Uteuzi wa Wajumbe wa Kamati zote za Bunge (Orodha) - Machi 14, 2013

Huu mpangilio/upangaji wa kamati za bunge sijaupenda kabisa. Kuna baadhi ya kamati zimewekewa wabunge vilaza kabisa.
Kamati kama za madini, hesabu za serikali, serikali za mitaa hazina watu makini.
Mwita Maranya , Nani amekupa huo uwezo wa kutukana wabunge wetu na kwa kufanya hivyo unawatukana pia wananchi waliowachagua. Au kwako kilaza ina maana gani?.

Kila mbunge ana taaluma na ujuzi katika nyanja fulani, mpaka tuna wabunge wanamuziki. Nitakuelewa ukisema kama kuna baadhi ya wabunge wamepangiwa kamati ambayo ni nje ya taaluma na ujuzi wao.
 
Last edited by a moderator:
Umeona eeh...! jamani sijamuona Joshua Nassari, yuko kamati gani, hata mdee sijaona jina lake. Ila kusema ukweli kamati zingine zimejaa vilaza watupu, huoni hata mtu wa kumbana waziri kwa maswali
WAJAMENI,
Nawaombeni msifanye hii kitu ya REPLY WITH QUOTE kwa vile mtawamaliza wale wanaotumia visimu vya mchina kuingia JF.

JUST REPLY ONLY WITHOUT QUOTE AND GO.
 
Mwita Maranya , Nani amekupa huo uwezo wa kutukana wabunge wetu na kwa kufanya hivyo unawatukana pia wananchi waliowachagua. Au kwako kilaza ina maana gani?.

Kila mbunge ana taaluma na ujuzi katika nyanja fulani, mpaka tuna wabunge wanamuziki. Nitakuelewa ukisema kama kuna baadhi ya wabunge wamepangiwa kamati ambayo ni nje ya taaluma na ujuzi wao.

Tatizo lako huwa unajifanya unajua kumbe hujui.......nenda kwenye website ya bunge uone taaluma za wabunge linganisha na kamati zao walizopangiwa , kamati hizi uteuzi wake kamwe hauzingatii taaluma za wabunge husika ndio maana unakuta wahasibu wanapelekwa kamati ya afya, wahandisi wanapelekwa kamati ya ulinzi na usalama, askari wanapelekwa kilimo na mifugo..........chukua muda soma CV zao hutauliza tena vijiswali kama hivi.

Aidha pitia wajumbe wa kamati ya nishati utakuta mtu kama Mwambalaswa ambaye yeye ni makamu mwenyekiti wa bodi ya TANESCO leo anakuwa mjumbe wa kuisimamia TANESCO hapo tunaenda wapi yaani yeye afanya maamuzi kwenye bodi kisha aje aanze kujisimamia na kujikosoa ........
 
Last edited by a moderator:
Umeona eeh...! jamani sijamuona Joshua Nassari, yuko kamati gani, hata mdee sijaona jina lake. Ila kusema ukweli kamati zingine zimejaa vilaza watupu, huoni hata mtu wa kumbana waziri kwa maswali
Mh. Mdee yuko kamati ya Katiba , sheria na utawala
 
  • Thanks
Reactions: ram
Tatizo lako huwa unajifanya unajua kumbe hujui.......nenda kwenye website ya bunge uone taaluma za wabunge linganisha na kamati zao walizopangiwa , kamati hizi uteuzi wake kamwe hauzingatii taaluma za wabunge husika ndio maana unakuta wahasibu wanapelekwa kamati ya afya, wahandisi wanapelekwa kamati ya ulinzi na usalama, askari wanapelekwa kilimo na mifugo..........chukua muda soma CV zao hutauliza tena vijiswali kama hivi.

Aidha pitia wajumbe wa kamati ya nishati utakuta mtu kama Mwambalaswa ambaye yeye ni makamu mwenyekiti wa bodi ya TANESCO leo anakuwa mjumbe wa kuisimamia TANESCO hapo tunaenda wapi yaani yeye afanya maamuzi kwenye bodi kisha aje aanze kujisimamia na kujikosoa ........
Unajibu bila kuelewa hata nilichokiandika. Ulichojibu ndicho hicho nilichojaribu kukueleza lakini siyo kusema wabunge vilaza.
 
Jaman eti Asumpter, Diploma ya Tourism anapewa kamati ya Bajeti na Kamati ya Fedha?? Angekwenda labda maendeleo ya jamii ingemfaa au huduma za jamii.

Kwa ujumla kama kungekuwepo na sheria ya kukataa uteuzi huo basi Kamati zote zingepigwa chin ili Kiroboto aanze upya.
 
Mbona watanzania tunapenda sana kulalamika lalamika tu?.

