na wananchi, tunajua jinsi uchaguzi unavyoendeshwa katika nchi yetu,bado siamini kama kura inaweza kumkomboa mtanzania kwajinsi chaguzi unavyoendeshwa

ndio maana kwa mtizamo wangu nasema wananchi wamechoka, hawana nafasi, inabaki bora liwe tu
 
Mkuu unajua fika kwene post zote nimesema kuwa kumiliki kiasi chochote cha mali ina ruhusiwa ili mradi iwe kwa njia halali sasa hapo pekundu sijui pame kujaje. Kubali to hoja yangu ni sawa kuwa si kinyume cha Mtanzania kumiliki kiasi chochote cha mali ili mradi iwe halali. Kwani Kimaro kamiliki ardhi nzima ya Tanzania mkuu? kama una ushahidi kaipata kifisadi sawa ila kama kaipata kihalali ni haki yake. Hata wewe kwa kulinganana uwezo wako waweza nunua kiasi chochote cha ardhi unacho kitaka. Hii ya kukimbilia kusema kila mwenye mali ni fisadi haina hoja. Labda utuambie wewe Watanzania wata milikije kiasi sawa cha ardhi tushauri serikali ifanye hivyo. Point ina rudi pale pale kwamba we are a capitalist economy labda useme turudi kwenye ujamaa.
Mkuu,
Kwenye suala la ARDHI nawaomba sana Watanzania wenzangu, Bunge letu, Mahakama yetu, Vyombo vya habari na Serikali yetu tubaki WAJAMAA. Hili ni moja kati ya mambo mema kabisa alilotuachia MWALIMU.
 
eti 'MIMI NI NDUGU YENU,RAFIKI YENU,na kwa wengine naendelea kuwa ADUI YENU MPAKA MSALIMU AMRI'

mwanakijiji UNA VIJEMBE WEWE!kama mwanamuziki wa taarabu
 
Ningefurahi sana kama hasira hizi za hawa wananchi zingekuwa zinaonyeshwa katika chaguzi mbalimbali ili tuwe tunawapata viongozi walio waadilifu.
 
Ningefurahi sana kama hasira hizi za hawa wananchi zingekuwa zinaonyeshwa katika chaguzi mbalimbali ili tuwe tunawapata viongozi walio waadilifu.
Watachaguliwa akina Kimaro tu wenye nazo sio pesa tu bali pia na ekari kadhaa za ardhi. Ukiwa mwadilifu hauwezi kugombea nchi hii labda uwe CUF na ugombee majimbo ya PEMBA.
 
Hili shamba nalifahamu sana. Mhe. Kimaro ameuziwa ekari 50 tu kwa ajili ya Hoteli yake ya kitalii. Sehemu kubwa iliyofyekwa na hawa wavamizi ni ile iliyokuwa na migomba ya Utafiti unaoendelezwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Kanda ya Kaskazini ilioko Selian. Hii ni kama Serikali imevamiwa.
Hawa watu wanafahamu kuwa kuna eneo la ekari 25 lililotengwa kwa ajili ya kujenga shule ya Sekondari. Kwa hiyo si kweli kwamba Kata ya Singisi wamekosa mahala pa kujenga shule. Inaonekana hii ni chuki wa "wageni weusi", au ni vijana wanaodhani kila mtu mwenye fedha ni fisadi. Mhe. Kimaro anajulikana anapiga vita ufisadi Tanzania.

Jambo ambalo lingewekwa wazi na Serikali ni bei iliyolipwa na Mhe. Kimaro. Huenda "ufisadi" ukajificha katika uuzaji wa eneo hilo. Wakati Wameru wanashauriwa wahamie Wilaya ya Kilindi, Mkoani Tanga ambako wanahofia kuna malaria, huenda wakubwa kama Mhe. Kimaro wanauziwa ardhi ya hapa Meru kwa bei poa.
 
