Utata kuhusu Hadithi ya gharika la NUHU na SAFINA

Hakuna gharika na wala hakuna safina.

Madame hebu nifafanulie hizi aya kuhusiana na Noah(Nuh)
Quran 11:36-37
Quran 11:40

Tofauti kubwa ninayo iona ni kwamba Quran haijataja mafuriko kama ni ya dunia nzima
Ila imetaja mafuriko kutokea, imeeleza kuhusu safina(Ark) na imefafanua kuhusu wanyama kuingia
 
Misri ni fumbo na hata hio Israel sio hilo Taifa mnalolichukulia kwa sasa Israel maana yake ni taifa la Mungu halihusiani na watu wa jamii fulani ndo maana kwenye agano jipya unaambiwa Yesu alikuja kuwafanya watu wa mataifa yote kua israel,......ni kwamba wawe taifa la Mungu kiroho hakumaanisha watu wawe hio Israel mnayoichukulia kimwili, Misri ni ile hali ya kua kwenye taifa la giza(shetani) kwahio alikuja kuwatoa watu misri ya kiroho ili wawe Israel(Taifa la Mungu) na kama mawazo yenu ni kwamba hii Israel ndo taifa la Mungu mmepotea maana humo wamejaa wazayuni ambao wana mambo ya kishetani na ndo wanaosapoti kwa kiasi kikubwa Agenda za LGBT na mambo mengine ya NWO
Kiroho ni nini?

Roho ni nini?

Unathibitisha vipi Misri ni fumbo na si mawazo yako ya kutaka kutengeneza stori ya uongo iwe kweli?
 
Nothing is more coded than the Bible...my friend
Coded na nini?

Code za Biblia zimesaidia nini dunia zaidi ya propaganda za kufikirika tu?

Kina Einstein wamekuja na code zao za kuvumbua Atomic bombs na mambo mengine mengi ya kiuvumbuzi.

Biblia hiyo unayo dai ina code haijafanya chochote zaidi ya stori uchwara tu zisizo na mantiki..!!!
 
KUHUSU Safina ya Nuhu
Kabla sijaanza kuangalia Hasa Inamaanisha nini maana Hii ilikuwa Ni code na sio Tukio halisi..
Tuangalie uhalisia yaani Tukio hili lilianza lini..

HISTORIA YAKE
Tunarudi Nyuma mpaka Miaka ya karne ya 18 BCE, au Miaka kabla ya Musa kuzaliwa....

Hadithi hii ilionekana katika nchi za Uru wa wakaldayo katika Vitabu Ambavyo leo hii vinaitwa Old Babylonian version books..(OBV)..

Kwa jina maarufu linaloitwa "The Epic Of Gilgamesh"

Katika Epic of Gilgamesh kuna Hadith ya Gharika ina itwa "The Atrahasis Great Flood"
kama ambavyo kwenye Biblia Imeandikwa kama "The Noah Great Flood"

"Baada ya maasi na Uovu Kuzidi Duniani Bhasi Mungu Enlil(ambaye pia wanamtaja Kama Yahwe Elohim) alikasirika na akaghairi kwanini aliumba Ulimwengu! Hivyo akaamua kuungamiza kwa maji kwa kutumia gharika..

Hata hivyo Mungu Enki(Ambaye anatajwa kama Jehovah) hakufurahi Adhabu hiyo kwakuwa aliamini wapo watu wema katika nchi wanaostahili kuokolewa ndipo alipomuagiza Atrahasis kuunda safina na kuitengeneza kwa ajili ya Flood itakayotokea na kweli story ikaenda kama ilivyoandikwa kwenye bible..

Hadithi hii Ipo.kwenye OBV (Old babilonic Version)..
Au hata Atrahasis tablets Au hata Epic of gilgamesh....

Na hii ndo story ya Kale zaidi kuhusu Gharika "The Great flood Of Atrahasis"

Ikifuatiwa na story ya hivi karibuni miaka ya 2000-1000 BC Ya "The Great flood of Noah"

Upande wa Historia ya Gharika hiyo nahisi nimeimaliza DeepPond

Kama ukisoma ukaelewa niambie nihame upande huu wa Anunaki story of Flood Nihamie kwenye bible story of flood..
Na maana yake..
Na kama una swali uliza mkuu nitajitahdi kujibu napojua na kuelewa
Dokta mbona hapa hujaweka code ya hiyo story ya Noah's ark, Zaidi ya umesimulia tena Stori ileile kivingine?

Code ni nini hapo?
 
Mnaosema Biblia ina codes, mueleze hizo codes zina apply wapi kwenye huu ulimwengu sio kuleta stori uchwara hapa...
 