Mkuu siyo kuanza kulalamika tu bila hata kuzisoma kanuni za bunge na kuzielewa.

Nani kakwambia spika wa bunge anateuwa wenyeviti wa kamati za bunge?. Fanya kwanza homework kabla ya kulalamika.

Spika hachagui wenyeviti wa kamati za bunge bali wao miongoni mwao ndiyo watajichagua kama kanuni inavyoanisha hapa,

(10) Wajumbe wa kila Kamati watawachagua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti kutoka miongoni mwao ambao kwa muda wote watakaokuwa Wabunge, wataendelea kushika nafasi hizo mpaka mwisho wa kipindi kilichotajwa katika fasili ya (7) ya Kanuni hii, lakini wanaweza kuchaguliwa tena.

Kanuni za bunge sio msahafu, wanaweza kubadilisha. Na hili limeshanyika maana kanuni za sasa zilifanyiwa marekebisho mwaka 2007.

Pili, huwezi kuendelea na mfumo mbovu kwa kisingizio cha kanuni! Tena kanuni ambazo zinarekebishika! Huko ni kufilisika maarifa. Mzee Sitta aliposhika usukani aliangalia kanuni zilizokuwepo na aligundua mapungufu yake, ndipo ak-initiate mabadiliko, and eventually kanuni zilirekebishwa. Makinda hajaonesha creativity yoyote tangu ashike usukani zaidi ya kupokea 'vimemo'.

Tatu, kuhusu wenyeviti wa kamati, Yes, wanachaguliwa na wajumbe, lakini kama una historia ya wajumbe kuchagua mtu ambaye hana ujuzi (taaluma) na sekta husika- yaani kamati atakayoongoza - basi ungeweza kuweka muongozo, kikanuni. Mfano, Kama kamati inayohusika na uchumi basi mwenyekiti na katibu wake lazima wawe ni backaground ya uchumi, hivyo hivyo kwa sheria, au huduma za afya, madini n.k. Kwa maana hiyo wajumbe wangechagua mtu/watu ambao wana backaground na sekta husika. Hii ingesadia sana kupata watu compentent na hasa wenye kujua ni kitu gani wanaangalia kwenye utendaji wa serikali.

Na mwisho, bado kuna kasoro kubwa ya kuwa na wajumbe utitiri kwa kamati moja. Spika (nasisitiza Spika) angekuwa na si mtu wa kufanya kazi kwa kurariri, angeshaliona hili.

Tuna uzoefu wa muda mrefu sana wa baadhi ya wabunge kutojua ni kitu gani wanaangalia kwenye sekta wanazosimamia, na hii inafifisha kabisa dhana nzima ya bunge kuisimamia serikali kwa niaba ya wananchi.

Halafu kuna mtu anaweza kueleza Kamati ya Ukimwi inafanya nini? Unakuwa na kamati ya wajumbe 22 wanashughulika na masuala ya UKIMWI - what exactly do they do? Na hapo ukumbuke, Malaria inauwa watu wengi zaidi ya UKIMWI, lakini pia kasi ya magonjwa ya moyo na kisukari inakuwa zaidi ya UKIMWI! Sasa ilikuwaje wakachomoka na UKIMWI?

Lakini pia, kwenye nchi ambayo asilimia kubwa ya population ni vijana, na vijana hao wengi wao hawana ajira, kwanini bunge lisiwe na kamati inayosimamia employment? Hapa namaanisha wachome employment kama walivyofanya kwenye UKIMWI. Madhara ya kukariri.
 
Huyu spika yupo bias kwenye kupanga hizi kamati iweje Waziri kivuli anaehusika na NISHATI NA MADINI(JOHN MNYIKA)asiwekwe kwenye Kamati ambayo inamuhusu na anayoifanyia kazi!!Kiukweli MNYIKA anamnyima usingizi huyu Mama ndomana anakuwa na kinyongo nae.

Madam SUPIKA anafikiri kuwa kamkomoa John Mnyika kumuondoa kwenye Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kumbe ndiyo anazidi kumpa mwanya wa kufumua madudu zaidi kwenye Wizara ya Ardhi, Maliasili na Utalii. Ngoma inapigwa kotekote (Simultaneously): Nishati na Madini kama Waziri Kivuli halafu Ardhi, Maliasili, na Mazingira kama mjumbe wa kamati. Yule mzee wa Tembo Kinana ajiandae kuvuliwa nguo uchi zaidi....SENKYU SUPIKA
 
Inakuwaje wakati Wabunge wengine hawakuchaguliwa kabisa kuunda hizi kamati ilihali kuna baadhi ya Wabunge wamechaguliwa kuingia kwenye kamati zaidi ya moja??
 