Jamani Shamba la Shukuru Kawambwa lilivamiwa wiki 2 zilizopita na yakafanyika mauaji. Ilipowekwa thread hapa "wanaharakati" wakalalamika kuwa kila si kila jambo lazima lijadiliwe hapa JF.

Hii ndio JF....
 
Its obvious and its high time tusome ALAMA ZA NYAKATI - wananchi kujichukulia sheria mkononi sio mara ya kwanza - hata MAFISADI walioiba mamilioni ya fedha wakati wananchi wanataabika itafika siku WATAPIGWA MAWE WAKIPITI NJIANI kwani TAIFA LETU LINA SHERIA ISIYOFANYA KAZI KWA WOTE - BALI WANYONGE TU - HAIWEZEKANI WANANCHI WANAOFIKIA 80 WANUNULIWE WOTE ETI WAKAHARIBU MALI YA MTU - HIYO INGEFANYWA NA FEW PEOPLE (WAHUNI) -
WATANZANIA WENGI WAMECHOKA - WATANZANIA SIO WAJINGA - NA KWA VILE HAWANA PA KUSEMEA (NANI ASIKILIZE WANYONGE) WANAAMUA KUFANYA LOLOTE KUTOKANA NA UCHUNGU, HASIRA NA SHIDA WALIZO NAZO - habari inasema KWANINI KUSIJENGWE SHULE, ZAHANATI ETC. MAHALI PALE KARIBU NA MAKAZI YAO VIKAWASAIDIA? HIYO NI HOJA YENYE NGUVU SANA - HILO SHAMBA LA EKARI 1,000 LINAWASAIDIA NINI?? YEYE NI MBUNGE WA HIYO SEHEMU AU KAJA TU NA KUAMUA KULIMA KATIKA YAO?
JAMANI MAMBO YANAYOFANYIKA TZ NI MAGUMU MNO - MFANO - TEMBELEA MAENEO MENGINE HAPA DAR - KIONGOZI (MSTAAFU MMOJA) ANAPEWA ALLOCATION YA 10 PLOTS - HALAFU ANAWEKA FENCE NA ZINAKAA YEARS HAJENGI - WAKATI WANANCHI WENGINE WANATAFUTA PLOT MOJA HAWAPEWI - HAKI IKO WAPI?? KILICHOTOKEA NI ALAMA ZA NYAKATI - TRANSPORT SYSTEM IS VERY POOR - WATU WANABANANA KWENYE PUBLIC TRANSPORT, WANAKAA VITUO MASAA - WANAFUNZI WANATESEKA (DAY SCHOLARS) KWA HAPA JIJINI - JAMANI IKO SIKU MAWE YATARUSHWA KWA MAGARI YOTE YANAYOPITA - OUR LEADERS SHOULD UNDERSTAND THAT THEY ARE LEADING HUMAN BEINGS AND NOT ANIMALS and A PROVOKED HUMAN BEING CAN TURN INTO AN ANIMAL - MUNGU ASHUSHE ROHO YA UVUMILIVU HADI VIONGOZI WATAKAPOAMUKA KWENYE NDOTO ZAO ZA KUJILIMBIKIZIA MALI NA KUSAHAU WANYONGE - WATAKAPOKUMBUKA KUWA - WATAVIACHA VYOTE HAPA HAPA DUNIANI
 
Lakini wananchi hao hao wanaendelea kupigia kura mafisadi. Tuna lalamika sana wakati njia pekee ni kuwaondoa kwa kutumia kura. hata kama wanaiba they can only steal up to a certain extent. Hauwezi kuendelea kulalamikia viongozi wakati wa uchaguzi ukifika una wapigia kura tena au hauendi kupiga kura ya kuwa pinga. Njia tunayo ambayo ni kura lakini hatuitumii tuna zidi kulalamika. Angalia chaguzi ndogo tu iliyo pita hapa juzi juzi, watu wameambiwa kuhusu ufisadi na madhambi yote ya uongozi lakini wame kichagua chama kile kile wanacho kilalamikia.