Kwa kweli inafikirisha!
Nadhani mimea haikuhusishwa pamoja na samaki na wanyama wa baharini! Lakini hata hivyo chini ya bahari kuna misitu ya mimea ambayo ipo karne nenda rudi,na kama sikose ni moja ya vyakula vya wanyama hao!
Hapana sidhani kuwa mimea haikuhusihwa ili husika, ndio maana naamini haikuwa dunia yote ni eneo la karibu tu na pale, mfano adhabu ya watu wa sodoma na gomora, watu wa nabii swaleh etc, ni adhabu zilizopiga sehemu husika tu.

Kuhusu miti nilifikiria hilo, ni kweli kuna miti chini ya maji, lakini ile huwa inapata mwanga wa jua.
 
Madame hebu nifafanulie hizi aya kuhusiana na Noah(Nuh)
Quran 11:36-37
Quran 11:40

Tofauti kubwa ninayo iona ni kwamba Quran haijataja mafuriko kama ni ya dunia nzima
Ila imetaja mafuriko kutokea, imeeleza kuhusu safina(Ark) na imefafanua kuhusu wanyama kuingia
Weka hizo aya.

Usilinganishe au kujaribu kuitafsiri Qur'an kwa kutumia vitabu vyenye mikono ya watu.
 
Weka hizo aya.

Usilinganishe au kujaribu kuitafsiri Qur'an kwa kutumia vitabu vyenye mikono ya watu.
11 SUURAT HUD
37. Na unda jahazi mbele ya macho yetu na kwa mujibu wa ufunuo wetu. Wala usinisemeze kuwatetea walio dhulumu. Kwani hao bila ya shaka watazamishwa.
38. Na akawa anaunda jahazi, na kila wakipita wakuu wa kaumu yake wakimkejeli. Yeye akasema: Ikiwa nyinyi mnatukejeli na sisi tunakukejelini kama mnavyo tukejeli.
40. Hata ilipo kuja amri yetu, na tanuri ikafoka maji, tulisema: Pakia humo wawili wawili, dume na jike, kutoka kila aina, na ahali zako, isipo kuwa wale ambao imekwisha wapitia hukumu; na watu walio amini. Na hawakuamini pamoja naye ila wachache tu.
41 Na akasema: Pandeni humo kwa Bismillahi, Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, kwenda kwake na kusimama kwake. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu

SUURAT AL-QAMAR
9. Kabla yao kaumu ya Nuhu walikanusha; wakamkanusha mja wetu, na wakasema ni mwendawazimu, na akakaripiwa. 9


54_10.gif

10. Basi akamwomba Mola wake Mlezi akasema: Kwa hakika mimi nimeshindwa, basi ninusuru! 10


54_11.gif

11. Basi tukaifungua milango ya mbingu kwa maji yanayo miminika. 11


54_12.gif

12. Na tukazipasua ardhi kwa chemchem, yakakutana maji kwa jambo lilio kadiriwa. 12


54_13.gif

13. Na tukamchukua kwenye safina ya mbao na kamba. 13


54_14.gif

14. Ikawa inakwenda kwa nadhari yetu, kuwa ni malipo kwa alivyo kuwa amekanushwa.

Naamini Tafsiri hii utakubaliana nayo
Naomba ufafanuzi kwamba hakukua na mafuriko wa safina 🙏🙏
 
Hakuna gharika na wala hakuna safina.
Quran 29 وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَى قَوْمِهِ فَلَبِثَ فِيهِمْ أَلْفَ سَنَةٍ إِلَّا خَمْسِينَ عَامًا فَأَخَذَهُمُ الطُّوفَانُ وَهُمْ ظَالِمُون
َ14. Na bila shaka tulimpeleka Nuhu kwa watu wake na akakaa nao miaka elfu kasoro miaka hamsini, basi mafuriko yakawaangamiza hali walikuwa madhalimu.

فَأَنجَيْنَاهُ وَأَصْحَابَ السَّفِينَةِ وَجَعَلْنَاهَا آيَةً لِّلْعَالَمِين
َ15. Na tukamuokoa yeye na watu wa (ndani ya ) safina, na tukaifanya (iwe mazingatio kwa walimwengu).
 
Quran 29 وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَى قَوْمِهِ فَلَبِثَ فِيهِمْ أَلْفَ سَنَةٍ إِلَّا خَمْسِينَ عَامًا فَأَخَذَهُمُ الطُّوفَانُ وَهُمْ ظَالِمُون
َ14. Na bila shaka tulimpeleka Nuhu kwa watu wake na akakaa nao miaka elfu kasoro miaka hamsini, basi mafuriko yakawaangamiza hali walikuwa madhalimu.