Kanuni za bunge sio msahafu, wanaweza kubadilisha. Na hili limeshanyika maana kanuni za sasa zilifanyiwa marekebisho mwaka 2007.

Pili, huwezi kuendelea na mfumo mbovu kwa kisingizio cha kanuni! Tena kanuni ambazo zinarekebishika! Huko ni kufilisika maarifa. Mzee Sitta aliposhika usukani aliangalia kanuni zilizokuwepo na aligundua mapungufu yake, ndipo ak-initiate mabadiliko, and eventually kanuni zilirekebishwa. Makinda hajaonesha creativity yoyote tangu ashike usukani zaidi ya kupokea 'vimemo'.

Tatu, kuhusu wenyeviti wa kamati, Yes, wanachaguliwa na wajumbe, lakini kama una historia ya wajumbe kuchagua mtu ambaye hana ujuzi (taaluma) na sekta husika- yaani kamati atakayoongoza - basi ungeweza kuweka muongozo, kikanuni. Mfano, Kama kamati inayohusika na uchumi basi mwenyekiti na katibu wake lazima wawe ni backaground ya uchumi, hivyo hivyo kwa sheria, au huduma za afya, madini n.k. Kwa maana hiyo wajumbe wangechagua mtu/watu ambao wana backaground na sekta husika. Hii ingesadia sana kupata watu compentent na hasa wenye kujua ni kitu gani wanaangalia kwenye utendaji wa serikali.

Na mwisho, bado kuna kasoro kubwa ya kuwa na wajumbe utitiri kwa kamati moja. Spika (nasisitiza Spika) angekuwa na si mtu wa kufanya kazi kwa kurariri, angeshaliona hili.

Tuna uzoefu wa muda mrefu sana wa baadhi ya wabunge kutojua ni kitu gani wanaangalia kwenye sekta wanazosimamia, na hii inafifisha kabisa dhana nzima ya bunge kuisimamia serikali kwa niaba ya wananchi.

Halafu kuna mtu anaweza kueleza Kamati ya Ukimwi inafanya nini? Unakuwa na kamati ya wajumbe 22 wanashughulika na masuala ya UKIMWI - what exactly do they do? Na hapo ukumbuke, Malaria inauwa watu wengi zaidi ya UKIMWI, lakini pia kasi ya magonjwa ya moyo na kisukari inakuwa zaidi ya UKIMWI! Sasa ilikuwaje wakachomoka na UKIMWI?

Lakini pia, kwenye nchi ambayo asilimia kubwa ya population ni vijana, na vijana hao wengi wao hawana ajira, kwanini bunge lisiwe na kamati inayosimamia employment? Hapa namaanisha wachome employment kama walivyofanya kwenye UKIMWI. Madhara ya kukariri.

Hayo uliyoyaeleza mengi sipingani nayo hata kidogo. Nia yangu ilikuwa kuweka sawa hoja yako pale uliposema Spika anateuwa wenyeviti wa kamati za bunge.

Kwenye ushauri wako wa kamati ya ajira ni spot on. Hata mimi sioni mantiki ya kuwepo Kamati ya Ukimwi kwa sasa wakati janga la taifa kwa sasa ni ukosefu wa ajira hasa kwa vijana.
Tatu, kuhusu wenyeviti wa kamati, Yes, wanachaguliwa na wajumbe, lakini kama una historia ya wajumbe kuchagua mtu ambaye hana ujuzi (taaluma) na sekta husika- yaani kamati atakayoongoza - basi ungeweza kuweka muongozo, kikanuni. Mfano, Kama kamati inayohusika na uchumi basi mwenyekiti na katibu wake lazima wawe ni backaground ya uchumi, hivyo hivyo kwa sheria, au huduma za afya, madini n.k. Kwa maana hiyo wajumbe wangechagua mtu/watu ambao wana backaground na sekta husika. Hii ingesadia sana kupata watu compentent na hasa wenye kujua ni kitu gani wanaangalia kwenye utendaji wa serikal
Kama wajumbe wa kamati wote watateuliwa wakiwa na taaluma au ujuzi katika sekta za zilizo chini ya kamati ya bunge, nafikiri itakuwa ni rahisi pia kumpata Mwenyekiti na makamu wake ambao ni competent. Tatizo linakuja pale wajumbe wa kamati wanateuliwa kwenye kamati bila kuwa na clue ya kile wanachotakiwa kukifanya kwa vile hawana hata taaluma au ujuzi.

Kuna kamatimzinginenzipo zipo tu kwa ajiri ya wabunge kujiongezea kipato kwa njia ya vikao, ndiyo maana wabunge wote wanatafutiwa kamati bila kujalisha taaluma na ujuzi wao.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom