Uvamizi wa Eneo Meru na Mahojiano na Aloyce Kimaro (MB)

that is the wrong approach. The right approach ni kuwa wale wanakijiji ni wahalifu wachukuliwe hatua. Vitendo vyao haviwezi kuhalalishwa na bei ya Kimaro kununua shamba au mwaka gani alinunua shamba hilo. Uhuni walioufanya hauwezi kuhalalishwa kwa kujua kama shamba alilinunua kwa nani.

Lakini zaidi kama kungekuwa na issue ya umiliki wake swali lingekuwa ni hawa wanakijiji wamechukua hatua gani za kisheria kuzuia umiliki huo wa Kimaro? Nadhani hicho ndicho cha kuulizwa. Ni wana kijiji wana burden of proof ya kuonesha kuwa Kimaro kalipata shamba kwa njia kinyume na sheria.

Mwanakijiji,

Ni kweli wanakijiji wamevunja sheria kwa kuvamia hilo shamba lakini pia ni muhimu kujua kwanini tumefika mpaka hapo? Kimaro kalipataje hilo shamba?

Kuna wanasiasa wengi ambao wamedhuluma mali za umma na sasa wanajifanya ni mali zao akiwemo Mzindakaya na wengine wengi. Sina uhakika na suala la Kimaro ila sitashangaa kama na yeye atakuwa kwenye mkondo huo.

Kama unapigana kwenye hivi vita ni wazi kuna watu watakuandama pia na kama wewe mwenyewe sio whiter than white hapo unawapa nafasi ya hao wabaya wako kufanya revenge na hilo kwenye siasa ni kitu cha kutegemea. Utakuwa very naive ukitegemea kwamba watakaa kimya.

Ingefaa kujua Kimaro kalipataje hilo shamba?
 
Maoni ya Mhariri wa Mwananchi

MWISHONI mwa wiki iliyopita wakazi wa kijiji cha Sing’isi, kilichoko Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha walifanya tukio la kusikitisha, pale walipovamia Shamba la Madira linalomilikuwa na Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro (CCM) kisha kufyeka mazao, miti, kubomoa nyumba 15 na kuziteketeza kwa moto.
Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na gazeti hili jana, wananchi hao waliojichukulia sheria mikononi, wanadaiwa kufanya kitendo hicho kupinga mbunge huyo kuuziwa shamba hilo lililokuwa linamilikiwa na mwekezaji wa kizungu badala ya kuliacha mikono mwao.



Wananchi hao wanadai kwamba, kwa kuwa shamba hilo liko katika eneo lao wangepewa ili walitumie kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kujenga shule, hivyo kitendo cha serikali kuliuza kwa mtu wa nje ya kijiji hicho ni kunyanganya haki yao.



Tumesikitishwa sana na kitendo cha wananchi hao, kuharibu mali ya mtu kinyume cha sheria za nchi. Inawezekana madai yao ni ya msingi; lakini kwa nini wasifuate taratibu za kisheria kulipata badala ya kumtia hasara mbunge huyo ambaye hahusiki na madai yao?




Kimaro hakuvamia eneo hilo, bali aliuziwa kihalali na kwa kufuata sheria. Sasa kwanini aingizwe kwenye mgogoro huo badala ya wananchi hao kuilalamikia serikali? Kama waliona wanapuuzwa, kwa nini hawakuchukua hatua za kisheria kwa kwenda mahakani kuweka pongamizi?



Tunashangaa zaidi kwa wananchi hao kufikia hatua ya kuteketeza mazao, wakati kama huu ambao taifa linakabiliwa na ukame pamoja na upungufu wa chakula katika maeneo mengi hapa nchini. Viongozi wa taifa akiwemo rais wanapata shida ya kutafita chakula ikiwemo kwenda kuomba misaada nje ya nje; lakini wenzetu wa Sing’isi wanateketeza mazao yaliyo shambani! Hiyo inashangaza na haingii akilini, kama kweli kitendo hicho kufanywa na watu wanaolithamini na kulipenda taifa lao.



Hata kama mazoa yaliyoteketezwa yasingewanufaisha moja kwa moja, tunaamini kuwa yangewasaidia wakati wa shida kwa kununu kutoka kwa mmiliki wake. Si hivyo tu, pia shamba hilo lingetoa ajira kwa wakazi wa eneo hilo na kuchangia shughuli nyingine za maendeleo ikiwemo hifadhi ya mazingira kutokana na miti aliyokuwa ameipanda ili kulirudisha eneo hilo katika hali yake ya asili.



Lakini pia inashangaza kwamba: Hivi utawala wa mkoa na wilaya ulikuwa wapi mpaka wananchi wanafanya uharibifu huo kwa karibu siku mbili bila kuzuiwa? Je, mkuu wa wila na mkoa hawakuwa na taarifa juu kuwepo kwa tukio hilo? Kama ndivyo, vyombo vya usalama vinavyowasaidia kupata taarifa vilikuwa wapi au havina watendaji wanaowajibika?




Kuna taarifa kwamba, polisi walienda katika eneo hilokwa kuchelewa na walipofika walikuwa wananchi wanaendelea kubomoa, askari walipowakataza hawakusikia na hata walipotumia mambomu ya kutoa machozi na kupiga hewani risasi za moto, waliendelea kukaidi! Kama hali imefikia hapo ni dhahiri kwamba, taifa letu linaelekea kubaya.



Hata hivyo, kuna madai kuwa uongozi wa kijiji ulitoa taarifa mapema kwa mamlaka za juu kutahadharisha juu ya hali hiyo, baada ya kusikia tetesi la kuwepo kwa tukio hilo, lakini hakuna kilichofanyika mpaka siku ya uharibifu ilipofika. Kama ni kweli, ni kwa nini jeshi la polisi na uongozi wa wilaya ulipuuzia taarifa hizo? Je, walitaka waone kilichotokea ndipo waamini.



Tunatahadharisha kwamba, tunakoelekea ni kubaya hasa ikizingatiwa kuwa tunakaribia uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani. Hali hii inaweza kuingiza siasa za chuki za uchaguzi na kulifanya taifa kuwa katika wakati mgumu badala ya uchaguzi kufanyika kwa amani na utulivu.



Tunaomba serikali ichukue hatua zinazostahili kwa kuwasaka wahusika wote na kufishisha katika vinavyo husika, paja na kudhibiti vitendo kama hivyo kutokea. Tunahofu kwamba, leo ni Arusha, kesho itakuwa mahali pengine na hatimaye kuena nchi zima; hivyo usalama wa taifa letu kwa hatarini.
 
tafsiri ya yote haya ni nini?
wananchi si wajinga kufanya hv,
 
Wana JF kuna tetesi kuwa El anahusika na vurugu zilizotokea kwenye shamba pinga mafisadi Kimaro.Inasemekana EL ana kituo kikubwa cha TV karibu na sehemu hiyo na hakikuguswa.Mwenye dataz Arusha tafadhali
 
Utitiri na ukubwa wa mashamba haya wanayonunua viongozi wetu tena kwenye maeneo jirani na watu wetu masikini kabisa ndio inayonisikitisha mimi. Bado tuna mapori makubwa tu nchi hii yanayohitaji kuendelezwa. Viongozi wetu hawayaoni hayo. Wananunua ambayo tayari yameendelezwa pamoja na ukweli kuwa wanao uwezo mkubwa tu wa kufungua mashamba mapya kuliko hao wananchi. Tupunguze UROHO na UBINAFSI wa Viongozi wetu vinginevyo milipuko ya aina hii baadaye itageuka kuwa vita kamili. Kimaro hawezi kuililia KIWIRA ambayo haina hata eka 20 wakati yeye anamiliki maekari mengi kiasi hiki.
 
mzee-mwanakijiji-albums-news-worthy-picture482-kimaro.jpg


Kwa usiku kucha kundi la wahuni waliojibatiza jina la "wanakijiji" na kutuchafua wengine walivamia eneo la Mhe. Aloyce Kimaro (Vunjo-CCM) na kuharibu mazao na kuchoma nyumba na kuiba mali mbalimbali, walifanya hivyo kwa kile ambacho gazeti la Mwananchi limeelezea kuwa "wanadai kwamba, kwa kuwa shamba hilo liko katika eneo lao wangepewa ili walitumie kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kujenga shule, hivyo kitendo cha serikali kuliuza kwa mtu wa nje ya kijiji hicho ni kunyanganya haki yao."

Kitendo hiki ni cha aibu na kina fanana na vitendo vya uvamizi kule Zimbabwe au vile vilivyosababisha machafuko makubwa Kenya vya Mungiki. Ni vya kulaaniwa na kila mpenda haki na mwenye kuheshimu utawala wa Sheria.

Ni kwa sababu hiyo tumepata nafasi ya kuzungumza na Bw. Kimaro jana kuhusu suala hili na kujaribu kutafuta maoni yake na kama kitendo hiki kitamfanya ahamishe uwekezaji huo wa Arumeru na kuupeleka sehemu nyingine kwani hawamtaki huko Arumeru!



Bonyeza Hapa Kusikiliza
 
Ina sikitisha kuwa hali ya ufisadi ime fanya kila kiongozi mwenye mali aonekana mwizi nawakati si kweli. Ni bora mheshimiwa ana wekeza tena nyumbani. Si kama wale wenzetu ambao wana tuibia, kuwekeza hawa wekezi kwa hiyo hela inaenda bure halafu on top of that hela wana ziweka mwenye account za nje.
 
Kwa kweli hali hii ya kujichukulia sheria mikononi inabidi idhibitiwe kabla maafa hayajawa makubwa. Kama leo wameru wamefanya hivi tukakaa kimya na kesho wakafanya wazigua kule Tanga si tutakuja jikuta watu wanafukuzwa katika mikoa ambayo si yao?
 
Ile ajali ya mhesh kimaro uchunguzi wake umeishia wapi?
wameru wana matatizo kwenye akili zao….nafikiri hii inaleta maswali zaidi nasikia hata jirani yake kuna watu wengine wekezaji lakini wamefuata la kimaro tu….
 
Uharibifu huu wa mali ni kitendo kibaya sana na ukizingatia hali ya njaa inayoikumba Tz kwa sasa then wanakata na kuharibu mazao kwa uchochezi wa baadhi ya watu. Je hao wanakijiji wamechochewa na nani? Au kwakuwa Kimaro ni mojawapo ya wanaopinga UFISADI?
 
Bwana Kimaro umekuwa mstari wa mbele kudai haki za wanyonge, nadhani inabidi uonyeshe utetezi wako kwa vitendo. Sidhani kama wavamizi hao ni kundi la wahuni bali wanatuma ujumbe kuwa ubinafsishaji wa ardhi unapofanyika basi tathmini ya kina lazima ifanyike ili kuona kama jamii inayozunguka ina ardhi ya kutosha. Tukio hili lichukuliwe kama funzo ili mambo yaliyotokea Zimbabwe yasitokee Tanzania. Hivyo ni vyema Kimaro ukatoa sehemu ya estate yako ili hao walala hoi wapate sehemu ya kulima.
 
Mbona wananchi walipojichukulia sheria kwa Ballali hamkulaani? Ndio maana wengine tunaipenda JF, rahisi kweli kweli kuona unafiki mkubwa ulioko hapa.

Kama tunalaani hizi tabia mbaya za wananchi kujichukulia madaraka mikononi mwao basi tulaani kwa kila mtu; tulaani hata pale hizo tabia zinapotumika kuchoma vibaka.

wananchi sio polisi, sio mahakama, hizi tabia za kuvamia na kuharibu mali za watu hazifai. Tusipoangalia tutaishia kuwa kama Zimbabwe.

Lakini pia wanasiasa nao waelewe kwamba kadri wanavyofanya deals mbalimbali za kuwaibia wananchi kwa kutumia system, kuna siku wananchi watashutuka na kuwafuata.
 
Mbona wananchi walipojichukulia sheria kwa Ballali hamkulaani? Ndio maana wengine tunaipenda JF, rahisi kweli kweli kuona unafiki mkubwa ulioko hapa.

Kama tunalaani hizi tabia mbaya za wananchi kujichukulia madaraka mikononi mwao basi tulaani kwa kila mtu; tulaani hata pale hizo tabia zinapotumika kuchoma vibaka.

wananchi sio polisi, sio mahakama, hizi tabia za kuvamia na kuharibu mali za watu hazifai. Tusipoangalia tutaishia kuwa kama Zimbabwe.

Lakini pia wanasiasa nao waelewe kwamba kadri wanavyofanya deals mbalimbali za kuwaibia wananchi kwa kutumia system, kuna siku wananchi watashutuka na kuwafuata.
tukumbushe ilikuwaje?
 
Yo Yo,

Kwanini JF ina search button? Ni kwa kazi kama hiyo, tafuta mwenyewe!
lol nitafute nini? wananchi kujichukulia sheria mikononi dhidi ya balalli? kuna thread nyingi za balalli.....
 
Bwana Kimaro umekuwa mstari wa mbele kudai haki za wanyonge, nadhani inabidi uonyeshe utetezi wako kwa vitendo. Sidhani kama wavamizi hao ni kundi la wahuni bali wanatuma ujumbe kuwa ubinafsishaji wa ardhi unapofanyika basi tathmini ya kina lazima ifanyike ili kuona kama jamii inayozunguka ina ardhi ya kutosha. Tukio hili lichukuliwe kama funzo ili mambo yaliyotokea Zimbabwe yasitokee Tanzania. Hivyo ni vyema Kimaro ukatoa sehemu ya estate yako ili hao walala hoi wapate sehemu ya kulima.

Hao wananchi wame tumia njia isiyo sahihi. katika kila jamii kuna masikini na tajiri, kamwe hatuwezi kuwa sawa. Mheshimiwa kapewa ardhi ili aiendeleze je hao waliyo fanya hivyo wange weza kuendeleza? Je uwekezaji wa mheshimiwa usinge wafaidisha na wao? Si kila siku serikali ina pigia kelele large scale farming. Ujamaa ulisha tushinda, kamwe watu hawawezi kuwa na mali sawa. Kama mtu kanunua eneo au kapewa kuwekeza ni haki yake na mali yake na halazimishwi kugawana na mtu.
 
Kwa mtu yeyote mwenye akili Timamu akisikiliza mazungumzo ya Mwanakijiji na Mh.Kimaro ataona kuwa Vurugu hiyo imepangwa ili kumkomoa Mh.Kimaro....Hapa kuna Tatizo na hii tabia ya watu kujichukulia sheria mikononi inabidi ikomeshwe mara moja.

Naweza kusema wazi kuwa ile ajali iliyotokea wiki mbili zilizopita naihusisha na tukio hili la kutaka kumpokonya eneo Muwekezaji Mbunge Kimaro.Ni haki ya kimsingi ya Mbunge Kimaro kumiliki eneo hilo kama alifuata taratibu za ununuzi wa Eneo hilo.

Polisi wataingilia kati kwenye Uchunguzi wa Tukio hilo na ni wazi wale wote waliohusika watafikishwa kwenye vyombo vya sheria na Mheshimiwa Mbunge atafidiwa gharama za uharibifu wa Eneo hilo.

"Utawala wa sheria unalegalega ndio maana watu wanajichukulia maamuzi wenyewe kwa kila Jambo"!
 
Back
Top Bottom