فَأَنجَيْنَاهُ وَأَصْحَابَ السَّفِينَةِ وَجَعَلْنَاهَا آيَةً لِّلْعَالَمِين
َ15. Na tukamuokoa yeye na watu wa (ndani ya ) safina, na tukaifanya (iwe mazingatio kwa walimwengu).
Hapo mmevunga, Kiarabu kinaseba imewachukua tufani, hakuna mafuriko kwenye hicho Kiarabu.

Hata ingekuwepo, "mafuriko" kwenye lugha hayamaanisha ya maji tu. Mara nyingi tunasikia "uwanja umefurika watu".

Huo ndio utamu wa lugha. Kingereza inaitwa 'metaphorical".
 
Mnyama Kama Kangaroo (anaepatikana Australia tu) aliwezaje kusafiri toka Australia, akakatiza bahari mpaka mashariki ya Kati na kufanikiwa kuingia kwenye SAFINA la NUHU.
Kibiblia Kabla ya Gharika kulikua na bara moja tu (scientists call it Pangaea) na ukisoma Mwanzo 10 kulitokea tetemeko kubwa kipindi anazaliwa Peleg na ndio kibiblia inadaiwa mabara yalikua yanaendelea kujitenga mdogo mdogo.
Crystalline Canopy Theory na gharika la Nuhu

Pili wanyama wa sasa sio wale wa antideluvian mfano ukisoma Bible walikuwepo cockatrice (Nusu kuku nusu Nyoka) pia centaur (nusu mtu nusu farasi) pia walikuwepo mamba warefu kuliko wa sasa, kulikua na dinosaurs, kulikua na viumbe wa ajabu kama Behemoth na Leviathan. So biblically na scientifically wanyama wa kale na sasa ni tofauti kabisa.
Wanyama Kama PENGUINS,
Waliwezaje kutembea Zaid ya km 7500 kutoka kwenye ncha za dunia (north Poles) Hadi mashariki ya Kati ili kuliwahi safina la NUHU?
Sio wote walisafiri, nilieleza kwenye nyuzi fulani kuwa Nuhu alikua na "handler" naitwa Oj Bin Anak ambaye ndiye alikua na kazi sio tu ya kusaka wanyama ila pia kukata magogo makubwa kutengenezea hiyo safina.... nilieleza kwamba kimsingi safina walipona watu 9 ila sababu Ogu alitokana na mixture ya "wana wa Mungu" na binadamu basi hakuhesabika kama ni "mtu".
 
Wakuu
Kwenye story ya gharika la Nuhu na safina,
Wanyama wakiwa wawili wawili (dume na jike) waliingizwa kwenye SAFINA Kisha yakatokea mafuriko na Giza likatanda kwa siku 40 mfurulizo, Kisha maji yakapungua na dunia ikaanza upya.

Nnachojiuliza,
1. Kama vitabu vimezungumzia khs wanyama tu, Ilikuaje sasa kuhusu mimea iliyoachwa?
Sidhani mimea mingi tuliyonayo duniani kwa sasa ingeweza kuhimili gharika la siku 40 imezama ndani ya maji bila mwanga wa jua ikaendelea kua hai hata baada ya gharika.

2. Mnyama Kama Kangaroo (anaepatikana Australia tu) aliwezaje kusafiri toka Australia, akakatiza bahari mpaka mashariki ya Kati na kufanikiwa kuingia kwenye SAFINA la NUHU.

Na baada ya safina Ni Nani aliyemerudisha Australia?

3. Wanyama Kama PENGUINS,
Waliwezaje kutembea Zaid ya km 7500 kutoka kwenye ncha za dunia (north Poles) Hadi mashariki ya Kati ili kuliwahi safina la NUHU?

Nawasilisha 🙏
Ulitakiwa ujiulize kwani Gharika ya Nuhu ilitokea dunia nzima ? Jibu ni kinyume chake.
 
Hapo mmevunga, Kiarabu kinaseba imewachukua tufani, hakuna mafuriko kwenye hicho Kiarabu.

Hata ingekuwepo, "mafuriko" kwenye lugha hayamaanisha ya maji tu. Mara nyingi tunasikia "uwanja umefurika watu".

Huo ndio utamu wa lugha. Kingereza inaitwa 'metaphorical".
Qur'an bibie haina Majazi.

Inaonekana una ufahamu mdogo sana juu ya Qur'an.
 
Back
Top Bottom