MwanaFalasafa,

Unazungumza kana kwamba wapigakura wameishabaini kuwa CCM imejaa wanachama mafisadi kwa hiyo hakuna mwana-CCM ambaye anastahili kupewa kura.

Sisi kijijini kwetu hakuna Chama kingine chochote wananchi wanachokijua zaidi ya CCM. Hata mtaani kwetu hapa jijini na mtaa wa pili na wa tatu tuna Wajumbe wa nyumba kumi wa CCM na wanatuhamasisha tukajiandikishe ama tuhakiki kadi zetu maana chaguzi zinakaribia. Huko kijijini, ukimuuliza mwanakijiji Mbowe ni nani hamjui, Slaa ni nani hajui, Zito ni nani hajui, Cheyo ni nani hajui, Lipumba ni nani hajui, Rostam ni nani hajui, Mengi ni nani hajui, Balali ni nani hajamsikia; Liyumba ni nani hajui, magorofa pacha ya BOT hajayasikia! Ukimuuliza Kikwete unamjua, atakwambia anamjua kuwa ndiye Rais wa Tanzania na ndiye alimpigia kura mwaka uleee wa neema ya kanga, tshirts, sukari etc CCM tulipofanya kampeni 'kabambe' hadi vijijini.

Viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani naomba mniwie radhi. Mnaudhi sana! Unapofika wakati wa uchaguzi ndio mnakurupuka kwenda kwenye majimbo kutaka mchaguliwe. Mkisimama kwenye majukwaa mnawatukana na kuwakejeli wananchi kwa kuwaambia ni wajinga kwa nini wanakipigia kura Chama cha Mapinduzi kilichojaa mafisadi! Mnaenda Mwembe Yanga mmetaja mafisadi 10 tu!

Chama cha Mapinduzi nasi tukienda kwa wananchi tunatoa uongo mwingi ili mradi tu tuchaguliwe na kuwafanya wananchi na wana-CCM wenzetu wa ngazi za chini wapumbavu fulani.

MwanaFalasafa, Elimu ya Uraia ni jambo muhimu sana iwapo kweli tuna nia ya kuleta mabadiliko ya kweli na yenye manufaa nchini mwetu. Vinginevyo tutaendelea na nyimbo zetu za kuwahamasisha wananchi tuchukiane wenyewe kwa wenyewe ama tuvichukie vyama ambavyo vina wanachama wengi safi ukilinganisha na waovu wachache.

Wapinzani wa CCM, hakitaeleweka chochote kwenye sanduku la kura mpaka mjipange vizuri, muwe na malengo ya pamoja yanayoeleweka na si kila mtu na agenda yake, mjitoe muhanga, mshirikiane, msibaguane, la sivyo Chama cha Mapinduzi kitaendelea Kudumu! Jifunzeni kutoka kwa Waasisi wa chama cha TANU, hawakuwa na elimu wala uwezo kifedha lakini kwa moyo wa kizalendo, walijituma na kujitoa muhanga wakaweza kuwafikia wananchi vijijini, na lengo lao lilikuwa linaeleweka. Sisi wazee tusio na meno hivi sasa, tunakumbuka kwamba tuliijua TANU tukiwa vijijini hata kabla nchi haijapata Uhuru na kwamba chama hicho kilikuwa ni chama cha kupigania Uhuru, sera kuu ilikuwa kuwaunganisha wananchi wote kuwa kitu kimoja ili mafanikio yaweze kupatikana.
 
Kwa mtu yeyote mwenye akili Timamu akisikiliza mazungumzo ya Mwanakijiji na Mh.Kimaro ataona kuwa Vurugu hiyo imepangwa ili kumkomoa Mh.Kimaro....Hapa kuna Tatizo na hii tabia ya watu kujichukulia sheria mikononi inabidi ikomeshwe mara moja.

Naweza kusema wazi kuwa ile ajali iliyotokea wiki mbili zilizopita naihusisha na tukio hili la kutaka kumpokonya eneo Muwekezaji Mbunge Kimaro.Ni haki ya kimsingi ya Mbunge Kimaro kumiliki eneo hilo kama alifuata taratibu za ununuzi wa Eneo hilo.

Polisi wataingilia kati kwenye Uchunguzi wa Tukio hilo na ni wazi wale wote waliohusika watafikishwa kwenye vyombo vya sheria na Mheshimiwa Mbunge atafidiwa gharama za uharibifu wa Eneo hilo.

"Utawala wa sheria unalegalega ndio maana watu wanajichukulia maamuzi wenyewe kwa kila Jambo"!


Sawa kabisa mkuuu Mwawado.
 
Hivi Tanzania kuna shida ya ardhi?

Sidhani. wenye nchi wanasema ardhi ipo ya kutosha ndo maana hata wawekezaji wa nje wamepewa maeneo makubwa tu maelfu kwa maelfu ili walime mazao ya biashara......

Huenda ni katika kudivert attention, na hivi bunge la bajeti linakuja...kwa maana ya ajali ya Mwakyembe, Kimaro, kuvamiwa shamba nk
 
Issue ni kuwa CCM ina ujanja mwingi mno - hata usipowapigia kura - watashinda tu - mie ndio naona JESHI lichukue nje for a while - tuwe na kipindi cha mpito - halafu kuwe na Raisi -sio lazima atoke kwenye vyama vya siasa - vyama viwepo ila tuwe na independent president - Sera za CHADEMA ni nzuri e.g. za majimbo (budget iende kwenye jimbo) at least hata Mbunge akirepresent wananchi - serikali ya jimbo inaona shida zilizopo pale etc. System ya Kodi ni mbaya mno - kila sehemu KODI KODI KODI - hela zinaenda wapi jamani???? mitaani hamna kinachofanyika etc. - VYAMA VYA UPINZANIA VITANGAZE SERA ZAO WAZIWAZI - KWENYE KAMPENI INAKUWA KAMA USHINDANI WA NANI ANAJUA KUSEMA ZAIDI YA MWENZAKE - WAZIANDIKE, WAZIHUBIRI SERA ZAO NA WATUELEZE WATAFANYA VIPI HAKI ITENDEKE KWANI TAIFA LETU SIO MASKINI - WATAWAFUKUZAJE WAWEKEZAJI WANAONYONYA NCHI YETU - E.G BARRIK GOLD - WANA MIKATABA TAYARI YA SO MANY YEARS - WATAWEZAJE KUVUNJA HIYO MIKATABA FEKI? NDIO MAANA NAONA JESHI NDIO PROPER - WALE HAWANA CHA MIKATABA OR WHAT - NI SHERIA TU
 

Sijakuelewa vizuri, samahani.
Hakuna mahali Bibi Ntilie amezungumzia mashamba ya Balalli. Kama yalivamiwa ni utovu wa nidhamu kwa sheria za nchi kwa kujichukulia sheria mkononi hata kama Balalli aliidhinisha fedha za EPA zichukuliwe! Kila mtu ahukumiwe kwa dhambi yake ya kuvunja sheria za nchi. Kama kuna waliovamia shamba la Mhe. Kimaro alilollipata kwa sheria zilizotungwa na Bunge letu wenyewe anayo haki ya kutetewa. Pia kama **** mkono wa mtu kuwashawishi watu wakavamie makusudi napo tunataka jambo hilo lifuatiliwe kikamilifu! Mwisho 'matajiri' wa nchi hii wanawajibuka kuangalia na kuwasaidia wananchi wenzao wasio na uwezo kama wao. Maana utajiri huo wameupata kupitia kwa wananchi.
Tuko pamoja Mtanzania!
 
Last edited:
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom